Paschal Mayalla, mwandishi na mtangazaji mwandamizi, ambaye amepata ajali mbaya ya pikipiki alipokuwa akisafiri kuelekea Dodoma akitokea Dar, amehamishiwa Hospitali ya Muhimbili kitengo cha Moi asubuhi hii na habari zinasema hali yake inaendelea vizuri.
Ndugu wa Paschal, Isaac Kasanga wa Easy Finance, kaiambia globu hii ya jamii sasa hivi kwamba mgonjwa alisafirishwa leo asubuhi kwa barabara baada ya kukosekana ndege.
Kasanga amesema Paschal anaongea vizuri tu ila analalamika kwamba ana maumivu makali kichwani na pia mkono wake wa kushoto umekufa ganzi.
picha ni kwa hisani ya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Upone haraka Paschal.

    ReplyDelete
  2. Pole sana Ndugu yangu lakini kweli hizi adventure kusafiri na pikipiki mpaka Dodoma jamani ai??

    ReplyDelete
  3. pole sana kaka yangu mwenyezi mungu atakuondolea maumivu,ugua pole.

    ReplyDelete
  4. Pole sana "Mzee wa kiti moto", Ila jamaa ana pikipiki kubwa sana nadhani ni 3500cc, kwenda nayo Dodoma si ajabu ila cha muhimu ni je ilikuwa katika condition yake, yaani nzima, maana bongo mtu anaweza safiri na gari yenye tairi zenye kipara kuna kamsema ka kuagia mtu akianza safari "HAYA NGOJA NIOMBE MUNGU"

    ReplyDelete
  5. pole sana kaka Mayalla,mungu akuponye na maumivu yote uliyonayo katika jna la bwana na mwokozi wetu yesu kristu."Hakika alichubuliwa kwa makosa yetu na kwa kupigwa kwake tumepona".

    ReplyDelete
  6. Pole sana Paschal, my prayers are with you for quick recovery.
    Mdau, USA

    ReplyDelete
  7. picha mbaya, inakatisha tamaa kwa wanaomtakia mayalla apone haraka.

    ReplyDelete
  8. Pole sana kaka nakuombea upone haraka.

    ReplyDelete
  9. Mambo mengine mnataka tu kumjaribu Mungu, mtu unasafirije na pikipiki? Anyway, ndio imeshatokea. Ugua POLE

    ReplyDelete
  10. Pole sana! Wamuangalie kaka wa watu asijekua anainternal bleeding. Bongo saa nyingine mpaka upate scan inakua too late

    Jamani lakini pikipiki kutoka Dar - Dodoma naona mbali sana tu. Na mavumbi yale sio nzuri kwa afya acha ajali za barabarani

    ReplyDelete
  11. yaani kweli mtu aendeshe pikipiki from Dar to Dodoma, thats a little too much. Anyway, get well soon, lakini huo mchezo ulioufanya siyo wa busara kabisa.

    ReplyDelete
  12. POLE KAKA PASCAL KWANI HIYO BARABARA YA DODOMA KUNA NINI JAMANI?, MBONA ITATUMALIZIA WATU!, AU NDIO KAFARA YA MAFISADI HIYO KUMALIZA WATU INOCENT MHN!...

    ReplyDelete
  13. I pray for your quick recovery brother Pascal. May you get well soon.

    ReplyDelete
  14. Hivi nani anashikilia rekodi ya kusafiri na pikipiki Tanzania?

    ReplyDelete
  15. kaka mayalla na mapikipiki haukomi ndugu yangu? Umeshapiga chini mara nyingi, i thought ungeacha utumie hata corolla,
    Anyway ugua pole, upone haraka na usirudi kwenye chombo cha miguu miwili na body yake ni mwili wako.

    Jirani yako, Sinza

    ReplyDelete
  16. Ni kumjaribu Mungu vibaya. Nashangaa wale simba wa Mikumi kwanini walimuachia apite.
    Pole Kaka

    ReplyDelete
  17. kweli kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake ila sijui wengine utafikiri hawaishi tanzania ooh mara simba wa mikumi kwani nani kakuambia kwamba kwenda dodoma toka dar lazima upite mikumi?
    Anyway mi kwa mtazamo wangu dar kwenda dodoma kwa pikipiki wala si mbali kama ambavyo watu wengi wamesema ila sema tu kwa sababu ajali imetokea kila mtu atasema lake.
    Pole sana pascal kwani barabara za tz kila mtu anaendesha kwa sheria yake ndiyo maana utakuta hata mabasi wana-overtake hata sehemu ambazo haziruhusiwi au lori linaharibika njia na linapaki bila hata kuweka viashiria kwamba kuna gari mbovu. Kwani ajali nyingi zinazotokea tanazania ni zile ambazo zinaweza kuzuirika kabisa kama maaskali wa usalama barabarani wangekuwa wanajua hizo sheria kwa kuanzia pale wanapotoa leseni kwani madereva wengi tanazania hawajui sheria za barabarani hasa walio dar es laam wengi ni wale wa kulipeleka gari mbele tu

    ReplyDelete
  18. Pole kwa ajali,lakini ninachoshindwa kuelewa ni kwamba tunasikia bongo imekuwa tambarale je inakuwaje hata ndege ya kumsafirishia mjeruhi ikosekane tena kwa mtu anayefahamika kama huyo? anyway maybe that's just me.mdau T.O

    ReplyDelete
  19. KWA MAREKEBISHO TU
    1. BARABARA YA DAR-DODOMA HAINA MAVUMBI KAMA MMOJA WETU ALIVYOSEMA. NI MKEKA. MNAKAA SANA NG'AMBO, HAMJUI HATA YANAYOFANYIKA KWENU.
    2. UNAPOENDA DODOMA KUTOKA DAR HUPITII MBUGA YA MIKUMI. UNACHEPUKIA MOROGORO MJINI (MSAMVU) NA MBUGA YA MIKUMI IPO NJIA YA KWENDA IRINGA.

    CHA MSINGI.

    TUSIMLAUMU NDUGU MAYALLA, USAFIRI WOWOTE ULE RUKSA, BAISIKELI,, PIKIPIKI, GARI N.K (KWANI BARABARA YA DAR-DOM NI SAFI NA SAFE.

    CHA MUHIMU.

    TUMWOMBEE NDUGU MAYALLA APATE MATIBABU MAZURI (KWANI KUMWOMBEA APONE NI KAMA MTOTO KUKIMBIA BILA KUPITIA STAGE YA KUTAMBAA KWA TZ). HAPA NINA MAANA KUWA MATATIZO MENGI YA HOSPITALI ZETU NI KUTOA TIBA NZURI. QUALITY QUESTION. HAPA NINA MAANA YA MGONJWA WA GOTI KUPASULIWA KICHWA (remember?).

    HOPE YOU GET BETTER BROTHER!

    ReplyDelete
  20. pole sana kaka Mayalla-Robert Mujuni

    ReplyDelete
  21. Pole sana 'anko'Paschal mungu atakubariki.
    Tusimlaumu Paschal:Kuendesha pikipiki nadhani ni 'obby'kuna watu wanapenda sana usafiri wa pikipiki.
    Huyu ni mwandishi wa habari:Mimi bado nadhani alikuwa haendi Dodoma tu,Paschal alikuwa ana 'program' ya kuingia na vijijini kwenye safari yake ambako barabara zetu ni mbovu kwa magari,usafiri wa pikipiki ni mzuri zaidi kupata habari za vijijini.
    Maoni mengine mmmh:Yameshajibiwa

    ReplyDelete
  22. POLE TENA SANA
    By FOTU

    ReplyDelete
  23. Pole kaka Paschal. lakini jamani vitu vingine haviingii akirini kiurahisi kwamba paschal huyu tunayemfahamu.ndio kachukua uwamuzi wa kusafiri na pikipiki mpaka dom?
    yaweza kuwa alikuwa anataka kuweka rekodi,ila ni kitu ambacho huwezi tegemea kwamba mtu kama paschal anaweza fanya vitu vya jinsi hiyo.
    tunaamini kwamba kifo hupangwa na Mungu lkn vingine mmh.
    Paschal kaka yangu usije rudia ujinga kama huo tena.

    ReplyDelete
  24. pole sana Pascal Mayala.

    Mungu akujalie upone haraka.

    ReplyDelete
  25. pole sana kaka mayalla duh hio kweli ni adventure!nakukumbuka kwenye white paper a.k.a kitimoto, mbuzi katoliki!!get well soon brother!

    ReplyDelete
  26. Ndugu zangu ajali haina kinga ila kuna mambo mengi yanayoweza kupunguza au kuepusha ajali, Kaka Mayalla kutumia pikipiki kutoka Dar hadi Dodoma ni jambo la kawaida kabisa na wala si la kushangaa kwani hizo pikipiki huenda mbalizaidi ya hiyo distance ila pikipiki inapopata ajali mara nyingi huwa mbaya sana.
    Kaka Paschal pole sana.
    MDAU ; TOKYO.

    ReplyDelete
  27. Pole sana Pascal, nakutakia uweze kurudia afya njema,ila napenda upone haraka ili nije kukuchapa vibao na ikiwezekana nikufunge jail kabisa kwa kosa la kutarisha masiha yako nakutupa sisi tabu ya kuanza kukuonea huruma na kutushtua roho, kwakweli kitendo unacho fanya sio haki kabisa na napenda nikushauri uachane nacho , kama ilikwua ni kusave nauli una save nini zaidi ya kuishia hospital ,tena Mungu mkubwa huja patwa na namadhara zaidi.

    Nachokuomba ukipona achana kabisa na Pikipiki ni chombo hatari sana ,please achana nacho tunakuomba!

    ReplyDelete
  28. Pole sana ndugu yetu Paschal, ninakuombea upate kupona haraka na bila ya kuendelea kuwa na maumivu mengi.

    Ninaunga mkono kwamba wana-Bongo walio mbali wawe wanafikiria kuitembelea nchi ya badala ya kuropoka bila kuijua hali halisi ilivyo huku.

    Pia, naomba kufafanua kwamba pikipiki yenye engine ya 3500cc itakuwa na engine kubwa kuliko hata Land Cruiser Prado au Land Rover za Defender/Discovery. Hata Valentino Rossi na wenzake hawafanyi mashindano na engine kubwa hivyo, kwani wanatumia mashine ya 800cc tu.

    ReplyDelete
  29. Pole our dear friend pascal, wana wa udsm facult of law 2007 tunakuombea kwa mwenyezi mungu upone haraka.

    Amen

    ReplyDelete
  30. Kaka Mayalla,pole sana.Ndugu zangu,imeishatokea.Huu siyo muda wa kumlaumu ila kumwombea apone haraka.Kwa uzoefu wangu,lolote laweza kutokea.Akipona,nendeni mkampe maoni yenu ana kwa ana maana hapo atakuwa anayahitaji sana.

    ReplyDelete
  31. FOTU

    Ni wewe uliyekuwa unakaa Masaki na kupiga picha?

    ReplyDelete
  32. jamani ndugu zangu watanzania hebu tuacheni hizi fikra za sisi wanyumbani na ninyi wa ng'ambo.kila mada ikija lazima watu wapigane vijembe,mara oh mnakaa sana huko ng'ambo bila kujua yanayotokea nyumbani,au nasikia bongo tambarare,mimi naona inazidi kuongeza uhasama.kwani sisi wote ni wamoja na kila mtu na sababu zake za kuwepo alipo, wote ni watu wazima.hakuna aliyetekwa nyara na kulazimishwa aishi alipo.kwa hiyo naona haina haja ya kukumbushana tulipo.asante sana,mungu ibariki nchi yetu na watu wetu wawe na upendo,pia bwana mayala apone haraka.
    ocd.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...