Kile ambacho kilionekana awali kama "kutaka kulipa kisasi" kwa wana-Simba waishio Washington Dc na vitongoji vyake kwa kipigo cha June 15, kiligeuka kuwa kilio kingine baada ya timu iundwayo na wana-Yanga wa hapa kuwatungua kwa mabao 7-3 katika mchezo uliofanyika katika viwanja vya michezo na mapumziko vya Middlebrook, Silver Spring MD.
Simba ambao waliwasili mapema uwanjani na kufanya "pasha moto" kabla ya wenzao, walianza vema kipute hicho kwa mabao mawili ya haraka lakini jinsi muda ulivyosonga ndivyo wana-Yanga walivyojipanga vema zaidi na kusawazisha na mpaka wakati wa mapumziko timu hizo zilikuwa sare ya mabao matatu.
Kipindi cha pili mambo yaliwaende kombo wana-Msimbazi wa DC baada ya kutunguliwa mabao manne, mawili kati yao yakiwa ni kwa njia ya Penati kutokana na mabeki wa timu hiyo kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Hata hivyo, Yanga wamshukuru mchezaji Kendo Laizer aliyejiunga nao baada ya kukosa namba ktk kikosi cha kwanza cha Simba na ambaye aliwafungia mabao mawili na kuwa mwiba mkali ktk purukushani zote za kusaka magoli yao.
Pia kipa wa wana-Simba Hillary Mshana alionesha uwezo mkubwa wa kuokoa hatari langoni mwao na kuwakosesha Yanga mabao zaidi ya manne ya wazi kiasi cha kusifiwa na wadau wa timu zote. Mbali na matokeo hayo, mechi ilikuwa yenye NIDHAMU ya hali ya juu na pia mjumuiko wa familia, nyama choma pamoja na michezo mbalimbali kwa watoto iliifanya siku hii ifane zaidi.
Wakati huo huo, lile "BASH LA UBWETE" kwa Labor Day Weekend limeanza kuwekwa vyema na ratiba ya awali imekwishatoka.
Katika ratiba ya Bash hilo liandaliwalo na Chama cha Jamii ya wa-Tanzania waishio Washington DC na vitongoji vyake (A.T.C Wash DC Metro) na ambalo hushirikisha waTanzania toka majimbo mbalimbali, siku ya Ijumaa kutakuwa na Disko litakalofanyika katika ukumbi wa Mirage (Mirage Hall) uliopo University Blvd Hyattsville MD.
Siku ya Jumamosi kutakuwa na michuano ya soka, michezo ya kifamilia na Nyama choma majira ya jioni katika viwanja vya michezo na mapumziko vya Middlebrook huko Silver Spring MD ikifuatiwa na Disko usiku huo na kisha Jumapili kutakuwa na fainali za soka zikiambatana na michezo na nyama choma zikifuatiwa na disko kali litarajiwalo kujumisha wakali katika mixing kama Dj Joe (WKYS 93.9 FM), Mix Master Dj Luke, Dj K Young Blood na wengine wanaoendelea kujipanga vema kabla hawajahakikisha ushiriki.
Timu zote toka nje ya DC Metro zitakazopenda kushiriki ziwasiliane na uongozi wa jumuia kwa email
ama kwa kumpigia simu Rais wa Jumuiya kwa namba
443-278-6119
Taarifa kamili za nini kitafanyika ndani ya muda gani zitawajia punde.
A.T.C Washington Metro
Taarifa kamili za nini kitafanyika ndani ya muda gani zitawajia punde.
A.T.C Washington Metro


Duh! Hadi marefa wa ughaibuni wanaibeba Yanga na mipenati.
ReplyDeleteNawapa pongezi wabongo wa DC metro kwa kuanzisha hii kitu(kukumbushana vitu vya home)lakini nina tatizo moja tu.Tunajuwa soka la tanzania(hasahasa Bara) lina defainiwa na Yanga na Simba.Tatizo ni hili hivi watu wanaotoka mikoani kwa nini wasianzishe timu zao ili ku-represent wanakotoka kama wanaotoka Mbeya waje na Tukuyu stars nk,Wanaotoka Mwanza(Pamba)Kagera(Kagera stars/Rtc kagera) Arusha(ndovu/whatever)Moshi(ushirika)Tanga(coastal/African sports)mtwara(bandari) Nk. Pia kwa wale watokao Visiwani waje na timu walizokuwa wanashabikia(malindi,small simba nk)
ReplyDeleteNaomba mnielewe hapa sina maana ya kubaguana kimikoa wala nini.Nachotaka kusema ni kuwa kuleta Yanga na simba tu hai-represent Tanzania kwa ujumla.Nadhani hii itatukumbusha vitu vya zamani tunavyovimisi toka home.
Just my opinion.
Mdau amekuja na wazo zuri kuhusiana na wadau kuanzisha timu za mashabiki wa wana Kimanumanu, TP Lindanda nk. Kinacholeta ugumu ni kwamba hata hizo timu za mikoani alizozitaja mdau nazo zinapohitaji kujigawa kwa ajili ya kufanya mazoezi huwa zinajigawa kwa misingi ya ushabiki wa Simba na Yanga (kumradhi wadau).
ReplyDelete