juu ni kikosi cha yanga na chini ni simba wa washington dc kabla ya mechi yao ilopita

Chama cha waTanzania waishio Washington DC na vitongoji vyake ( A.T.C Metro) kinawakaribisha nyote kwenye nyama choma itakayofanyika Jumapili hii tarehe 3 saa 10 jioni katika viwanja vya michezo na mapumziko vya Middlebrook Park, Silver Spring MD.


Mbali na nyama choma na fursa ya kukutana pamoja kama wana-familia, pia kutakuwa na mechi ya soka ya marudiano kati ya Washabiki wa Simba vs wale wa Yanga.


Ikumbukwe ktk mechi ya awali iliyofanyika Juni 15, wana-Yanga waliondoka na karamu ya magoli dhidi ya watani wao hao.


Nyote mnakaribishwa


Uongozi

A.T.C Washington DC Metro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. wasiwasi wangu wataingia mitini hao Yanga si tumeona kaka zao walivyoyeya AIBU.
    Watatoka nduki hao baadae waanze kuleta lawama

    ReplyDelete
  2. "Double D" unakumbuka ulivokosa goli la wazi mechi ya PCM vs PCB? Badala ya kupiga mpira kufunga goli ukaishia kubamiza ugoko kwenye chuma cha goli.. I can't forget that moment bro...

    Kisede.

    ReplyDelete
  3. Wachovu nyie! Changanyikeni nyote Simba na Yanga mje ATL tuwamiminie mabao! Tanzanite Fc ndio baba lao!! Kwa mawasiliano please pitia www.tanzanitefc.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...