Miss Universe Tanzania 2008, Amanda Ole Sulul akikabidhi vifurushi vyenye zawadi kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Suleiman Muttani, alipozuru hospitalini hapo, Dar es Salaam jana kwa lengo la kusaidia wagonjwa. Katikati ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe. Zain ilimdhamini Amanda.
Miss Universe Tanzania 2008, Amanda Ole Sulul (katikati) akimfariji mgonjwa, Halima Ramadhan aliyelazwa Hospitali ya Mwananyamala, alipozuru hospitalini hapo, Dar es Salaam jana kwa lengo la kusaidia wagonjwa. Kushoto ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe.
Miss Universe Tanzania 2008, Amanda Ole Sulul akikabidhi kifurushi cha Zain chenye zawadi anuwai kwa mgonjwa, Farida Pius aliyejifungua watoto pacha, Kulwa na Doto katika Hospitali ya Mwananyamala, alipozuru hospitalini hapo, Dar es Salaam jana kwa lengo la kusaidia wagonjwa. Katikati ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe. Zain ilimdhamini Amanda.
Dar es Salaam,
Septemba 10, 2008
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain inayotoa huduma katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, imemdhamini mrembo anayeshikilia taji la Miss Universe Tanzania 2008, Amanda Ole Sulul kwa lengo la kusaidia shughuli mbalimbali za jamii. Ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kauli mbiu yake ya A Wonderful World (Ulimwengu Maridhawa).
Zain imemdhamini Amanda Ole Sulul anayeshikilia taji la Miss Universe Tanzania 2008 linaloandaliwa na Kampuni ya Compass Communications, kwa kumwezesha kuandaa kazi mbalimbali za hisani ikiwa ni pamoja na kusaidia watoto na akina mama wajawazito waliolazwa katika wodi za hospitali za Serikali.
Hospitali mojawapo ambayo mlimbwende huyo alizuru na kufanya kazi za hisani kusaidia jamii ni ya Mwananyamala ambako Amanda alinunua bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na khanga, nguo, mashuka, manukato na mengineyo kwa ajili ya watoto na akina mama wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.
Pia Amanda amejitolea kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati mrembo huyo alipozuru hospitalini hapo leo, Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe, alisema: "Zain kama kampuni tunawajibika kusaidia jamii ambayo imekuwa ikituunga katika biashara yetu.
“Zain itaendelea kudhamini shughuli mbalimbali za hisani kwa jamii katika Hospitali ya Mwananyamala kutokana na ukweli kwamba, tumekuwa na uhusiano mzuri na hospitali hii.
"Mtoto wa Zain alizaliwa hospitalini hapo Agosti Mosi, mwaka huu saa 6:05 usiku, siku ambayo Zain ilizindua upya jina lake Tanzania, na habari njema ni kwamba mtoto alipewa jina la Zain ambalo ni kampuni yetu.
"Kwa maana hiyo, huu ni mwendelezo wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na Zain kwa jamii," alisema Tunu.
Amanda aliyeambatana na warembo wenzake, Miss Universe namba mbili, Jamillah Nyangasa, Miss Universe namba tatu, Eve Babuely na Miriam Odemba, awali, alikabidhi vifaa hivyo kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Suleiman Muttani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tunaipongeza sana compuny ya zain kwa kujua mahali panapohitaji msaada. Hizi Hospital zetu za serikali tunajua siku zote huwa kunakuwa na watu ambao wanakuwa na uhitaji mkubwa haswa word ya akina mama na watoto.

    Mwaka jana kuna mrembo mmoja ambae niliona alipeleka zawadi yake pale Aghakhan hospital kwakweli hapo ni kama kumwongezea aliyenacho kwani sijui kama kuna mtu anaweza kulipia laki 5 za kujifungua pale Aghakhan hosp. ashindwe kununua packet ya pempas. Ahsanten sana Miss Universe na timu yako nzima mkiongozwa na wadhamini wenu Zain.

    ReplyDelete
  2. Anon hapo juu, kujifungua Agakhan sio kuwa na pesa, kuna kampuni nyingi ambazo wafanyakazi wao wanatibiwa hapo kuanzia mabosi hadi wahudumu. kama ni hivyo basi hata wananchi wa vijijini walalamike kwanini misaada itolewe hospitali za DSM.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...