Kaka Michuzi,
kile kilio chetu kimesikika na wapiga debe wakuu ingawa ni aibu watu toka nje kuja kutupigia debe kwenye suala ambalo sisi kaka zetu na dada zetu wanaumia.
Chama kisicho cha kiserikali kimeamua kulivalia njuga suala la Mauaji ya Albino na hii ni kutokana na Group niliyo anzisha kule Facebook kukusanya Signature kwa ajili ya kuziwakilisha na hii ni Mail Yao kwangu:-
Hi Mr Pius!
My Name is Kim, I work for Positive Exposure, an arts organization dedicated to fighting the stigma that people with genetic conditions often experience. PE has worked extensively with the albinism community around the world and is planning a trip to Tanzania in October.
We were wondering if it would be OK to use the names from this Facebook group to show the President of Tanzania when we meet with him and other government officials next month.
Our organization's website is
We also have a Facebook page. The trip is being organized by an organization called Under the Same Sun
Any publicity you could give to Under the Same Sun, whose mission is to make a real difference in the lives of people with albinism in Tanzania, would be appreciated.
Please let me know if it is okay,
and thank you for calling attention to the atrocities going on in Tanzania.
Kim
Mdau
Pius Pius Mikongoti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. nilishatoa tamko hapa kwamba wapatiwe passport ili wakaishi nchi a ulaya na marekani ambapo wenzao waungu wapo. Hao ndio wazungu wetu mungu aliutujalia. Ndio wawekezaji wazawa

    ReplyDelete
  2. Tumaini sikuelewi unaongea nini,
    Mtu kazaliwa Tanzania mama yake ni mweusi apelekwa akaishi Ulaya kwasababu ni albino.
    Hivi wewe una watoto?, na kama huna subiri utakapopata tuone kama itakua rahisi umuache mwanao akaishi nchi nyingine kwasababu ni albino.
    Wengine hili jambo wanalichukulia mzaha.

    Ni kuambie basi hata hao watanzania ambao sio albino na wanakaa nchi za nje ni kwa ajili yakutafuta tu, kama nchi yetu ingekua imeendelea sijui kama ingekua sababu awaache wazazi wake miaka miwili mitatu bila kuwaona kwa ajili yakutafuta maisha

    ReplyDelete
  3. HONGERA SANA PAPAA PIUS,

    HUU NI MFANO TOSHA KUWA MIONGONI MWETU POPOTE PALE TULIPO IWE KWA VIKUNDI AU MMOJA MMOJA, KWA UWEZO WETU MKUBWA AU MDOGO TUNAWEZA KUFANYA MABADILIKO CHANYA KULE NYUMBANI KWA FAIDA YA JAMII MZIMA.

    NASHAURI TUTUMIE MFANO HUU KUZUNGUMZA NA KUFANYA KWA MATENDO PALE TUNAPOWEZA BADALA YA KULALAMIKIA WENGINE KWA NINI HAWAFANYI.

    NAWAKILISHA.

    SOAMES, UK.

    ReplyDelete
  4. MFANO WA MKUU PIUS NI WAKUIGWA NA KWA KUSHIRIKIANA NA BLOG YA JAMII, HII INAONYESHA WATU WAMEIKUBALI HARAKATI NZIMA KWANI NA MI NILIIONA KUPITIA GROUP YA FACEBOOK AMBAYO BWANA PIUS ALIIANZISHA NI BAADA YA WANAFUNZI WENZANGU HUKU USA KUNITUMIA NA KUNIAMBIA KUHUSU HILI SUALA.
    NAKUTAKIA MAFANIKIO MKUU NA USICHOKE NI KWELI TUUNGANE KWA PAMOJA TUNAWEZA.
    KIZAKO - TEXAS

    ReplyDelete
  5. Swala hili si lautani hivyo waandishi wa makali hizi tafadhalini chungeni uchanguzi wa misamiati yenu hapa nakemea kuelezea hii habari ya kusikitisha kama "upele"

    ReplyDelete
  6. Tumaini PUMBAA!
    Una ubongo wa samaki!

    ReplyDelete
  7. We tumaini unachefua sana, watu wako serious wewe unaleta mzaha. Comments zako zinaboa sana. Kama huna cha kuchangia sio lazima uandike.

    Great job Pius.

    ReplyDelete
  8. kaka michuzi naomba uwe unadelete comments za Tumaini manake most of the times ni ujinga tu. watu wakiwa serious yeye anadhihaki. Ila sishangai sana manake alikuwaga kichaa wakati fulani kwahiyo yawezekana maradhi yamemrudia.

    ReplyDelete
  9. ubongo wa samaki ndio maana nakamatwa kwenye nyavu. hakuna upekwe ni familia mzima inasafiriswa. ila kuna mdau hayuko tayari mtoto wake apate visa yaani hata shangilia huu ni uzalendo wa hali ya juu.

    ReplyDelete
  10. mlongo piusi good job. nipiganisha kala. wavi wapele kwanza. kalembwana mlongo

    ReplyDelete
  11. Tumaini si mzima ata kidogo.
    Anyway nafikiri kuna haja ya serikali kutoa tamko kuhusu hili na si tamko tuu bali utekelezaji wa kina ni aibu kuona watu wa nje ndio wanaishinikiza serikali wakati mdau Pius analeta hapa mezani ni wachache walichangia na wengi tulipuuza (nikiwemo mimi) leo roho inanisuta kwa mafanikio yaliyofikiwa.
    Kwangu naitya mafanikio kwani mpaka hapo angalao kilio kitafika.

    Kwako mdau ulie kerwa na neno Upele..." kwangu mi naona ni sawa kwani ulikuwa upele uliokosa mkunaji na sasa umepata mkunaji, kwa maana litapigiwa kelele mpaka kielewe, mpaka upasuke so kichwa kiko sawa.
    Hongera Pius, Hongera Michuzi

    ReplyDelete
  12. kumbe tumaini alishaugua kichaa,,sishangai why aandika ivi
    na uyu mwandishi nahisi aliugua degedege yan waandika 'upele umepata mkunaji?'kweli??
    na wewe ulieandika kikabila gani sijui apa koma
    michu usipost htz kinds of rubbish
    TUNDELEZE MAPAMBANO DHIDI YA UNYAMA WA ALBINO,,niliwatch kipindi iki mama mmoja avoelezea jinsi mwanae mdogo navoogopa ata kutoka nje,,,utalia machozi

    ReplyDelete
  13. mlongo pius ne nguyenda kulanda mtela nguyisa, ukutila ng'odu wahavi myangu? usiogope hiki ni kidamba

    ReplyDelete
  14. Pius Pius Mikongoti nakuaminia a.k.a Baba 3G's endeleza Libeneke thidi ya waonevu kaka.

    Wako Lyimo

    ReplyDelete
  15. Ndugu zangu wanajamii wapenzi wa Blog hii huwa nashangazwa na kitu kimoja, ni kwamba humu hatuchukulii vitu serious au ni nini? Maana kila kinapowekwa kitu cha maana huoni Post zaidi utapata 10 ila ngoja kiwekwe cha kipuuzi tuu utaona watu kibao wanachangia. Nahisi ili kuifanya hii Blog kuwa ya jamii lazima tumuunga mkono Michuzi kwa jitihada za kutuhabarisha, halipwi na mtu kunapotokea mambo ya kijamii tujitoe kama walivyo na umoja wasomaji wa Bongo Celebrity.
    Hongereni sana Michuzi na bwana Pius Mungu atawalipa.
    Mdaudau - New F/Land

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...