Mwenyekiti wa CCM, JK, akisalimiana na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba (kushoto ) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mbunge wa Ismani, William Lukuvi (wa pili kua) baada a kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 9, 2008 kuongoza vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. duh, mkuu wa nanihii usiniambie na we kutua tu Dar ukaruka tena kwenda Dodoma. Kama ni hivyo pole na kazi, ndio kutafuta ugali bwana au sio. Ila watoto wasije wakasahau tu baba anafananaje, maana kila siku uko njiani kaka Michu. Tehe tehe

    ReplyDelete
  2. Mkuu wewe ni mtaalamu,mrudishe nape,kijana makini sana na ukilitakia mema taifa.Usidanganywe na hao wazee walioshachoka kufikiri.Nape atalikomboa Taifa na UVCCM.Unless hatari sana ya kufa kisiasa.

    ReplyDelete
  3. Mkuu, naomba kamuokoe NAPE jamani, hayo maamuzi yaliyotolewa si halali kabisa.

    ReplyDelete
  4. Jamani Nape, lakini yote muachie Mungu... lililo wazi halitajificha miaka soon everything will mwaaa

    ReplyDelete
  5. Michuzi,
    Najua unafika mbali sana na ndio maana unafuatana na mheshimiwa kila anakoenda.
    Tunaomba utufikishie hili kwa Mheshimiwa makamba...."hizo siasa za kutosamehe na mpaka kufikia kutoa kauli za vitabu vitakatifu bila kujari maana halisi ya maandiko hayo... inaonyesha jinsi gani anang'ang'ania katika mambo yaliyopitwa na wakati....hivi yeye alipomtia mimba mtoto wa shule Kigoma, kama asingesamehewa angekuwa hapo alipo. Huyu mzee naona amefirisika kimawazo mpaka anasahau utu.
    Nape Nauye..hakufanya ketendo kiovu ukilinganisha na yeye alivyomtia mimba mwanafunzi na kumharibia future, Nape Nauye alikuwa anatetea maslahi ya nchi na wananchi, lakini mueleze huyo mzee wa watu, hii ni karne ya 21, hatuhitaji just a tick box thinking za hao wazee, tunahitaji new thinkers ambao wanatoa uamuzi kulingana na hoja na sikutoa hoja kulingana na maamuzi.
    Nchimbi yeye sina shida naye kwani kijana mdogo lakini anaonekana amekalia "convetional wisdom"...ajue sasa hivi dunia imebadilika, na haihitaji watu waliojengewa majina kwa sababu zisizo za msingi....muda wa Mtoto wa fulani umeshapitwa na wakati, na hii imejidhihirisha sasa hivi kuwa huyu Emmanuel pamoja na Umri wake mdogo utafikiri amebeba akili na uwezo wa kufikiri wenye umri kama wa baba yake au kama wa Makamba....Aangalie vijana kama akina Zitto, Ezekiel Mayige na wengine wanavyofanya kazi.....Nchimbi umeingia siasa kwasababu ya familia unayotoka na ndiyo sababu mambo mengi unayoyafanya hayana upembuzi yakinifu bali "ni convetional wisdom'inakuongoza ..Kinachotisha kwa Bwana mdogo Nchimbi anavidhalilisha hata vyuo vilivyomtunuku shahada alizonazo. Nchimbi nenda kaulize "youth movement ya trade unions" dunia hii inaongozwa na watu wenye umri gani? jaribu kwenda hata hapo kwenye ofisi za vyama vya wafanyakazi uulizie watakueleza na pili ujue ukitaka wanasiasa halisi nenda vyama vya wafanyakazi...ndio wamezoea matatizo ya wananchi na kuyatatua....siyo wewe na hiyo design ya tick box design.
    We need watu wenye mapenzi mema na nchi na siyo watu wanaopenda sifa kama Nchimbi...we need Obama's, self made with true conviction and clear vision.
    Makamba, Nchimbi...tumechoka na urembo wenu wa sanaa. Msikilizeni Msuya na wazee wengine ambao wako exposed na dunia hii na siyo nyie mumekaa munakariri kila kitu mpaka vitabu vitakatifu....makamba kama unajua maandiko fungua ministry kama Kakobe na siyo kila siku unatutisha na maandiko usiyoweza hata kutoa tafsiri sahihi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...