Mahakama kuu inayosikiliza kesi ya mauaji ya wafanyabiashara inayomkabilia aliyekuwa Mkuu wa upelelezi Kamishana Abdallah Zombe na wenzake leo ilihamia kwa muda msitu wa Pande ambako marehemu wanadaiwa kuuawa. Kabla ya kufika kwenye msitu huo Mahakama ilipita pia 'ukuta wa posta' eneo ambalo ilidaiwa na askari ndiko yalikofanyika majibishano ya risasi kati ya askari na marehemu hali ilikuwa tete katika msafari wa kutembelea maeneo hayo yaliyokuwa yakitolewa ushahidi na Mkuu wa Polisi Tabora, Bw. Emsom Mmari, ambaye ni shahidi wa 30 upande wa serikali.
zombe na watuhumiwa wenzie wakielekea sehemu ya barabara ya sam nujoma
hapa ndipo mashahidi upande wa mashtaka wanadai walikouliwa wafanyabiashara
shahidi mmari akitoa maelezo sehemu inayodaiwa kuwa ya tukio
kamishna zombe akihoji shahidi sehemu inayodaiwa kuwa ya tukio
kamishna zome na watuhumiwa wenake wakiwasili msitu wa pande
kamishna zombe akiwa na mh. jerome msemwa, mmoja wa mawakili wanaomtetea

ndugu ya wafanyabiashara waliouwawa
mahakama ikiwa maeneo ya sinza kwenye nyumba waliyofikia wafanyabiashara
shahidi namba 30 mmary akitoa ushahidi wake karibu na
wauhumiwa wakiwa karibu na ukuta wa posta




ny

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kazi kweli kweli!!
    Ila big up kwa upelelezi, noo rushwa kutembea na haki itendeke
    Dada Lao

    ReplyDelete
  2. uyo aliyetoa ushahidi atapewa ulinzi au maana Zombe hakuwa peke yake kuna mtu amepotea katika watuhumiwa

    ReplyDelete
  3. nimependa sana jinsi ulivyoripoti na picha kuelezea every step. Vey nice and keep up the good one. Am very interested in the case so hope to hear more on it. mtuhumiwa kapotea as in alikua arrested akatorokaa au?

    ReplyDelete
  4. hongera sana bro kwa kutupa vitu live,lakini nchi hii bwana, utashangaa kuona at the end of the day zombe anaachiwa, yani hakuna haki kabisa!!!!

    ReplyDelete
  5. i thank God the almighht who empower people. imeandikwa ole wake autwaaye uhai wa mwenzake kwa sababu ya kujipatia fedh aau mali au chochote alichonacho mtu.GOD forbid them.

    natumaini rushwa haitatumika kuwasaidia wauwaji kuonekana kana kwamba hawakuuwa

    ReplyDelete
  6. Tanzania.kama wale wanaotakiwa watutetee ndo wanatumaliza sasa¬ tufanyeje? nina imani rushwa haitatumika and god will forbid those who are conserned with the killing of those innocent people. damu zao zitawalilia daima. imagine watoto na familia za hao marehemu wanavyolia na kuteseka kwa sababu ya zombe na wenzake.tamaa huzaa mauti.kwa macho ya kibinadamu tunaona zombe na wenzake wangali hai lakini wame..... God will forbid them.ooohhh asante kwa picha na maelezo ndugu michuzi,nakufagilia sana kaka

    ReplyDelete
  7. Nadhani hili jambo la kufanyia kesi ktk Crime scene ni kupoteza Muda na inaonyesha ni jinsi gani Mahakama zilivyo nyuma na karne hii ya Sayansi na Tekelinalokujia.Hivi polisi,waendesha mashtaka(prosecutors),mashuhuda walishindwa kwenda kwenye sinza na kuchukuwa Picha(photo,video) zinazoonyesha hayo yote na kuzifikisha mahakamani kisha kuelezea jinsi mauaji yalivyofanyika?
    Ama kweli wenzetu wanakimbia sisi bado tunatambaa

    ReplyDelete
  8. tunataka si tu haki itendeke bali pia inonekane kutendeka.

    ReplyDelete
  9. WOTE WALIOSHIRIKI KWENYE MAUAJI WALIFANYA KITU MBAYA SANA. LAKINI SASA WAKIFUNGWA WATAFAIDIKA VIPI WAFIWA??? WANGEPEWA ADHABU YA KUTUNZA HIZO FAMILIA KUANZIA MALAZI HADI CHAKULA MPAKA MWISHO WA MAISHA YAO

    ReplyDelete
  10. Kesi Za EPE,RICHMOND,CHIFUPA,BALAL Zingekua Hivi Ingekua Bomba Sana Lakin Du Mazishi Tupu..Job true true

    ReplyDelete
  11. hii danganya toto,,,kesi itaishia tuu wala tusijue ivokufa,,
    nani afahamu ya KASUSURA??YAKO WAPI
    ata hii ya EPA na RICHMOND HAKUNA WA KUMSHTAKI MWEZIE WOOOOOTE WAKO KTK LINE MOJA
    jamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...