wadau kunradhi, kuuliza si ujinga....

hivi ni sababu gani iliyopelekea muislamu anayekula mchana wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani akaitwa kobe?
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Ze Kobeeeeeeeeeeeeeeeeeeezi!

    ReplyDelete
  2. hata si ujinga,mimi mwenyewe ningependa kujua.Wadau changamkeni tena.

    ReplyDelete
  3. Michuzi, we si mwuisilamu?
    Hukufundishwa madrasa hayo mambo?
    Nilitarajia mtu ambaye si wa hiyo dini kuuliza hilo swali. Anyways, ndiyo libeneke lenyewe.

    ReplyDelete
  4. NGOJA NIJARIBU WAJAMENI..KOBE HUWA ANAKULA KWA KUJIFICHA FICHA TUU,NA MUISLAMU ANAYEKULA MCHANA ANAITWA KOBE MAANA HUWA AKILA ANAKULA KWA WASIWASI KWA KUJIFICHA FICHA...SIJUI KAMA NI SAWA MICHUZI!!!NADHANI NA MICHUZI KOBE

    ReplyDelete
  5. ni kweli kobe juwa anakula kwa kujificha ficha. na labda ndio maana muislamu asifefunga wakti wa mfungo uitwa KOBE! ndio maana waswahili wanasema, ukitaka kumchinja kobe, kuahitaji TIMING!

    ReplyDelete
  6. Jibu ni kwamba Kobe huwa anakula mchana na usiku analala, ndio maana mtu akila mchana ktk mwezi mtukufu wa ramadhan anaitwa KOBE

    ReplyDelete
  7. Ndudu Michuzi,

    Mimi ni kobe, tena kobe mkubwa. Nakula kama kawaida, sioni bado sababu ya kukaa na njaa. Mimi ni muislamu.

    Pia nategemea kwenda katika pati hivi jioni.

    Karibi wote msasani.

    ReplyDelete
  8. Hongera Anon September 15, 2008 11:00 AM, usiyeua hata kuandia Ndugu Unaanduka Ndudu?
    eti mimi Ni muislamu sioni bado sababu ya kukaa na njaa..hehehe Ama kweli Elimu kitu muhimu, unakataa nguzo za uislamu halaf unajiita Muislamu? kwa Kigezo kipi??
    Allah Akuongoze. na Atuongoze sote inshaallah.

    ReplyDelete
  9. Mwislamu anayekula mchana wakati wenzake wamefunga hufanya hivyo kwa kujificha ficha huku akiwa na woga wa ku take cover iwapo akibambwa na wale wanaomjua vilevile ambavyo Kobe ataingiza kichwa chake ndani ghafla ili kujificha au asijulikane pale atakapo stushwa au kuwa hatarini!Tendo la kula kwa woga woga huku akijifacha kunafanana na tabia ya Kobe kuficha kichwa chake akistushwa au kuwa hatarini.Hapa nimetumia common sense tu kufafanua.Nisijifanye najua sana.Lakini Ukikosa Mguu Hata MKONGOJO UTAUONA MGUU!(wa maana).Zee La Nyeti.

    ReplyDelete
  10. wewe unaekula mchana na unaenda kwenye pati ramadhani na huku unajiita Muislamu kama huna sababu maalum ya kufanya hivyo then sisi hatuna haj ya kujua kwani humfungii mtu unamfungia mungu wako hivyo wewe ona sifa bali utajibu na Mungu wako !!! sema naomba tuu kukuuliza swali moja vile umejinadi kwa nguvu zote kuwa wewe ni Muislamu, je unazijua nguzo za uislamu ?? Na kam unazijua nguzo za uislamu na hauzitekelezi hata kuonyesha nia ya kutaka kuzitekeleza then uko katika hasara kubwa na kwa taarifa yako Uislamu si jina ni wa vitendo so wewe jinadi tuu mimi ni muislamu misifa itakupeleka payaba na sisi ni binadamu tuu hatuna la kukufanya lolote hatuna uwezo huo lakini sote tutajibu n aMungu wetu so its a free world fanya utakalo but ujue mwenyewe Subhannahu Wa T Taala ndie ataekae kujudge sio sisi na nasema haya kama wewe ni Muislamu kweli unaejua maana na unafanya mzaha pole maskini...... Inshallah Mwenyezi Mungu akughufirie na akuongoe !!

    ReplyDelete
  11. wewe sio muislamu wewe ni kobe!!wenzako wote wamefunga wewe unajidai unakula!!hata ukienda kwenye party unamtishia nani sasa?kuwa mstaharabu na wewe..acha ulimbukeni

    ReplyDelete
  12. Annoy wa September 15,2008 11:00 AM,huwezi kuwa muislamu bila ya kufahamu maana na nguzo za kiislamu, ikiwemo hiyo funga ya Ramadhan...kumbuka kwamba uislamu sio jina hata kama unaitwa Abdalla,Suleiman, Hassan n.k bali ni kufuata masharti ya huo uislamu.Nimemaliza la kama una ajenda nyengine ya kutaka kuudhihaki Uislamu, pole kaka!

    ReplyDelete
  13. Jamani kobe japo azomewa lakini ni bora saana kuliko anayekula wazi. Kobe anajuwa anachofanya. Asiye kobe huonyesha jeuri na kiburi yake kwa Mola na kwa watu.

    Huyu aliye chini ya kobe, japo anaweza kujisifu ni liberal, ajuwe nguzo tano ni package, unabeba yote au iache yote.

    ReplyDelete
  14. nadhani ni busara wa2 kuacha kukosoana mwenzio anapokosea kuandika.Anony wa Sept 15th,11:00 AM nawe pia umechafua hali ya hewa hapo baada ya kumkosoa mwenzio.au nyani haoni .........

    ReplyDelete
  15. Huyu jamaa amabye hata ukobe umemshinda inawezekana anajuwa analolifanya. Yuko makini.

    Mtume kasema akaa njaa bure asiyeacha utesi/utetaji, usengenyaji, uongo, umbeya, mdomo, zinaa za macho na mengineyo.

    Kwa hiyo inawezekana huyu jamaa hizi ndo tabia asizoweza kuacha ndo maana ameamua asifunge asije kaa njaa bure!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. huyo kobe hapo katabasamu au kauchuna??

    ReplyDelete
  17. hahahahah nimecheka san eti kobe anakula mchan ana usiku analala. sasa viumbe wote si ndio hivyo jamani kasoro wachache kama bundi na popo tunakula mchana na usiku tunalala.
    Au kuna wanaokula usiku na mchana wanalala? ....this is so funny

    ReplyDelete
  18. Jamani wanakijiji wacheni kumsema sana huyo islam kobe. Wengine chakula kizuri na party wameanza kuzijulia ukubwani sasahiyo yeye kwake ni bigi DILI maana yake anaweza kutoa chochote ilimradi umpe msosi au mwasemaje?

    ReplyDelete
  19. wewe ndudu michuzi hasara yako nikisema ndudu michuzi nakusudia anon september 11:00,watu wanatenda makosa lakini wanajificha lakini wewe umejidhihirisha kuwa wewe ni muisilamu halafu hufungi na unakwenda kwenye party sasa umesema hivyo ili iwe nini???mada inayoongewa hapa kuwa michuzi kauliza swali kuhusu kobe na wewe unaleta issue nyingine kabisa,imencipate yourself from mental slave non but yourself can do that.

    ReplyDelete
  20. Huyo asiyeona aibu kukosea kwa makusudi inawezekana anapenda kale ka-wimbo ka-watoto kasemako:

    Kiongozi: Kobe
    waitikiaji: Kobe la mchana
    kiongozi: kitoweo
    waitikiaji: panya wa juzi

    wimbo mzuri kabisa huuu!tehe...

    ReplyDelete
  21. MNYAMA KESHA SEMA YEYE KOBE SASA UNATEGEMEA NINI SI SHETANI UMBILE LA BINAADAAM.

    ReplyDelete
  22. Mi-mposi ehhh (mi-mposi ni michuzi kwa lugha ya kina mwakyembe) huyo mshikaji mshamba sana

    ReplyDelete
  23. Kumbukeni lugha laini hata kama huyu kazidiwa na kobe lakini bado ni binadamu mwenzetu. Na kama hajafahamu maana na faida za kufunga basi InshaaLlaah atafahamu baadaye na atafunga.

    Bora uhai na afya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...