futari kwa jamii ikiandaliwa
inasubiriwa adhana kabla ya kuanza kufuturu

Habari za mfungo Kaka !

Hapo ni nje ya msikiti wa Manyema mtaa wa Mafia na Manyema (Samahani, sio Mahiwa kama ulimi ulivyoteleza awali) hapa Kariakoo Kila Mwaka Vijana Takribani Wote Wanaoishi Mitaa Hiyo HujikusanyaWakisubiri Muda Wa Adhaa Ili Wapate kufungua Kinywa Na Waislamu WenzioWanaokuja Kuswali Msikitini Hapo.


imekuwa ni Utamaduni Wa Kila Mwaka Unapofika Mwezi Wa Ramadhani Vitafunio Tafouti Matunda Mchanganyiko Hukusanywa Na Kuwekwa Pamoja ili Wapate Kuwafungulisha Kinywa Wote Kila Anaekuja Na Matunda au Kitafunio huwekwa Hapo Na Kuchanganya Na Wenziwe Kumbuka Na Kahawa Na Juice Ya Matunda Mbali Mbali Pia Huwekwa
Karibuni tufuturu wafungaji
by mdau shebbe Jeizan

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi Mimi Naitwa Mbegu naomba kuchukua fursa hii kumrekebisha mdau aliyetoa taarifa za Futari naona Swaumu ilimkaba sana leo kwa kupotosha kauli ya kusema hapo ni msikiti wa manyema mtaa Mahiwa, Mimi nimezaliwa hapo ni mjukuu wa marehemu bi bahati hapo mtaa wa mahiwa, Msikiti wa Manyema haupo mtaa wa Mahiwa upo Mtaa wa Mafia Na Ukame, Msikiti ulipo mtaa wa Mahiwa ni Mskiti wa Mtoro. Anyway nami natoa Shukrani wa ushirikiano huo wa Kufuturu pamoja na pia nawatakia Ramadani njema sisi tuou Ughaibuni tuna miss sana mitaa hiyo ya Mahiwa na Mafia hususani katika mwezi huu wa Ramadhani, Wasalaam Aleykum Barakatul Ramadhani

    ReplyDelete
  2. Nami naomba kumrekebisha ndugu yetu aloleta hii habari. Hakusubiriwi Adhaa ila kunasubiriwa adhana, pia ni kufuturu sio neno sahihi na lina maana mbaya kwa sehemu nyengine hasa za pwani, ni furari (kufutarisha, kufutari, futari)

    ReplyDelete
  3. ukifunga wafungulia kwa vitu baridi??si ndo mwanzo kuumwa tumbo??
    waanza na kitu joto kdg then,,,,

    ReplyDelete
  4. naona wabongo huwa tunapata "balance diet" ya uhakika mwezi wa Ramadhani tu.Wengi wetu mlo wenye matunda,Juice,maharage,wali,samaki,snacks tofauti hatuvipati.Alhamdulilah.

    ReplyDelete
  5. Nomba kuuliza. hapo hao wakila hivyo ndio basi tena mapaka kesho yake au kunakuwa na mahali wanakula tena Usiku.

    Ni din ilakini I feel for those people. Naona hapo ni sweets tu. Kama immune system sio strong honesty kwa afya ya mtu sio nzuri .

    ReplyDelete
  6. wewe anonymous wa september 13 8:06 name nikuulize, hivi una umri gani na unaishi ulimwengu gani? masuali ya kitoto na kujifanya ni mtaalamu wa mambo ya diet, utumbo mtupu!

    ReplyDelete
  7. Naimiss sana hiyo mitaa yetu, haswa kijiwe cha wajanja pale mtaa wa Ukame; GOGO VIVU, I hope washkaji wote hamjambo hapo; Gashu, Viriyala, Kitumbo, Iddi Kibonge na wengine nakuona Anelka(Kasimu) unafanya kazi ya uandazi hapo! vipi Denmark kulikushinda baba!

    Mdau
    Kwa George Kichaka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...