kivuko kipya cha feri kikiwa katika hatua za mwisho kukamilika

UJENZI wa kivuko kipya cha Kigamboni utakamilika katikati ya mwezi ujao na kuanza kutoa huduma za usafishaji wa abiria na mizigo kati ya Feri Magogoni na Kigamboni, Dar es Salaam.
Hatua hiyo inatokana na kukamilika kwa ujenzi kivuko hicho kwa kiwango cha asilimia 95.
Kauli hiyo ilitolewa leo hapa Dar na Meneja Mwendeshaji, Fuad Saadun, kutoka Kampuni ya Ujerumani ya Neue Ruhrorter Schiffswerft GMBH wakati akiwaeleza maofisa habari na mawasiliano kutoka wizara mbalimbali waliokwenda kuangalia hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa kivuko hicho.
Alisema kazi ya ujenzi wa kivuko hicho imekamilika kilichobaki ni kuweka nyaya za umeme, kupaka rangi pamoja na kuweka viti kwa ajili ya abiria.
Saadun alisema kivuko hicho kinachotengenezwa na kampuni hiyo ya Kijerumani, kina uwezo wa kubeba tani 500 ambapo kitakuwa kikichukua abiria 2,000 na magari 60 kwa wakati mmoja.
Alisema kivuko hicho kimeundwa katika hali inayoruhusu abiria kutumia njia zao katika kuingia ndani na kutoka tofauti na zile za vyombo vya usafiri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

    ReplyDelete
  2. ANGALAU KITAFANANA NA KILE CHA LIKONI - MOMBASA, KENYA. WAO WANA KAMA SITA VYA AINA HIYO VINAVYOHUDUMIA WATU WA LIKONI NA MOMBASA KUVUKA ULE MKONDO WA BAHARI UNAOTENGANISHA LIKONI NA MOMBASA MJINI.

    ReplyDelete
  3. lile daraja la kufunguka limefikia wapi

    ReplyDelete
  4. Kwani hilo daraja ni la kwenye sinema ndani ya masaa 2 limeshafanyiwa kila kitu mpaka kujengwa? Litachukua muda ujenzi wake tena si mwaka, miaka mpaka likamilike, sasa tusubiri daraja bila ya kuwa na kivuko cha maana wakati vilivyopo hali yake si nzuri? Wajameni mbonaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete
  5. ANGALIA HUYO BWEGE HAPO JUU!KWANI CHAMA CHA MAPINDUZI NDIO KIMEWEKA KIVUKO?ACHA USHAMBA WEWE.TATIZO LA KIVUKO KWISHA NI KUWEKA DARAJA TUU..HAPA SEREKALI ITAKUWA IMEFANYA JAMBO LA MAANA SANA...MICHUZI SOGEA MBELE KATULETEE SULULU MCHEZAJI WA KIKAPU WA JESHI STAR..TUMWONE

    ReplyDelete
  6. KWA KWELI MIMI MPAKA LEO SIELEWI JAMANI KWA NINI DARAJA HALIJENGWI HAPO KIGAMBONI ETI MIMI KWA USHAURI WANGU NAONA HELA ZA EPA ZINGEJENGA DARAJA PALE KWA KWELI INGEHARAKISHA SANA UCHUMI WA ENEO LILE HASWA KWA UPANDE WA UTALII.

    BALTAZAR
    WWW.KIPEPEOTOURS.COM

    ReplyDelete
  7. Badala ya kununua Ferry mpya tuna-ripea ferry ya zamani.Huu ndiyo mwendo wa kibongo-bongo weka kiraka, mafundi viatu wa kumwaga hakuna haja ya kununua viatu vipya.hahahahaha

    ReplyDelete
  8. Inaleta ahueni kiasi fulani,kwani mapotoni yaliyopo ni Mazee kupindukia.Haya Karibu Pantoon jipya Na wakati huohuo wakazi wa Mji wa kigamboni na vitongoji vyake msisahau,kuwa bomoa bomoa lina karibia nalo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...