Jina: Capitalist Nigger
mwandishi: Chika Onyeani
Mchapaji: Timbuctu Publishers
Mdurusu:Beda Msimbe

KATIKA moja ya vitabu ambavyo marafiki zangu walinipatia kusoma na kutafakari kimsimamo ni kitabu cha Chika Onyeani ambacho ni best seller nchini Marekani cha Capitalist Nigger.
Kitabu hiki cha Kiingereza tangu mwanzo kinashambulia tabia ya kutokujiamini na kuendekeza ukoloni mamboleo hadi katika vichwa.
Kimeandikwa maalumu kwa namna nyingine kuchokoza kwa upana wake mada za kusema kwamba waafrika hawakuendelea na hawawezi kuendelea kwa sababu jamaa wametuweka katika utumwa na kupora mali zetu.
Akichambua kasoro za nadharia za utajiri katika mawazo mufilisi ya waafrika, Chika Onyeani anazungumzia barabara ya mafanikio kwa namna ambavyo inastahili hasa anapowataka Waafrika kuachana na dhana ya kudeka, kubembeleza na kuomba.
Anasema watu wote walioendelea hawakubembeleza wala kuomba wala kudeka walichofanya ni kuhakikisha kwamba wanatumia kila nafasi iliyopo kukamua na kuendeleza libeneke kiasi cha kuogofisha.Lakini pamoja na kuwataka Waafrika kuamka na kujikita mbele, hakutaka Waafrika hao kujitengenezea ufisadi lakini kwa namna ya pekee amezungumzia Waafrika na kusema kushindwa si dhana njema kwa mtu anayetafuta.
Ndani ya kitabu hiki kilichochapishwa na Timbuktu Publishers, An African telecom, Inc. mjini New York, Onyeani ameonya kuwa hii tabia ya kujiendekeza imetufanya kuwa ombaomba wa kutupwa duniani na kitendo cha kuringia historia ya miaka 2000 iliyopita eti tuliendelea haina maana.
Akitumia vyema fani yake ya uandishi Onyeani amesema wazi kwamba kinachotuua waafrika ni kubaki kuwa watumiaji badala ya kuwa wazalishaji huku tukilaumu mfumo wa dunia wa kibiashara na mitaji.
Amesema tabia hii ya utegemezi kiutamaduni katika chakula, mavazi na lugha kunafanya kila kitu kionekane kama chakuja. Akisema wazi kwamba Waafrika wamekuwa watumwa kiuchumi kwa sababu hawataki kujaribu kuthubutu kama wanavyofanya Waasia na pia hiki ni changu tabia ya wazungu.
Anasema kwa maneno makali kabisa bila kubadili utamaduni huu wa kutothubutu Waafrika watabaki hapo walipo wakiwa watumwa wa wengine.
Kitabu hiki kinafaa sana kutumiwa kuamsha moyo wa kuthubutu na ni vyema wengi wetu tukakipata kitabu hiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. KIKWETE ANAPASHWA KUSOMA HIKI NA KUACHANA NA KUOMBA OMBA NA KUTETEA MARAIS WANAOUA WATU, ETI WASISHITAKIWE NA KUWADHALILISHA, KUSHITAKI MHALIFU NI KUDHALILISHA! NA HAO WATU WANAO-RAPEWA NA KUUWAWA SI KUDHALILISHWA? ACHA AFRICAN BROTHERHOOD, NDO ULICHOMA MAFUTA YETU WEEK MBILI ZILIPITA KWENDA SUDAN KUCHUKUWA USHAURI HUO TOKA KWA RAIS WA SUDAN, MWAMBIE AACHE KUUWA WATU, HATOSHITAKIWA. najuwa michuzi hutopost hii kwa vile kikwete na wewedamu damu

    ReplyDelete
  2. Yes ni kitabu kizuri sana. Nimekisoma na kinatia hamasa kwa kweli.

    ReplyDelete
  3. Asante sana mdau,ni bahati mbaya sana kwamba watanzania tu-wavivu wa kusoma vitabu.Asante sana kwa 'summary' kwa ambao hawajakiona wala kukisoma kitabu hiki nikiwemo na mimi.
    Ni kweli kabisa sisi waafrika ni wavivu wa kufanya kazi lakini hakutakiwa kutuponda sana(Ukweli unauma eh?)

    ReplyDelete
  4. Eeh hii imeingia kwa oblangata. kila sentensi ni fact tupu!!!. Kwa kutumia dhamana ya ubalozi ulionao bwana Michuzi, nakutuma kaongee na Waziri Magembe ili afanye mpango wa kukiingiza kweny mtaala wa kufundishia vijana wetu kule secondari.Japokuwa za kata sio mbaya hata ikiwachukua miaka mitano kuelewa itatusaidia huko mbeleni. Aluta kontinua!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Binafsi nivutiwa sana na maelezo kuhusu hicho kitabu.Tuko kipindi ambacho uwezowakutumia taarifa ndio utakaoamua nani atabaki nyuma na nani ataendelea. Ni vizuri kusoma hiki na vingine vingi na kuyatekeleza kwa vitendo yale tunayoyasoma.Bila shaka kila kiongozi wa serikali:Rais, Mawaziri na Wabunge na Wanasiasa wengine ni vizuri wakikisoma kitabu hiki kwani wao ndio wanafanya maamuzi katika mambo ambayo kwaupande mkubwa umechangia kuturudisha nyuma kimaendeleo. Hebi fikiri toka mwaka 1961 tunapambana na umaskini,ujinga na maradhi lakini kila siku zinavyoenda nduyo umaskini,ujinga na maradhi vinaongezeka wakati viongozi wananeemeka.

    ReplyDelete
  6. Hichi kitabu nimekisoma miaka miwili iliyopita na mpaka leo nakumbuka maneno yake. Naomba kama inawezekana Taasisi zetu za lugha zitafsiri hiki kitabu ili tuwe na makala ya Kiswahili ili kiweze kufikia watanzania wengi zaidi. Kwa jinsi nilivyomsoma huyu mwandishi sidhani kama atakataa kitabu kutafsiriwa kwenda kwenye lugha ya kiafrika kama kiswahili. Haitokuwa mara ya kwanza kitabu chenye umuhimu kutafsiriwa kwani hata hayati Baba wa Taifa alitafsiri vitabu viwili vya Shakespeare Julius Kaizari na Mabepari wa Venice. Baada ya kutafsiriwa mashirika kama haki elimu yanaweza kusaidia kusambaza kwenye mashule ya msingi na sekondari nchi nzima. Ahsanteni

    ReplyDelete
  7. September 26, 2008 5:18 PM


    Anon wa tarehe na muda wa hapo juu una akili nyingi sana! Tuna Watanzania wengi sana wenye akili kama zako ila tatizo mfumo wetu wa uendeshaji wa serikali umejaa ubabaishaji na ujinga (na ushirikina kwa mbali). Ndio maana wasomi wengi hawapendi sana kujihusisha na siasa. Wameaachia kina Makamba wenye elimu za kuunga unga. Halafu tunagegemea maendeleo.

    nayway, inatia uchungu, lakini ni nchi yetu, ni bara letu na mkataa kwao ni mtumwa!Tukaze buti tu ipo siku tutafika. Lakini kwa kifupi mambo yanayoendelea ndani ya bara la Africa na ndani ya nchi yetu ya Tanzania ni mambo ya kukatisha tamaa sana, na wala hakuna matumaini ya maendeleo ya kweli katika kizazi hiki. Labda kizazi kijacho!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...