Habari kaka Michuzi,

Pole sana na kazi za kila siku maana nimesoma kwenye blog ya jamii na nimeona umeongezewa tena majukumu ya kuwa balozi wa Zain,hongera sana.

Msaada ninaoomba ni kunitafutia dada mmoja ambaye nafananishwa naye sana,dada huyo anaitwa Jane Kamasho na baba yake zamani alikuwa meneja wa kampuni ya Matshushita iliyokuwa barabara ya pugu, walikuwa na nyumba Chang'ombe na nafikiri mpaka leo wanaishi hapohapo.

Nimekuwa nikifananishwa sana na dada huyo sana kiasi ambacho inabidi kutoa kitambulisho cha kazi na kusema mimi sio Jane,lakini bado huwa naambiwa nimebadilisha jina.
Kwa hiyo kaka yangu nakuomba unisidie,
nakutakia mfungo mwema.
Wasalime wote huko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. duuh! umenikumbusha mbali sana, zaidi ya miaka 20.nilisoma nao Chang'ombe primary.vilevile sunday school.hata mimi tafurahi nikipata link yao

    ReplyDelete
  2. Binti nataka nikupe ushauri wa bure....uwe na akili...haya si mambo ya kuanika hadharani kabla hujafanya uchunguzi wa kiutu uzima....hapo wa kuhojiwa ni baba yako mzazi au mama yako mzazi kama kuna forgery yoyote waliwahi kucomit nje ya ndoa zao....shauri yako

    ReplyDelete
  3. Mimi nakufananisha nadhani kama sikosei nilishawahi kukuona Minesota-USA

    ReplyDelete
  4. wewe anon wa pili wacha kuropokwa tu, kwanza fikiri kabla hujakaata keyboard na kuandika utumbo. Je nawe umefikiri labda huyu dada nae kaingiwa na wasiwasi fulani na anataka kujuwa ukweli ulivyo na ndio akaona aanzie kwa kumuona na aone kama ni kweli amefanana nae na ndio aanze kuuliza masuali?

    ReplyDelete
  5. Huyo jane inawezekanahayupo dunia hii tena ni siku nyingi! na kaka yake mmoja aliuwawa south Africa mwakajana kama sijasahau ok! habari ndiyo hiyo!!!!

    ReplyDelete
  6. Kusema ukweli umefanana nae sio hivyo kwa kuwa sijamuona jane kamasho kwa muda mrefu tumekulia mtaa mmoja temple road changombe uwindini na nitafurahi nikipata mawasiliano nao na kuna mtu namtafuta anaitwa nuru sovellah kama kuna mtu ana mawasiliano nae ani email mncs_2008@hotmail.com

    ReplyDelete
  7. Dada- Komashos hao unaowasema walishahama pale Chang'ombe uhindini(Temple Road)...Anold kaka yake aliuwawa SA na nafikiri huyo Jane Komasho au one of the sisters alifariki...Tito mdogo wao wa mwisho bado yupo SA. Mama yao alirudi uchagani.
    Mdau ambaye bado naishi Chang'ombe.

    ReplyDelete
  8. Wachaga Bwana!
    Dada yangu, na akili yako nzima, umekuja huku KUMTAFUTA SUPER STAR JOHN MASHAKA? Yule ni ugonjwa wa moyo wa wakina MANKA MUSHI NA Jovinata Kileo. Hau mnamkimbilia kwa sabau ya vijisenti vyake?

    Wall-Street imeporomoka sasa mtaambulia nini, sijui kama ana kazi tena. Sasa hivi anauza vitumbua hapa NY

    Haya kama unataka kuawsilaina naye kwa njia za janja ya panya basi hapa nambari yake 1-914-177-5432 au jmasha1980@yahoo.com

    ReplyDelete
  9. KAKA MICHU MIE NAOMBA UNITAFUTIE DADA MMOJA ANAITWA HALLE BERRY, WATU WANASEMA TUNAFANANA SANA. NITASHUKURU KWA MSAADA WAKO

    ReplyDelete
  10. cathy na uhahkika ukimpata huyu dada jane utafurahi sana hawa walikuwa majirani wazuri watu wazuri sana na uhakika akipata hii habari lazima ata contact na wewe mie namtafuta mtu mwingine changombe anaitwa nuru sovellah alisoma kibasila alikuwa anakaa railway kama kuna mtu ana mawasiliano nae email mncs@hotmail.com

    ReplyDelete
  11. Anonym. wa 6:43 wanakusanifu tu, wala hufanani naye hata kidogo. Mi naona unafanana sana na Dr Remmy Ongala, sijui ni mwanae!

    Ok, kwa anayemtafuta DaNuru kwa taarifa yako kaolewa na ndugu yangu, mtoto wa binamu wa shangazi yake na mama yetu wa kambo. Halafu mumewe ana wivu hata hataki kabisa tuwasiliane na DaNuru Sovellah. Sasa rafiki yangu kama mimi nduguye hataki nionane na shemeji yangu hata nikakupa anwani yake sijui utawasilianaje naye, sana sana ni kutaka kumvurugia ndoa yake tu. Acha kabisa tafahali ndugu yangu.

    ReplyDelete
  12. Nuru Sovera kama bado hajabadili kazi atakuwa DAWASCO so kaanzie pale kumtafuta.Ni kweli kaolewa siku nyingi kdg

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...