Habari kaka michuzi,
Mi ni dada wa Kitanzania na ninaishi Tanzania. Ni mfuatiliaji mzuri wa blog yako. Ninapenda kukushukuru na kukuomba msaada uniwekee ombi langu kwenye blog yako.
Ombi langu hasa ni kutafuta mwenzi. Najua consequences za kukuomba uposti ombi langu kwenye blog kuwa naweza kupata negative responses but I am ready for that maana nisipojaribu nitabaki na what ifs kibao.
Nilijigundua kama ni HIV+ve kama miaka mitano hivi iliyopita. Nilikuwa na ndoa lakini ilivunjika, si kwa sababu ya status yetu (maana na mwenzangu nae pia ni muathirika) ila ni jinsi ya kuishi baada ya kujua tuna matatizo. Mwenzangu hakutaka kufuata masharti kama kutumia protection etc na alikuwa na mahusiano ya nje.
Hii ilisababisha ugomvi wa mara kwa mara na nikaona bora kuachia ngazi maana hata madaktari wanashauri kuepuka stress ukiwa na hali hii. My ex ana mahusiano mengine kwa sasa na amezaa na huyo mwenzie (kwa kweli namuona ni muuaji maana hajamuambia mwenzie kama ana matatizo - na mie siwezi kum-expose kwa kuhofia stigma maana akijulikana yeye mgonjwa na mie nitajulikana mgonjwa vile vile - na Tanzania unyanyapaa bado ni issue).
Kinachonisumbua kwa sasa ni upweke. Nahitaji mwenzi lakini ambaye atakubali status yangu. Na ninaona ni vizuri zaidi na yeye akiwa HIV+ve. Nimekuwa nikifuatwa na wanaume wengi tu, lakini nakataa kwa kuogopa kuwaambia ukweli.
Nilishajaribu kumweleza mmoja maana ali insist kuwa ananipenda sana, lakini baada ya kumwambia ukweli aliingia mitini.
Hamna kitu kibaya kama rejection, inauma sana hasa kama mtu alishaanza kukuingia moyoni. Hivyo nimekuwa muoga kabisa wa kujenga mahusiano (ambayo yataendea kuwa mapenzi) kwa hofu ya kukataliwa baada ya kumweleza mtu matatizo yangu. Na siwezi kukaa kimya na kumuambukiza mtu makusudi maana hata condoms zina some % ya uwezekano wa kumuambukiza mtu.
Naishi peke yangu, sina mtoto na si tajiri lakini nina uwezo wa kujihudumia mwenyewe hivyo naomba wadau wasidhani kuwa natafuta financial support. Shida yangu hasa ni mtu wa kushare, wa kunipenda, wa kusaidiana na wa kufurahi pamoja.
Nina marafiki wa kike wengi and they give me a lot of support, lakini haitoshi. Nadhani wadau watanielewa. Naomba kwa mtu aliye serious awasiliane nami kwa e-mail


Dada nimeguswa na email yako kwa ujasiri ulioonyesha na upendo ulionao. Mungu akuongeze katika kila ufanyalo na akubariki uishi miaka mingi yenye afya na mwenzi wako mtarajiwa. Believe and it will happen. Mdau MD
ReplyDeletemh kwa ukweli ni ngumu lakini mie nachokuombea ni allah akupe subira na mume anayekupenda kwa dhati badala ya kuwa na kinyang'anya. Na ninapozungumzia mume ni kwamba upate mume atakayekupa wewe na kukutizama maana mambo ya urafiki au uboyfriend yana tabu yake ukiwa na homa kidogo mtu anaanza kufikiria vengine. Mie binafsi ningekuwa sijaoa ningelikuoa kwasababu ndo fadhila zenyewe pole dada nakuombea mmungu akujaalie subira
ReplyDeleteDada yangu nimekuelewa sana.
ReplyDeleteAngalia post zako
Mdau Holand
Dada pengine mie ningetuma maombi ya kujaza nafasi uliyoitangaza lakini siwezi si kwa sababu kwamba wewe ni HIV+ bali ni kwa sababu WEWE MWENYEWE na au wakala wako aliyekutangazia hii nafasi kuwa mfano mzuri wa kuunyanyepaa Ukimwi na Wagonjwa wenye Ukimwi!
ReplyDeleteInawezekanaje utangaze nafasi kwa kichwa cha habari kinachomtambulisha Mwanadamu mfano wa Mungu kwa ugonjwa alionao eti "Mdau HIV+ Adafuta Mwenzi" na zaidi ya hapo wewe mwenyewe unaanza kufafanua wasifu (CV) wako kwa kueleza ni lini uligundua kuwa unaumwa! Mbona hukueleza ni lini uligundua una malaria au minyoo au matatizo mengine ya kiafya ambayo naamini yaliwahi kukupata?
Mbona uchukuwe yapata 90% ya tangazo la nafasi ya uchumba kwa maelezo ya ugonjwa kama vile ulikuwa unaandika insha juu ya madhara na adha wapatayo walio HIV+ badala ya kueleza sifa zako (mapendeleo, elimu, umri, mitizamo yako, imani, matarajio n.k) ulizonazo kama mtafuta mchumba na pia sifa uzitakazo toka kwa muomba nafasi hiyo.
Hofu batiri (phobia) ya kuogopa kukataliwa ndio kichocheo cha stigma yenyewe unayoiongelea!
Mimi ni HIV- (wa leo maaa sijui kesho)lakini nawapenda wote HIV+s na HIV-s kama viumbe wa Mola wanaostahili kuheshimika kwa utu wao sawa na positives wa Malaria, Schistomiasis,UTI,Ascariasis,Dracuncuriasis n.k
Dada nakupa pia kionjo cha nguvu kuwa taasisi NDOA ni zaidi ya tendo NGONO.
pole dada, story yako nami imenigusa sana. kwa hali ilivyo tanzania ya namna mwenye ugonjwa huu anavyotendewa naona uko katika mashak makubwa. Kama ulivyosema mtu akikujuwa tu anatoka bomba, sasa hapo ndio tatizo utajuaje anekuandikia ni kweli nae ni +ve au anatafuta umbea tu ili akupakazie kila kona? kuna website tele za waswahili wanapita wakipakiziana uongo huu, seuze wapate ambae wanajuwa 100% +ve? ushauri wangu ni kuwa muangalifu unapopata emails na usitowe details zako hadi pale unapoamini kweli kweli kuwa akuandikia yuko serious.
ReplyDeleteDada ubarikiwe, mungu akupe maisha marefu.Dada ni shujaa kweli kweli.Mimi naona tayari utakuwa na maisha marefu sana.Na namwomba mwenyezi mungu huo ugonjwa utoweke ghafula kwenye mwili wako na uwe mzima wa afya sasa hivi.Ninaomba hayo kwa jina la yesu kristu.Amina.
ReplyDeleteMdau
USA.
Wadau kulingana na kanuni za HIV nikwamba asilimia kubwa inaambukizwa kwa michubuko. Najiuliza hivi kama unamuoa mwenye ile kubwa na yako ndogo kiasi hakuna michubuko si naweza kusave?
ReplyDeleteNijibuni kwani nataka kujaribu bahati yangu wazee!!
Mimi
Pole saana ila unaonekana una roho nzuri na ujasiri.
ReplyDeleteLakini ukumbuke kukaa kimya usimfichuwe x wako unaendelea kuwa mshiriki wa kosa la mauaji. Mfichue huyo.
Bora unyanyapake (na utanyanyapaka kweli) kuliko kuvumilia watu wakifa. Piga moyo konde.
Halfu waatjirika wenzako wawza kuwapata chamani.
Ningependa kukupa tahadhari. Mtu mwenye virusi vya UKIMWI anaweza kuambukizwa tena (Re-infected) kama atakutana kimwili na mtu mwenye aina nyingine ya virusi vya UKIMWI. Hali hii inapelekea mwathirika kupata UKIMWI mara mbili (dual infection). Dual infection inaweza kumfanya mwathirika kudhoofika kwa kasi zaidi.
ReplyDeleteUSHAURI: Unaweza kutafuta mwenza aliye mwathirika au asiye mwathirika. CHA MSINGI NI KUCHUKUA TAHADHARI KAMA VILE HAUJAATHiRIKA NA UGONJWA HUU.
Mdau
http://drfaustine.blogspot.com/
Pole, ila nahisi umekosea.
ReplyDeleteKama ulijua mumeo ni HIV+ halafu ukaruhusu aoe mtu mwingine, ni kama umeruhusu aoe.
Najua woga wa kuwa kunyanyapaliwa, lakini sasa mtu na mtoto watakufa ilhali ungeweza kuzuia.
Ulikuwa na uamuzi wa kuokoa maisha, na ingekufanya uwe na amani zaidi.
Kama unakataa wanaume kwa nia ya kuzuia kuwaambukiza, kwa nini usingeweka wazi hali yako na ya mumeo ili kuokoa maisha zaidi?
Haiwezi kuwa siri milele....
na kama ungeweka wazi, ungekutana na HIV+ wengine kwa urahisi zaidi.
Huo ndio mtazamo wangu
dada hongera kwa kuwa muwazi na jasili,inaonyesha jinsi gani ulivokuwa na busara na ustaarabu
ReplyDeleteahsante kwa hilo.kweli umenigusa sana.
USHAURI MARIDADI WA BURE.....!
ReplyDeleteMimi nakushauri usali sana maana hata huyo mtu ukimpata ataweza kukuongezea virus ambavyo vimo mwilini.Ukakuta labda wewe sasa hivi ni hiv career na mwezio siyo career hii inaweza kukuletea taabu baadaye. MIMI NAKUSHAURI UACHANE NA TAMAA MAANA HIYO TAMAA IMEKUFIKISHA MAHARA HAPO ULIPO KUMBE NI VIZURI UMRUDIE MUNGU KULIKO TAMAA YA KIMWILI, CHUKUA MUDA WAKO ULIO BAKI DUNIANI KUWAELIMISHA WATU IKIWA NI PAMOJA NA HUYO ALIYEKUWA MUME WAKO KWAMBA UKIMWI UNAUWA NA ALIVYO FANYA KWAKO NA KWA HUYO MWINGINE SI JAMBO JEMA NAJUA UTACHUKIWA LAKINI UTAKUWA UMEFANYA KITU KIZURI KWA JAMII NA VIZAZI VIJAVYO. SIONI FAIDA YA WEWE KUJUA EX WAKO ANAENDELEA KUUA NA KUUMIZA WATU LAKINI WEWE UKIJUA FIKA UNAKAA KIMA HUKU UKITAFUTA KISIRISIRI MTU WA KUENDELEZA TAMAA ZA KIMWILI.KAMA MUNGU YUPO UNAFIKIRI ANAJISIKIAJE KWA HII TAMAA YAKO? HUONI NI AFADHALI WATU WAKUCHUKIYE AMA HATA WAKUTUPIE MAWE LAKINI UMEOKOA MAISHA YA WENGI? KAMA MUME WAKO ANAENDELEZA LIBENEKE LA NGONO HUKU AKIJUA NI HIV+ NA WEWE UNAKAA KIMYA MIMI NAONA WOTE NI WAOVU, SI VEMA KUONA JIRANI YAKO ANAKUFA ETI WEWE UKIOGOPA YAKWAKO YATAUMBUKA NA KAMA UNAPATA SUPPORT YA MARAFIKI SIJUI NI KWANINI WANASHINDWA KUKU SAIDIA KUFIRI MAMBO YA MUHIMU KAMA KUPATA DAWA ZAKUREFUSHA MAISHA, MAZOEZI NA LISHE BORA LAKINI WANA KUSAIDIA KUKUPA USHAURI AMBAO NDIYO HUO UMEKUFIKISHA HAPO ULIPO! NAKUSIHI DADA YANGU ACHANA NA TAMAA YA MWILI NENDA KAMURUIDIYE MORA WAKO KISHA MUOMBE AKUPE NGUVU ILI UWEZE KUWASAIDIA WALIO WENGI AMBAO BADO HAWAJUI MADHARA YA HUU UGONJWA ULIO KUPATA BILA WEWE KUTEGEMEA. MWISHO NAKUTAKIA KILA LA HERI NA MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU ILI UWEZE KUISHA MIAKA MINGI NA UTASHI WA KUKUWEZESHA KUWASAIDIA WATU WENGI AMBAO PIA WANAUPATA UGONJWA HUU KWA NAMNA ULIVYO UPATA, NI HERI UPUNGUZE KASI ZA MAAMBUKIZO KWA JAMII KULIKO KUACHA JAMII ITEKETEE HUKU UKIKAA KIMYA BILA KUSEMA NA MWISHO TAMAA YA MWILI INA MWISHO WAKE. NATUMAINI USHAURI WANGU UTAUPOKEA NA KUUFANYIA KAZI NA TENA MUNGU AKUBARIKI SANA! NDIMI PETER NALITOLELA EX MUZUMBE!
Inshallah katika mwezi mtukufu huu wa ramadhan nakuombea kheri. Mungu akupe nafuu, akuweke na akupe yule atakae kupenda na hali yako atakae kua nawe kwa shida na raha, kwa dhiki na faraja. Inshallah usivunje moyo kwani wambiwa subira uvuta kheri. Lakini kwa ur ex-husband, lazima useme ukweli kwani akiwa anaathiri watu nawe unajua basi nawe pia huenda pata dhambi kuliko yeye sababu wewe unajua ukweli and u can stop him from spreading HIV. Usione aibu, if u save a life of one or two women basi hizo thawabu tosha kwako. Lakini ukikaa kimya na kumuacha mume wako wa zamani awambukize gongwa wenginewe basi dhambi hizo dada angu. Lakini Inshallah mola akujalie kheri.
ReplyDeleteKILA MTU ATAJIJU, UMEAMBIWA SIKU NYINGI NGOMA INAUA LAKINI UMEKALIA KUACHIA TIGO WATU WANAKANDAMIZA TU UNAJUAJE KAMA HUYO MUMEO NDIYO KAKUPA NGOMA? LABDA NI WEWE UMEMPA? KAMA UNADILIKI KUTAFUTA BWANA WAKATI UKIWA KATIKA MATATIZO KAMA HAYA? MIMI NILIDHANI UNGEKUWA KATIKA DIMBWI LA MAWAZO NA MAJUTO LAKINI UNATAFUTA TEJA LINGINE LENYE NGOMA HIVI WEWE UNA AKIRI KWELI, GOIGOI SANA, UTAENDELEA KULIWA TIGO PEKUPEKU IF YOU ARE NOT CAREFUL. KWANINI HUTAKI KUMTAJA ANAENDELEZA KUUA? UTAKUWA NI WEWE TU UMEMPA SASA UNAOGOPA ATAKUCHINJA UKIENDELEA KUMUUDHI
ReplyDeletenalitolela kumbe ukikaa kimya sometimes unaongea point kama mtu aliye maliza mzumbe! hii ndiyo point unapaswa kupost siyo kama zile ulizo weka kwa mugabe, I was shocked because we know you!
ReplyDeletePole sana Dada.Hopefully utampata tu
ReplyDeleteDADA YANGU NAOMBA NIKUPONGEZE SANA KWA UJASIRI WAKO KWA KWELI NDUGU ZANGU WATANZANIA SWALA LA UKIMWI LINAWEZA KUZUNGUMZIWA KWA MAPANA SANA NA LINAWEZA KUMPATA MTU YEYOTE.
ReplyDeleteDADANGU HAPA KAMA MWANADAMU MWINGINE YEYOTE ANAHITAJI MTU WA KUFANYA NAE MAPENZI NA ANAHITAJI MUADHIRIKA MWENZAKE HILO NI JAMBO LA BUSARA SANA AMEAMUA KUWA WAZI NAMPONGEZA SANA TENA DADA YANGU WEWE MUNGU ATAKUZIDISHIA MAISHA SANA KWANI KUNA WATU WENGI SASA HIVI WANAUA MAKUSUDI LAKINI WEWE DADA YANGU NIMEKUPENDA SANA NA MAAMUZI YAKO YA KUWA MUWAZI, MIMI NTAOMBA TU KUWA MSHAURI WAKO WA KIAFYA NA KISAIKOLOGIA KWANI NILIFANYA KAZI NA DOCTOR WITHOUT BORDER NA HIV NA TB IT WAS ONE OF OUR PROJECT, KITU UNAWEZA FANYA JOIN HIV MEMBERS THEN FROM THERE YOU CAN CHOOSE A MAN FOR YOU BUT KITU CHA KUNYA UKIPATA MWANAUME USIFANYE NGONO KILA SIKU FANYA HATA KWA WIKI MARA MOJA NA UKIWA UMEKULA VIZURI.
KWA KWELI NAWASIKITIKIA SANA WATANZANIA WANAOKUTOLEA MANENO MACHAFU KWANZA HAO UNAKUTA HATA HAWAJAPIMA WEWE DADA USIWE NA MASHAKA KABISA HAKUNA MTU ATAISHI MILELE WOTE SIKI YETU IKIFIKA TUTAKUFA ILA WEWE NI JASIRI WA HALI YA JUU UKIITAJI MSAADA WOWOTE WA KIMAWAZO AU DIET AINA YEYOTE NAOMBA USISITE KUWASILIANA NA MIMI.
WATANZANIA TUWAPENDE WAADHIRIKA WA UKIMWI.
BALTAZAR ATHANAS
KIPEPEO TOURS
mimi mdau kwanza napenda kukupa pole dada uliyejitokeza kwenye blog hii na kulielezea liloko moyoni kwako. Kwanza namshangaa huyo aonymous sept 05 4:27am kuhusu huko kulaumu kwa kota tigo. Ugonjwa huu huwezi jua ni nani ambaye anaweza kuuleta hata wewe unayemlaumu au kumnyooshea vidole mwenzako labda pia nawe unao ila binadamu hatuishi kulaumu. Unaweza kupata maambukizi kwa sindano au pia kama utatumia mikasi au vitu vyenye ncha kali kwa ajili ya kuweza kupata damu ambayo mwenzako aliiacha hivyo kama kuna lawama haifai mshikaji kinachotakiwa ni kumrudia Mungu na kusali sana aepukane na tamaa na awe na matumaini ya kutafuta watu ambao wataweza kumshauri vizuri. Pole dada ila vizuri kumshauri ex-boy friend wako kuachana na uambukizaji wa wengine ikiwezekana hata kumtangaza kwenye vyombo vinavyohusika ili kuweza kuokoa wengine.
ReplyDeleteMungu akupe uvumilivu dada na uyashinde majaribu ya shetani!
ReplyDeleteNankupa 5 NALITOLELA umeongea point mno.
Sijafurahishwa na anon wa Sept 5 2008 7:06AM, ulichoongea ni sawa na mtoto wa chekechea pumba tupu na hata humuogopi Mungu wako lol!mrudie Mungu hiyo Tigo alikupa wewe nini??au alikuchukulia???
Mwisho kabisa dada sikiliza ushauri wa NALITOLELA na wengine wenye mapenzi mema..kila la heri!
Hogera sana dada kwa busara zako, ni mdada wa pekee katika kuishi maisha ya kikweli yanayobalance mahitaji ya mwanadamu yaani( physical needs,physioligical needs social needs, psychological needs na moral needs).Kujamiiana ni moja ya social needs/physiological hali mradi sex iwe regulated in order to be accepted and to feet into cultural requirements. Hujakosea kitu dada mdau!!!!!!! wastahili kuwa na mwenzi hali mradi haumuambukizi VVU.
ReplyDeleteNashangaa sana wachangia mada bullet No 4-Nyakurunga, bullet no12-NALITOLELE na bullet No14. Hawa wote ndio wanaonyanyapa wenzao, nawaombea wapate VVU ili waonje joto ya jiwe ya kuishi na virus na wakaachwa wapweke kama wanavyokutakia wewe na wengineo waishio na VVU.
Bullet no 4, unawezaje kumtuhumu huyo dada eti angetangaza na maradhi mengine yaliyokwisha mpata maishani? Hayahusiani na tatizo lake la sasa.
Bullet no 12, Usilete unafiki katika ukweli, Mungu hajaleta VVU kuua watu wake; wataka kusema watoto wanaozaliwa na VVU (up to 40% infection from mother to child if no any intervention)wao hawajamrudia Mungu?, Jifunze kubalance mahitaji yote ya mwanadamu na sio kushikia bango jambo moja kuhukumu wenzako. Dada huyu anakushinda ujasiri sana tu wewe waongea pumba tupu,
Bullet 14. Usimuhukumu huyu dada as if wewe hujawahi kujamiiana. Elewa age na hormons vinaenda sambamba na age is just a number, we do differ a lot, hali mradi mtu akitenda kinyume na age yake hapo tutamshangaa. Badala ya kumpa ushauri unalaanini na kukandia, ni mwanadamu huyu, usimnyanyapae wapo walio tiyari kumuoa waachie wajimwage viwanjani,
Dada Mdau wa HIV, Nakushauri sali sana, nasi tunaungana nawe kukuombea, usijali sana kwa negative respoce; just take them as the positive challeges and I assure you you will make it soon.
WEWE NALITOLELA UNA UHAKIKA GANI KAMA ALIUPATA HUO UGONJWA COZ YA TAMAA?AMESEMA ALIKUWA AMEOLEWA U NEVER KNOW KWAMBA MUMEWE NDIO ALIMLETEA, JAMANI KAOMBA USHAURI HAKUOMBA MTU AMJAJI
ReplyDeleteDada hongera kwa ujasiri wa kulitoa ulilonalo moyoni. Huyu ambaye ni anonymous Sept 5, 4:27am
ReplyDeleteanavyomshutumu mwenzake kwani yeye ni Pilato ambaye anatoa hukumu. Kuna sababu gani ya kusema alikula Tigo na maneno mengi. Kwani hajaelemika bado na anajua kwamba ugonjwa kama huu unatokana na kuambukizwa ama kwa sindano au vitu vyenye ncha kali. Ila hatuna uhakika kwamba either aliupata wapi labda mwenzetu anajua ndio maana anasisiitiza Tigo hiyo siyo sahahihi rekebisha huo usemi. Unapomsnyooshea mwenzako vidole ja wewe una uhakika gani kwamba huna ndugu??????????? heri yeye alijieleza ukweli wake ila kinachotakiwa ni kumueleza huyo mume wake aache kuusambaza kwa kuwapa wengine mimba na yeye mwenyewe kama inawezekana kumrudia Mungu yaani KUOKOKA. Maisha ambayo yatampa raha zaidi ni kuwa na YESU MOYONI na kutafuta washauri wazuri wa kuweza kumsaidia na kumpa ushauri ambao utaweza kuyafanya maisha yake yakawa marefu na mazuri. Nakutakia Mdau maafanikio mema kwani ulijieleza kwamba unakubaliana na yote ambayo wadau watayaweka hadharani.
mimi nashauri kama kweli unataka mwenza,bora ungehudhuria kitengo cha ukimwi kilokuwepo karibu nawe,huko utapata marafiki mbalimbali wa kike na kiume na wataalamu zaidi watakaokupa ushaurı nasaha jinsi ya kuishi.
ReplyDeletekuna hiv+ na AİDS unaweza ukawa + na ıkachukua muda mrefu kupata ukimwi,inategemea na kinga yako ya mwili na tahadhari unazochukua.
Nyakarungu wa coast point yako ya kusema kwamba anajibagua mwenyewe na kuna maradhi mengine si kweli,sote tunajua hiv inaambukizwa kwanjia ya kuchanganyika damu hasa sexual intercourse especially homosexual,ukıangalia maradhi mengine uloyataja yanaambukizwa kwa oralfecal au direct touch na maradhi hayo dawa zake zinapatikana ni rahisis kupona huwezi kulinganisha na hiv+.
na ingekuwa weye pia sidhani ungechukulia kama hivyo ulivyosema.
au mkuki kwa nguruwe...?
Mmmmmmmmmmmmmmm! ngoja kwanza nifikilie ntakujibu dada!!! mdau midland ,ukerewe
ReplyDeleteNAJIBU MAPIGO YA LAWAMA HAPO JUU...
ReplyDeleteMIMI NALITOLELA SIDHANI KAMA USHAURI WANGU NI MBAYA KILA MTU HUMU BLOGINI AMEGUSWA NA HII ISSUE INGAWA WENGINE WANATUMIA MADA HII KUTOA UTANI. NIMESEMA NI TAMAA YA MWILI KWA SABABU KUU MOJA, KITENDO CHA KUJAMIIANA NI TENDO LA TAMAA YA MWILI REGARDLESS UMEOA AMA HUJAOLEWA, KWANI NI VIUNGO FULANI VYA MWILI PAMOJA NA UBONGO VINAKUWA NA HAMU AMA SHAUKU YA KUJAMIIANA SIYO VIDOLE WALA MIGUU NA HIVYO VIUNGO/KIUNGO WOTE TUNAVIJUA/KIJUA KUMBE HATA KAMA ATAKUWA NA MTU WA KUM KEEP BUSY KIMAPENZI HUKU EX HUSBAND WAKE ANAENDELEZA KUTOA DOSE NA YEYE ANAMUHIFADHI ILI JAMII IKIENDELEA KUTEKETEA SIDHANI HILI NI JAMBO ZURI, SASA NDIYO MAAMA NIKASHAURI ATAFUTE NJIA ILIYO YA AMANI
1. AMTAJE HADHALANI HUYO EX HUSBAND ILI WATU WASIENDELEE KUTEKETEA NA WENGINE KUAMBUKIZWA
2.AHAKIKISHE ANAWAELIMISHA WALE AMBAO HAWAJAPATA VIRUS ILI WAJUE MADHALA YAKE NI PAMOJA NA KUWA MPWEKE NA PENGINE KUTENGWA NA JAMII PIA WALE AMBAO WANAO WAIGE MFANO WAKE WA KUWA MKWELI
3. AISHI MAISHA YA KUFANYA MAZOEZI YA MARA KWA MARA, KULA LISHE BORA IKIWA NI PAMOJA NA MATUNDA. KUTAFUTA DAWA AMBAZO ZITAMSAIDIA KULEFUSHA MUDA WAKE WA KUISHI AMBAZO NI DAWA ZA KUSAIDIA KUONGEZA NGUVU YA KINGA MWILINI
4. HII SASA NI YA MWISHO KAMA ITATOKEA BY CHANCE MTU AKAKUPENDA WAKATI AKIJUA UNA VIRUS BASI HII SI KITU KIBAYA LAKINI KUANZA KUTAFUTA MTU WAKATI WENGINE WANAENDELEA KUSAMBAZA VIRUS UNAKAA KIMYA BILA KUWATAJA SIDHANI KAMA MUNGU ATALIFURAHIA HIYO SIKU YA JUDGEMENT KAMA ITAKUWEPO AMEKUPA UTASHI WA KUJUA BAYA NA JEMA SASA HILI SI JEMA!
MWISHO NARUDIA NAKUTAKIA AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU, KUMBUKA UKIMWI NI UGONJWA PEKEE AMBAO HAUNA KINGA KUNA MAGONJWA MENGINE MENGI TU KAMA SOME KINDS OF CANCER, HAPETITIS C, DIABETES,ATHMA N.K BALI HAYO YOTE YANAWEZA KUKUWEZESHA KUISHI MUDA MREFU KWA KUSALI NA KUFUATA MASHARTI YA MADAKTARI. KUNA MIFANO MINGI TU UNAWEZA KUPATA LAKINI KUTAFUTA BWANA HII NAONA INGEKUWA NI ISSUE YA MWISHO KABISA KUIFIKIRIA. ASANTENI HUU NI USHAURI TU SI LAZIMA UUFUATE KAMA UNAONA NI WAKIPUUZI. NALITOLELA EX MUZUMBE CHUO KIKUU
Du!!!!!!!! Nalitolela, angau umeonyesha ubinadamu, hee !!!! katika kujibu mapigo.
ReplyDeleteNIMESIKITISHWA NA MAONI YA WENGI HUMU KTK MAADA HII.
ReplyDelete1. SIKU ZOTE MNAAMBIWA KESHENI MKIOMBA MAANA HAMJUWI SIKU WALA SAA
SASA USEMI HUO MNAUTAFASIRI VIPI??
HIVI NYIE WATU MNADINI AU MPO TU? NIMETAMANI KULIA.
NINACHOTAKA KUSEMA NI HIVI, HAPA DUNIANI SI KWETU WOTE TUNAPITA. MTU AKIWA NA HIV AU HATA ADIS HAINA MAANA NDIYE ATAKAE KUFA WA KWANZA. NA ASIYE NDIYE ATABAKI.
KWANI NI MARA NGAPI HUFA DR. NA MGOJWA KUBAKIA? HAYA NI MAMBO AMBAYO YAKO NJE YA UWEZO WETU BINADAMU. NIKHERI KUKAA KIMYA KAMA HUNA USHAURI.
PIA MSISUBILI MPATE SHIDA NDIYO UKIMBILIE KUOMBA MUNGU KWANI ANAKUELEZA WAZI KESHA UKIOMBA MANA HUJUWI SIKU WALA SAA.
2. HIV SIO LAZIMA UIPATE KWA NJIA YA NGONO JE HIZO AJALI ZINAZOTOKEA KILA SIKU NI DAMU ZA AINA NGAPI HUCHANGANYIKANA??
KULINGANA NA MAISHA YA BINADAMU HIVI SASA HUWEZI KUJIONA MZIMA KAMA UNATUMIA USAFILI WA BARABARANI KWANI MDA WOWOTE WAWEZA PATA AALI NA UTAKUWA KTK HATARI YA KUPATA MAGONJWA KAMA HIV.
JE UNAPATA VIPI NGUVU YA KUJIONA MZIMA KWA HILO??
3. YULE MME WA YULE DADA HAINA MAANA YEYE KUOWA NA KUZAA NDIYO AMEMUAMBIKIZA HUYO DADA KWANI HATA MUADHIRIKA ANARUHUSIWA KUZAA
JA MNAJUWA VIPI YULE MKEWE WA SASA NI MZIMA AU KAMA WOTE NIWAGONJWA NA WAMEAMUA KUZAA??
NATAKA MKAE MTAFAKARI KABLA HAMJATOA USHAURI NI NINI CHA KUSHAURI. MNAJIITA MMESOMA MLICHOSOMA NYIYI NINI?? AU KUSOMA NDIYO USIWE NA BUSARA UNAROPOKA TU KAMA WEWE SI BINADAMU.
HUKO KTK VYUO VYENU MUZUMBE HAMKUWA NA WALIMU WA DINI??
AU NI NINI KINACHOWAFANYA MUONE MTU AKIADHIRIKA AMUMRUDIE MUNGU ALIWAAMBIA ALIMUKANA MUNGU??
AU MTU MWENYE HIV DIYO MWENYE ZAMBI? AU KAULI YA KUSEMA ASALI SANA INATOKA WAPI?
MIMI NINAWASIWASI NA HIZO ELIMU ZENU HUENDA MNAFUNDISHWA ZARAU NA SI MAISHA NA HEKIMA.
TUJIFUNZE KUISHI NA JAMII!!
Kiukweli dada nakuonea huruma, na ndivyo wadada zetu wanavyoletewa zawadi watakazodumu nazo milele. dada wa watu kafunga ndoa kumbe ndoa yenyewe ilikua ndoana.
ReplyDeletewanawake wengi tu tanzania wanaambukizwa na mabwana zao hasa huu mtindo wa nyumba ndogo. sina uhakika nani kamuambukiza mwenzake lakini kama jamaa amemzalisha mwanamke mwengine bila kumuambia basi yeye ndiye aliemletea huyu dada zawadi ya maisha.
jamani chungeni ndoa zenu, sijui nyumba ndogo zitatumaliza.
dada nakuombea mungu utapata mwenzi wako atakayekufahamu, ni bora ulivyoachana naye huyo jamaa.
Watu wengine waliojibu hapa hata sijui ni waelewaje...
ReplyDeleteNi kuwa ufahamu wa huu ugonjwa ni mdogo sana sana ...na bado sana Tanzania. Wengine wanamsemea kwa hasira na kama wanapressure vile sijui hawajui stutas zao.
Na hao mnaosema akae kimya kwa vile siku zake ni chache za kuishi well, hamjui hilo kwa vile nyie sio Muumba.
Wenye ugonjwa huo kama wamefahamu mapema, wanatumia dawa, wanafuata masharti, kwenda counsel na good group support wanamaisha marefu tu...
Mimi nashindwa kuamini kwanini mpka leo watu wanona ni stigma kuwa na ugonjwa huu na pia hawataki kusema wakati nchi zingine mwenye nao yuko so open na freely kuwaeleza watu kuwa anao.....wakati nchini kwetu tunavosoma kwenye news ni 1 in every 5 or 10 people anao na nchi za wenzetu ni 1 in every 1000.
We need to pray hard and I hope dada yangu utampata mtu unayemtafuta
Nalitolela aka McZobizobi.. za siku nyingi kaka!? hapo mimi nakuunda mkono..
ReplyDeleteNilijua utakuwa viwanja hivi, zaza tuendelee kusaidia jamii.
holla back!
ndugu wadau, kuna mtu anayepost kwa jina la Nalitolela ambaye kwa muda mrefu nilimpuuza ila naona anazidi sasa. Na hapa kadiriki to go further and use my fullname, Peter Nalitolela. I would just like to make it known kwa wadau kuwa I am not related even remotely to this character. It seems he is on a personal mission to taint my name, for whatever reason, as he always posts under my name and his comments are usually derogatory, demeaning and offensive to others.
ReplyDeleteI always post here using my blogger account, that's how you can tell the difference between the post from the real Peter Nalitolela and this other person. I have already reported him to Kaka Michu and he promised me to make an effort to block his/her comments.
This person, whoever they are, must have seen reference to my time at Mzumbe (Secondary School) being made by one of my mates from High School and mistook Mzumbe to mean the University and he has been posting as NALIOLELA from Mzumbe/Muzumbe University or NALIOLELA Ex-Mzumbe/Ex-Muzumbe.
ndugu wadau, kuna mtu anayepost kwa jina la Nalitolela ambaye kwa muda mrefu nilimpuuza ila naona anazidi sasa. Na hapa kadiriki to go further and use my fullname, Peter Nalitolela. I would just like to make it known kwa wadau kuwa I am not related even remotely to this character. It seems he is on a personal mission to taint my name, for whatever reason, as he always posts under my name and his comments are usually derogatory, demeaning and offensive to others.
ReplyDeleteI always post here using my blogger account, that's how you can tell the difference between the post from the real Peter Nalitolela and this other person. I have already reported him to Kaka Michu and he promised me to make an effort to block his/her comments.
This person, whoever they are, must have seen reference to my time at Mzumbe (Secondary School) being made by one of my mates from High School and mistook Mzumbe to mean the University and he has been posting as NALIOLELA from Mzumbe/Muzumbe University or NALIOLELA Ex-Mzumbe/Ex-Muzumbe.
No one can assure himself/herself a full protection against HIV as the current status reveal out there.Sister I appreciate your strength of being open.There is a lot of people with HIV spreading the viruses to their partners purposely or without knowing their health status.i understand ure concern of being protective even in this situation;this is a big step.I believe u will get a partner of your type and with the same vision.Most important is to stick on ure point/focus and follow constructive instructions.
ReplyDeleteDada hongera kwa kuchangamsha baraza.
ReplyDeleteKama uko serious naomba uongee na wahusika katika clinic unayoenda wakushauri.
Huwa wanao ushauri mzuri sana kwa mambo kama ya kwako.
Hapa unaburudisha watu tu, na pia itakuchukua muda kupata mtu hadi uje umwamini.
Ujue asilimia kubwa ya wadau hapa kupima bado (nadhani unajua asilimia ya watanzania waliopima, ndio iliokupa michango hapa)
Wengi si weledi wa mambo haya zaidi au wanayajua kwa mtaani na kwa jirani.
Kama uko serious, na nafsi yako kawaeleze waliokupima wakakupa majibu na wanaoendelea kukushauri.
kama unatafuta soul mate utapata huko na ushauri jinsi ya kuishi mtapewa pamoja kwa upendo.
Nasema hivi, niko sceptic kwani najua wadada hatupendi upweke sana na ni rahisi kukurupuka kutoka kwenye kikaango na kurukia mtotoni.
Huu sio tena muda wa kufanya makosa.
Nachukua nafasi hii kumpa pole na pia kumpongeza huyu dada kutoa yake yaliyo moyoni. nasikitika sana na hao wote wanomlaumu huyu dada japo ni kwa kiasi kidogo kutoka kwenye post hizi. mimi ninafanya kazi na research pia kwenye hii miradi ya ukimwi ningependa kuelewa kuwa mtu akiwa ameathirika eti sio kama anaacha kuwa binadamu na hisia zake zinakufa mwilini, anakuwa ni kama tu binadamu wengine wenye mahitaji yao ila wao wanahitaji support na mapenzi zaidi. cha msingi tu ni muathirika anatakiwa awe na uelewa mkubwa kuhusu huu ugonjwa kuwa hatakiwi kuambukiza wengine na njia bora ya kuishi ili maisha yake yarefuke. kujitangaza ni hiyari ya mtu cha msingi usimuambukize mwingine wewe jua tu imekukuta wewe basi it is your fate na Mungu amependa iwe hivyo inabidi ukubali. hao wanaotaka ajitangaze naomba muelewe pia kwa Tanzania stigma/unyanyapaa bado upo sana kuanzia kwenye familia zetu mpaka jamii inayotuzunguka, na pia inategemea na status ya mtu kwenye jamii. hivi mbona sijasikia hawa wabunge, mawaziri na viongozi wengine wakitangaza au kulazimishwa? ni kwanini? ina maana wao wote wako safi? Hapana lakini wanajua kuanzia vyombo vya habari, watu wanaowaongoza na jamii nzima watawanyanyapaa badala ya kuangalia kazi wanazozifanya. inaumiza na pia yataka moyo kujitangaza na zaidi tujue tu huu ugonjwa unaweza kumpata yoyote yule na sio lazima kwa njia ya ngono kama wengi wanavyofikiri.
ReplyDeleteHabari wadau?
ReplyDeleteNamponeza dada kwa ujasiri wa hali ya juu. ni shujaa.
Naomba tuwasiliane kwa mail yangu frankharold575@yahoo.com
Cure for HIV / aids has been available for a long time through Dr. Iyabiye, he treat and cures HIV. It's just that most people didn't know about it and even those people that was treated and cured didn't testify or notify people about it because they don't want to be known to have lived with HIV before. You can reach the doctor through: iyabiyehealinghome@gmail.com or WhatsApp and phone call: +2348072229413
ReplyDelete