
Ukiona katuni hiyo ya Robert Mwampembwa aliyotoa mwaka 2006 kwenye globu hii ya jamii, basi ujue kuna kwikwi ya nishati.
Naam! Libeneke la mgao wa umeme umeanza toka leo baada ya mitambo mitatu ya kampuni ya Songas kupata kwikwi. Mgao huo, kwa mujibu wa afisa wa habari wa tanesco, bi. badra masoud, utaanzia asubuhi hadi saa nne unusu usiku.
hata hivyo kuna habari njema kwamba kundi la wataalamu toka marekani linawasili kurekebisha kwikwi hiyo. Endelea kusoma hapo chini na hadi kwenye link ya gazeti mama la daily news. ila habari ndiyo hiyo. mambo ni mgaozzzzzzzzzzzzzzzzzzz
A GROUP of technicians from the US multinational General Electric (GE) are expected to arrive in Dar es Salaam today to fix the grounded Songas generators that have led to power rationing in the country, the Minister for Energy and Minerals, Mr William Ngeleja, has said. For more on this story click here: www.dailynews-tsn.com
Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya nanihii na balozi wa ......! Habari yako muzee? Naomba niulize wadau, kwamba Tz si tuna-Ma-engineer wenye degree za electrict technology na vyuo kibao vya taaluma hiyo kikiwemo chuo kikuu cha Dar (UDSM) chini ya kitivo cha taaluma hiyo nyeti; sasa inakuwaje hivyo vimtambo vya kuzakisha umeme vikichemsha ni mpaka wataalam watoke nje? Waya unaopeleka umeme Zanzibar uliungua, na ikabidi wataalam watoke nje vilevile. Sasa hao wanaoitwa wataalam wa electronics hapo bongo wanasemaje juu ya hili? Au wanajua ku-solve culculus tu? Hao mafundi wanaotumwa kuja huko bongo ni mafundi vishoka tu wa huku majuu! Hembu washtue hao ma-engineer wa hapo mlimani wafanye mambo basi ili kuokoa vijisenti vya bongo jamani. Au ni ma-engineer jina? Wadau hili linakaje juu wa hawa watu wanaojiita ma-engineer wa umeme? Hawa watu wamesomeshwa kwa kodi za wabongo, sasa ni vipi washindwe kuwaangalia wabongo?
ReplyDeleteWEWE MTOWA MAONI WA KWANZA KABISA UMENIKUMBUSHA JAMBO MUHIMU SANA, KUNA WEBSITE MOJA KAMA SIKOSEI INAITWA JAMII FORUM, WANAFUNZI AU WATU WALIOSOMEA UNI OF DAR WANATAMBA SANA KUSEMA UNI OF DAR NDO YENYEWE VYUO VINGINE NI FAKE TU, NDO MAANA WATU WOTE WANAOENDA UNI OF DAR NI DIVISION ONE VIPANGA MABUNDI SASA MBONA VIMTAMBO HIVYO VIDOGO TU VINAWASHINDA?
ReplyDeleteHUWA WANAPONDA SANA WATU WALIOSOMA VYUO VINGINE.
MARA NYINGI HAO WATU WANAOKUJA KU-FIX KUTOKA HUKU MAJUU WALA HAWANA HATA DIPLOMA ZA KAZI HIZO NI UZOEFU KAZINI TU.
WANAFANYA APPRENTICE TU HUWA WANAJIFUNZIA KAZINI MPAKA WANAFIKA KUJUWA UFUNDI KAMILI. shule za tanzania ni za karatasini tu kusolve mambo on paper vitendo ni sefuli.
Hii inashangaza na kusikitisha kama wenzangu msemavyo, kuna wataalamu kibao waliosomeshwa kwa kodi zetu ili walitumikie taifa ila hakuna wanalofanya, vitu vidogo kama hivi na vyenye kutia hasara kubwa Taifa letu ni mpaka waje wanao jiita wataalamu kutoka nje jamani? angalia tatizo la Zanzibar lilivyochukua muda mrefu kutatuliwa. Mfumo wa Elimu yetu bado haumsaidii/ haumuandai mwanafunzi katika mazingira halisi ya utendaji kazi. Hili ni la kufanyia na Wizara husika.
ReplyDeleteNdugu zangu Watanznia,jamani tuache haya mambo ya kudharau mainjinia wetu kwani kurekebisha hitilafu hiyo kunahitaji wazungu toka Marekani kuja kutengeneza?tuache haya mambo ya aibu..kwani wakituuzia mitambo si kunakuwa na mpango wa kuwafundisha/kuwaonyesha mainjinia wetu jinsi ya kuendesha na kutatua matatizo kama hayo?Hapo ni naona kuna kaufisadi kanataka kutokea..maana sirikali itapigwa bili ya kufa mtu/watu,na kama kawaida watu fulani watakula 10% na baadae kuita 'visenti'...tunao wasomi wa kufanya hiyo kazi ila ni 10% tu ndio inasumbua.
ReplyDelete