HABARI KAKA MICHUZI.
Mimi ni mdau mkubwa sana wa blog yetu hii ya jamii niliyepo masomo huku ASIA.Katika kukaa kwangu huku kwa miaka minne,nakaribia kumaliza shule hivi karibuni. Mungu kanisaidia nimejikusanyia vitu mbalimbali ambavyo ningependa kurudi navyo nyumbani.
Sasa kuna tetesi nilisikia kwamba kwa mwanafunzi aliyeko masomoni nje ya nchi ya tanzania anaruhusiwa kuingiza contena na vitu vyake BURE kabisa bila ushuru,yaani yeye alipie usafiri tu ikiwa kwamba alikaa kimasomo kwa zaidi ya miaka mitatu.
Sasa nilikuwa nauliza kama kuna mtu mwenye taarifa hizi anisaidie,au nijue nijiandae vipi na usafirishaji wa hivi vitu.
NATEGEMEA USHIRIKIANO WENU WAUNGWANA
Hizo ni personal effects zako hupashwa kulipia kodi yoyote ile na si miaka mitatu ni mwaka mmoja, cha msingi hivyo vitu viwe ulikuwa unavitumia huko zaidi ya mwaka mmoja, kama ni gari pia iwe umeinunuwa zaidi ya mwaka mmoja na uwe ulikuwa unaitumia huko, na sheria hii si kwa wanafunzi tu ni kwa mtu yoyote ambaye ni mtanzania alikuwa nje na alikuwa na hivyo vitu akivitumia kwa zaidi ya mwaka mmoja, ukiwa na ushahidi huo hutalipa kodi yoyote zaidi ya ada za TICS bandarini na watu wa Fowarding and Clearing kwani kuna sheria siku hizi huwezi kwenda kutoa mizigo mwenyewe hadi utumie hawa watu, huu ni ukiritimba na ni wazi kuwa hawa walipendekeza hivyo kwa TRA ili wapate ulaji na rushwa ilitembea hapo ili ombilao lipitishwe. Hata hivyo jiandae na watu wa TRA ni wabaya na wasumbufu sana, watakuangaisha na kukubana na pengine kuto kukuamini na kukubambika kuwa unasema uongo hivyo vitu hukuwa navyo siku hizo zote na watakulipisha kama so kodi yote watakulipisha VAT, ni watu wabaya nisema wazi, lakini yote ni kwa sababu ya rushwa, wanataka wakusumbuwe hadi uone umuhimu wa kutowa rushwa, kwani kusema wazi wanaogopa siku hizi. Ki msingi hii sheria walitunga kwa kujitungia wenyewe hasa familia za vigogo wa serikali na mabalozi ambao zama hizo walikuwa wanaenda nje peke yao, sasa kwa vile watu wengi wanaenda nje basi wanaponea hapo hapo, serikali haiwezi kubagua tena. So it is free of tax if you can provide evidences that those things were in use for more than a year there where you been.
ReplyDeleteYaani ukizungumzia TRA nasikia kama kutaka kutapika, hivi huwa wanasomaga kwenye blogu angalau basi wakajirekebisha? Sijui ni watu wa namna gani, ila jamani cha msingi kupambana na rushwa ni kukataa kutoa rushwa basi, watakuona mbaya unataka kuwaharibia kazi unawachongea lakini hakuna dawa nyingine ni hiyo tu, hata ikibidi kwenda kuchukua pesa za PCB nenda tu maana watu wana roho mbaya za kwanini sijui wakoje hawa watu. Walilizuia gari la kijana mmoja masikini ya mungu alikuwa dereva taksi akadunduliza pesa yake miaka, nafikiri mnaelewa hali za madereva taksi, ilivyotosha tukamsaidia kununua gari kwenye mtandao, akalipia kila kitu kinachotakiwa. Gari kufika bandarini haikutoka mpaka baada ya karibu miezi miwili, sababu haisemwi, kila ukiuliza wako kimya! Nungu nungu kweli hao jamaa. Wengine ni wanaohusika na kulipa mafao ya watu, popote pale walipo wawe hazina au nssf au popote pale, wakiona kapesa kanazidi 1m, basi wameona pesa nyingi lazima mgawane nao. Nawauliza hivi nyie watu wakati watu wanakatwa kwenye mishahara yao hizo akiba zao mlikuwa mnawasadia kwa lolote mpaka siku anapokuja kuchukua pesa yake mnataka mgawane au mnamnyanyasa kama vile kaja kuomba mkopo ilhali ni pesa yake mwenyewe kadunduliza? Mtu aniombe rushwa au aonyeshe tu kadalili ka macho ka kutaka rushwa, atakiona cha mtema kuni!! Kudadadek
ReplyDeleteMdau aliyetangulia ameshauari vizuri na kitaalam ila amemtisha sana mwobaji kuhusia na ubaya wa TRA ukweli hayo yalikuwa mambo ya kale siku hizi watu wamebadilika mizigo kama hiyo tunatoa kila kukicha na hauna urasimu wowote TRA kama umezingatia masgarti yao kwa msaada zaidi tuandikie intermarine999@hotmail.com tutakupa msaada wakutoa hilo container lako pasipo usumbufu wowote kwa 100%
ReplyDeletewadau wameongea vizuri hapo juu. Ila kuna huyu mdau aliyetoe email yake hapo juu ni wakuwa makini kwani kama ni kw akutumia hotmail kwa hiyo anayoiita intermarine ni swala la kutilia mashaka. ndio hawa hawa wale 10% ama contena lisionekane kabisa. Ni mtazamo tu..
ReplyDeleteKama umekaa nje kwa aina yoyote na vifaa vyako ulivyo vitumia,hautolipia ushuru ilimradi viwe si vipya vioneshe kweri vimetumika baada ya ukaguzi,na wewe utajaza fomu ya TRA inayo itwa BD FORM,ambayo utaambatanisha na passpot yako ili kuhakiki kweri ulikuwa nje pia ni vyema kama ulibadari passpot baada ya mwanzo kuisha uwe nazo zote,wewe utakachoripia ni PORT CHARGES ya bandari,SHIPPING CHARGES ya line ya meli na AGENCY FEE ya wakala,kuhusu wakala mzuri ni vyema utizame YELLOW PAGE uchague na muelewane kabla amjapeana kazi na kuhusu TRA usitishike awana usumbufu kwa sasa.
ReplyDelete