Ndugu Watanzania wote wa Machester na vitongoji vyake, mnakaribishwa katika mkutano wa wa Watanzania wote utakaofanyika Katika ukumbi wa Ourlady’s Parish Centre, Ruby street, Moss Side, Manchester M16 7JQ.
Tarehe 18 mwezi wa 10 saa 12 jioni.
Madhumuni ya mkutano huo ni kuundwa rasmi kwa jumuiya ya Watanzania Manchester, siku hiyo viongozi wa jmuiya hiyo watachaguliwa Tunawaomba Watanzania wote kuhudhuri siku hiyo iliwaweze kushiriki katika kuchagua viongozi wa jumuiya hiyo, kufika kwako ndio kufanikisha shughuli hiyo tunaomba unapopata ujumbe huu waambie na Watanzania wengine.
Kiingilio ni bure, vinywaji na chakula vitatolewa bure pia,
karibuni sana.
Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana na
Daudi Mwakimwagile 07534499405
Hamphrey Mhada 07523457951
Modibo Keita 07961797910
Herman Livingstone 07899806500

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mambo si hayo! Watanzania wa Manchester kwa mtaji huu tunawapongeza na kuwatakia kila la kheri kuunda jumuiya ya Watanzania kama hiyo mnayokududia bila kubaguana. Kama kuna sifa moja ambayo huwa inawabainisha wabongo kutoka kwa mataifa mengine ya kiafrika wanapokuwa ughaibuni ni kutanguliza huo utanzania (utaifa) kabla ya mengine yote. Ninawafagilia kwa asilimia mia.

    ReplyDelete
  2. Mambo si ndio hayo sio CCM CCm CCM.

    Watu wakiwa nje ya nchi wote ni wa moja no matter chama unachokipenda huko nyumbani Nashangaa sana CCM ikikomalia kufungua mashina nchi za watu.

    Au ndio ile wanasema desperate mind...


    Wahindi, wanigeria na wakenya wamekuja huku toka miaka ya 30 lakini huoni hata siku moja wanafungua nyama na maendeleo yao huko kwao tunayaona.

    Siye generation ya kwanza imekuja mika ya 70 na leo tunaanza vyama....Kama sio kutafuta haja ya kutugawanya nini nini ninii

    UMOJA HUO TUTAKUJA WENGI

    Tanzania HOYEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  3. Samahani kama nitaonekana mbaguzi. Nimeelewa kuwa ni mkutano wa wabongo sasa "hiyo Modibo vipi na hiyo Keita vipi" - au ni majina tu yamefanana na ya watu wa kule nanihii...

    ReplyDelete
  4. annon wa 10.25am,,,hahahaaaaa modibo na keita,,aya watueleze au ndo baba nanihii na mama m-Tz??
    jaman hongereni saaaana wa-Tz inapendeza sana kuwa na umoja nchi za mbali ili muwe na na mawazo +ve kujenga Tz,,,na kuendeleza uzao
    kila la kheri

    ReplyDelete
  5. Wana wa Manchester "IWAPO" mnakutana kuanzisha jumuiya ya kusaidiana wakati wa Sherehe na Shida mnapoteza muda wenu.

    Nawasihi muanzishe Jumuiya ya Kibiashara au Uchumi.

    Kila Kheri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...