Watanzania wote wa Manchester na vitongoji vyake mnakaribishwa katika mkutano wa Watanzania wote utakao fanyika tarehe 13 mwezi wa tisa saa 12 jioni katika ukumbi wa
Our Lady’s Parish centre,
Ruby street,
Moss side,
Manchester
M16 7JQ.
Madhumuni ya mkutano huo ni kuanzishwa kwa Jumuiya ya Watanzania Manchester, siku hiyo viongozi wa jumuiya hiyo watachaguliwa.
Madhumuni ya mkutano huo ni kuanzishwa kwa Jumuiya ya Watanzania Manchester, siku hiyo viongozi wa jumuiya hiyo watachaguliwa.
Tungependa Watanzania wote tushiriki kwa kuhudhuria shughuli hiyo, vinywaji na Chakula vitatolewa bure. Utakapopata ujumbe huu naomba uwafahamishe watanzania wote.
Karibuni sana
Kwa ufafanuzi zaidi wasaliana na
Daudi Mwakimwagile 07534499405
Hamphrey Mhada 07523457951
Modibo Keita 07961797910
Karibuni sana
Kwa ufafanuzi zaidi wasaliana na
Daudi Mwakimwagile 07534499405
Hamphrey Mhada 07523457951
Modibo Keita 07961797910


ahaa hizi ndio jumuia tunazitaka na kutufaa huku nje, ni jumuia za watanzania, zinatujumuisha sote, zinatuunganisha wote na kujuana sio mambo ya kufungua matawi ya ccm kila leo, hayo hututenganisha kwani asokuwa mwana ccm hajumuishwi. Tutafika ndugu zangu tudumishe umoja wetu huku nje.
ReplyDeletemambo mawili tu ningelipenda kugusia
1. Je kuna fomu za maombi kwa atakae kugombea nafasi za uongozi? kama zipo zinapatikana wapi? pia kuna nyadhifa ngapi za kugombewa?
2. hapo mahali pa mkutano na utangazwaji wa kuwepo vinywaji na vyakula huenda ndugu zetu walio katika mfungo wa ramadhani kusita kufika huko
baadae tawi la CCM!
ReplyDeleteNina imani hatua inayotegemewa kuchukuliwa na watanzania waishio Manchester (UK) hiyo tarehe 13.08.08 ni ya muhimu mno katika jamii ya kitanzania waishio hapa. Hivyo kila mmoja wetu ambaye anaamini ni mtanzania ahudhurie siku hiyo ili apate nafasi na haki yake ya kumchagua Mwenyekiti, Katibu na mweka hazina wa jumuiya.
ReplyDeleteNielewavyo ni kuwa hapatakuwa au hakuna forms za wagombea. Nilivyosikia kutoka undani wa waandalizi ni kuwa wahusika watajitahidi siku hiyo kutumia sehemu ya demokrasia jinsi itakavyowezekana ili kila mmoja wetu ikiwezekana ataje jina , au majina ya wagombea wa nafasi hizo. Alafu kura zitapigwa kwa kutumia majina hayo yatakayo-pendekezwa na kukubaliwa na wahudhuriaji.
Nakubali kuwa tukio hili limekuja wakati wa mfungo wa Ramadhani, huenda ni baraka!!!!, nakubali kuwa patakuwa na vinywaji, na makulaji, yote ni kheri kwa jamii yetu, hivyo nitakacho-waomba watanzania wote nikujitahidi kuelewa umuhimu wa yote haya na kuwa kila jambo hapa lina umuhimu wake hivyo tutumie busara zetu kufanikisha tukio hilo la uchaguzi.
HAYA WOTE SHIMEE WATU WANGU.
Enhe, eheeee!! mmeanza!Manchester na nyie mmeanza!! No, sorry,SAMAHANI. kumbe ni wana jumuiya, Duu, safi sana. Nilikurupuka nikadhani ni wale sijui wa kufungua mashina, mara matawi na mizizi ya wakereketwa. Lakini ka ni jumuiya, RUKSAA. Nawatakia mkutano mwema wa Amani.
ReplyDeleteQ