
Meneja Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo wa Kanda yaKusini na Kati Willy Magehema (kushoto) akikabidhi sehemu ya vitabu500 vya hisabati vilivyotolewa msaada kwa Mbunge wa Mbozi Mashariki,Godfrey Zambi kwa ajili ya shule 10 za sekondari katika jimbo hilo.Hafla hiyo ilifanyika pamoja na na uzinduzi wa kampeni ya Tigo ElimuBora Tanzania kwenye ofisi za mkuu wa wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya juzi. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Swaleh Simba na Kaimu Mkurugenzi wa Mbozi, Ngaikwela Lington.

Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (wa pili kushoto)akiangalia sehemu ya vitabu 500 vya hisabati vilivyotolewa msaada nakampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa Mbunge huyo kwa ajili ya shule10 za sekondari katika jimbo hilo. Hafla hiyo ilifanyika pamoja nauzinduzi wa kampeni ya Tigo Elimu Bora Tanzania iliyozinduliwawilayani Mbozi Mkoani Mbeya juzi. Wengine kutoka kushoto MenejaBiashara wa Tigo Kanda ya Kusini na Kati Willy Magehema, KaimuMkurugenzi wa Mbozi, Ngaikwela Lington na Kaimu Katibu Tawala wawilaya hiyo, Swaleh Simba.

Meneja Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo wa Kanda yaKusini na Kati Willy Magehema (kulia) akikabidhi sehemu ya vitabu 50vya hisabati vilivyotolewa msaada kwa Kaimu Mkuu wa shule ya sekondariIsangu, Owden Kamwela shuleni hapo Mbozi mkoani Mbeya juzi. Awali Tigoilimkabidhi Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (wa pili kulia)vitabu 500 kwa ajili ya shule 10 za sekondari katika jimbo hilo. Haflahiyo ilifanyika pamoja na na uzinduzi wa kampeni ya Tigo Elimu BoraTanzania iliyofanyika wilayani humo. Wa pili kushoto ni Ofisa Elimu waWilaya ya Mbozi, Gift Kyando Enock.

Meneja Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo wa Kanda yaKusini na Kati Willy Magehema (kulia) akikabidhi sehemu ya vitabu 50vya hisabati vilivyotolewa msaada kwa Makamu Mkuu wa shule yasekondari Nalyelye, Moses Simwinga shuleni hapo katika wilaya yaMbozi mkoani Mbeya juzi. Awali Tigo ilimkabidhi Mbunge wa MboziMashariki, Godfrey Zambi (wa pili kulia) vitabu 500 kwa ajili ya shule10 za sekondari katika jimbo lake. Hafla hiyo ilifanyika pamoja na nauzinduzi wa kampeni ya Tigo Elimu Bora Tanzania iliyofanyika wilayanihumo. Wa pili kushoto ni Ofisa Elimu wa Wilaya ya Mbozi, Gift KyandoEnock.

Meneja Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo wa Kanda yaKusini na Kati Willy Magehema (kulia) akikabidhi fulana na sehemu yavitabu 50 vya hisabati vilivyotolewa msaada kwa Mkuu wa shule yasekondari Myovizi, Jaston Hankungwe shuleni hapo katika wilaya yaMbozi mkoani Mbeya juzi. Awali Tigo ilimkabidhi Mbunge wa MboziMashariki, Godfrey Zambi (wa pili kulia) vitabu 500 kwa ajili ya shule10 za sekondari katika jimbo lake. Hafla hiyo ilifanyika pamoja na nauzinduzi wa kampeni ya Tigo Elimu Bora Tanzania iliyofanyika wilayanihumo. Wa pili kushoto ni diwani wa kata ya Myovizi, Patson Nzoa.
Well done tigo hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inahitaji kuzaliza wanasayansi wengi na siyo wanasiasa tena(Jakaya Mrisho Kikwete-Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania).
ReplyDeleteNyie wanafunzi-jitahidi kuvitumia hivyo vitabu kwa uangalifu,viwasaidie nyie na wadogo zenu siku za mbele.
JAMANI HIVI MMEKOSA KWELI KAZI ZINGINE ZA KUFANYA HUKO MBOZI, KAMA MBUNGE ALISHAPOKEA HIVYO VITABU KWA NIABA YA SHULE 10 SASA KUNA SABABU GANI TENA KUKABIDHI KWA KILA SHULE MOJA MOJA???? INAWEZEKANA HAPO HATA SHULE ZOTE 10ZILIFUNGWA KWA AJILI YA UPOKEAJI WA HIVYO VITABU....BE SERIOUS TANZANIANS PLEASE...
ReplyDeleteKuna jamii yoyote ambayo inaweza kuwa imara na kuendelea kwa kuwa na wanasayansi tu bila wanauchumi, wana saikolojia, wana lugha, wana diplomasia, wanasheria, wanasiasa bora, na kadhalika? Tuelimike jamani, na tuachane na hili wazo kuwa sayansi ndio pekee inayohitajika.
ReplyDelete