JUMAMOSI TAREHE 27/09/2008
ALI KIBA ATAKUWA WICHITA, KANSAS
ambapo amepania kuwaburudisha
MASHABIKI WAKE WENGI
wanaomsubiri kwa hamu kubwa.
Njoo userebuke na "cinderella" "Mac muga" "Nakshi Nakshi" na vibao vingine vipya sita vitavyokufanya ukubali mwenyewe kwamba kijana ana kipaji. KUONGEZEA VIUNGO,
mwanamuziki anayekuja kwa juu mno kwenye chart za bongo flava kutoka Houston Texas "LBT" ataperform kibao chake kipya kinachotamba hivi sasa "addicted".

Hakikisha TAMASHA HILI LA KUPINDUA ARDHI
lililoandaliwa na vijana mashuhuri wenye kujua kazi wa
U-1 ENTERTAINMENT OFFICE
halikukosi. Usingoje kuhadithiwa, fika mapema.
KWA MAELEZO ZAIDI INGIA
Alikibausa.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ali Kiba Ali Kiba tushachoka sasa. Alikiba mwenyewe mchovu tu nyimbo nzuri mbili unataka kututoza $25 kwa mtu. Ukumbi mwenyewe wa kishenzi sasa $25 ya nini Nyie U-1. Msitake kutajirikia kwa migongo ya watu na uchumi wenyewe unauona haujakaa sawa.

    ReplyDelete
  2. nakumbuka ilitangazwa humu ktk hii Sirikali ye2 ya jamii kuwa maonyesho ya huyu msanii yatasimamishwa kwa kile kilichoitwa "Kuunga mkono comments za Wadau wengi" juu ya mwezi Mtukufu.Acheni kuona wanajamii kama chekechea.hamkutaka kusema ukweli kwamba mlisitisha kutokana na Hurricane kule Houston na mkaja na danganya toto.
    Inabidi Mkueeeeee.toeni sababu zilizo za kweli.

    ReplyDelete
  3. Huyu dogo asituyeyushe kuwa bado ana perform hapa MAREKANI.Tuambie ukweli kuwa umekimbia MAVUMBI ya Bongo.Hakuna mwanamziki yeyote Anaye-perform miezi miwili.Hao kina Jay Z,Usher tunawaona wakienda TOUR wanaperform wiki 2,3 halafu wanageuza.Sasa wewe kama umekuja MAREKANI kupiga BOKSI bora useme ukweli kuliko kujificha chini ya mwamvuri wa MUSIC TOUR.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...