Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (kushoto kwake) wakimtazama Mratibu wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto wa Wilaya ya Mpanda, Agnes Chami aliyekuwa akionyesha jinsi ya kuweka dawa ya kuangamiza mbu katika chandarua wakati alipozindua Mradi wa Ugawaji Vyandarua na kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Kashaulili,mjini Mpanda , September 20, 3008. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Daniel Ole Njoolay, Mkurugenzi wa PSI, Mary Mwanjelwa, Mbunge wa Viti Naalum, Anna Lupembe na Mbunge wa Mpanda Kati, Arfi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi chandarua kilichotiwa dawa, mototo Consensa Kinoku wakati alipozindua Mradi wa Ugawaji Vyandarua na kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda September 20, 2008. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu, Mkurugenzi wa PSI, Mary Mwanjelwa na kulia ni Mlezi wa Mtoto huyo, Aurelia Katakwa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi chandarua kilichotiwa dawa ya kuangamiza mbu, Mtoto Agnes Joseph wakati alipozindua Mradi wa Ugawaji wa Vyandarua na kuhutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda September 20, 2008. Kushoto kwake ni Mkewe Tunu na kulia ni Mkurugenzi wa PSI , Mary Mwanjelwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Excellent Hon.PM.Jitahidi kupambana na Malaria nchi nzima.Malaria imekuwa na inazidi kuwa tishio la Taifa letu hasa maeneo ya vijijini.

    ReplyDelete
  2. huwezi prevent malaria kwa kugawanya vyandarua,koz kinatumika wakati wa kulala,je unapokaa sebuleni usiku kabla ya kulala kwa mazungumzo au kuangalia luninga,vijana wanaokaa maskani usiku mbu pia wanapatikana,

    kama kweli mnataka tokomeza malaria viongozi wadumishe mazingira safi mito na maziwa isichafuliwe,vidimbwi vya maji machafu visipewe nafasi kuwepo mitaani.
    mazingira safi kila sehemu tz.apo ndipo malaria yatatokomea,

    otherwise viongozi wanadanganya wananchi wao eti mradi wa kutokomeza malaria,,hayataondoka ngo na watu kulalia vyandarua vyao

    ReplyDelete
  3. mimi nauliza swali dawa ni kuwadhibiti mbu au kununua vyandarua? kipi rahisi (gharama)mbona hapo zamani iliwezekana?madimbwi yote yalimwagiliwa dawa na malaria haikuwa tishio hivyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...