Toka shoto ni Bashiri Chuma "Teves", Abdulshareef, Elvis Mnyamuru "Doto", Sajo, Said Chambuso"Jogoo", Down from left; Khamza Liganga "Liga", Mzindwelha Mswazi "Muzi",Mbhekwa Dlamini"Machine", Togoleni Kirumbi"Togo", Hadji Saeedia "Helper", and Fredric Mburushi"Capt. Dunga". Chini ni wakati wa mtanange mmoja hivi karibuni
Hiyo ndio safu kamili ya kikosi cha Tanzanite Fc ya Atlanta ambacho kinatazamiwa kushiriki ligi daraja la tatu hapa Atlanta Georgia(ADASL).

Ligi hiyo inayotazamiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu na kumalizika mwezi wa tano mwakani inategemewa kuwa ni changamoto tosha kwa vijana hawa machachari wa Tanzanite FC ambao hawajapoteza hata mchezo mmoja toka June 2007.
Pia timu hiyo itakuwa na nafasi ya kupanda daraja kama ikimaliza mmoja ya washindi katika kundi lao. Kushiriki kwao katika michuano hiyo kunawapa nafasi vijana hao kushiri katika US CUP ambayo hujulikana kama Perrin Cup.

Michuano hiyo inayoendeshwa kwa mtoano itaipa nafasi timu hiyo kukutana na timu kubwa hapa US ambazo zinashiriki katika Major League au United Soccer League kwani michuano hiyo inafananishwa na FA Cup kule UK.

Timu hii ambayo imekuwa ikiendeshwa kwa nguvu za wachezaji na viongozi wawili watatu ambao wamekuwa wakijitolea walichonacho kuwasaidia vijana hao.

Hivi tunavyozungumza timu iko mbioni kujitoa katika ligi baada ya kushindwa kutimiza ada ya ushiriki na hii itakuwa ni pigo kubwa sana kwa vijana hawa ambao wamekuwa na wamepania kuitangaza Tanzania hapa Marekani.
Gaharama za timu zinajumuisha vifaa vya mechi na mazoezi, Madawa, Bima ya ajali kwa wachezaji na marefa, Gaharama za viwanja, Usafiri(ikiwa inahitajika kuifuata timu nje ya state hasa kwenye US CUP) na gaharama za usajili.
Kwa maana hiyo timu ingependa kuomba misaada ya kila aina kutoka kila kona ili kufanikisha jukumu hili.

Hii pia inayalenga makampuni huko Nyumbani na hapa US bila kusahau watubinafsi (ZAIN, TIGO,VODACOM,SBL,METL,NCNBC, etc) Tungeomba michango yenu pia.

Kwa taarifa zaidi tafadhali pitia website ya timu na wasiliana na
Khamza Liganga @ 404 457 1578
or email him
or fax 770 491 1259.
or
www.tanzanitefc.blogspot.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. tafuteni wadhamini huko huko.hao wadhamini wa bongo acheni wadhamini timu zilizopo bongo.
    just for help,jaribu kuwasiliana na jamaa wa Konyagi USA.ni vyema kama mkatangaza biashara ya kiTZ ambayo tayari ipo huko.hao wadhamini uliowataja sidhani kama washavuka mipaka hadi USA.
    Pia wasiliana na Kajumuro hapo Seattle.nadhani anaweza kuwasaidia na kama hana uwezo huo pia anaweza kuwa anajua michongo miwili mitatu ya kuwaunganisha somewhere else.
    Good luck.

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na mtoa maoni wa kwanza. Lengo la kudhamini ni kujitangaza zaidi kuliko kujitolea.
    Sioni kivipi kampuni ya simu ya simu ya Tanzania itanufaika kwa kujitangaza ktk local league iliyo nje ya Nchi .

    ReplyDelete
  3. hadji naona umekimbia Philly.Vipi umeshaleta demu mwingine toka Bongo?hahahahahaha.Zile traffic ticket ulishazilipa?

    ReplyDelete
  4. We Bashiri Chuma wacha uhuni wewe Mpira umejulia wapi? Wakati sisi tunacheza mpira makutopora Jeshini tulikuwa hatukuoni Uwanjani,Wewe ni Mr Smart tu.................Mpira hakuna.Togoreni Kirumbia Mrefu kama Twiga yeye anajitahidi kidogo lakini akiacha maringo mpira anaujua mtoto wa Chang'ombe. Washikaji Mnakumboka Makutopora John Tough,Terence Ngole,Augustine (Bob Tino) Frank Mchau,Timu ilikuwa imekamilika kwani hata Kwesi alikuwa hpati namba.................HAHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    Londoner

    ReplyDelete
  5. ha ha ha ! Mdau wa makutupora jeshini unavituko .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...