akitangaza uamuzi huo leo, makamu wa rais wa tff, cresentius magori, amesema uongozi wa tenga umeleta tija na maendeleo lukuki katika soka nchini na kwamba miaka minne ya mwanzo aliyotumikia kuongoza imeweza kuweka sawa mambo kibao ikiwa ni pamoja na utawala wa sheria, kufufua ari ya mchezo pamoja na kuweza kurudisha kwa nguvu imani ya wafadhili kwa shirikisho hilo na pia kuweka dira ya mchezo kwa kuelekeza nguvu kwenye nyanja ya kutafuta na kulea vipaji vichanga.
sir tenga mwenyewe ameomba muda kufikiria pndekezo la kwamba atagombea ama la, akisisitiza kwamba kipaumbele kwa sasa si nani atakuwa kiongozi wa tff kwa miaka minne ijayo bali kuhitimisha ratiba ya shirikisho katika kila eneo, na sana sana kuimarisha maazimio na utekelezaji wa mikakati ya kufufua soka nchini.
globu hii ya jamii inaungana na kamati ya utendaji ya tff kumuomba sir tenga asifanye mtimanyongo kwa kukataa kugombea kwani imani tuliyonayo wadau wa soka ni kubwa na kama alivyosema magori ni kwamba kama ni ndege ndiyo mwanzo inataka kupaa, na itakuwa vizuri aachie pailoti mwingine wakati iko hewani salama salimini
sir leodgegar chilla tenga upo hapo??
kumbe hili jamaa ni SIR,YES,NIMEKUBALI
ReplyDeleteNanukuu:
ReplyDelete"globu hii ya jamii inaungana na kamati ya utendaji ya tff kumuomba sir tenga asifanye mtimanyongo kwa kukataa kugombea"
Sahihisho:
Ninaheshimu sana wazo la mleta hoja, lakini hili aliwezi kuwa wazo la 'BLOGU YA JAMII' pasipo hata kwanza kuishirikisha JAMII YENYEWE. Pengine ungeomba kwanza hata kupata 'opinion poll'hapa kabla ya kufikia majumuisho.
Angalizo:
Michuzi hii kamwe haiwezi kubaniwa simply kwa sababu natofautiana na wazo la mleta ujumbe!!!
Ndugu wadau naomba niulize swali kutokana na hii Article "Kwamba Tenga Aombwa Agombee Tena" Mwanzo nilivyosoma kichwa cha habari Sikuelewa nilifikiri kuwa ameombwa na Watanzia wote au waliowengi, lakini baada ya kuisoma kwa kina nikaona kumbe ni mtu mmoja wa kuitwa Bw. Magoli, sasa basi kwa kuendelea ni kwamba ndugu michuzi ningeomba hii Article either ibadlike na badala yake iwe "Bw. Magoli amuomba Tenga Agombee tena na sio Tenga Aombwa agombee tena, Kwa uwelewo wangu hii inaonekana kama Bw.Magoli anamfagilia collegue wake kwa kuwa yeye ni Vice President wa Tff. Naomba kuongeza kwamba mimi binafsi siamini ya kuwa Bw. Tenga amefanya mengi ya muhimu ktk masuala ya maendeleo ya soka nchini humo, kama Uwanja ni msaada wa Japan na kwa maana hiyo ni hivi juzi tu Rais Kikwete ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya japan kwa msaada wao wa kutujengea uwanja, Na kama maendeleo ya soka ndio kabisa kachemsha pale tuliposhindwa kuwafunga Msumbiji ktk harakati za kucheza fainali za kombe la mabara ya Afrika. Hapa naomba nitoe duduku kwa kukilaumu chama cha soka kwa kulazimisha kuichezesha mechi ya mwisho muhimu katika kiwanja hicho kipya hali ambayo sisi wenyewe yaani (wachezaji wetu) hawajakizoea kiwanja hicho. Tukiangalia tu tunaona uongozi huo wa Tenga na wenzwiwe ni upumbazi usioweza kusahameleka kwani ni sawa na ulimbukeni wa kuonyesha kuwa tuna kiwanja kizuri lakini end of the day tumeshindwa kukitumia that`s useless,what the point of home ground? (Kiwanja cha nyumbani)? Ni sawa na kuhamia nyumba mpya, na imani kabisa siku za mwanzo itakuwa ngumu sana kupata usingize kwani hata choo chako utakuwa ukijui kiko ubazi gani. Natumai mechi ile ambayo tulihitaji ushindi mmoja tu ku-qualify laiti kama tungeipeleka Mwanza natumai ni ushindi mkubwa sana ungepatika na na Tanzania tungeliweza kufikia ktk Fainali za kombe hilo la ubingwa wa Afrika. Sasa leo kusoma Article hii na kuona mtu mmoja kwa interest zake anataka ku-force Tenga aendelee,... mimi binafsi nalipinga katakata. Kukubaliana na swala hilo ni kuendelea kuamini kwamba Nchi yetu yakuwa haina wenye mwamko wa soka na badale yake imejawa na wapumbavu wakutosha. Naomba ndugu wadau tuliangalie suala hili kiundani na tuonyeshe kwamba tumechoka na hao Mafisadi waliojaa kila pembe ya nchi yetu. Sina chuki na Bw. Tenga mimi kijana wa miaka 35 na Tenga anaweza akawa km Babaangu lakini twende na wakati uongozi sio ufalme sasa km ni hivyo kwa nini basi tuendelee na sura hizo hizo karne na karne? Tanzania ni nchi yenye population zaidi ya watu milioni 44 sasa ina maana hakuna watu wengi ktk hizo milioni zote wakuweza kupata hizo chance za kujaribu ideas zao? Au tuamini hao kina Tenga tu ndio singled out? ahhhh tuache hizo.Ndugu Tenga naomba miaka yako ikiish utoe chance kwa wengine nao, na wala usisite pale utakapoombwa Ushauri na hao viongozi wapya. Ahsanteni mdau Mbegu, Reading, UK
ReplyDeleteMichuzi.
ReplyDeleteHivi zile katiba za TFF mikoa zimekamilika? Hivi kuna utaratibu wowote wa kuhoji mambo yanayotokea ndani ya TFF? Sina tatizo na watendaji wa TFF bali mfumo mzima ni kizungumkuti. Mara wanafukuzana, wanafitiniana FIFA, wanatoa maamuzi kuegemea klabu zao. Tazameni Uganda na Kenya kila mashindano makubwa wanapiga hatua, sisi mmhh.Sasa tufanyeje tubadilike? Wadanganyika amkeni.
Mdau wa Soka, Dar.
Wadau nisaidieni nielewe. Huyu Bw. Tenga amepewa na nani hii heshime ya kuitwa Sir na amepewa lini ? Au ni kama wale wanaobandika mabango na kujiita Profesa Nanihii na kudai wanatibu matatizo ya kukosa bahati au kupandishwa cheo?
ReplyDeleteNaomba kuuliza: Bwana Tenga mie najua kuwa ni Mhandisi, Je hicho cheo cha "Sir" amepewa na nani? Ninavyojua hiki cheo mtu hupewa na Mfalme/Malkia wa Uingereza.
ReplyDeleteNawasilisha.
Sishangai sana kuona wajumbe wa kamati ya utendaji kumpigia debe tenga kwani wananufaika na uwepo wake hata yule aliyeondoka alimudu kuwepo pale kwa muda mrefu kwa kuwa kamati tendaji ilikuwa inanufaika na uwepo wake lakini hakuna jambo la kujivunia alilolifanya Sir kama si mkono wa serikali , nadhani sote tunakumbuka tff iliposhindwa kutafuta kocha ambaye serikali ilishakubali kumlipa mpaka serikali ikabidi iingilie kati
ReplyDelete