Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Bi. Tunu Kavishe akimkabidhi vitabu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla wilayani Kilolo mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. Zain ilitoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya sh. milioni 18 kwa shule 18. Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Bi. Anna Msolla.

Walimu wa shule 18 za Wilaya ya Kilolo wakipiga picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla (wa tano kushoto nyuma) baada ya kukabidhiwa vitabu wilayani Kilolo mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Bi. Tunu Kavishe

Waimbaji wa kikundi cha sanaa cha Ilote Special cha Ilula kinachohamasisha utunzaji mazingira na mapambano dhidi ya UKIMWI, wakitumbuiza wakati Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania ilipotoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya sh. milioni 18 kwa shule 18 za Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa mwishoni mwa wiki.

Kampuni ya simu za mkononi yenye mtandao katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, imetoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya sh. milioni 18 kwa shule 18 za Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Vitabu hivyo vinavyotolewa katika programu ya Zain ya Build Our Nation (BON) kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini, vilitolewa mwishoni mwa wiki mjini Kilolo na Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Bi. Tunu Kavishe aliyemkabidhi Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla.

Shule zilizokabidhiwa vitabu na majina ya walimu waliowakilisha shule hizo katika mabano ni Shule ya Sekondari Lukosi (Mwalimu Naboth Mlemka), Shule ya Sekondari Masisiwe (Romwald Boniface), Shule ya Sekondari Lulanzi (Lugarata Ng'weshemi), na Shule ya Sekondari Mtitu (Hassan Msungu).
Zingine nie Shule ya Sekondari Kilolo (Seraphina Chodota), Shule ya Sekondari Selebu (Nolasco Mdewasmi) na Shule ya Sekondari Dabaga (Anderson Ndelwa). Nyingine ni Udzungwa (Vallence Kihwanga), Shule ya Sekondari Ukwega (Labrey Urassa), Shule ya Sekondari Kitowo (Charles Myanga), Shule ya Sekondari Madege (Charles Chang'a), Shule ya Sekondari Ilula (James Anyandwile), Shule ya Sekondari Nyalumbu (Secilia Myinga)
Pia Shule ya Sekondari Irole (Yahya Mpongwe), Shule ya Sekondari Mazombe (Heshima Kasuga), Shule ya Sekondari Uhambingeto (Selsus Mwilike), Shule ya Sekondari Udekwa (Alto Kinunda) na Shule ya Sekondari Mlafu (Selemani Motto).

Akikabidhi vitabu hivyo, Bi. Tunu alisema Build Our Nation ni mradi wa Zain Tanzania wenye lengo la kusaidia na kuwajibika kwa jamii ambayo imekuwa ikichangia vitabu kwenye shule za sekondari kwa mikoa yote 26 ya Tanzania, ili kuhakikisha kiwango cha elimu kinaongezeka Tanzania.

Bi. Tunu alisema Zain imedhamiria kusaidia jamii na itaendelea kufanya hivyo ikiamini mchango huo katika sekta hii utasaidia kukuza kiwango cha elimu Tanzania na kuboresha maisha ya wanafunzi.

Naye Profesa Msolla aliipongeza Zain Tanzania kwa mchango huo na huduma inazotoa kwa jamii, hususan sekta ya elimu, na akatoa mwito shule za sekondari ziendelee kujengwa katika Kata za Wilaya ya Kilolo yenye shule za sekondari 31, kati ya hizo 20 zikiwa za Serikali na 11 za binafsi na mashirika.

"Natoa mwito kwa wana Kilolo, wenzetu wanapotembea, sisi tukimbie ili tuwapite. Wilaya yetu bado changa, lakini kwa hatua tuliyopiga mpaka sasa, hata wilaya kongwe za Mkoa wa Iringa kama Makete na Ludewa sasa tumezipiku.

“Elimu bora ndio urithi katika dunia ya sasa ya utandawazi na ushindani, na Serikali pia inaamini mchango wa Zain katika sekta hii muhimu utasaidia kukuza kiwango cha elimu Tanzania na kuboresha maisha ya wanafunzi wetu na kusaidia kuimarisha uchumi wetu karne hii ya sayansi na teknolojia, asanteni Zain kwa mchango huu,” alisema Profesa Msolla.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo, Bw. Bosco Ndunguru na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Bi. Anna Msolla, walitoa mwito kwa wazazi kuwa wachochezi wa elimu.

Zain Tanzania ilizindua programu ya ‘Build Our Nation’ Mei 10, 2004 na programu hiyo inadhihirisha uwajibikaji wa kampuni hiyo katika kusaidia kuinua elimu nchini.
Mradi huo umegawanywa katika awamu nne ambapo ya kwanza, shule moja kutoka kila mkoa inachaguliwa katika bahati nasibu inayoendeshwa kwa kompyuta ili kupata vitabu vyenye thamani ya sh. milioni 1.

Hii inaiwezesha Zain kuepuka uteuzi wa upendeleo kwa shule husika, na kutoa kipaumbele kwa shule zote. Katika kila awamu, shule 26 zinachaguliwa kutoka mikoa yote Tanzania.

Baada ya kuchaguliwa, Zain inapata orodha ya vitabu vinavyohitajika zaidi katika kila shule, na inachukua jukumu la kununua na kuvikabidhi.

Bi. Tunu alisema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu 2008, Zain itakuwa imetumia zaidi ya sh. milioni 500 katika kutekeleza programu hiyo na zaidi ya shule za sekondari 516 zitanufaika kutokana na mradi huo.

Katika mradi wa BON, pia Zain inatoa ofa ya kuwasomesha wanafunzi wanane bora wa kike na kiume wanaopata ruhusa kutoka vyuo vikuu nchini. Kufikia mwishoni mwa mwaka 2008, Zain itakuwa inasomesha wanafunzi 31 katika programu hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mosi, asanteni sana Zain kwa kutoa msaada wa vitabu kwa shule zetu.

    Pili, nimemzimikia Tunu Kavishe, height OK, figure OK, pia inaonekana na upstairs zimo! Je ameolewa? Kama hajaolewa something serious can take place. Kama ameshaolewa, basi namtakia maisha mema ya ndoa!

    Mdau,
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  2. Mdau huyo alikuwa anaitwa Tunu Towo amebadilisha sasa ni Tunu Kavishe kwa maana hiyo ni mke wa jamaa mmoja anaitwa kavishe umechelewa kidogo sana kama mwaka hivi

    ReplyDelete
  3. jamani huyu dada ni meneja gani asiye jua kuvaa mbona bong kusuka sio dili hivyo. sasa tuliomtoni tutasemaje maana vitambaa vya kichwa kilamahara mpaka ana boa. nadhani unahitaji makeover dada. mdau uk.

    ReplyDelete
  4. Acha ushamba hujui huu ni mwezi mtukufu wanawake wote wa kiislamu wanafunga vitambaa kichwani

    ReplyDelete
  5. Hivi zain ni CCM mbona rangi zao sawa. Hebu balozi wao tueleze...maana ya kuwa balozi ni kulitangaza jina lao...sio bure manake ubalozi always unakuja na package.....maana ya hiyo color ya kijani ninini?

    ReplyDelete
  6. Mdau Anon 12:22 PM

    Kwa taarifa yako huyo Tunu unayemfundisha eti kwasababu wewe uko nje ya nchi mwenzio amekaaaaaa marekani amechoka sasa amerudi mwaka juzi kutafuta zake maisha bongo pia Kitambaa ni mwezi mtukufu pili mavazi ni pendeleo la mtu sio ushamba watu wengi hawainvest kwenye mavazi wanainvest kwenye kichwa na maisha ya mbeleni sasa sijui wewe vipi wewe uko kwenye kundi lipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...