mwenyekiti wa umoja wa afrika JK na mfalme mswati III wa swaziland washangilia wakati mpatanishi wa zogo la zimbabwe rais thabo mbeki wa sauzi akimpongeza morgan tsvangirai kwa kufikia muafaka wa kuunda serikali ya mseto huko kw jongwe leo
mezea mzee....anaonekana kusema rais robert mugabe wa zimbabwe wakati akibadilishana nyaraka za mapatano ya kuunda serikali ya mseto na aliyekuwa hasimu wake mkuu morgan tsvangirai (hutamkwa shangirai) leo huko harare kwa jongwe
sio wote dam dam na mambo yote ni mswano sasa.... rais thabo mbeki wa sauzi akiwashikisha mikono rais robert mugabe, morgan tsvangirai wa chama cha mdc na profesa arthur mutambara wa chama cha mdc-m baada ya kumwaga wino wa kuundwa kwa serikali ya mseto kumaliza zali mchana wa leo huko harare. picha na mdau freddy maro wa ikulu.
habari kamili nenda www.dailynews-tsn.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Kaka Michu,

    Naomba unibandikie haya masikitiko yangu.
    Inasikitisha sana kuona Raisi kikwete akishangilia suluhisho la kistaarabu la mgogoro wa Zimbabwe wakati hapa kwakwe wamefanya kila njia kukatisha tamaa juhudi za kumaliza matatizo ya kule zenji kwa njia ya amani.

    Iweje Mhe. Kikwete ashindwe kutumia nafasi zake kama Mwenyekiti wa AU,Raisi wa TZ na mweyekiti wa chama tawala CCM kuingilia moja kwa moja sula la kumaliza mgogoro wa zenji ambao umedumu kwa zaidi ya miaka kumi?
    Mbona Mugabe pamoja na ukorofi wake hakutoa kisingizio cha kutaka kufanyika kura ya maoni kwanza kabla ya kuundwa serikali ya mseto?
    Kwa nini tunataka mpaka watu wauwane ndio tutafute suluhu? Nina hakika ikiwa watu wataanza kuuwana kwa wingi kule Zenji basi haraka Raisi Kikwete atashughulika na atapata ''pressure'' kubwa kutoka nje.Ni aibu jamani.

    ReplyDelete
  2. KIKWETE WE CHEKELEA TU NAKUPIGA MAKOFI, 2010 WAKINA LIPUMBA LAZIMA WAANZE KASHESHE NA KUTAKA POWER SHARING AGREEMENT..

    YETU MACHO

    ReplyDelete
  3. HONGERA RAISI KIKWETE KWA KUMWAMBIA MZEE BUSHI KWAMBA HAYA MAMBO TUTAYAMALIZA HII NI SIFA YAKO YA KIPEKEE DUNIA HAITA KUSAHAU KAMWE. NA BIRTHDAY YETU INAKARIBIA OCTOBER 7 INABIDI TUALIKANE TUPONGEZANE VIZURI

    ReplyDelete
  4. hayawi hayawi...sasa yamekuwa. Wadau wote waliokuwa wanamsifia Jongwe sasa mmpo wapi? Kina G7 hao na kadhalika. Ubabe haudumu na haukupeleki popote. Tchangarai 4 life.
    Hawa jamaa historia yao inaanzai mbali kweli...kwanzia enzi Tsvangirai akiwa Union leader. Jongwe alituma watu waje kumtosa kutoka ghorofa ilipokuwa ofisi yake. Ukitaka kujua zaidi soma kitabu kinaitwa "The Shackled Continent" by Robert Guest chapter inayoongelea Zimbabwe. Jamaa katoka mbali huyu...si mchezo. Big up sana! Change for 4 life...sio kila siku status quo tu. Mugabe angejiuzulu tu...sasa atatoka kwa aibu. Kina Nyerere wajanja...waliona boti inaseremeka 'wakang'atuka'(neno alilolitunga mwenyewe)...yeye anabaki...kudadadeki. Safi sana Tsvangirai.


    mtoto

    ReplyDelete
  5. mugabe kafunga bao la kisigino hapo. watu wote walijua kibano alichokuwa akipewa na uk na usa angeachia ngazi. lakini wapi!!!

    sasa tuone kama uk na usa hawataondoa vikwazo walivyokuwa wamemuwekea mugabe.

    sasa ukweli ndiyo utajulikana kwamba tatizo halikuwa mugabe, bali vikwazo na hujuma za uk na usa.

    tayari dr.kaberuka, raisi wa adb, ameshaahidi msaada wa 1 billion usd kwa zimbabwe.

    ReplyDelete
  6. JK shangilia makubaliano yaliyofikiwa huko Zimbambwe kwani wewe ni kiongozi wa Afrika.
    Kuhusu mgogoro wa Zanzibar, JK pamoja na CCM yake siyo kikwazo sana ila kikwazo ni CUF na Maalim Seif (Madevu) na tatizo kubwa katika hili ni kwamba wapemba wanataka kujitenga na unguja na ndiyo maana hawataki wagawane madaraka. Mimi nadhani mgogoro wa Zanzibar utaisha pale tu wapemba na waunguja watajiona wote ni sawa, wana haki sawa na hapo ndipo watakapopuuza ubinafsi wa wanasiasa ambao wanatumia mgogoro kama agenda zao. Ushauri wangu kwa wanzanzibar ni kwamba msitumiwe kama muhuri na watu wachache kwa manufaa ya wachache (viongozi wanasiasa) ambao kazi yao kila siku ni kufanya mbinu chafu ili waendelee kubaki. Pia kumbukeni Zanzibar siyo ya CUF wala CCM bali ni ya wanzanzibar wa juzi, jana, leo, kesho na keshokutwa hivyo basi njia pekee ya kuifanya kuwa bora ni kukubali tofauti zenu za kimawazo ili nchi yenu (sorry kumbe zanzibar si nchi! tehee!!! teheee!!!) iwe bora.

    ReplyDelete
  7. kama mwafrika nashukuru kuwa kuna suluhisho lililofikiwa kwani hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya na ni wananchi wa kawaida kama mimi na wewe waliokuwa wanaumia. Lakini kwa upande wa demokrasia, huu mtindo wa kugawana madaraka sio mzuri kwa Afrika. Hii itaendekeza tabia ya viongozi walio madarakani kung'ang'ania na kuleta ubabe pindi washindwapo uchaguzi, ili mwisho wa siku mshindi halali anyuooshe mikono na kukubali uwaziri mkuu au umakam ambao huwa haumpi madaraka sawa na aliyeshindwa. Kuna waangalizi wa masuala ya kisiasa walilaumu kitendo cha Raila kukubali uwaziri mkuu na kusema inajenga mazoea mabaya. Haya tunayaona sasa Zimbabwe pia; sijui nani watafuata baadae. Afrika tujifunze kuwajibishana na kukubali demokrasia ya kweli

    ReplyDelete
  8. Hakuna mpya hapo, it is long said, if you can not change the system...you better join it.

    African democracy is different from any other democracy, and it should be different kwani we have different history.

    G7
    !!!

    ReplyDelete
  9. hehehe...G7 bwana. Wewe hapo unaona nani kashinda...Mugabe au Tsvangirai? Mugabe ndo ka-lost...jamaa alijifanya mjanja mara sijui nini na nini...kudadadeki. Kimebaki kuzomewa na watu wake wenyewe. Iyo ni aibu sana.
    Unanifurahisha na idea yako ya Africa's democracy is different from other democracies. How is it different?

    mtoto

    ReplyDelete
  10. siwezi kushindana nawe kwani umesema hapo before kwamba Tchangarai for life. Ndio maana before nilikuuliza are u kidemu? sidhani kama mtu mwenye akili anaweza kusema mimi fulani for life, kawa mumeo? or mungu wako?
    Nadhani jamaa na wazungu walitaka mugabe amuachie kila kitu, africans through our democracy tukasema no... we no what can be done there!! na leo muafaka. unadhani muafaka unapatikana kwenye democracy za wazung??

    ukikua utajuwa mtoto!
    G7
    !!!

    ReplyDelete
  11. tehehehe...unaendelea kuonyesha unanga wako G7. Ni kweli hizo masters huko wanagawa sasa. Ni chuo gani hicho unasoma tena? Na shule haisaidi mtu kama anabaki na fikra duni!
    Unajua maana ya democracy au hujui? Inabidi ukasome kwanza maana yake alafu ndo uelewe topic zaidi. Nimekuuliza African democracy unayoitaja taja ni nini hasa...kimya. Unaropoka vitu tu ili mradi uonekane msomi. Hio ni sign moja ya kuonyesha ujinga. Wewe eleza African democracy ni nini tuendelee na debate.
    Alafu kila siku matusi hayo hayo...duh!! Itabidi tukupeleke kwenye shule ya kashfa...ujifunze angalau variety ya kashfa usiwe unabore watu bure.
    Ninaposema Tsvangirai for life...wewe unashida gani? Freedom of expression hiyo...au huelewi na hicho pia? Unajiita msomi...kha!
    Wewe unaelewa maana ya serikali ya mseto. Alafu na umuhimu wa kuwa na upinzani wa serikali? Au ni kelele nyingi tu zisizojua kitu. Maliza kulipia hiyo masters yako ndo uje kwenye debate forum tukufunze vizuri.
    Kinachosikitisha zaidi ni watu wanaoenda kusoma nje kubaki na fikra duni zile zile.
    Mtoto ni alias ninayotumia katika kuchat. Mimi sijali kama utaikebei. mtu anayemkebehi mwenzake in a blog bado ana fikra duni zile zile...hehehe

    mtoto

    ReplyDelete
  12. This is called "THE MODEN AFRICAN DEMOCRACY' ukishindwa uchaguzi unagoma kupokea matokeo, then zinapigwa, watu wanakufa, mnashare power, maraisi wanachekelea life goes on. Au vipi Mimposi?

    ReplyDelete
  13. Ndio maana nimekuambia wewe Tchangarai for life sibishi. go on.. lakini unatakiwa ujuwe maana ya for life. Kwa wakristo kiapo hicho hupeana wakati wa kuoana wakimaanisha for mabaya na mazuri. kwenye sport watu husema wakimaanisha kwamba whatever happens hawezi kuhamia timu ingine.. sijawaona watu wenye akili timamu wakisema ronaldo, bush or any for life, and that is why nikashangazwa na freedom of expression... unajuwa hata fools have their freedom ndio maana nikasema hongera.
    Kuhusu democracy ya Africa nadhani ni very open. Dunia na democracy inatekelezwa tofauti. Mfano nani kamchagua Gordon brown? why Algore hakushinda wakati popular vote alipata nyingi USA? .... hapo utaona kwamba democracy inatekelezwa tofauti duniani, sio wote wanatumia same approach.
    Hata ukitumia akili ya mjinga jiulize kama dunia inataka democracy, how come umoja wa mataifa inawanachama wenye VETO? how many times maamuzi ya UN yanapinduliwa na mtu mmoja kwakutumia VETO? is that person a dictator?--hapana kwasababu democracy ya UN inaheshimu wenye nacho.. same to african democracy kwamba tukiona kibaraka hatumamini then hatumpi nchi yote bali tunashirikiana naye.. kwa nchi ambazo tunawaamini walioshinda tunawapa!
    Unajuwa mtoto sio lazima kila kitu usikie kwenye kitabu, redio ndio uelewe dunia inaendaje kwani waandishi wa vitabu ni kama wewe tu.

    ukikua utaelewa mtoto!!!!
    G7
    !!!!

    ReplyDelete
  14. Kweli nanga ni nanga 4 life...hehehe
    Naona umeamua kuwa technical na hiyo phrase ya 4 life. Nikusahihishe kidogo basi...kwenye marriage vows...hawasemi 4 life bali wanasema "mpaka kifo kitakapotutenganisha". Sasa kama wewe uta-argue kuwa hiyo inamaanisha ni 4 life...kila la kheri. Alafu ngojea nikuulize...watu wangapi wanaosema timu fulani ya mpira 4 life huwa wanakuja kubadilisha badae? Wengi sana tu. Kitu kidogo wanabadilisha timu. Hata ndoa zenyewe ambazo unadai zinatumia maana hiyo hiyo nazo hazidumu. Mbona mahakama zisikushikie katika huo mkataba ulio-sign katika ndoa 4 life? Zinajua kuwa hiyo ni expression mtu anatoa ikiwa haina umuhimu wowote. Its just an expression to show support. Wewe kama umeamua kuichukulia kuwa ukweli...kila la kheri. Unaendelea kutuonyesha fikra duni zako za kuchambua mada hapa...hehehe
    Tsvangirai akifanya ujinga nime-support ya kazi gani? Mimi sijawa wewe ushindwaye kuona ujinga wa Mugabe na kubaki kum-support. Unabaki ukiimba wimbo huo huo...ukoloni mambo leo.
    Alafu nani alikuambia kuwa UN is a democratic organisation? Nionyeshe kifungu kinachosema ivyo katika katiba yake. Umesikia hii ni kama EU yenye parliament...tehehehe. WACHA UNANGA WEWE!
    Wewe Bush kushinda Urais na Gordon Brown kuwa PM zinatokana na katiba zao walizotunga wao na kuona zinawafaa wao. Na kwao zinafanya kazi vizuri na kuwapa maendeleo. Nitajie moja katika bara la Africa inayofanya kazi vizuri?
    Alafu nadhani unachanganya a republic state na democracy. Kwa nini TZ inaitwa republic na Uingerez/US haziitwi Republic? Soma zaidi mwanangu...upate ujuzi zaidi...alafu ilipie iyo masters vizuri uweze kwenda kudanganya nayo watu bongo. Wanakuuzia kiasi gani...na mimi nipate ya pili aise?
    Nani mwenye nguvu zaidi Uingereza? PM au bunge?...hehehe. HUJUI!
    Alafu nikuelimishe kidogo...Africa haiwezi kuhesabiwa kama moja. Nina pinga sana watu wanaotaja Africa kama jumlisho la watu wote, sera zote, nk. We are all very different.
    "Tukiona kibaraka hatumpi nchi yote"...msijiite kuwa mna democrasia basi ili kieleweke vizuri...au sio mzee wa kununua masters...hehehe

    mtoto

    ReplyDelete
  15. Nadhani mtoto hujavunja ungo bado!!
    Ukilala soma tena comment zako and relate na hoja zangu!!!
    1. republic state vs democracy??? vinafanana nini hivi????tofauti kabisa... they are two different concepts... wala sijatumia hayo maneno kimsingi mmoja.

    2. Soma tena uelewe jinsi gani nimeihusisha democracy na UN, pia hizo nchi zingine. (nilikuwa nakuambia kwamba sio wote lazima tufuate democracy kama ya nchi fulani na ndio maana hao wakubwa nao wanatofautiana jinsi wanavyo itekeleza!) SOMA- ELEWA- JIBU

    3.Literary for life means mpaka kufa, so kama unatania then its you!!!
    4. kuhusu success ya implementation ya democracy africa compared na ulaya na nchi zingine? well fanya uchunguzi wakina, mimi siwezi nikutafunie nikutemee kama kinda...

    5. Nashangaa mpaka leo unafikira za kibumbuazi mtoto. Hivi kuna degree or shule isiyonunuliwa? mawazo finyu, mpaka usome kitabu ndio ujuwe imeandikwa. sikiliza, vitabu, reports journals na kila kitu kinaandikwa na watu kama wewe. so usidhani kama kitu kikubwa saaana, na ndio maana utaona kila siku baada ya new discoveries wanabadili some few things!!!

    well endelea kusoma toka kwa wakubwa zako mtoto, ukikuwa utajua.

    G7
    !!!!!

    ReplyDelete
  16. Na ungo wa mamako ulivunjika mwaka gani...59?au...hehehe
    Wewe hata hujui unaongelea nini! Inaelekea unafikra finyu sana. Ndo maana nakwambia tena...malizia kununua masters yako ukadanganye nayo watu Tz. Alafu mbona hutaji
    chuo gani hicho tuje na sie tupate za bure? Maana unabiga boksi alafu wapeleka hela tu kupata cheti...hehehe
    Wala hata siwezi kukupotezea muda wangu kukuonyesha tofauti katika miundo mbalimbali ya democracy...which a republican state is one of them. Ndo maana haiitwi republic of USA...HUELEWI?
    Sababu niliyosema ivyo ni kuwa wewe umedai kuwa Al Gore alishinda popular vote. Sasa kasome vizuri kuhusu mambo ya electron vote ndo uje uchangie mada. Alafu unakuwa mmbishi kweli...mama anakunyima kitamu-tamu nini?...hehehehe
    Wewe sikiliza bwana...Mfano wako wa Marekani na Uingereza umekuwa wa kipumbavu...be a man and face up to your mistakes. Wewe umedai kuwa kuna aina nyingi za democracy na ukatumia hiyo mifano kujaribu ku-illustrate hoja yako. Sasa mimi nimeiponda. Mbona unakuwa fara sana.
    Nikakuuliza kuhusu hiyo idea yako ya democracy in UN...nionyeshe katika katiba ya UN inayosema kuwa ni a democratic organisation. Hata siku moja haijakaa kusema WE ARE A DEMOCRATIC ORGANISATION. Democracy has its limit lakini sio ambacho Mugabe afanyacho. Nikakuonyesha tofauti ya UN na EU parliament. Lakini bado huelewi. Sasa sijui mpaka tukuchoree kabisa. Alafu pia sio lazima uwe member wa UN. Kama hutaki na hupendi idea ya VETO power unaweza kujitoa. Wazimbabwe wanaweza kujing'oa uraia?
    Ndo maana nikamalizia kwa kusema...Hizi nchi zitangaze kabisa kuwa hatufuati demokrasia. You a democracy or not. Power to the ppl 4 life. Hakuna cha African democracy...labda uwizi wa kura tu na ufisadi.

    G7 mzee wa kurukupia vitu...hadi uingereza unaenda kurupukia tu huku hujui chochote. Kha! Ukisikia Mtu mzima ovyo...wewe ndo wawakilisha. Mzee wa fikra duni...tehehehe
    Sasa sisi tukiandika vitabu wewe unashida gani mwanangu?...watu tumesoma...which pays...na watu kibao watafuata ideas zetu.
    we achaga unanga...mimi najaribu kukuelimisha hapa wajifanya mjanja...sawa bwana.
    Kila la kheri na demokrasia yao ya UN...endelea kuitafuta

    P.S: Naona umehofia kutoa any backup to your arguments...maana last time nilikuonyesha ujinga wako na link uliyotoa.
    Nenda shule kijana...uondoe ujinga!

    mtoto

    ReplyDelete
  17. Tofauti yetu hapa nikwamba wewe umezowea kila kitu usome ndio ukariri na ndio uone kina exist. kwamaana ingine u are thinking in side the box. Go on!!
    I will never argue with the fool, I am a gentleman, I know what am doing.. nashangaa that mara nyingi unapenda kujinyegeza kwangu.. mara G7 yupo wapi...binti yatakushinda. Kama unapoint just toa why unakuwa muda wote lazima G7?G7...pumbavu? mentally nadhani unaproblem.

    Napenda kusema mtoto kama umeweza kupass exam hata elimu ya juu basi itakuwa through kutazamia watu. for sure hausound reasonable. Nenda shule mtoto na ukienda basi usome sio ukariri.

    ukikua utajua mtoto!
    G7
    !!!!

    ReplyDelete
  18. sawa balolo G7...usiwe unachangia changia ujinga tena....tehehehe
    Uwe na adabu na heshima kwa waliokuzidi kisomo.
    Na usiropoke ujinga tu..."african democracy"
    Wajifanya unajua kumbe kapa...au tukuite nazi...maana ndani ni maji tu...hehehe
    Nikutafute nakuomba ukoo?hehehe
    Napendaga kusikiliza ujinga wako...nifurahi....alafu nikuelimishe. Am only trying to help u...sio kukufanya uwe mjinga zaidi.

    mtoto

    ReplyDelete
  19. haha, G7 kapatikana. Mi nimekuwa nafuatilia kwa karibu malumbano ya wadau... G7 alikuja na moto na misifa na kujifanya anajua; na dharau kibao. Kaumbuliwa ndio anajifanya gentleman, gentleman ungekuja kwa matusi namna hii?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...