Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Nimegundua kutokana na matukio mengi niliyopata kuyashuhudia, WABONGO HATUJALI USALAMA WETU HATA KIDOGO.

    Yaani tunayachezea maisha kana kwamba tutapewa nafasi ya pili ya kuishi au ukipata ajali na kupoteza kiuongo kiomja wapo cha mwili wako utarudishiwa na kingine.
    Jamani tuwe SERIOUS.
    Kwanza ni kosa kudandia gari kama hivyo,
    pili hana protective gear ya aina yeyote.
    Na tatu anatishia usalama wa mtu anaendesha gari nyuma ya hiyo coaster kwa hofu ya kumgonga kama itatokea akaachia mikono aliposhikilia.
    PUMBAFU MKUBWA.

    ReplyDelete
  2. hili nisemalo sio utani lakini kuna mtanzania alifanya hayo huku uk miaka kama mitano iliyopita. kafika guildfor train alokusudia kuchukuwa kwenda london ishafunga milango na inaanza kuondoka, amini usiamini jamaa aliruka na kusimama nyuma ya treni watu wacha waanze kupiga kelele, salama treni ilikuwa bado haikuondoka yote kwenye platform, dereva akasimama. jamaa akashikwa, kuchukuliwa ndani anajifanya hajui kiingereza kumbe kinapanda ile mbaya, halafu akajifanya kama haoni tatizo liko wapi eti anaonyesha ticket yake na kujitetea kuwa hakutaka kuchukua lifti ya bure!!!!!

    ReplyDelete
  3. Kibaka mwizi huyo mwanangu.

    Mbona hiyo kawaida gari za kwenda Mbagala kwao akina Michuzi.

    Wale mnaopenda kukaa viti vya dirishani mtakoma.Ukizubaa tu anakwapua simu,pochi ya akina mama kama umelipakata,Heleni za dhahabu kwenye sikio,simu au hela kwenye mfuko wa shati halafu anateremka na anatoweka kama umeme.

    Hapo anajipanga namna ya kuwakwapulia abiria wa dirishani kulia au kushoto kutegemea hali ya hewa ikoje.

    ReplyDelete
  4. KATIKA HIO PICHA NAONA KUNA KIPANYA PEMBENI YA COASTER INAELEKEA OPPOSITE DIRECTION.CHA AJABU MBONA ZIKO KARIBU MNO NA HAKUNA HATA MSTARI WA KUGAWANYISHA LENI ZAO? AU NI MACHO YANGU TU? NA JE HIO NI SALAMA? KUHUSU HUYO JAMAA NI WAKUKAMATWA TU.

    ReplyDelete
  5. anon number mbili: niliwahi kusikia stori hii mimi nilidhani ni joke kumbe ni kweli imetokea?

    ReplyDelete
  6. Huu uzembe huu na serikaliinajifanya haioni. mpaka afe mtu ndio wataanza kutuma tume ya uchunguzi...What is this? Traffic wale tunawaona wengi inamaana hawawezi kumshika huyu mtu?
    halafu niliona sijui ni week ya usalama wa barabarani. Hii aonyeshwe mkuu wa usalama na watraffic police wote kwenye njia hiyo walulizwe walikua wamelala au walikua wapi kuachia mtu akae kwenye gari hivi. tena downtown

    ReplyDelete
  7. Wewe subiri adondoke apoteze kiungo chochote halafu akimbilie kwenye mablog ya jamii kuomba msaada wa matibabu hapo MOI. Kwa kweli wabongo hatupo serious kabisa na masuala ya usalama barabarani. hivi inamaana njiani pote hakuna askari wa usalama barabarani? Au kwa wao ni kawaida tu. Acheni maskhara ndugu zanguni.


    Q

    ReplyDelete
  8. Huyu mtu ni mpumbavu, yaweza akawa si kibaka lakini anatafuta sifa na kujifanya kasafiri bure!Kumbe anahatarisha usalama wake kama enzi zile za makonda kuning'inia mlangoni. Na mimi sioni sababu ya kulaumu polisi. Nafikiri ningekuwa polisi mtu kama huyu ni kumshushia mangumi tu mbele kwa mbele kumpeleka kituoni ni kupoteza muda!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...