Home
Unlabelled
ali kiba aiteka new jersy
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
I am not a hater, but lets be realistic. Ukimuondoa Jay Dee, Wasanii wetu wengine bado hawajafikia kiwango cha kimataifa. kuitwa na jamii ya watanzania waishio ughaibuni na kuimba kwenye kumbi za shule, community or local clubs, ni dhihirisho tosha. Linganisha na wasanii kama R.kelly, Usher, TI nk.sehemu wanazopafomu na publicity zake. Naishukuru sana blogu hii ya jamii kutupa picha halisi na matukio, kwani huko nyuma tulipokuwa tukisikia Fulani kaenda kupafomu ughaibuni tulijua bonge la kiwanjaaa!! kumbe ni uchochoroooni tu.
ReplyDeleteCHEAP, CHEAP PUBLICITY NDIYO JADI YETU. HIVI NI KWELI HUYU AMEMZIDI KIWETE JOSE CHAMELION? AU TULAZIMISHANE KUKUBALI KWASABABU TU NI MTANZANIA MWENZETU? HIVI PIA MZEE WA VUNJA MIFUPA MAPANGALA HAONI NDANI KWA HUYU MTANZANIA? JE, NIKWELI TANZANIA INAONGOZA KATIKA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI! KAMA NI HIVYO NA MAJIRANI ZETU WAMETHIBITISHA HILI, BASI TUMEENDELEA SANA, LICHA YA MUZIKI WETU KUTOJULIKANA KWINGINEKO. BONGO TUAPENDA SANA KUJIPA SIFA ZISIZO NA TIJA, MNAMKUMBUKA YULE MHESIMIWA ALIYESEMA `UCHUMI WA TANZANIA UNAPAA!'
ReplyDeletePole pole atafika kiwango cha kimataifa.Kiwango cha kimataifa hakifiwi tu from nowhere,ni kama hivi anavyofanya hata kama anaimba kwenye kumbi za chekechea,kesho ataimba kwenye kumbi za shule za misingi kesho kutwa ataimba kwenye kumbi za shule za sekondari na kuendelea.Ndivyo nyumba inavyojengwa.Nawapongeza sana wanaom-promote huyu kijana.Hao tunaowaona kwenye picha wakicheza I am sure siyo watz tu,kuna watu wa mataifa mengine.Michuzi,I dont know this guy(Ali Kiba) lakini hawa waliobuni hili jambo wamefanya vizuri tuwashukuru.Tunao wasanii wengi tu TZ, baada ya Ali Kiba,kama uwezo utaruhusu, wapeleke na wasanii wengine.
ReplyDeleteNdugu anonymous hapo juu, haijalishi kama wasanii wetu wanaimba kwenye kumbi za shule nk. lakini kumbuka kuwa mwanzo daima huwa ni mgumu. Inabidi tujivunie hata kuona wasanii wetu wamefikia hapo walipo. Tunachotakiwa ni kuwatia moyo siyo kuwavunja moyo, hatimaye nao watakuja ku-perform kwenye kumbi zinazoeleweka hapo baadae. Watanzania tunatakiwa tuwe na umoja pamoja na upendo, siyo kukosoana kila leo.
ReplyDeleteBinafsi namkubali Ali Kiba kwa nyimbo nzuri lakini picha mnazotuonyesha zinaonyesha zilipigwa 05/2008 huku nyie mnadai ni za 10/2008. Msitudanganye. tumieni marketing strastgies nyingine na sio uongo. Balozi wa Zain nawe jaribu kuwa makini na baadhi ya picha kwani zinakuchafulia sifa yako.
ReplyDeleteUkibana comments zangu poa tu kwani nimekuzoea
Nakubaliana na point moja alotowa mchangiaji wa mwanzo, kuhusu sehemu wanazokwenda kufanya maonyesho hao wanaojiita au kupachikwa title sizizowafaa. mimi simpendaji wa musiki na wala siwajui hawa jamaa, lakini sipendi tabia ya kujivunia na kudanganya watu kama mleta habari hii alivyozidisha chumvi. Naam picha hizo hapo zinaonyesha dhahiri sehemu aliyofanya show yake ni kakumbi kadogo tu. sasa kudai kuwa mamia walifika hapo ni kutudanganya. Mia ngapi za watu ziliingia katika kakumbi hicho? ona hata distance baina ya dj, yeye na washabiki wake ni ndogo mno. ona distance ya alipo yeye na yalipo maspika nashangaa hajaingia uziwi. halafu hata sehemu ya kuweka makoti hakuna yaani wanaweka humo humo (ona picha ya mwanzo). picha ya mwisho inaonyesha dhahir ukubwa wa ukumbi huo toka alipo ali mpaka mwisho wa ukumbi. kwa ufupi msitudanganye kuwa wasanii wanapokwenda nje wote huwa wanafanya shoo zao kwenye sehemu zinazofahamika, ilali wanafanya kwenye kumbi za pub na college!
ReplyDeleteWadauu, wajameni mimi ndio nilioanzisha hii changamoto ya kwanza. kama niliyosema I am not a hater.Naungana na mdau mwenzangu, tuwe wakweli, unapojidangaya katika mafanikio yako, unajidangaya mwenyewe. Eti uko juu, wakati bado uko chini, tukiukubali ukweli na media za bongo zikiandika ukweli wa wasanii hawa, watapata challenge hatimaye watafanya kazi super, kama waafrika wenzetu wengine walio juu. Ukweli unabaki kwamba wana -perform kwenye vijikumbi vidogo visivyo na title.wakirudi bongo wanajiona wameshakuwa mega stars.kwa mtazamo huu hatafika.naungana na mdau aliyemsema Mh. (jina kapuni)eti uchumi wa tanzania unapaa!!
ReplyDeleteNakubaliana na wadau wengi hapa kuwa kiwango chetu cha muziki ni kidogo sana. Sio haki kumwita Mwanamuziki huyu Superstar wakati chati yake haijaenda Gold Billboard.
ReplyDeleteTunamtakia kila la kheri ndugu yetu, tunategemea atafika katika Billboard hiyo. Kwa taarifa tu, ni lazima uuze CD milioni mmoja kupanda chati ghorofa moja na Mwanamuziki awe na umaarufu wa kimataifa, yaani awe ana uwezo wa kununua ukumbi wa kutumbuiza watu kwa laki kila kona ya dunia sio mia moja katika ukumbi mdogo wenye taa nadhifu na watu 50. Aluta Kontinua.
ndugu anonymous wa october 06 11:07 ni sawa kuwa haijalishi wanaimba wapi. tatizo ni pale tunapodanganywa, wanaleta taarifa zisizo za kweli kwa nini? ni kwa nini hawasemi tu wamefanya onyesho sehemu fulani watanzania wamejitokeza na limefana, badala ya kujitangazia masifa yasio na ukweli.
ReplyDeleteJamani huo ukumbi ni kajamba nani?
ReplyDeleteUmetoa dala zako unaenda kulundikwa hapo?
Hapo hata ingetokea cheche moja ya moto tu watu wangeuana kama yaliyotokea Tabora.
Hivi USA hawaangalii ukubwa wa ukumbi na watu wangapi watahudhuria?
Yaani hili shoo haina tofauti na shoo za bongo
05/10/2008 ni Tarehe Tano Mwezi wa Kumi mwaka Elfu Mbili na nane lazima saa za afrika mashariki...kwani show lazima ziwe majukwaa MAKUBWA? Mpeni tough dogo...muombeeni mazuri na yeney neema na yeye asaidie wengine wafike mbali.
ReplyDeleteHili swala la ukumbi nimesikia sana likikashifiwa hapa mara nyingi.HIVI unapokodi ukumbi kwa kufanya shoo huwa unaangalia kitu gani hasa? Idadi ya mashabiki katika eneo hilo au unaangalia umaarufu wa mwimbaji?
ReplyDeleteNasema hivi kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiponda ukumbi za nje ya nchi kwamba ni kumbi za vichochoroni.kila state ina idadi tofauti ya watanzania ,wakenya na wa uganda kwahio watu wanapoandaa lazima upige hesabu kwani ni biashara hii.huwezi ukajiingiza gharama nyingi kuchukua hall kubwa wakati watu watakaojitokeza ni wachache kuweka kurudisha hela na kupata faida.
Tuacheni kelele nyingi ,tunajua kwamba "debe tupu aliachi kuvuma" lakini hata hilo debe tupu lenyewe saa nyingine huwa alivumi.
Mdau mzawa
Kimarekani ni tarehe May 18
ReplyDeleteKiswahili tarehe 18 mwezi wa tano
Nyie pigeni kelele, ALI KIBA ENDELEA MBELE. Ndio sio Usher au TI, lakini ni Superstar KIBONGO, na sisi washabiki ndio tunamkubali na nyimbo zake tunazipiga majumbani na kwenye magari, so semeni kumbi na kadhalika, lakini ndio keshatoka Bongo na Kutembea katembea sana duniani, kwa hiyo,let the guy breath,LIVE WITH IT.
ReplyDeleteNyie bwana kila siku mnalilia ukumbi ukumbi ukumbi.
ReplyDeleteWatu nje ya nchi swala la ukumbi sio kama unavyoona wewe. Ukumbi una kodi inayotozwa kulingana na seheme (Zip Code), idadi ya watu wa kuingia, muda wa kufunga na saa za kuuzwa vinyaji.
Kumbi zote za muziki ziko 24/7 active kwa ma-beats yao ya kinyamwezi na sio miziki ya kiswahili , hivyo huwezi enda piga miziki yako ya mduara au njenje au bongo flava hapa hovyo hovyo.
Nenda Bilicanas leo hapo Bongo na upige miziki ya kijaluo au kihaya usiku mzima uone kama hutatolewa baruuu.
Hivyo utaenda kutafuta ukumbi/sehemu, au bar wanayopenda kunywa wajaluo au wahaya au wanyalukolo ,mazense/Temeke au mburahati au Gongo la mboto kuupiga mziki wako na sio down town au Masaki.
same issue na Ali Kiba katika tour US na Binamu katika tour UK.Wenzetu nje hawajali kumbi , wanataka muziki wa waliemleta na sio makumbi makubwa ya miziki.Uliza kwa masaa wanayopiga huku nje wanalipwa bei gani , then linganisha na TZ.Linganisha hilo halafu uelewa kutengeneza dollar $1000 au Pound 900 kwa masaa mawili tu kwa Ali kiba au Binamu tour ni faida kwa nani? then sema TZ kwa masaa mawili huwa wanapata bei gani.
Suala sio kumbi , suala ni watu wamecheza, wamekumbuka nyumbani, na Binamu au Ali Kiba kupata mshiko wake na anasonga mbele kwa mbele na exposure na mambo mampya kiakili, kimziki na kimaisha.
Guys!!!! whats wrong with ya? wanamuziki wa marekani wanaokuja bongo huwa wanaona diamond jubilee one of the cheapest ahll ever !! na bado wanaperfom kuwafurahisha nyie, coz wanaelewa thats what you can afford !!! so its the same thing as Bongo flava artists wanaokuja U.S wanatufurahisha na tuna enjoy , there is no way tuwapeleke Madison sq garden.... kwanza ili iweje?? heee nyie vipi nyie eti ooh local clubs? kama hamjui there is no way 50 cents angefanya concert kwenye ukumbi kama diamond jubilee in America!! wanawaonea huruma tuu!! looo haya kina ali kiba and others njoeni sana Us tunawapenda sna ana tunajivunia kufikia hatua hii ya kuleta our local tanzania artists in U.S !! KWA RAHA ZETU
ReplyDeletekila kitu kina mwanzo wake... i'm so happy that I can now go and enjoy my own TZ music ... away from home.
ReplyDeleteNitaenda hata kama watafanya concert chini ya mwembe.
wanamziki wa marekani wanakuja Bongo kuperfom ukumbi hazini hata AC !! ndo iwe sisi waTZ mamtoni kuenjoy bongo flava kwenye our local clubs???tatizo nini? HAMNA KITU KIZURI KAMA KUPATA FLAVA ZA NYUMBANI UKIWA NJE YA NCHI !!
ReplyDeleteTarehe ni hiyo hiyo ila walikosea kuset time fresh kwenye hiyo camera.
ReplyDeleteJamaa superstar kwa miziki ya kibongo yani kwa maeneo yale amabayo miziki yake watu wanasikiliza na kuelewa mbona mna hubishi wa ajabu na wivu usio kua na maana.sasa billboard imetokea wapi hapa kwenye bongo flava? Some of u need to use ur common sense.
ReplyDeleteKwanza mdau wa october 6th @ 4:25 got it to the point. Huyu artist ametoka tanzania, je mlitegemea kwamba akienda america ataenda ku-perform kwenye a football field or a basketball court? c'mon guys mbona mnakuwa na mentality za mbuzi? na ndiyo maana hata hizo shows 11 zime-target cities ambazo zina population kubwa ya east africans. Na pia mna assume kwamba hizo picha basi zime capture ukumbi mzima? Mimi kinachonishangaza ni kwamba watu wanakaa tu nyuma ya computers zao na kupiga domo, nyanyuka uende kwenye one of his shows, halafu ndiyo utakuwa ume earn haki ya ku-criticize. Kwanza just to let you know, wote hao artists (usher, r.kelly, wyclef, John Legend etc) huwa na wao wanafanya concerts na pia wanafanya shows ndogo tu kwenye clubs. sometimes huwa zinakuwa na watu less 100 depending on the size of the club and the purpose of the show. Waulizeni watu walioenda kumuona ali kiba wawaambie ilikuwaje.
ReplyDeleteKama kuna jambo Watanzania inabidi kujifunza basi ni namna ya kufanya constructive critisism. Kweli kuna mambo ya kuboreshwa lakini tunatakiwa kueleza. Hivi promota gani mwenye akili kamili achukue ukumbi wa bei ghali bila kuwa na hakika ya return on investment?. Jambo la msingi ni kujifunga na kuboresha. Jambo moja ninaloungana na watu wa mlengo wa kulia ni ulewaji wa sifa wa wasanii wetu hivi Mr Nice na Saida Karoli ambao walitingisha Afrika Mashariki wako wapi? Jibu rahisi Kulewa sifa na kuacha kufanya mazoezi na kulenga mbali zaidi. Hapa Lady JD amewashinda.
ReplyDeleteLakini kuna mambo amabayo watanzania tunahaki ya kusifia mziki wa bongo; Kenya Bongo flavor is on top of their music matatu bila bongo flavor watu hawapandi!.
Jinsi ya kufikisha changamoto ni tatizo kwetu tulio wengi. Mtoto kakosea kwenzi!!. Badala ya kuonyesha njia mbadala.
Kwenu wasanii, ni wakati wa kuanzia tovuti na barua pepe za kupata maoni ili muweze kujifunza zaidi.
Positive Thinker
Vichwa vya habari vya magazeti na BLOG za wabongo!
ReplyDelete...amwaga lazi(radhi)
...awacha washabiki hoi
...hapakaliki mtu
...afunika washabiki...
...ateka washabiki kibao...
...mtu nyomi (kibao hata pa kutema mate hakuna)
...hapatoshi
...aendeleza libeneke
...mtu kama kawa
...tambarare
na mengine kibao ambayo sidhani kuna hata mojawapo yanatumika kwenye mitihani ya kiswahili kwa shule za msingi na sekondari huko Bongo.
Media zinazeza kujenga ama kuvuruga kabisa lugha.
Kama hivi inabainika kuwa Kenya na Uganda wanapinania kuzungumza Kiswahili SANIFU na pengine wanaweza kuifunika Bongo na kufanya lugha hiyo imetoka kwao! Mnashangaa! Shangaa na Mlima Kilimanjaro wenzenu wanatangaza ni wa kwao...tupo hapoooo
Kaka Michuzi, BREAKING NEWS, ile blog ijulikanao kama UTAMU imeshafungwa, kweli mimi nasupport sana. Ilikuwa inadhalilisha watu bila sababu. Na kudhalilisha watanzania wanaopoteza muda au kuiba muda wa kazi kuandika upuuzi kwenye ile blogu. Excellent!!!
ReplyDeleteanony wa Oct 6, 11:21, tunashukuru kwa taarifa. Ni kweli nimehakiki mwenyewe, theutamu haipo hewani tena, hii ni habari njema kwa wadau wa blogu tunaopenda kutumia kwa kujenga - kuelemisha, kutaarifu, kuburudisha - na sio kwa kukashifiana na kuweka picha-ngono.
ReplyDeleteKurudi kwenye mada husika, kwanini watanzania tunapenda kujishusha na kushushana? Kuna mdau aliyegusia kuwa tusijipe sifa zisizostahili na kujibweteka. Hili ni wazo zuri; mtu unapaswa ujue ukweli wa kiwango chako, ili uweze kujua wapi pa kurekebisha na ukazane kwenda mbele. Ila tutambue machache yafuatayo:
1. Mara nyingi sifa zinazotolewa za ku-"hype" huwa sio mwanamuziki mwenyewe anatoa, bali ni mapromota na waandishi. Hii ni kujenga hamasa na kuongeza hamu ya wapenzi; na haimaniishi kuwa kweli promota/mwandishi/msanii mwenyewe kweli anaamini kuwa ye ndio mwisho wa dunia.
2. hata mapromota wa nje na wanamuziki wenyewe huwa wanakuwa na maneno ya kujisifia... i.e I am the best, etc, etc. Hiyo haimaniishi kuwa lazima ye kweli ni bora kuliko wote duniani.
3. Usupastaa ni wa kiwango kwa kiwango... na hawa wetu tunawaita masupastaa wa Bongo. Na ni kweli kwa Bongo unakuta wanajulikana sana na kazi yao imekubalika.
4. Kuna mtu kagusia suala la kuwa wanamuziki wetu hawafui dafu kwa jirani zetu. Hii nakataa kabisa; wanamuziki wa Tanzania kiujumla wanapendwa na kuheshimika nchi za jirani. Ninaishi nje, na huku nina marafiki toka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, na wengi wao (hasa kenya) wanawakubali sana Bongoflava artists kuliko waimbaji wa Genge. Kuna wasanii kama Necessary Noise, Chameleo, Bebe Cool, Redsun etc wanaofanya kazi nzuri sana na wanaheshimika A. Mashariki kote. Ila wasanii wetu pia wanatikisa sana, kama Ali Kiba, Matonya, Jaydee, Saida karoli wanapendwa sana nchi za jirani sasa na hata wale ambao wametulia kidogo kama Mr. Nice, walishawahi kutikisa pia.
Pia kiujumla, naona idadi ya wanamuziki wa Tanzania wanajulikana na kupendwa Kenya, Uganda, ni kubwa kuliko idadi ya wa kwao wanaojulikana nyumbani.
5. Suala la ukumbi nje naona limeshajibiwa vizuri, na waliotoa analogy ya Diamond Jubilee wametoa mfano mzuri sana. Kwa kiwango Diamond ukilinganisha na kumbi kubwa za nje mnazotaka kuziona ni bilabila. Hata ukumbi wa chuo nachosoma ni mzuri zaidi mara 100. Pia kumbuke kuwa wanaorganize hizi trip za nje sio kwamba ni mabilionaire. Ni watanzania kama mimi na wewe ambao wamekumbuka nyumbani wakaamua kuleta msanii awatumbuize wakumbuke kwao. Sasa unategemea wataanzia wapi kukodi kumbi kubwakubwa za gharama? Hivyo kama promota/mtoa mwaliko hana uwezo wa kukodi ukumbi mkubwa kwani ni kosa la msanii? Maana Ali Kiba hajakodi ukumbi mwenyewe. Unadhani kama kwa mfano wandaaji wa tamasha wangekuwana uwezo na sababu ya kukodi ukumbi kama Madison Square Ali Kiba angekataa kuperform huko?
Be honesty watanzania tulikua wangapi hapo?
ReplyDeleteNaona watu wengi wamechoka miyeyusho. Aliyeniambia hii kitu ipo NJ alisema ni $20 kufika huko $25....jamani jengo lenyewe lile!!!!!! You guys could do better
Halafu humo ndani kila mtu alikua ....ni sasa...niaje...sema...wachache sana ndio tulikua mambo.....yaani naona watanzania wanapenda kusuuport wakwao lakini kwa mwendo ule...unakwenda ni nyimbo tunazisikia kila siku .....mwenyewe anaingina nakuimba sijui nyimbo ngapi then basi tena .....Aghhhhh
We anony wa mwisho unakuwa mbaguzi hivyoooo hii ni miziki ya afrika mashariki na kati kwa hiyo mambo ya kubagua sujui kina ...sasa...sema...niaje tena hao wanamfeel ali kiba kinoma kwa hiyo kama ukumbi ulijaa inatosha bibie sio kuwa mbaguzi kwanza inahuko NJ kuna wabongo wengi???
ReplyDeletePili...ulitaka aimbe nyimbo ngapi?? atumbuize usiku kucha!!! acha kuongea wewe masaa mawili yanatosha na nyimbo angeimba mpya we ungekuwa unzifeel kweli wewe nyimbo hata hujui kibwagizo chake.....Aksante kwa kwenda though
HAPA JAMBO NI, KWELI HUYU NDIYE BINGWA WA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI? KAMA MWANDISHI ANAVYODAI.
ReplyDeleteWa-tanzania hatuna tabia ya ku-support artists wetu wenyewe, angekuwa ni artists wa kikenya hapo wote mngeenda, au mkiambiwa artist ambaye ana struggle in america anakuja TZ, basi mnaenda, lakini waki-TZ hamuwa support. At the same time siyo lazima ku-wa support, ila pia muache kubonda. kama hamna interest waachieni watu wenye interest wa-enjoy. Hizo zote ni kasumba tu, mnaona vya kutoka nchi nyingine ni bora kuliko vya kwenu wenyewe. mko radhi kuvaa mitumba kisa inatoka majuu badala ya kushonesha nguo. Kasumba tu hizo
ReplyDeleteYou are not a hater but you are trasherer!! Una chochote chuki zimekujaa. Swali; hivi niambie ni wabongo wangapi walioko nje ambao walikuwa wanakwenda au wanasikiliza nyimbo za DDC, Super Matimila, Vijana jazz wakati wakiwa nyumbani?? Jibu; niwachache sana na kama wapo basi kule kunaitwa hakuna choice. lakini ndugu tumefika ughaibuni tumejifunza kuwa hakuna kitu kizuri kama kuthamini chako, kuthamini chako, kuthamini chako. sasa basi huku tulipo sote sasa tunajali nyumbani bila kujali huyu wamasaki na huyu wa TMK. Wote tunapenda Bongo flava, Muziki wa dansi na tunazipiga kwenye redio zetu na magari yetu. Haya ni mapinduzi makubwa sana ambayo mtanzania ana budi kujivunia kwani pindi itakapofika wakati tunaamua kurudi nyumbani basi tutayaendeleza hayo. lakini cha kushangaza wenzetu mlionyumbani ndio kwanza mnauendeleza ubaguzi wa huyu wa wapi huyu wa kule.
ReplyDeleteKusema kweli pamoja na kumiss home l;akini sasa muziki wa nyumbani unavutia. na imefika wakati basi nasi tuwapongeze na kuwatia moyo sio kuwakashifu. Mwisho: najua utaumia;"" Demu wako anapenda bongo falava, dad ako, na wanawehuka Kiba akipaerfom sasa hivi hii haikuingii akilini kwamba jamaa ni mkali??
I am sorry kama umenifikiria mimi niko bias....I am not ...but I needed to vent...ukweli ni kuwa mimi the last time nimeenda kuangalia show ya mtu aliyetoka Bongo ni miaka mingi sana.....na nimekuwa nafeel guilty kila ninaposoma humu kwenye blog kuwa wabongo hatupendi kusupport wasanii wetu....lakini ukweli ni kuwa mimi ninapokwenda ni kama kiu ya maji vile nataka niienjoy only our music for that day....sio nyimbo tunazozisikia kila siku halafu msanii mwenyewe akija anakuja too late na kuimba kidogo ...then miziki hiii hii ya huku inawekwa kumalizia....ukiondoka unakuwa kama umeomba maji ya kunywa ukapewa soda.....
ReplyDeleteKweli wabongo tuko wengi sana NJ ....ila Jersey city ndio sijui mtu huko mimi na kama kitu ni kizuri watu wanadrive more than 100 miles na wala mimi sitajali wakinicharge $100 kwa kiingilio lakini iwe hall nzuri...at least kama concert vile watu tukae tufuahie na kuenjoy msanii wetu....si watu tunaingia broadway shows na tunalipa more than that?.....hata kama ni muimbaji wa sijui bongo flava ...lakini wakiweka kimazingira mazuri I am sure watu wengi wataenda...Ile mazingira ya night clubs sio wengi wanaopenda...ukizingatia umri, professional, personal beliefs etc etc...sasa ikiwa kwenye hall zuri tu na kuweka kama concert na mazingira yanayoeleweka turnout itakuwa kubwa sana.
KIJANA WA WATU ANAIMBA VIZURI SANA NA ANAKIPAJI KIKUBWA SANA LAKINI NYIE MAHALL MNAYOMUWEKA NDIO MNAMVUNJIA HADHI YAKE.
Halafu it was easy for me to point out about our neighbors kwavile walikua wanashari sana mle ndani...kidogo tu ugomvi...sijui nani kachukua kiti cha nani...mara nitakutwanga mimi...mara sijui nani kamshika bibi yake the way he didn't like it ohhhhh ilikua shari....Sasa watu wengine hayo mambo hatujazoea....
Kwa wanaopromote haya mambo wajitahidi kubadili mazingira na watapata watu wengi sana....msanii kutoka bongo sio lazima awekwe kwenye night club environments...