
Mh Balozi na mkuu wa wilaya ya nanhii.......
Mzee katika soma soma yangu ya huku ughaibuni, nimekutana na hii taarifa ya maswala ya Ushindani Duniani katika sekta ya utalii.
Report ya World Economic Forum 2008 inaonesha Tanzania ni nchi ya 88 katika ushindani wa kuvutia watalii duniani, watani wa jadi Kenya na Uganda ni wa 101 na 110 kwa mfuatano(table 1).
Hii inaonesha tumewafunika watani vibaya. Na zaidi ya yote katika kijisekta kidogo cha mvuto wa maliasili kiutalii Kaka tumefunika Dunia nzima sisi ni wa kwanza (table 4).
Nilihudhuria presentation ya Dr Diana ambaye ni Mchumi Mwanandamizi wa UNCTAD aliyoitoa wiki mbili zilizopita hapa chuoni, ameisifia na kuifagilia sana Tanzania na anasema kutokana na mwelekeo unavyoendelea Bongo siku za usoni itatisha katika nyanda za kiuchumi Africa na Duniani kwa ujumla.
Warushie wadau wa Blog ya jamii wajivunie!!!!.
Ila ufisadi ipo issue!!! hahaaahhaaaaa....
Bongo oyeeeee!
Mdauzzz
kungekuwa hamna rushwa za vijisenti ingetisha siku za usoni
ReplyDeleteNi kweli kama anon hapo juu..hali ya uchumi ingeinuka sana kama tungeanza hapo mapema hata kabla ya mambo ya ugaidi kuchafua hali ya hewa..asilimia kubwa ya watalii na hata wawekezaji kwasasa huwa wanajiuliza mara mbili..anyway ni step nzuri tuzidi kujitangaza..
ReplyDeleteTudo Jones(Grumeti Tented)hawa ni watu wenye hela nyingi sana U.S.A hapo Connecticut(CT)Sorry speling if any,wana mpango wa kununua Serengeti so far wameshanunua ardhi kubwa sana Northern Serengeti inaitwa Serengeti Reserve mimi nimefanya kazi huko kwa kweli tunakoelekea wataidevelop sana hiyo serengeti mpaka itapoteza authenticity as Serengeti itakua zoo as a lot of tourist complains about parks like Krouger N. Park in South Africa which is over developed.
ReplyDeleteKuhusu park zetu kuwa overdeveloped in a near future naomba michuzi uweke hewani tujadili na wadau wenye data watueleze,mimi niko tayari kuleta data zangu.
sio mbaya imekuwa nchi ya 88 kama ufisadi"ufisimaji" hauto endelea itakuwa nafasi nzuri lakini inaweza kurudi nyuma
ReplyDeleteanony wa 1:06 kanena. Utalii, Tanzanite, Dhahabu, Gesi, n.k tele. Tatizo ufisadi mwanangu, ufisadi unatuua!!
ReplyDeleteHadi ukokotoaji wa GDP ya Tanzania nashauri urekebishwe kuruhusu nafasi ya ufisadi kupunguza % kadhaa za ukuaji uchumi!!
Tumewekwa mbele ni kama nchi ya kwenda na kujichotea bila shida. Watani wa jadi wanajikomboa kiuchumi na hawataki kutawaliwa ndio maana mabepari wa nchi za nje wanakuja tanzania. Tatizo sio mafisadi, ufisadi ndio matokeo ya mfumo wa kisiasa ya kibepari tunaofata hivi sasa. Wachahe watanufaika na wengi wao ndio watakuwa masikini. Bila shaka nchi hii inaenda pabaya itafika muda watu watahamka hapo ndipo zitakapo pigwa wenyewe kwa wenyewe kati ya mabepari (mafisadi) na walala hoi (wananchi wengi na wanao watetea)
ReplyDeleteNakubaliana na October 02, 2008 12:32 PM.Kenya ndio inayosifika dunia nzima kwa utalii hata Mlima kilimanjaro unajulikana upo Kenya.
ReplyDeletePamoja na machafuko ya hivi karibuni wakenya bado wamfunika mashimo.Sisi tupo wapi?
Ripoti ya Benki ya dunia iliyotoka hivi karibuni inasema kuwa Tanzania ni sehemu ngumu kuanzisha biashara.
Amin amin naapia, ufisadi hautaisha na kasi ya maendeleo itaendelea kudoda if and only if we young people are not MEANINGFULLY involved to take control of our resources.
ReplyDeleteOle wenu mlio madarakani kwa kunyonya jasho la mzee Hamza, bibi Tina, na wengineo walio masikini kama mimi na mnakimbizia vijisenti nje. Vijana tuamke, na wazee walio mlio madarakani badilikeni kwa kutubu na kuungama.
Ubarikiwe ulieleta habari hii na sote tulio na uchungu wa nchi hii ya Tanzania. Amen
Amin amin naapia, ufisadi hautaisha na kasi ya maendeleo itaendelea kudoda if and only if we young people are not MEANINGFULLY involved to take control of our resources.
ReplyDeleteOle wenu mlio madarakani kwa kunyonya jasho la mzee Hamza, bibi Tina, na wengineo walio masikini kama mimi na mnakimbizia vijisenti nje. Vijana tuamke, na wazee walio mlio madarakani badilikeni kwa kutubu na kuungama.
Ubarikiwe ulieleta habari hii na sote tulio na uchungu wa nchi hii ya Tanzania. Amen
Nimefurahi kusikia hili, ila naomba kama utatupa data zaidi kuwa kwa UFISADI sijui bongo tupo namba ngapi.
ReplyDeleteQ