SERIKALI IMELIFUNGIA GAZETI LA MWANAHALISI KWA MUDA WA MIEZI MITATU KUANZIA LEO.
AKITANGAZA HATUA HIYO WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO KEPTENI GEORGE MKUCHIKA, AMESEMA SASA HIVI HAPA DAR KWAMBA HATUA HIYO INAFUATIA KILE ALICHOKIIRA UKIUKWAJI WA MAADILI YA UANDISHI KWA KUJIFICHA NYUMA YA MGONGO WA 'UHURU WA HABARI'
NYUUZZZZZ ZAIDI BAADAYE KIDOGO.
ILA KWA SASA....
HABARI NDIYO HII...
SERIKALI imelifungia kwa miezi mitatu gazeti la kila wiki la MwanaHalisi Kwa maelezo kuwa limekuwa likiandika habari za uchochezi mara kwa mara.
Gazeti hilo limefungiwa kuanzia jana ikiwa ni adhabu kutokana na kuandika kilichoelezwa na Serikali kuwa ni uandishi wa mara kwa mara wa habari za uchochezi, mara ikiwa katika toleo la Jumatano iliyopita lililochapisha habari inayosema ‘Njama za Kumng’oa Kikwete zafichuka, Mwanawe Ridhiwani atumika, Watuhumiwa ufisadi wajipanga’.
Akitoa tamko hilo la Serikali, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika alisema ofisini kwake Dar es Salaam jana kuwa kutokana na mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ameamua kulifungia gazeti hilo.
“Adhabu hiyo inaanza leo, kwa mujibu wa amri ya serikali namba 208A iliyochapishwa na kutolewa jijini Dar es Salaam Oktoba 10 mwaka huu,” alisema.
Mkuchika alisema kuwa katika habari ya mwisho ya gazeti hilo inamgombanisha Rais Kikwete na mwanawe, Ridhiwani na kuleta mtafaruku katika familia; inapandikiza uhasama kati ya Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM na viongozi waandamizi katika chama chake ambao ni aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, Mbunge wa Igunga Rostam Aziz na wenyeviti wanane wa mikoa wa chama hicho.
Pia inachochea chuki na uhasama kwa kulinganisha hali iliyofanya Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini ajiuzulu na hali ilivyo nchini; imetumia vibaya uhuru wa kuandika habari kwa kuvuka ukomo wa uhuru wa mhariri unapoishia na kuingilia uhuru wa wengine; imedanganya kuwa juhudi za kumpata Rishiwani zimeshindikana na bila uthibitisho habari hiyo imedai Ridhiwani anahusika kumdhoofisha baba yake.
Alisema kutokana na habari hiyo ofisi ya Msajili wa Magazeti ilimwandikia barua Mhariri Mkuu wa gazeti hilo atoe maelezo lakini Mhariri huyo alikataa kukiri habari yake ilikuwa ya uchochezi na kueleza kuwa haoni sababu ya kuwajibika kwa habari hiyo.
“Ofisi ya Msajili wa magazeti imekuwa ikiwaita wahusika wa gazeti mara kwa mara na kuwaonya kwa mdomo na kwa maandishi na wakawa wanaahidi kujirekebisha lakini wamekuwa hawatimizi na kufuata ushauri wa Msajili”, alisema.
Katika utetezi wake wa maamuzi hayo, Mkuchika alisema kuwa gazeti hilo limeshaonywa mara tatu mfululizo kutokana na habari zake mbalimbali na kutolea mfano wa habari ilizoandika na kuonywa kuwa ni ‘Miguu ya Rais Kikwete imeota malengelenge’ na ‘Ajali ya Salome Mbatia, Mlengwa alikuwa Zito Kabwe’.
Alisema wamiliki na Mhariri wa gazeti hilo wamekataa kubadilisha mtindo wao wa gazeti wa kuandika habari za uchochezi dhidi ya viongozi wakuu wa seriakli na dhidi ya serikali yenyewe. Kwa upande wa Mhariri Mkuu,
Saed Kubenea alisema kuwa gazeti hilo halijapata taarifa rasmi za kufungiwa bali amesikia kwa watu tu na kuahidi pindi watakapopata watatafakari na kujua hatua ya kuchukua.
Hata hivyo alisema; “Taarifa hizo tumezipokea kwa mshtuko mkubwa. Mimi sikuona kosa kwenye habari hiyo lakini nimeshangazwa na nchi ya kidemokrasia imeziona ni uchochezi kuandika kuwa kuna watu wanataka kumharibia Rais wa nchi.”
Alisema walikuwa wameshaanza kuandaa gazeti la wiki hii ambalo linatakiwa kutoka kesho hivyo kuzuiwa kutawasabishia hasara.
Gazeti hilo linachapwa nakala 70,000 kwa wiki. Mbali na kufungiwa gazeti lake, Mhariri wa gazeti hilo ameitwa polisi kwa kutoa maelezo kwa kuandika habari za uchochezi.
Hata hivyo aliachiwa baada ya kuwekewa dhamana na wakili wake, Mabe Kutokana na kufungiwa kwa gazeti hilo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datoo amesema wameshtushwa na uamuzi huo wa serikali na leo watakutana na kuamua hatua za kuchukua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Huu ni ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari kwani Raisi ndo nani kutoandikwa kuwa anaweza kupinduliwa madarakani kidemokrasia katika chama chake kuna ubaya gani huu ni ujinga sasa CCM inaenda kubaya mnanitia kichefuchefu angaliaeni msije mkalamba matapishi yenu baadae! hii inaonyesha jinsi Mafisadi walivyo na nguvu katika serikali hii. Nakushauri Kubenea uende mbele ya sheria mtumie Tindu Lissu mambo yatanyoka!

    NB: Misupu usinibanie hii comment ukibana wewe ni mwana mtandao!

    ReplyDelete
  2. Vyombo hivyo hivyo vya habari viliposema Chacha Wangwe ameuawa na Chadema hawakuvichukulia hatua hii tunaita 'double standards', imekaa vibaya hii. Mnampa Kubenea umaaarufu mzee gombea ubunge Temeke unachukua chaka 2005 kupitia Chadema. Wana TMK hatutaki upuuzi kama huu!

    mwana Halisi oyeeeee!

    NB: usiniibane hiyo Michuzi

    ReplyDelete
  3. Wapi uhuru wa vyombo vya habari? Hilo gazeti limechapisha habari gani mbaya au ya kashfa mpaka lifungiwe? Inabidi kila kitu kiwekwe wazi.

    ReplyDelete
  4. For news to be credible, it needs three vital things, which are BALANCE, TRUTHFULNESS AND ACCURACY.

    Let's ask ourselves. Do Kubenea stories carry the three mentioned elements?

    If they have, then the government has muzzled the press and should be taken to task immediately.

    But if Kubenea stories were lacking even one of the three elements mentione above, then editor should not be allowed to practice journalism in this country, and Mwana Halisi ought to be banned.

    ===================

    KWA KISWAHILI. Habari yoyote inahitaji Ukweli, uwiano kutoka pande mbili husika, na UMAKINI. Kama habari za Kubenea zilibeba mambo haya matatu, basi serikali imekuwa pumbavu kumfungia gazeti lake na inabidi imwombe radhi na kulifungulia hili gazeti haraka iwezekanavyo. Lakini kama habari za Kubenenea zinakosa mojawapo ya hizi pointi tatu, basi serikali imefanya jambo muhimu kuliadhibu MWANA HALISI. Mpoooo?

    ReplyDelete
  5. Leo Kimboka,

    acha upuuzi kuna uongo gani wa habari za Kubenea? siku zote zina ukweli wewe ni mwana mtandao mwingine sidhani kama una uchungu wa nchi hii!Kama habari zake zina uongo mbona hata Lowassa alinywea kwake! huu ndo tunaita kukandamiza habari na CCM haiipi unafuu kufungia vyombo vya habari bali inavipa unafuu vyama Pinzani. Mchawi wa CCM ni kushiba hela za ufisadi na hizo fedha zina laana zitawatokea puani!

    ReplyDelete
  6. LELO KIMBOKA acha uzushi. Wa wapi wewe? Habari zinazuiliwa pale zinapomchafua mtu jina lake. Lakini kusema habari ya mapinduzi ndani ya chama...kuna kosa gani?
    Ukweli, Balance na Accuracy is for the people to decide. Sasa kwa nini tabloids hazifungiwi? Zinaandika ukweli?
    Ingekuwa inaongelea mapinduzi ya nchi sawa...lakini mapinduzi ndani ya chama. Hii waende mahakamani tu...no need to argue! Tena wanalipwa fidia ya muda wote wanapokuwa hawauzi magazeti...alafu mahakama nayo iburuze kesi...watakoma.
    Fundisha adabu!

    Alafu kama tunaangalia ukweli...kumefanyika investigation yeyote kuhusu hiyo habari?...
    Mbona sijasikia tume ikiundwa? Alafu kama imeundwa mbona hii imefanya kazi haraka namna hiyo...kawaida si miezi sita jamani?...hehehe

    mtoto

    Michuzi usibane comment...plz brother

    ReplyDelete
  7. Jamani tuwe wakweli na waungwana. Mbona the same story iliandikwa kwenye RAI ambalo mmliki wake ni Rostam Aziz lakini hakuna hatua yoyote ambayo serikali ilichukua with the heading " Waziri ajiandaa kumng'oa Kikwete 2010". Wapi uhuru wa vyombo vya habari? Kuna haja ya kuwa na wanasiasa ambao wamekomaa na si kukurupuka tu. Yote yana mwisho wake. Hivi ikitokea yaliyoandikwa na MwanaHalisi yakawa ya kweli, mtakuja kusema nini baadaye?
    Wako wapi wale 11 waliotajwa kwenye list of Shame? walisema wataenda mahakamani; nani kaenda hadi leo. MwanaHalisi iliandika na hakuna gazeti hata moja liliandika lakini ukweli si ulijulikana kama ni kweli. Serikali haiwezi kushindana na nguvu ya Umma na vyombo vya habari pia. Jukwaa la wahariri mpo wapi? Mnaonaje mkiaanza kwa kutoandika habari zozote zinazoihusu serikali hii, nani ataumia???

    Yote yana mwisho.
    "Michuzi plse publish this"

    ReplyDelete
  8. jamani watanzania inasikitisha kuona mambo yanavyotendeka na hasa ukiangalia nchi inaendeshwa kibabe ila kisiri siri.
    tatizo watanzania wamekalia kugombana wenyewe kwa wenyewe kutokana na itikadi ya vyama.

    waswahili wanasema wapiganapo panzi ni furaha ya kunguru maana huwala kwa urahisi kwakuwa wamesha choka.

    na hii hivyo ndivy tulivyo watanzania tunagombana na kujiumiza bila kutafakari tunachopigania ni nini na kwa maslahi ya nani.

    jibu ni rahisi kwa mtu mwenye kutumia akili badala ya miguvu kama punda.

    tunapogombana tunawapa nguvu mafisadi ili kuiba zaidi na kusafirisha pesa nje kwa ajili ya vizazi.

    nasisi majinga kazi yetu kushangilia vyama bila kufikiri kuwa katika kushangilia ndio tunawapa nguvu mafisadi na kuwahalalisha.

    watanzania imefika wakati wa kutafakari na kujua ubaya na uzuri na hata kama umefanywa na wazazi watu maana kutomfichua mtu mabaya yake ni kwenda kinyume na jamii na hata kwa muumba wetu MOLA.
    tumeambiwa tumweleze mtu anappfanya mabaya hata kama ni mzazi wako.

    tuukemee ufisadi na uongo kwa ajili ya manufaa ya taifa.

    Yaani sisi wenyewe na watoto wetu na siyo ya baadhi ya watu.

    leo fujo lizotumika tarime badala ya kutumia busara ya kwenda ikulu kwa raisi na kumuomba kujua lini hatma ya mafisadi itajulikana mahakamani.

    leo gazeti limefungwa mara moja kwa ajili ya kumgusa kigogo lakini ufisadi ambao unaathari taifa zima la tanzania.
    hadi leo serikali imeshindwa kuwatoa hao mafisadi na kesi yao imekuwa isoyo na mwisho yaani hadithi ya buricheka.

    wananchi tuungane pale haki inapotendewa ubaya hata ikiwa mtu mmoja akidhulimiwa maana vimumbe wote ni sawa mbele ya MUNGU.
    MUNGU IBARIKI HAKI NA WOTE WANAODHULUMU TUNAMUOMBA MUNGU AWA HUKUMU MAANA MAHAKAMA YAKO NI YA HAKI ILIYOKAMILIKA AMEN.

    TUACHE TABIA YA KUJIPONDA KWENYE MAGAZETI WAKATI MTU ANAZUNGUMZA HAKI INAKUWA TUNAPOTEZA LENGO.

    ReplyDelete
  9. What else could that Mpachika have done ,skunk? Did you know what Bootlicking was all about? Swali,ni Je,kulifungia gazeti la Mwanahalisi kwa miezi mitatu ndiyo kutaziba watanzania Midomo wasiseme au kukosoa? Fisadi si Fisadi tu hata kwa lugha yeyote,kumbe je!HATUKUSHANGAA KWA HATUA HIYO.Rai walitoa habari kama hiyo pengine mbaya zaidi lakini kwasababu FISADI NA HASIDI WALA CHUNGU KIMOJA halikuwa issue hat kidogo!Labda nimwombe Kubenea kitu kimoja.Kwamba atupe mtandao wake kupitia Blogu hii ili tuweze kuwasiliana naye kwa faragha.Nitoe rai kwa wadau wote wa MwanaHalisi kwamba licha ya gazeti hilo kufungiwa kwa miezi mitatu,Hizo ni sawa na issues,matoleo kumi na mbili ambayo hayatotoka.Na kila toleo labda kuna nakala zipatazo 500,000.Zote hizo ni sawa na nakala 6,000,000.Na kila nakala inauzwa shilingi 300/=.Kwa nakala zote hizo ambazo hazitotoka Kubenea atakuwa kapata hasara ya shilingi 1,800,000,000/= bila kutoa gharama za uendeshaji.Hiyo itategemea ni nakala ngapi za MwanaHalisi zilikuwa zikichapishwa kila toleo.Ni Hasara kubwa na jinsi gani serikali hii isivyo heshimu uhuru wa vyombo vya habari!Kama Kubenea anaweza kutupatia habari za siri kuhusu nakala halisi ambazo zinatoka kila toleo ili sisi wasomaji wake wa kila siku tuweze kumfidia pesa hiyo kwa kipindi chote ambacho MwanaHalisi haitokuwa ikitoka barabarani.Kwamfano mimi sikosi kila nakala ya MwanaHalisi inapotoka.Kwa hiyo katika kipindi hicho cha miezi mitatu au wiki kumi na mbili nitakosa nakala 12 za MwanaHalisi sawa na ambavyo Kubenea atazikosa shs.3,600/= tu kutoka kwangu kwa kutonunua magazeti hayo 12 katika miezi hiyo mitatu.Mimi nasema hivi kwamba niko tayari kumpa Kubenea hizo shs.3,600/= kwa magazeti yote hayo ambayo ningeyanunua iwapo yangechapwa kama kawaida.Vivyo hivyo,kila msomaji makini na wa kweli wa gazeti la MwanaHalisi aliyeguswa na hatua hizi zilizokosa ustaarabu na heshima kwa vyombo vya habarinkila mmoja wenu atoe kiasi hicho hicho cha shs.3,600/= kwa Kubenea ili asipate hasara isiyo na mpango.Vita dhidi ya Ufisadi bado iko palepale!Njia nyingine ni kwa Kubenea kwa kipindi hicho cha miezi mitatu anaweza kupenyeza makala zake kupitia gazeti dada lingine na yeye ni kiasi tu cha kutufahamisha sisi wadau wake ili tulinunue gazeti hilo ili aweze kufidia pesa yake atakayo ikosa iwapo MwanaHalisi haitotoka.Tayari CCM imesha chapwa bakora katika uchaguzi wa Tarime na kushindwa vibaya na Chadema.Hasara walioipata CCM kule Tarime ni kubwa zaidi kuliko hii utakayoipata Kubenea katika miezi hii mitatu!Mungu huwa anajua jinsi ya kumzawadia mtu kwa yale alioyafanya!So Keep Cool!Mwachie yote Mungu!Tuone hiyo 2010 Kikwete ataiweza au CCM wataula wa Chuya?

    ReplyDelete
  10. KAMA NI UONGO AU SIO UONGO AENDE MAHAKAMANI BASI, ACHENI UJINGA SIO KWA SABABU KUBENEA ANAANDIKA HABARI ZA MAFISADI HATA AKIANDIKA UONGO TUMKUBALI TU, ATOE VITHIBITISHO , SIO KUANDIKA NHABATRI KAMA ZA UDAKU! HATA UDAKU WENYEWE UNA PICHA, ACHENI HIZO. AFUNGIWE NIMEFURAHI, HAYA SASA TUONE VITHIBITISHO ASIPOTOA, TUFANYEJE? HATA HABARI ZA MIAKA YA NYUMA TUTAZIAMINIJE???? SERIKALI HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. Serikali ya magaidi CCM inalikoroga sasa. Mbona ndo habari zitatokea kwingine? Wafungie vyombo vyote vya habari sasa.
    Wakumbuke ya Tarime cha mtoto shughuli inakuja 2010

    ReplyDelete
  12. Uhuru wa vyombo vya habari una mipaka yake hawa wajamaa wanaongoza kwa kuvuka mipaka hiyo.safisanaaaaaaaaaa mkuchika

    ReplyDelete
  13. cha kumsadia mwenzetu ni kutuma malalamiko yote katika magazeti ya internationa waone jinsi tanzania inavyo kandamiza haki za binadmu bindi inapowagusa wakubwa.
    times of america na kdahalika pia niko tayrai kutoa mchango wangu

    ReplyDelete
  14. We Kubenea usipoteze muda wako kubishana na Wajinga!Acha watwange maji kwenye kinu.Gazeti la Rostam linawatosheleza!Kubenea tupe namba yako ya akaunti ya Benki kama ni CRDB AU Benki nyingine ili sisi wadau wako tukutumie shilingi elfu tano tano tuone wataishia wapi?Au hata hiyo akaunti ataagizwa Fisadi mmoja akaifunge?Believe me there a million plus of sympathisers outta there!You will recover all your financial losses!Achana na Majinga hayo!Tumia miezi hii mitatu kujipanga sawasawa!Ukija toka unatoka bomba zaidi.

    ReplyDelete
  15. Waifungie na THE UTAMU basi. Mwanahalisi sio mzushi kama wa the Utamu. Duh, kumbe the Utamu inadhaminiwa na Google; ndo maana haijafungwa.

    Google iko wapi?? USA. Huko kuna uhuru wa habari. Mwanahaklisi iko wapi?? Bongo. JIBU MNALO

    ReplyDelete
  16. kama mahodari wa kufunga funga basi nawakaifunge utamu!

    ReplyDelete
  17. Hapa naomba tuelimishane, hivi hawa wanasiasa wanavyowaambia wananchi ahadi ambazo azitekelezeki (Mfano maisha Bora kwa watanzania wote) Je ni nani anawahukumu au anawafungia wasiwe wanasiasa? Je hayo wanayoyasema yanaukweli wowote au ndio sheria kwa watu wengine na wao wanasheria yao wenyewe.

    Huu ni Upuuzi mara ngapi watu wanafanya Kashfa au Wizi wa mamilioni ya pesa na hakuna hatua zozote zinachukuliwa. Inawezekana ni kweli gazeti hilo lieandika habari za uongo lakini tujiulize mara ngapi wanasiasa wanaongopa na hakuna sheria yoyoe ambazo zinachukuliwa ju yao.##

    Mnakumbuka kashfa ya EPA ilipopelekwa bungeni, wabunge wa CCM na waziri wao wa Fedha walipinga kwa nguvu zote kwamba hakuna wizi wowote wa fedha na ilipoundwa tume na kuonekana kunawizi, Ni hatua gani walichukuliwa wabunge wale na waziri wao?

    CCM na Serikali yao ni wapuuzi na hawataki kufanya Fair Game na hii ni mbaya sana itatupelekea Nchi yetu pabaya. Achenu ujinga wenu mbona amuashitaki mafisadi

    ReplyDelete
  18. Michuzi umefurahi sana naona kuona Mwanahalisi limefungiwa kwa sababu wewe ni mshabiki sana wa MAFISADI...Unashangaza sana! Na unaudhi kupita maelezo.

    ReplyDelete
  19. THE ONLY AND LASTING SOLUTION: Let new generation have the control on resources; let CCM ak.a mababu zetu rest in and for peace.

    Ukiona nchi inakandamiza vyombo vya habari tena kwa mambo ya ukweli, IMEOZA. Michuzi, kama kusema nchi IMEOZA nako kutatatiza blog yetu nijulishe nijitokeze wanimwagie tindikali.

    Kuna wakati siamini kama mambo kama haya yanaweza kutokea Tanzania ambako hata khanga zimeandikwa "we cherish democracy."

    Mtafunga mitandao? Is jambo forum existing or not? Mnajiabisha tu. Kulifungia miezi mitatu sio suluhu. Tutaendelea kupata habari kama kawaida. Habari zilianza kuandikwa na wengine, wao mmeaacha, kwa kuwa ni wadau wa kudhamini chaguzi siyo?

    Kwamba, wakidhamini chaguzi mtashinda kila mahali; kuanzia Tarime hadi *&^^&%^&%nyie!

    Kikwete, unapotoka! Hivi kusema kuna njama za kumwangusha kikwete ni kosa gani ndani yake? Kuna tofauti gani kusema hivyo na kusema MBOWE, MREMA, MTIKILA n.k wamakaa vikao tofauti ili wamwangushe Kikwete? Why are you so blind kifikra?

    Nashawishika kusema kuna vitengo vina waandamizi wasio na taaluma husika kupitisha mambo. Hivi, kama MKUCHIKA na wengineo hawakupoteza even muda japo wa kusoma mawili matatu juu ya habari, walikosa washauri? Au walipinga ushauri kwa kuwa wao ni wakongwe?

    Ole wenu wazee wa CCM. Nawaapia, twaja!

    ReplyDelete
  20. Hawa serikali sasa wanapotoka,sijui ni uoga au maana hawa watu si kwamba shule hawakwenda hapana wanaelimu nzuri tu tatizo wameathirika na uchama kimoja eti waziri wa habari anasimama bila haya akisema kwamba habari iliyoandikwa kuhusu Rais Kikwete kutoingia madarakani mwaka 2010 itahatarisha amani ya nchi,italeta ugomvi kati yake na mwanawe pamoja na mafisadi,ni kichekesho sana.Aliposema Makamba kwamba upinzani hawatatawala Tanzania milele mbona ye hawakumfungia mdomo kuongea? msitupeleke enzi ya ukomunisti kwa maana ulisha kufa. Kubenea safi sana cha msingi anzisha gazeti jingine litakalotuhabalisha kwa muda huo wa miezi mitatu likiwa na theme ileile ya mwana halisi.

    ReplyDelete
  21. watu waandika michuzi usinibanie..je mmesikia Bro Mithupu ana koleo cha kubania watu.........

    serikali tu ndio inaweza kukubania pale ukienda sivyo ndivyo!!

    Kwenye blogu ya jamii ukichafua hewa unabaniwa!

    Swali la kujiuliza je Mwana halisi lilichafua hewa!?
    mpita njia!

    ReplyDelete
  22. Kwa mtazamo wangu naona bwana kubenea hii ni changamoto kwako, na wala isikukatishe tamaa. Unajua watanzania bado tupo enzi zilee za magazeti ya UHURU, MZALENDO na DAILY NEWS,yalipokuwa yanaandika habari za mazuri ya chama tawala basi. Nadhani Mh. BAlozi umefanya Daily news kwa muda mrefu na unaielewa hali halisi.Leo Mwanahalisi limefungiwa kwa kusema tu kuna mpango wa mapinduzi ndani ya chama, aaaakh!!! sipati picha nduguzanguni.Any way, tutafika.halafu serikali haini ya kuwa sasa ndio wanampandisha chati Kubenea???Hivi hawa washauri wanamaono gani hasa.

    BIG UP SANA KUBENEA.

    Q

    ReplyDelete
  23. MIMI NAFURAHI SANA KUONA WATANZANIA WA SASA WAMEAMKA, LAKINI BADO NINA WASIWASI KUWA BADO TU WAOGA TUNAZUNGUMZIA GIZANI. MAONI YANGU NI KUWA 2010 IKIJA TUJIPANGE VIZURI TUING'OWE CCM DOLANI TUKIPE CHAMA KINGINE TUONE NIAJE NAO WAKIBORONGA TUWATOWE PIA,2010 IKIJE VIJANA TUKAJIANDIKISHE KUPIGA KURA TULETE CHANGE, IT IS TIME NOW FOR A CHANGE, SIO SIRI CCM TUITOWE. TUTAFANYA KAMPENI KUPITIA BLOGS NA WEBSITE ZINGINE, TUANZE SASA KUFUNDISHA WATU NAMNA YA KUPATA HABARI TOKA BLOGS, HIZI NDIZO ZITAKUWA SILAHA ZA MAPAMBANO YA UCHAGUZI CCM WAMECHOKA NA WAMEJISAHAU, TUWATOWE DOLANI- MICHUZI USIBANIE HII, USIOGOPE KUNYIMWA TRIP NA WAKUBWA, HAYA HUSEMI WEWE NASEMA MIMI HAYAKUHUSU KABISA. NATAKA KUFIKISHA UJUMBE KWA WANAHASIRA WENZANGU

    ReplyDelete
  24. Mie naona ni sawa tu. Pamoja na kwamba baadhi ya makala zake huwa ni nzuri, tatizo kubwa la kubenea ni kwamba katika baadhi ya makala zake, anakoza ushahidi unaoweza kuthibitisha hoja anazotoa, au anatumia zaidi ushahidi wa mazingira na stories za vijiweni hata katika hoja nyeti. Nadhani uamuzi wa serikali ni sahihi kabisa.

    ReplyDelete
  25. Kubenea gazeti lako sasa tunalihamishia mtandaoni ambapo wahariri hatuonekani, hatushikiki wala hatufungiwi! Na muda wa suspension yao ukiisha usifungue gazeti hilo tena tuone sasa watakuwa wamefunga na kufungulia maoni ya nani.
    GAZETI LAKO KUTOKA LEO LINAITWA;
    'SAUTI YA MUENDELEZO WA TARIMEISM'

    Anayeleta siasa za kushambulia utu wa Mtu badala ya hoja majibu yake akamuulize McCain na Sarah wake.

    Waziri amekurupuka na itatucost bure!

    ReplyDelete
  26. HAKIKA NI KWELI WATANZANIA IMEFIKA KUITOA CCM KATIKA MADARAKA KAZI KUBWA YA CCM KUWADANGANYA WANANCHI WAMELETA MAENDELEO NA KADHALIKA.
    UKWELI UKITAKA KUJUA KAMA WAMELETA MAENDELEO MBONA WANASHINDWA KUJIUNGA KIBIASHARA NA AFRIKA MASHARIKI KWA KUIOGOPA KENYA IKO MBELE SANA KIMAENDELEO WAKATI UHURU ZILIPATA KARIBU WAKATI MMOJA.

    CCM KWELI IMEENDELEZA UMASIKINI KWA WATU WA CHINI NA KUTAJILISHA WACHACHE KATIKA CCM.

    TATITZO INASKITISHA WATANZANIA WANACHEZEWA KAMA MPIRA WA SOCKS YAANI DUNI MTU ANANULIWA KWA KITU KIDOGO SANA NA KUKUBALI KUPOTEZA HAKI YAKE MUHIMU.

    CHUKULIA KITENGE AU FULANA INAMFANYA MTANZANIA ASIWEZE KUFIKIRIA KUWA KURA YAKE NI MUHIMU LAKINI ANAPIGA BILA KUJALI MASLAHI YA TAIFA BAADA YA KUPEWA FULANA AU KANGA YA CCM.

    WATANZANIA AMKENI NA KUCHAGUA CHAMA CHENYE MASLAHI YA NCHI NA SIYO MAFISADI.

    CCM MIAKA 40 INATOSHA TUJARIBU NA CHAMA KINGINE TUKIONA NAO TAABANI TUNAWATOA KWA KURA LAKINI HATUWEZSI KUJILAUMU KWA VILE TUMEJARIBU.

    UKITAKA KUJUA CCM IMELETA MAENDELEO LINGANISHA NA KENYA JIBU UTALIPATA KWANI KUDANGANYWA.

    WATANZANIA KUMSAIDIA NDUGU YETU KUHUSU GAZETI NA HATA YEYE KUJISAIDIA NI KUTUMA MAONI KATIKA MAGAZETI INTERNATIONAL PIA HATA TV KAMA JAZEERA WAO WAKAO TAYARI KUTANGAZA LIVE.

    DUNIA YA LEO NI KUVUTUMIA VYOMBO VYA HABARI VIZURI WAO WAFUNGE MAGEZETI YA TANZANIA NA VIPI YA AMERIKA.

    TENA LA MUHIMU NI KUWAANDIKIA OPEN LETTER NCHI ZA ULAYA NA USA KUELEZEA JINSI DEMOKRASI INAVYOTUMIWA NA VIONGOZI WETU WA TANZANIA.
    DEMOKRASI UKINADIKA MAMBO MAZURI YA VIONGOZI ILA UKISEMA UKWELI BASI HAPO HUFAI NA SERIKALI HUTUMIA NGUVU YA UMMA KUMFUNGIA MTU GAZETI.

    AMKENI WATANZANIA TUMIENI MAGAZETI YA NJE NA NI BORA ZAIDI NA YANA NGUVU KULIKO YETU SIKU ZOTE INAKUWA NI HADITHI HAMNA MAHAKAMA WALA NINI BALI MAFISADI WANAZIDI KUIBA TENA KWA HASIRA KAMA SIMBA ALIYEJERUHIWA.
    MUNGU IBARIKI HAKI

    ReplyDelete
  27. WAPAMBEEEEEE! MSIPIGE KELELE TU KWENYE MTANDAO, KAMA USHAHIDI WA YALIYOJIRI MNAO BASI KELELE ZA NINI? MSAIDIENI KUBENEA KUPELEKA HUO USHAHIDI NA VIELELEZO VYOTE HUKO ALIKOFUNGIWA.TUNAMJUA KUBENEA TOKA ALIPOKUWA MWANDISHI MAGAZETI YA MTANZANIA ENZI YAKO CHINI YA JENERALI ULIMWENGU MPAKA LEO. TATIZO JE ALICHOKISEMA KINA UKWELI SIO KUCHUKUA HADITHI YA ANC SOUTH AFRIKA, MAMBO YA ZUMA NA MBEKI HALAFU KUYAFIKIRIA KATIKA MAZINGIRA YA TANZANIA NA KUSEMA KUWA HAYA NDIYO YATATOKEA HAPA KWA SABABU YAMETOMEA SOUTH. INGEKUWA MIMI SERIKALI NINGEMSHTAKI KWA TREASON! AU ALETE USHAHIDI WA KUTHIBITISHA ALIYOANDIKA. KUBENEA HUWA UNASOMA MTANDAO, NAKUULIZA JE HUJAACHA TU ZILE TABIA ZAKO ZA ZAMANI!!!! ULIJUA TU HUNA HOJA NA HAYO ULIYOYAANDIKA LAZIMA SERIKALI ITAKUCHUKULIA HATUA, HIZO NI STRATEGY ZA MSHIKAJI ZA KUTAFUTA UMAARUFU MPAKA NJE YA NCHI!! JE MWANAWANE MIE NA WEWE HALI ZETU TUNAZIJUA NANI ALIKUPA MTAJI WA KUFUNGUA GAZETI? MAANA ULIPOTEA MUDA KISHA HUYOO UKAIBUKIA NA GAZETI LAKO, TUAMBIE NANI HASA NI MMILIKI WA HILO GAZETI LAKO JE NI HUYO AMBAYE UNAMWANDIKA SANA NA KUMWANDALIA NJIA YA KUPITA. MAANA HATA BAD PUBLICITY INALIPA NA HUFUTIKI KICHWANI MWA WATU! SIASA BWANA NI MCHEZO MCHAFU KWELI KWELI! HAKUNA ETI CHA UCHUNGU NA NCHI WALA NINI KUMBE NI MAMLUKI!

    ReplyDelete
  28. Huyu Mkuchika si ndo aliwahi kusema wimbo wa wagosi wa kaya wa tanga kunani upigwe marufuku kwa kuwa unaongelea hali halisi ya maisha ya tanga wakati akiwa mkuu wa mkoa tanga?

    ReplyDelete
  29. MAMBO YA KENYA !! HAKUNA KULALA HADI KIELEWEKE 2010

    ReplyDelete
  30. Michuzi;niko nje kidogo ya Mada lakini karibu hapo hapo:Sipendi kuingilia biashara za watu;lakini haya matangazo yanatoka kwenye magazeti yanahusu dawa za kuongeza nguvu za kiume na lugha nyingine siwezi kuziandika hapa,binafsi nao;ba serikali iyapige marufuku au yatafutiwe njia nyingine za kuyatangaza kama ni lazima kuwepo kwa matangazo hayo:Kimaadili watoto wadogo wakiwa wanayasoma inakuwaje?Halafu tuna janga la ukimwi yanakuwa na indirect impact.Ni mawazo yangu yanaweza yasiwe na ukweli;Post tujadili

    ReplyDelete
  31. Demokrasia ni pamoja na kusikia usiyoyapenda. Hivi kusema wenzie ndani ya CCM wanamkakati/mawazo ya kumtoa JM 'Mwasupili' Kikwete kutoka ikulu ni kosa? Mbona mwenzie Thabo Mbeki alitolewa kafara na wanachama wenzie wa ANC na hakuna aliyehojiwa na polisi wala magazeti yalioandika habari hizo kufungiwa.

    Pili hivi siku hizi usalama wa Taifa wanashindwa ku-influence public opinion kwa njia laini mfano asubuhi asubuhi kununua makala za magazeti kwa wingi za Mwanahalisi ktk miji wanayofikiria wasomaji wakiona habari hizo watamtosa kiongozi wao mkuu?

    Njia hiyo mbadala ndio bora zaidi ya kufungia gazeti kwa vile watakuwa wanausalama na wanapropaganda watapata nafasi ya kuelewa nini kinatokea ndani na nje ya CCM yao.

    ReplyDelete
  32. What Mkuchika has done in banning MwanaHalisi is far more disastrous than what if he should have simply decided to Shut Up!Sending a popular newspaper like MwanaHalisi Underground is like hiding timebombs under the soil!Far more danderous!The Govt will loose touch,will also loose revenue,will send thousands of papervendors jobless,will suppress freedom of expression,will solidify elements of dictatorship in our fragile democracy,will put our democracy at stake,and all this for whose Gain?This matter was to have been left to the Baraza la Habari to have dealt with the issue if there was one!Mkuchika being on the side of the Govt,the Govt being the victimised(?),could have never been the accuser,the prosecutor and the Jugde all by himself?What kind of Justice is that!

    ReplyDelete
  33. The International Monetary Fund (IMF) has not declared the External Payment Arrears (EPA) account issue closed as reported by the local media in recent weeks, IMF officials have said.

    Neither has the fund softened its stance on other pending good governance issues in its relationship with the Government.
    Officials handling Tanzania's docket said IMF would continue to pursue the EPA case to its conclusion and ensure that all pending issues were comprehensively addressed to its satisfaction.

    The position was stated at the Bretton Woods Institutions annual general meetings in Washington following claims in some official quarters that the IMF had given Tanzania a clean bill of health on the matter. This prompted some Opposition leaders to accuse the IMF of impeding the war on corruption by refusing to adopt a hardline stance against the Government.

    Numerous bloggers say the ruling party's operatives want to make political capital out of the reports that the IMF had declared the case closed, and that the Government is using the reports to repair its dented image on good governance.

    The argument is that the matter should be closed following the IMF's statement and even the donor community had agreed to fund this year's budget, having previously threatened to withhold their money pending action on grand corruption scandals, including the EPA scam.
    However, IMF officials said that expressing satisfaction with the measures the Government had taken so far in handling the multi-billion-shilling scandal did not mean that the case had been closed.
    Source:The Citizen newspaper 15/10/2008 and the annual IMF/World bank meeting in Washington DC

    ReplyDelete
  34. Balozi wa Jamii,
    Habari nzuri kuhusu washiriki wetu vijana ktk Mashindano ya Commonwealth Youth Games mjini Pune, India october 2008.

    Dada wa kitanzania Naali Mary Xwaymay ameshinda medali ya shaba juzi ktk mbio za mita 3000.

    Hizo ni habari nzuri kwa umma wa Tanzania na pia Wizara ya Habari, michezo na utamaduni, Balozi tafuta nafasi ktk blogu hii kuhusu ushindi huu.
    Source http://results.cygpune2008. com/RIS


    Mdau
    Rocky
    London

    ReplyDelete
  35. Balozi wa Jamii,
    Masahihishi kidogo, ktk mashindano ya Commonwealth Youth Games(12th-18th. October 2008) mjini Pune, India.

    Tanzania imetwaa medali ya shaba ktk mita 3000 kupitia kwa dada yetu Mary Xwaymay Naali leo jioni tarehe 16/10/2008.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...