Waziri wa ardhi na nyumba ambaye pia ni katibu mwenezi wa ccm Kepteni John Chiligati Akihojiwa na mtangazaji mkongwe Othman Miradji wakati alipotembelea studio za Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani leo. Mh. Chiligati na mheshimiwa Faida Mohamed Bakar mbunge wa mkoa wa kusini pemba walikuwa ziarani hapa Ujerumani. Mh. Chiligati alielezea hamu ya radio Uhuru inayomilikiwa na CCM kushirkiana na DW ili kuisaidia kupata utalaam kutokana na uzoefu ambao DW inao katika masuala ya utangazaji na uandishi wa habari Toka shoto ni Aboubakar Liongo, Mh. Mbunge Faida Bakar, Othman Miraji, Kepteni John Chiligati na Thelma Mwadzaya wakiwa studio za Idhaa ya Kiswahili ya Redio Ujerumani. Asante mdau Mayer Drayer kwa picha mwanana na habari za uhakika toka ulimwenguni kote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Haisey ! yaani Bwana N'zee Abubakar
    Liongo Umpendeza na suti na kofia ya baraghashia!! umetoka mchicha!
    Sema Mheshimiwa Chiligati alistuka kidogo !alidhani yuko bega na Mrema! si lakini Mrema anavaaga suti na viatu vya raba ya kunchupa!!!
    Hongera sana bwana Liongo vazi lako zuri kweli

    ReplyDelete
  2. Eh!bwana kaka Liongo !yaani sio utani kaatika wote hapo wewe umependeza sana! sasa mimi ningekushauri kuwa hiyo hiwe ndiyo
    Liongo sutiz!!!!!!!! au ? kama utakuwa unatoka nayo ktk kila mahafari basi utakuwa unapeperusha bendera yako yaani Liongo sutiZZZ!!!na baraghashia.

    ReplyDelete
  3. Niliyasikia majibu ya Chiligati akihojiwa na sauti ya ujerumani nyakati za asubuhi hivi karibuni.Kweli bado tuna safari ndefu sanaaaaa katika siasa nchini Tanzania!Siku nyingine namshauri Chiligati atafute ushauri kwanza hata ikibidi nje ya CCM kuhusu yale atakayo yatamka katika vyombo vya habari kama sauti ya ujerumani inayosikika dunia nzima ili atathmini athari zake kuhusu 'his own personal reputation and integrity'kwa akiba yake ya mbeleni.Leo yuko CCM kesho atajikuta Mwenyekiti wa Mtaa,huwezi jua!Watu wasomi walioko nje ukiwaambia kwamba mwizi wa fedha zetu tunamjua lakini tumempa muda kwanza azirejeshe ndipo tumfikishe mahakamani watu watashindwa kukuelewa Mze!Porojo kama hizo waeleze mazumbukuku wa huku Bongo lakini Majuu watabaki wanakustahi tu,kwasababu siyo sahihi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...