dj chullu (shoto) na dj endru wakiwajibika katika disko maalumu la sherehe za iddi uholanzi jana
mtu kati kama kawa
pekecha pekecha
baadhi ya wadau waliohudhuria disko hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. hivi madisko ya ulaya watu wanakatazwa kunywa vinywaji? Hata soda sioni.

    ReplyDelete
  2. YES YOU ARE RIGHT. MADISCO YOTE YA KISTAARABU ULAYA HURUHUSIWI KUBEBA KINYWAJI KWENYE DANCING FLOOR. UKINYWA NI KWENYE MEZA YAKO AU KANDO MBALI NA DIMBA, IT IS FOR HEALTH AND SAFETY REASONS.

    ReplyDelete
  3. Wee anon namba 1 ulaya tofauti na Bongo na Usa wanaocheza na silaha mkononi huku wakati wakudansi kila kitu kinabaki mezani.

    ReplyDelete
  4. Leila nakuona ulivyonona hongera!! mwanao hajambo??

    ReplyDelete
  5. ukumbi mkubwa watu 12!

    ReplyDelete
  6. Nini maana ya kupekecha pekecha ?

    ReplyDelete
  7. Andrew Chiduo naye siku hizi DJ................Poa babaake.Vi pi wanasemaje mademu wa Amsterdam? Umeoa wewe au bado unaendekeza lebeneke.

    Mboro

    ReplyDelete
  8. Afu wamejadhajadha hao!!!

    Mpiga box

    ReplyDelete
  9. Kweli nimejua kwamba wa ulaya ni wastaarabu kushinda Bongo na Marekani.

    Yaani unarudi nyumbani wala hunuki jasho la watu waliobanana.

    ReplyDelete
  10. jamani wadada wamepoa sio kama huko uk, mmependeza sana ila mhmm kha huyo aliyeingia kati mhmm ngoja ninyamaze....

    ReplyDelete
  11. Babaake acha kabisa kulinganisha vitu usivyovijua kabisa.
    kama huwezi linganisha Holland na UK, utawezaje sasa linganisha US na Holland bwana.
    Acha kabisa kabisa hiyoooooooo.
    US ni habari nyingine. Hiyo ni viinchi vyoteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee 24 vilivyo jumuiya ya ulaya na kuongeza vingine 26, sijui utavipata wapi ndo USA.
    Au kwa lugha fupi vinchi vyote 24 vya EU mara mbili nanusu ndo unaipata USA.
    Elewa kwanza California ukiifanya kama nchi, inakuwa ni ya saba duniani kwa Uchumi(Economy).
    Hayo ya muziki wewe cheza, kunywa soda au bia yako na nenda kesho kasome chuo au fanya kazi zako za kutafuta fedha. Na sio kuanza mamabo ya kulinganisha nchi au ustaarabuuuuuuuu.
    Marekani unaweza fika Birmingham , Alabama ukaja ukasema ulikuwa US, sawa lakini ni kama Rukwa kwa Tanzania. Wakati huo huo kwa marekani huo ni mji mmoja kati ya miji 150. Lakini Holland ukifika Amsterdam umefika Holland zaidi ya hapo hakuna pa kujipinda zaidi ya masaa manne nchi imekwishwa.
    Baabake tuliza boli na US , haya maji mazito.

    ReplyDelete
  12. Mie nimekaa hapo , watu wanabaiskeli kishenzi na kutegemea student pass za treni. Watu wenye magari wachache kweli hapo kama sio mazee zeeee.
    Jasho unalo mwenyewe wala sio la disco, na ustaarabu ni wa mtu binafsi na baadaye nchi.

    ReplyDelete
  13. No joke watu wanakula maisha kwa kwenda mbele, kina dada mmependeza sanaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  14. DUUH WADADA WA HOLLAND MASHWALAH

    ReplyDelete
  15. Anon oct 6, 2008 6:13 pm

    Kweli usilolijua nikama usiku wa giza. Bado na wewe una ile hadithi yakusema Amsterdam ndio Holland.

    Je unajua kwamba katika dunia hii ni nchi moja tu duniani ambayo majiji yake makubwa yametengeneza ring [pete]? Kwa maana hio nikwamba kama ni USA hio miji yenu mikubwa ya states imetengeneza pete. Ukitoka AMS mwisho wa jiji ndio unaingia jiji lingine hivyo hivyo mpaka unafanya mzunguko wa kurudi tena AMS na hapo katikati ndio wanapoalezea
    Since a few decennia planning policy with regard to urbanization in the Netherlands has centered around the 'Randstad' concept: the highly urbanized, ringshaped, economically most important arm in the western part of the Netherlands, consisting of the four major cities Amsterdam, Rotterdam, Den Haag and Utrecht. The rural area in the middle of the ring, is called the "Green Heart" and is of agricultural, environmental and recreational importance. Urbanization of the "Green Heart" has been avoided where possible.

    Kwahio hapo ukitaka kwenda out na una muda wakuyamaliza hayo majiji yote unachagua uanze kulia au kushoto mpaka unarudi tena nyumbani.

    Hayo ni majiji manne kuna Mengine south na north ambako vijana wengi hupendelea kwenda vyuo vikuu.

    Hivi huko USA kuna jiji ambalo ni 24 hours? Holland liko jiji kama hupati usingizi na ukitoka nje kwenda centre kumekucha utawakuta watu kibao wanatumbua vyao.

    ReplyDelete
  16. hahahahaahahah halo haloooooooooo kwa kuyajua majiji ya watu hamjambo, wabongo bwana, maana hapo umebakiza kutaja na wabunge wa kila majimbo uliyotaja, wakati hata mkuu wako wa mkoa humfahamu.

    ReplyDelete
  17. wewe uliyesema US haiwezi kulinganishwa na nchi yoyote ,sawa tunaelewa ni nchi kubwa na iliyoendelea lakini kuna vinchi vidogo sana huko europe ambavyo vina ustaarabu wa hali ya juu zaidi ya hii nchi kubwa USA,lazima ukubali kuwa kila kizuri kina mapungufu yake.kuna vinchi huko europe vipo safe kuliko hii america.

    ReplyDelete
  18. ujanja wa kukaa marekani na UK kujiona ndio kila kitu ni utoto mkikuwa mtaacha!
    katika rank za standards of life marekani na uk hazipo kwenye top ten,
    watu wanakimbia kimbia tu na maisha
    high rate of divorce, low security, watu mmechanganyikiwa mnaishi kazini tu ili mlipe bills na morgage ili mstabilise uchumi wa mzungu!
    tv mnalipia, vipindi vingine hamuoni,mnafanya kazi za mabox kusoma mshashindwa,
    mi nawasubiri mkue kidogo mrudi nyumbani , ama mtazeekea nursing home?
    tena msingoje mkazeeka sana mje na nguvu zenu
    nyie jifanyeni marekani marekani!sijui california,sijui holland sijui wapi, wakati kwenu ikwiriri
    hehehehe!

    Mkulima part time mvuvi
    Boko bunju

    ReplyDelete
  19. Nimjue mkuu wa mkoa wa Bongo atanisaidia nini wakati mimi naishi huku NL?

    Mkuu mwenyewe wa mkoa ndio hao kina Kandoro na yule msambaa aliyepita Makamba!!?.

    Wanachokifanya au walichokifanya ninini? barabara zenyewe za hapo jijini ndio wahandisi feki. nguzo ya umeme katikati ya round about, sasa hapo kuna RC mwenye akili kweli?

    Tuacheni sie tunaoishi nchi za watu wanaojua ustaarabu.
    Hatujui mambo yakugombania daladala, tukienda maofisini kuhudumiwa tunatumia namba au kuweka miadi, aliyewahi kawahi aliyechelewa kachelewa. hapo bongo kama mko kituoni watu ishirini mnasubiri kipanya, hata kama kiko tupu mtauana mlangoni kwa kugombea, sasa ndio ustaarabu huo?

    Ukiniuliza namjua nani Bongo labda kiongozi anayeongoza kwa ufisadi lakini kiongozi anayefanya mazuri simjui.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...