

hivi champeni inapofunguliwa inatakiwa ilie ama iwe katika sailensa?
nauliza sababu nimekuwa napata maelezo tofauti kila wakati, hasa champeni inapobuma na mfunguaji akishindwa kuifanya ilie poo! kama mdau mushi zindonga anavyoonekana pichani.
vile vile ningependa nami kupata maelekezo ya namna ya kuifungua maana kuna mnuso mmoja nimealikwa na kamati ya maandalizi imenichagua nitakuwa mfunguaji champeni. na mie sijawahi hata mara moja kufanya hivyo, naogopa kuumbuka. naomba klasi wadau, ikiwa ni pamoja na hilo darasa la poo! ama kisailensa...
-michuzi
kwa sisi watanzania champeni inapo toa poo na kumwagika inakuwa kama haijafunguka vile; lakini kwa unfungua wa kawaida na pia kwa wenzetu mlio hauna maana na pia champeni haipasi imwagike kwa sababu ukimwaga unakuwa umepoteza karibu nusu ya chupa kwa hiyo kwa maelezo yako hapo juu fuata ya wabongo tikisa hilo chupa halafu zungusha waya taratibu, ukishatoa waya kwa kutumia dole gumba la mkono ulioshika shingo ya chupa sukuma kizibo. itatoa mlio na pia nusu/chupa mzima itamwagika na wewe utaonekana bingwa
ReplyDeletesi lazima ilie poo!!!ni mfunguaji tu avotaka iweje,wengine wafungua kimya-kimya wengine,yalia,yamwagika au isimwagike
ReplyDeleteBro Michu kwa BONGO bila kulia POOOO!!! unaonekana umechemsha. Ila kwa hizi champagne za bei ya madau hata ukimwaga sawa tu ila kuna wenzeti wana champagne mpaka laki 5 sasa ukiimwaga bilautaratibu inakuwa sooo na pia inategemea mandhari, je ukiwa kwenye carpet utamwaga? hayo ndiyo yangu!
ReplyDeleteKumwagika au kufumka kwa champeni inategemea ni tukio gani kama ni kushangilia ushindi au kombe ikifumuka kama kwenye picha ni sawa ila kwenye harusi kikiruka kizibo tu hata isipotoka inatosha, sasa unakuta mtu anafungua chmpeni kwenye harusi ikisha funguka anaweka kidole gumba na kumwagia watu tutakunywaje na we umeweka dole lako jamani???!! tuwe wa staarabu.
ReplyDeleteKwa sisi wazoefu wa kufungua champeni kwenye maharusi/send off na party nyingine ni ivi kaka
ReplyDeleteUnajua unapota bahati ya kufungua champeni sehemu kwanza unatakiwa uwe smart ile mbaya na uwe mbunifu pale unapo fungua lazima unesenese si unajua kimziki nyororo kinapigwa? sio ujisimamishe kama mlingoti .
chukua champeni yako nenda wakaibariki meza zote kuu the tikisa sana tena sana ili isikupe shida wakati unaifungua.
Anza kutoa kikalatasi taratibu wala usitetemeke thn kile kichuma thn anza kubinjua na kidole gumba ule mfuniko wake kama rangi ya mbao vile.Nikigumu kidogo ila kama umeitikisa wala sio ngumu kufunguka.
Mda si mrefu utasikia kifuniko kinaruka ukooooo na utakuwa umefaulu na kupigiwa makofi na vigelegele kama sio matarumbetaaaaaa.
Unapoitikisa sana ndio povu linajaa sna ila ukiitikisa kidogo haitomwagika saana,Chaguo ni lako.
Nakumbuka siku ya kwanza kwangu mwaka juzi nilifungua vizuri km vile nilishawahi kufungua ila mm nilikuwa najiamini sana ndio maana wengi hawakunigundua km mm ni mgeni.
Kaka nakushauri uende tena mm km mm siamini km huwezi kufungua naona km unatudanganya vile.Twende kazi braza acha uoga.
Theeeee newsss is that.
Mdau wako no 1
www.waukweli.blogspot.com
Bro Michuzi umenichekesha sana, nikajikumbuka pale shereheni ambako inakuwa imebaki chupa moja ambayo haina mfunguaji, na mfunguaji anatafutwa, huwa natamani kuingia chini ya meza kuepusha soni...
ReplyDeleteKwa wataalam wa ufunguaji naomba mnisaidie, ni utaalam gani unaotumika kufungua with a pop sound, bila umwagaji bali kanabaki kama kamoshi mvuke flani hivi ndio kanatoka!
Kama wadau wengine walivyosema, cha muhimu kujiamini. Kwa wabongo bila kifuniko kuruka kule na yenyewe kuona povu limekwenda juu hutapata vigeregere tarumbeta za nguvu. Kwa Bongo, pitisha mbele ya meza kuu ibarikiwe, then fuata muziki kwa kuitikiza taratibu ila watu wasione unaitikisa kweli, then ondoa kifuniko cha karatasi, benjua kichuma taratibu kama ni nzuri baada ya chuma utaskia msukumo we kwa dole gumba fanya kusukumiza kwa juu mara utasikia poo na kifuniko kuruka juu kifuatwa na pofu. Ila kiustaarabu wa wenzentu huitaji kutikisa maana itakiwi kumwagika, fungua taratibuuuu na kifuniko kitaruka na poo itatoka ikifuatwa na moshi tu. Angalia kuna nyingine ngumu hasa hasa zile za bei ndogo au za non alcohol, unaweza kuumbuka mwenzetu
ReplyDeletemnaona biiig deal! Mila za watu mnazikumbatia tu, jiulizeni maana yake ni nini na hiyo mila ilianza vipi! Wengine juzi tu mmetoka kwenye ramadhani na karibu mtasheherekea xmass bila hata kujiuliza xmass ilianza lini. Yote hayo + kuua albino yanatokana na ibada za miungu ya uongo! Jifunzeni!
ReplyDeletemmmhh.. wala msinikumbushe kuna mtu alipewa kazi ya kufungua champen wacha animwagie..nilichukia kweli wallah! but if u really want to know how u can buy ten or twent bottles and try to open @ home.PRACTICE MAKE PERFET so they say!ha ha haaa..
ReplyDeletemdau Ars.
you start with da bitrhday party for one year baby
ReplyDelete