Kaka Michuzi habari za kazi,Naomba msaada wakumpata dada huyu pichani ambae amemuibia bosi wangu vibaya sana, amemuacha mweupe, sijui inawezekana kutumia blog yako kupost picha yake?
tuna vithibitisho vya polisi na tayari ametoka kwenye baadhi ya vyombo vya habari vya hapa zenji kuwa anatafutwa.
Huyu dada alidai anaitwa Neema Rajabu, na alikuwa akimfanyia kazi bibi mmoja maeneo ya Mombasa nyumba za Mchina, Zanzibar kwa muda wa kama miezi miwili hivi.
Siku aliyofanya huu mkasa wenyenyumba walitoka wote ndipo alipopata nafasi ya kukumba vitu na kutokomea navyo, inasemekana ilikuja gari akapakia mizigo na kuondoka. Wenyewe wamejitahidi kutafuta mpaka kuweka guard bandarini lakini hakuonekana mpaka leo.
Zawadi itatolewa kwa atakaetoa habari zitakazopelekea kupatikana kwa huyu dada.
Natanguliza shukurani zangu
mudy
Zanzibar
Natanguliza shukurani zangu
mudy
Zanzibar


aah tabu yote ya nini yakhe? Mwivi atafutwi hivyo yakhe kama huko Zenji siku mambo hayapandi mwendeeni Lamu au Tanga, nakwambia atarudisha mwenyewe kila kitu, au mwendeeni Pemba kule visiwa vya wakojani au hata hapo jirani Tumbatu yakhe!
ReplyDeletenimesikia habari ya huyu dada, la kushangaza ni kuwa amefanya huo wizi mchana kweupe, kaleta gari na kupakia kila kitu na hakuna alomuuliza kitu! majirani jamani!
ReplyDeleteNEXT WEEK KUINGIA BLOG YA ITHA MITHUZI NI SH 100 NA USD 1 £ 1 Uero 5. Ahlaaaaaaaaaa wakati boss anapewa vitamu vitamu nakshi nakshi mpaka kajisahau kamuwachia fisi mfupa fisi kaula hahaha inshallah mtampata ila mie ushauri wangu mkimpata jaribuni kufanya uwanadamu muwekeni chini muulizeni tatizo lilikuwa nini? mpaka akaviiba then mumsamehe kwani ni binadamu mwenyezimungu atawapeni vengine tu vitu duniani vipi na tutaviwacha nyuma mkimuonesha uwanadamu naye sizani mbele kama ataendelea tabia yake au mnaonaje wadau? duh jamaa juu anataka mwenzake aendewe kwa waganga hatari simoooooooo from Haji Bin Tumbo Bin Pandu Bin Faki Bin MAkeme Bin Makupuli ngangariiiiiiiii.
ReplyDeleteHuyu aleleta hili tangazo humu tutamuamini vipi?kama kweli dada huyu mwizi au anataka kumpakazia tu,tuwe makini na watu kama hawa,kama kapata picha yako wanakupakazia,peleka polisi na wao watatangaza kwenye magazeti sio wewe utume kwenye michuzi,ukashifu watu,kuna sheria za kufata.
ReplyDeleteMsichana mzuri hivi kumbe mwizi? Sasa hivyo vitu vitampeleka wapi.
ReplyDeleteMke wa kaka yangu alishamwibia kaka yangu pia. Kahamisha vitu mchana wakati kaka yupo kazini jioni anarudi majirani wanasema mbona mkeo amesema mnahama leo?
Hamna aliyemwonea huruma kabisa nyumbani kwetu kwa vile alikatazwa kumwuoa huyo mwanamke lakini hakusikia.
Mwanamke alikua hana background, walijuana kwa muda mchache sana na kwenye harusi hakukuwa na ndugu yake hata mmoja. Ila kwa uzuri alikua mzuri sana tu.
kweli muungano una raha yake jamani tusiuvunje kwani tuko karibu wakati shida kama hi,msijali kwetu bara kama tukimuona tutamtia mkononi tumlete akapale miwa chuo cha mafunzo,msingi muwe na subira
ReplyDeleteMie nawaambia hawa "vichogo" wafukuzeni zanzibar hamtaki, sasa ngoja wawaibie, wawachome watoto wenu sindano za HIV,wawabake,wawa chune ngozi, n.k mtakoma...!
ReplyDeleteNdo basi tena.. mmekula kunguru mwasema mmekula kuku...!
brotehr michuzi nilidhani unakuwa unasoma comments zote kabla ya kuziruhusu kutokea hapa, naona sasa kwa nini umeruhusu hii ya anaejiita mzanzibari 100% kutokea?
ReplyDeleteannon wa October 12, 2008 6:13 PM
ReplyDeleteusipige kelele bure huyo binti hakusingiziwa taarifa zake ziko polisi na katika vyombo vya habari. ni kweli kabisa ameiba na hivi sasa anatafutwa na polisi.
hii tabia ya wafanyakazi wa ndani ni kweli inakera mtu anaaminiwa halafu hujitoa uaminifu, na sio kusema vichogo hata huko zanzibar pia hao wafanyakazi wandani wakiznzbar nao wezi,utaona mfanyakazi wa kuja na kurudi sio wa kulala basi atamaliza kazi zake anakuaga kumbe huku kishachukua kilo ya mchele au sukari hukificha kifurushi kila siku huchukua kidogodogo au hukuchukulia vyombo sahani ukitahamaki vitu huvioni kama umeweka guia lamchele kwa mwezi basi hata mwezi haujesha guniala mchele limeisha.Taia hii wala sio nzuri utamuona mwanamke mzuri au mtu mzima anaheshima zake utamuamini kumbe atakuchota tu,tuwe wangalifu nao.
ReplyDeleteHuyo binti ninaye naishi naye singida;kiomboi
ReplyDeleteContacts:Steven Madundo
P:O:Box 78
Kiomboi;singida
Simu 07821155473
Samahani sikufahamu kama anatafutwa na polisi
Kabla ya kuanza kumlaumu huyo binti inabidi tuulize maswali kwanza:-
ReplyDeletea) Alikuwa analipwa kiasi gani kwa mwezi?
b) Je! amelipwa fedha zake kama mlivyopatana
c) Alikuawa na mahusiano yeyote ya kimapenzi na baba mwenye nyumba?
d) Ni kabila gani?
e) Ulimpata wapi/ulimwajiri vipi
f) Unafahamu ndugu zake wa karibu
g) Unauhakika gani kwamba huyu binti ndo ameiba? inawezekana pia kuwa dinti yuko matatizoni pia.
h) Kiasi gani uko tayari kutoka kupatikana kwa huyu binti?
Jibu hayo mawswali kabla hatajaanza kumtafuta Bro!