
watoto toka kila pembe ya jiji la dar wakisherehekea sikukuu ya iddi ufukweni karibu na hospitali ya aga khan ambako bomba la maji machafu ya jiji hutemea kago lake. hawana pa kwenda, wafanyeje? bustani ya mnazi mmoja gaden imefungwa na haina tena mabembea, inafunguliwa siku JK akienda kuweka ngao na mkuki siku ya mashujaa. viwanja vya wazi vyote aidha vimejengwa majengo ama vinaachama tu bila shughuli yoyote. yaani utadhani jiji halina viongozi kuanzia kwenye shina hadi kwa madiwani na mameya kibao. inatia hasira kweli, hasa ukikumbukia maafa ya watoto kule tabora ambako baada y kukosa kwa kwenda wakajazana disko toto. hii haki naivalia njuga hadi kieleweke. wallahi tena... ukitaka kuona adha hii katika video
bofya hapa
bango linalokataza kufanya shughuli yoyote kwenye sehemu hii ya ufukwe kwa sababu ambazo mababa wa jiji wanazijua wenyewe. landlover ulionalo ni la kukamata magari yanayoegeshwa hapo. yule jamaa mwenye pick up kuleeee mbele keshapigwa mnyororo. alipotoa kitu kidogo akaachiwa. ndani ya landlover mna jamaa wa breakdown na askari wa ffu (bila shaka kaacha lindo aje kusanya, maana humo tunajua anakaaga mgambo na trafiki). wakali kweli ukiwahoji mbona wao wamepaki wanapokataza wengine. ukiwahoji kwamba mkishamkamata mtu aaliyeegesha gari hapo mnampeleka wapi sikukuu yote hii tena saa kumi na moja jioni... nongwa. tena inasemekana magari hayo ambayo nasikia hata bima hayana na minyororo ni biashara ya wakuwa wa nanihii. bongo tambarare kweli wadau!
afande saidi mwema upo???
HUO NI UJINGA KWA NINI WATU WAKATAZWE KUFANYA SHUGHULI ZAO, TATIZO NI JIJI LENYEWE LINAKUSANYA KODI KWA AJILI YA MISHAHARA TU NA POSHO ZA SEMINA, KUFANYA USAFI WA JIJI LAA, AU KUWEKA MAENDEO WATU WANAWEZA KUEGESHA GARI NA KUFANYA SHUGHULI ZAO HUKO WAKIPUNGA UPEPO HATA KWA KUWALIPISHA KIDOGO HAWATAKI, ACHENI UNYANYASAJI NCHI NI YEU SOTE NA TUNATAKA KUFAIDI PIA, WEKENI MAZINGIRA YA WATU KUFANYA SHUGHULI ZAO KAMA KAWAIDA.
ReplyDeleteMichuzi hawa jamaa wenye hiyo Landrover wanatakiwa washikwe na camera za picha wakati wanachukua rushwa halafu ziwekwe kwenye You-tube.
ReplyDeleteHapo hakuna hata Life-guards wa kuangalia watoto wasizame ni uzembe tupu.
mambo yanasikitisha sana.
Imefika wakati tuwe na public parks, na public beaches. Jiji lenye watu zaidi ya million tatu, haina hata garden park? Maana tukisema mnazi mmoja pale ni padogo, landscaping ni mbovu na kuna majengo lukuki. Kila beach, kuna ilani kama hiyo, sasa ndo kusema haturusiwi kufaidi rasilimali zetu?
ReplyDeleteBwana waweke utaratibu watu waweze kufaidika na hizo beach,bila ya kuharibu mazingira, hilo linawezekana. Na hakuna hata miundo mbinu kuhakikisha usalama wa watu na familia zao...kila leo kuna watoto wanazama hata kama siyo sikukuu.
Aisee lazima yatengwe maeneo ya wazi watu waweze kupata picnic na kupumzika...nasema ni lazima, lasivyo kuna sababu gani ya kulipa kodi? Lazima wananchi wadai kwa nguvu haki yao....hii sasa ni too much. Ndhani tunaponzwa na upole, imefika wakati tudai kwa nguvu uwajibikaji kutoka kwa hawa wanaojiita viongozi.
Halafu kwanini matangazo hayo kuhusu maegesho wasiweke sehemu zote za beach iko sehemu mmoja tu? Walai michuzi nakuunga mkono mapambano na hali hii, this situation is pathetic!