MJI wa Tabora jana uligubikwa na simanzi na vilio miongoni mwa wazazi, walezi, ndugu na jamaa wakati wakiitambua miili ya watoto 19 waliokufa juzi jioni katika kumbi za disko za Bubbles Night Club na Top Five Disco Sound mjini hapa baada ya kukosa hewa.
Miili ya watoto hao wenye umri wa kati ya miaka saba na 18 ilianza kuzikwa leo katika makaburi mbalimbali ya hapa, kwa kufuata imani zao za dini.
endelea kusoma kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Innalillahi wainna ilayhi rajiun,ni msiba mzito M/Mungu awalaze mahali pema peponi na awape subira wana familia wote katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  2. Wahanga Michuzi ni watu wanaojitolea kwa makusudi kufa kwa nia ya kutetea jambo fulani,iwe dini,utamaduni nakadhalika.
    Kiswahili kinapotoshwa kuwaita watu waliokufa katika ajali au jango lolote bila ya wao wenyewe kudhamiria kufa kama wahanga,wale vijana waliokufa Tabora hawakuwa wahanga kwani hawakwenda kwa dhamira ya kufa kutetea jambo fulani na tuwaite waathirika wa janga au ajali ya kukanyagana katika ukumbi wa disco.
    Wale Wapalestina wanaojiviringisha mabomu na kwenda kujiripua kwa makusudi wakitetea ardhi yao dhidi ya Israel ndio tunaweza kuwaita WAHANGA.
    Mwenyezi Mungu awape mapumziko ya amani vijana waliopoteza maisha yao katika mkasa wa disco Tabora na pia wazazi na walezi wa vijana wale Mola wape moyo wa subira.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...