Na Mwandishi Maalum, Tabora
Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana amekutana na kuwapa pole binafsi wananchi wa mjini Tabora, ambao mwanzoni mwa mwezi huu walifiwa na watoto wao 19 katika tukio la kusikitisha kwenye Sikukuu ya Idd El Fitr, Oktoba Mosi, mwaka huu.
Rais, ambaye ameanza ziara ya kikazi ya siku nane ya mkoa huo, amekutana na wazazi na walezi 16 wa watoto hao waliopoteza maisha kwenye ajali ya kubanana kwenye ukumbi wa disco wakati ulipotokea moto kwenye ukumbi huo kwenye jengo la NSSF mjini Tabora.
Watoto wengine 16 walilazwa hospitali kutokana na kuumia katika tukio hilo. Mpaka sasa wote wametibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani, isipokuwa mmoja ambaye amehamishiwa Hospitali Kuu ya Taifa ya Muhimbili, Dar Es Salaam, kwa matibabu zaidi.
Baada ya kuwa amempata mkono kila mfiwa o katika tukio hilo nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, mjini Tabora Rais amewaambia wafiwa hao:
“Siku ile ya Idd El Fitr, nilipata habari za kusikitisha za msiba wa watoto wetu. Nikamtuma Waziri Kapuya (Profesa Juma Athuman Kapuya – Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana) kuja kuungana nanyi kwa niaba ya Serikali kwenye msiba huu. Lakini maadamu nimepata nafasi ya kuja hapa mwenyewe, nimeona ni jambo zuri nikutane, ili niweze kuwapeni pole mimi binafsi.
Ameongeza Rais: “Nataka mjue kuwa msiba wenu, ni msiba wetu sote. Majonzi yenu, ni majonzi yetu, Masikitiko yenu, ni masikitiko yetu. Kila mzazi hupenda mtoto wake aweze kukua na kumzika yeye. Lakini pia Mwenyezi Mungu ana mipango na maamuzi yake. Nawapeni pole na kuwafariji wa namna ya pekee.”
Wazazi hao nao wamemshukuru Rais Kikwete binafsi, na uongozi wa wilaya ya Tabora na mkoa wa Tabora kwa namna ya pekee ambayo walishiriki katika kuwafariji wakati wa msiba huo mkubwa.
Mara baada ya kutokea ajali na msiba huo, Rais alitoa ubani wa sh 500,000 kwa kila motto aliyepoteza maisha na sh 100,000 kwa kila mtoto aliyeumia.
Miongoni mwa watu wengine ambao walitoa ubani ni mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, na Mbunge wa Igunga, mkoani Tabora, Rostam Aziz.
HUO NDIO UUNGWANA. AHSANTE MH. RAIS WETU.
ReplyDeleteje unajua chochote kuhusu hili jambo la kifo cha Prof Nzali...
ReplyDeletehttp://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19728-prof-nzali.html
tupashane?
Huyu Rostam si mtu wa Tabora wilaya ya Igunga. Sasa alikuwa wapi anakwenda kuhani kwa kuambatana na Rais na hali ni mtu wa uko. Ukombi huo au ndio ushoga wao
ReplyDelete