Hi Michuzi..Greetings!!!!
Ninashukuru sana kwa kuendeleza libeneke katika globu yetu ya jamii. Ninaamini kwamba hata viongozi mbalimbali wamekuwa wakiifuatilia kwa ukaribu, hivyo basi ninaomba kutoa kero yangu kwako.
Kero hii inahusiana na madereva wetu wa mabasi hususani daladala za Dar es Salaam mimi nikiwa mmoja wa wahanga wa tukio lililotokea jana ukijumuisha na mengine mbalimbali yanenayoendelea kujitokeza kila siku.
Jana jioni majira ya saa 12 kasorobo nimenusurika ajali mbaya ya kugongwa na treni katika reli karibu na taa za kuelekea chang'ombe kama unatokea ilala. Dereva wa gari namba T210 AAH mali ya Felician S. Masawe wa Box 1402 Moshi linafanyalo safari kati ya Gongolamboto kwenda Msasani limenusurika kusababisha maafa makubwa eneo hilo kwa uzembe wa dereva wa gari hilo.
Tulipokaribia reli muongoza treni alitusimamisha na kibendera chake cha rangi ya denja ili treni ipite kwanza na akatii amri lakini kwa gafla treni ilipokaribia aliamua kuliingiza gari kwenye reli ili apite kwa haraka awahi kituo cha mbele kuongeza abiria wengine.
Bahati mbaya wakati akifanya hivyo gari lilizimikia katikati ya reli na kusababisha hofu kubwa na hata baadhi ya watu kutaka kuanza kuruka madirishani. Kwa nguvu za mola gari liliwaka na tukaweza kupita inchi kidogo tu karibu na treni yaani tumeponea tundu la sindano.
Baadhi ya abiria wakaanza kumgombeza dereva kwa uzembe na kwa jinsi alivyokuwa na kiburi hakujali wala kuomba radhi akidai yeye haogopi chombo chochote cha dola.
Imenitia simanzi kubwa kuona jinsi vyombo husika wanavyodharaulika na madereva wanaohatarisha maisha ya watu kwa uzembe namna hiyo. Ninaomba vyombo husika walishughulikie suala hili kwa umakini na huyo dereva achukuliwe hatua ili iwe kama mfano.
Nadhani wakitaka ushahidi watoe tangazo waone ni watu wangapi watakuja na majina na namba za magari yanayohatarisha maisha kila siku.Nimekereka sana na jambo hili na hata kunisababishia kukosa usingizi vizuri jana kwa kumbukumbu ya kutaka kugongwa na treni ukizingatia ni wiki moja tu tangu nishuhudie treni ikigonga basi mida ya asubuhi eneo hilohilo ikiwa imesababishwa na dereva mwenyewe.
TANZANIA ITAJENGWA NA WATU WENYE AFYA BORA AU WALEMAVU WA VIUNGO, AKILI NA WAFU?
Naomba kuwasilisha.
Kazi njema,Mdau Joan.


Yani nyie abiria wote kwenye hilo basi mmeshindwa kumpiga makofi huyo dereva? Mlitakiwa mumpige kama mwizi kwani madereva wazembe kama yeye washaua watu wa kutosha na kipigo kingesaidia siku nyingine asirudie kitendo hicho.kama hio ndio trip yake ya kila siku anaweza kurudia hicho kitendo na kusababisha maafa makubwa.
ReplyDeleteMadereva wa aina hiyo wako wengi sana Bongo. Kuna wakati ninapokuwa naendesha, niko main road na dereva mwenzangu yuko pembeni anataka kuingi main road, huwa nashangaa sana. Kinachonishangaza ni kuwa ninapokuwa mbali (lakini katika speed) dereva husimama kabisa kama vile amenisubiri nipite kwanza. Lakini nikishasogea sana na alipo, mara namwona ndiyo anaingiza gari lake main road! Siyo mmoja wala wawili, ni wengi mno wa aina hiyo. Sijui kuna driving school Bongo inayofundisha hivyo?
ReplyDeletePili, kuna madereva wengi mno Bongo ambao huwawashia taa walioko main road ili wasimame na kuwaacha wao walioko barabara ndogo wapite kwanza! Hata kama kuna nafasi ya kusubiri sekunde chache tu za yule wa main road kupita kwanza na wao kuingia main road safely, utawaona wanalazimisha wa main road asimame! Hii pia inanishangaza sana.
Tatu, kuna hawa madereva wenye magari makuukuu ana malori yenye speed ndogo ambao huamua kuendeshea fast lane - lane ya kulia kabisa. Sijui ni kiburi tu au ndio driving schools za Bongo zinavyofundisha?
Usimamizi wa sheria ni mbovu Bongo. Mara nyingi naona magari yanavunja sheria za barabarani mbele ya askari wa usalama barabarani na kuondoka tu! Barabara ni ya lane 2 tu, dereva anaamua tu kutengeneza lane ya 3 au ya 4 mbele ya traffic police. Na traffic police anaona na ananyamaza tu! Hii sijawahi kuiona nchi nyingine.
Mwisho, madereva wa Bongo hawana SUBIRA kabisa. Kukosa subira kunawafanya wavunje sheria za barabarani kwa makusudi. Hili ndo tatizo kubwa pamoja na usimamizi mbovu wa sheria ni matatizo ya msingi.
WEWE UNGEKUWA RAIA MWEMA BADALA YA KUTAKA MSAADA USIO NA TIJA TOKA BLOG HII, UNGEKWENDA KWENYE KITUO CHA POLISI AU UNGEPELEKA MALALAMIKO KWA ASKARI WA USALAMA BARABARANI AMBAO WAPO KARIBU KWENYE KILA NJIAPANDA KUBWA, HATA HIVYO HAUJACHELEWA UNAWEZA KUFANYA HIVYO UWE NA TIKITI YAKO. LAKINI PIA UNGEWEZA KUPIGA SIMU POLISI KWA KUTUMIA NAMBA 112 NA KUWAELEZA NAMBA YA GARI LILIPO NA TATIZO LILILOTOKEA.
ReplyDeleteJamaniits high time hawa madereva washughulikiwe!Wahusika kazi kwenu,contacts zote ziko hapo,tunaomba hilo swala lifatiliwe.This is so pathetic.Likifungiwa macho mtatusikitisha sana.ITS TIME TO ACT!!!!!!!
ReplyDeleteYani kweli kupanda daladala roho mkononi,yani kuna madereva rafu sijawahi ona.unakuta mwingine kapaki stendi anashusha abiria,na akiingia barabarani anaingia mzimamzima hata kama kuna gari nyuma linakuja kwa kasi.
ReplyDeletemi mwenyewe nshawahi kunusurika barabara ya mandela,siku hiyo kulikua kuna foleni hivyo wakapita service road na yenyewe ilikua na mabonde kibao.hivyo dereva akawa anakimbiza gari huku linainamainama kwenye makorongo hayo gari jingine likawa linakuja kwa nyuma ili lipite kwa pembeni na wakati huo linapita na gari letu ndo lilikua linainamia upande huo.basi gari letu likalidondokea hilo gari bahati nzuri hatukuumia.ila madereva hawako makini na roho za watu.inasikitisha sana tena sana.
Wewe na abiria wenzio mmekuwa waoga mno, huyo dereva yuko peke yake ndani ya gari nyie mko sijui zaidi ya ishirini ukizingatia madcm yanavyojaa pengine mmefika 50. Hivi kilichowafanya mkashindwa kumchukulia hatua hapo hapo ni kitu gani? Mtu anataka kuwaua hivi hivi huku mkiona na bado unakuja kutuelezea humu jinsi mlivyponea kwenye tundu ya sindano na unategemea watu wengine wachukue hatua kwa ajili ya usalama wa maisha yako? Mlishindwa aliposimama kituoni kumvamia na kumtoa kwenye usukani na kumpeleka polisi? Wote nyie mliokuwa ndani ya basi mulikuwa waoga kiasi hicho? Yaani mngemkata, mkatoa kwenye usukani kuwa hafai, narudia tena HAFAI kukabidhiwa dhamana ya maisha ya watu? Nina uhakika kulikuwa na askari wa usalama barabarani, nyie mngemshusha chini, askari angemwambia konda wake, na kunakuwemo na daywaka humo hasa hayo mabasi ya masafa, apeleke basi kituoni! Mngepoteza nauli zenu lakini mngekuwa mmechukua hatua ya kunusuru maisha yenu. Mie ningempa na makofi mawili matatu, especially kwenye kundi la watu wengi, potelea mbali mahakamani ningesema nilifanya hayo kutokana na shock. Dereva au konda wa dala dala huwa hachezei maisha yangu hata siku moja tena mie ni mwanamke, na mara nyingine nikikemea mwendo mbovu wanaume huwa wananiona ni mwoga, lakini ni salama kwangu. Madereva wa eneo la kwetu wengi wananijua na wakimess up napiga simu saa hiyo hiyo polisi! Ala watu kama nyie ndio mnasababisha hizi tabia za kizembe za kutojali maisha ya watu zikomae!
ReplyDeleteHivi kuna "Citizen's Arrest" Bongo? I say let the citizens arrest and haul his ass to nearest police station, preferebly after kamkong'oto kidogo asirudie tena next time again pia!!
ReplyDelete