nimekuwa nikipokea maswali na mamalamiko kibao toka kwa wadau wakitaka kujua sababu kwa nini hotuba za mwalimu nyerere hazipatikani, wakidai kwamba wakienda kuulizia TBC wanaambiwa hazipatikani.
Pia wamelalamika mtindo wa tv na redio kwa kubania hotuba hizo ambapo hutoa kisehemu kiduuuuuchu cha hotuba hizo na kuacha wadau wakiwa na kiu.
Jumanne ijayo ni siku ya Nyerere Day na wadau wengi wana hamu ya kusikia hotuba za muasisi huyu wa taifa hili, lakini jamaa wanabania. wanauliza wadau kwa nini wamatumbi tunakuwa na mawazo ya kiajabu ajabu hata kubania hotuba za mwalimu? wanamwekea nani? kwani zao? hawana haya?
na kila unayemuuliza anakwambia hotuba za mwalimu alizotoa wakati wote wa uhai wake zililenga kipindi hiki hasa, na wanasema kila neno lina maana sana, kiasi cha kumuona huyu mwalimu ni kama nabii.
hii imekaaje wadau?



Hotuba za Mwalimu zinabaniwa kwa kuwalinda mafisadi.
ReplyDeleteKaka michuzi swali zuri sana.lakini wewe si huko daily news serikalini? Sasa au na nyinyi mmekatazwa? Tuwekee japo kwenye tovuti yenu.
ReplyDeleteNgoja nikupe jibu la swali lako sasa hotuba nyingi za nyerere zilikuwa zinakemea maovu ambayo ndio yanafanywa na uongozi wa ccm sasa .na hio ndio sababu kubwa kuzipiga marufuku.
Mdau mzawa
HEKIMA NA BUSARA HUWA HAVIPOTEI WALA KUSAHAULIKA ! PAMOJA NA JITIHADA ZA WENYE KUFIKIRI/KUPANGA KUZIBANIA HIZO HOTUBA ZENYE WINGI WA MIONGOZO KWA SISI WADANGANYIKA HAITASAIDIA KITU NI SAWA NA KUJARIBU ZUIA JUA LISIKUCHE AU LISIZAME ! NA ZIKIBANWA NDIO ZITAKUWA ZENYE THAMANI ZAIDI.AMETUTOKA KIMWILI LKN ATABAKI DAIMA MILELE KTK NYOYO ZA WADANGANYIKA WAKE ALIOWAPENDA SANA NA KUWATHAMINI,KUWAJALI NA HILO NDILO LINALOTUUNGANISHA KATI YETU NA JULIUS !
ReplyDeleteMzushi !
Mimi ninaafiki kabisa, tukubali tusikubali baada ya karne kadhaa itakujabainika wazi kuwa JKN hakuwa binadamu wa kawaida. Kitu kimoja ambacho huwa sisahau katika maandishi na hotuba zake ni mtazamo wake kuwa "UBEPARI NI UNYAMA". Watawala walioufutia wamelazimishwa kuukumbatia lakini bado unyama wake uko pale pale. Anayebisha afuatilie kinachotokea "WALL STREET" na madhara yake kwa dunia nzima.
ReplyDeleteKWeli hata kwenye Youtube sioni wala zile za enzi za Uhuru za Kenya naona michuzi naomba tuoneshe picha za wale jamaa waliachiwa huru na mwinyi waliotaka kumpinduwa nyerere waliwachiwa mwinyi alipomaliza wadhifa wake. Kina Uncle Tom na mcgee. from Haji Bin Tumbo Bin Pandu Bin Faki Bin MAkeme Bin Makupuli ngangariiiiiiiii.
ReplyDeleteNi aibu kubwa kwa busara za Mwalimu Nyerere kufichwa.Watanzania hatujawa na kiongozi msemakweli kama huyu. Tukipaa mwingine kamahuyu utakuwa ni upendeleo wa ajabu kwetu sisi wa mwenyezi mungu- hakika tutakua taifa teule. Tulipokuwa nae hatukumthamini ipasavyo. Alipoondoka wengine ambao maneno yake yanawasuta na yatawasuta hadi kaburini wanaficha na kufunika aliyoyasema.Ole wenu watanzania huu ndiyo utajiri wa kudumu kuliko hata Tanzanite na dhahabu na mabenki amabayo sasa yamekwishaporwa nawageni na watawala wenu.Mkizubaa hata maandiko yake na hotuba zake mtaambiwa zimepotea zimeharibika haijulikani zilipo. Njia pekee ni kudai zisamabzwe kote nchini.
ReplyDeleteYaani serikali ya CCM inaogopa hata kusikiliza hotuba za Mwalimu?
ReplyDeleteMimi nawashauri TBC wasiogope maana kuna mazuri ya kupata kutoka ktk hotuba zake na pia kuelewa yale yaliyosokewa kipindi cha nyuma.
Hivi hotuba hizo zirushwe kwa urefu wananchi wapate kutafakari mema na yale mapungufu.
mchonga sio mchezo kaka michuzi kama anaoteshwa vile!!otherwise mzee apumzike salama..
ReplyDeleteprof tibaijuka alimuelezea mzee kama STATE PERSON sijui unanielewa kaka !!!
kiongozi unaongoza nchi kwa misingi ya katiba na sheria ukishindwa inabidi upime mwenyewe!!ni hayo tu kaka..kubana airtime lazima ili wasiumbuke ...
Michuzi naona maswali kama haya uwe unayajibu ili kueleimisha watu. Nadhani kabla ya swali hili watu wajiulize ni nani mmiliki wa hotuba hizi baada ya hapo utakuwa na mwanga kwa nini azipoatikani.
ReplyDeleteHII HAIJAKAAA SAWA KABISAA! NI KWELI ALIKUWA NA BUSARA LAKINI ANA MAPUNGUFU YAKE KAMA WANADAMU WENGINE, KWAHIYO HUWEZI KUMFANANISHA NA NABII KABISA!
ReplyDeleteHakuna script au kama zilikua zinawekwa kwa vitabu basi zichapishwe kwenye magazeti kama wanaona kuweka kwa redio ni nona
ReplyDeleteHi! Mr Michuzi na Watanzia wenzangu kwaujumla popote pale mlipo!
ReplyDeleteNime furahi sana kuona kwamba hikikitu kumbe kime wakera watu wengi!
Mimi hapa niko nje ta Tanzania, nanilikua nataka kuandika article kuhusiana na mambo aliyokua ameyasisitiza mwalimu na alioyo yafanya, iliniweze ku publish kwenye moja ya the most authentic
journal
in this world, nahii nimoja ya shughuli ninazo fanya hapa nilipo,Lakini nime tuma vijana hapo Tbc, pamoja na kwenye jengo la sanaa la Mwalimu, lakini wame kataa kuwapa! sasa hebu fikiria wewe kama mwananchi unataka kuandika mambo muhimu kuhusu nchi yako na ambayo yanakubalika hata nje ya nchi yetu na watu muhimu, sasa unashindwa kufanya hivyo kwasababu yauzembe wakufikiria wa watu wachache tu!
Mimi naungana nakilio cha nduguzangu wengine walio toa maoni yao hpo juu!
naomba Mr Michuzi wewe uko hapo nyumbani hebu tusaidie ili hilo tatizo lipatiwe ufumbuzi! au wanataka mpaka tuandamane ndo wajue tunahitaji?
Tafadhali sana.Imefanya hii topic niliyo kua nataka kuandika niiache kwanza, naomba utusaidie ilikufanikisha baadhi yamambo tunayo fanya wenzenu huku.!!!!
Mdau!
"Hata yale ya msingi tunyawekea Question Mark!!!" Haya yalikuwa maneno ya JKN na bado yana ukweli na mantiki kubwa sana katika jamii yetu kwa sasa na hata baadaye. Sishangai kuona hotuba zake zinabaniwa (dRU)
ReplyDeleteAstaghafiru llah.. . kawa nabii sasa?!!! Ndo basi.. tena mwajisifu mna ng'ombe kumbe mna makinda ya mbwa!
ReplyDeleteHuyo ni nabii wa watanganyika tu!
KISHERIA HAMNA MWENYE HAKI YA KUZUWIA HORUBA ZA MWALIMU, WALA KUSIJE NA SWALA LA HAKI MILIKI HAPA KWA VILE NI MALI YETU SOTE, ALIKUWA ANAHUTUBIA AU ANAFANYA KAZI KWA AJILI YETU SISI NDIO TULIKUWA MWAAJILI WAKE TULIMUAJILI ATUFANYIE KAZI KWA KUMCHAGUWA KWA KURA ZETU HIVYO HOTUBA ZAKE NI MALI YA WATANZANIA WOTE, HAKUNA HATA MTU MMOJA MWENYE HAKI YA KUSIFICHA, KWANI KUFANYA HIVYO NI KUWANYIMA WATANZANIA HAKI YAO YA MSINGI. HUKU KWA WENZETU WATU HUENDA KWENYE MAKUMBUSHO YA MARAIS WAO WALIOPITA KUANGALIA NYARAKA ZAO BILA YA MALIPO YOYOTE. KI MSINGI HOTUBA ZAKE NI MALI ZETU, MTU AKITAKA APATIWE BASI APATIWE, AU KAMA WANATAKA KUZIUZA WANAWEZA KUZIWEKA KWENYE CDs NA KUZIUZA NA PESA ZAKE ZISAIDIE WATOTO, WAZEE NA MASIKINI PAMOJA NA MIRADI YA KIJAMII YA MAENDELEO.
ReplyDeleteMIMI NIMELIFANYIA KAZI HILI SWALI LA KUFICHWA HIZI HOTUBA ZA MWALIMU.KINYUME NA WANAVYOFIKIRIA HAO WANAOSEMA KUWA MWALIMU NI NABII,UKWELI NI KUWA MWALIMU ALIKUWA NI BINADAMU NA MWENYE MAPUNGUFU MENGI. MAWAZO YA MWALIMU YALIJENGWA NAKUEGEMEA KWENYE SIASA ZA KIKOMUNISTI ZA KICHINA NA KWA WANAOKUMBUKA,MACHINA,WARUSI NA WAJERUMANI MASHARIKI NDIYO WALIKUWA MARAFIKI ZAKE WAKUBWA WAKATI WA UTAWALA WAKE.NI SIASA ZA NDOTO ZILIZOJAA MANENO MAZURI YA KUONDOA ''UNYONYAJI'' NA WATU KUWA NA HALI SAWA LAKINI KIUTEKELEZAJI NI ILE ILE DANGANYA TOTO.MWALIMU ALILAZIMIKA KUACHIA NGAZI BAADA YA KUONA UKOMUNISTI UMEGONGA UKUTA NA UMEANZA KUPOROMOKA KUANZIA KULE UJERUMANI MASHARIKI. HAKUTAKA YA MKUTE YALIYOMKUTA RAFIKI YAKE MKUBWA, ERICK HONECKER. PIA ASINGEWEZA KUPANDA JUKWAANI NA KUURLEZA UMMA WA WADANGAYIKA KUWA YALE MAHUBIRI YOTE ALIYOKUWA AKITOA NI WACHINA NDIO WALIOMPOTOA,SASA VUENI VILE VISUTI VYA CHUN LAI,TUANZE UPYA. KAZI HIYO ALIMWACHIA MWINYI AMBAYE ALIIUFUTA UJAMAA KISIRISIRI.
ReplyDeleteKWA HIVYO HOTUBA ZAKE NYINGI ZINAZUNGUMZIA NDOTO ZA ALINACHA AMBAZO ZIMEFELI KILA PAHALA DUNIANI NA HATA HAO WAALIMU WAKE WAKUU WAMEGEUZA KIBAO.UKIZISIKILIZA BAADHI YA HIZO HOTUBA NI FEDHEHA KWA ULIMWENGU WA SASA ULIVYOGEUKA.KWA HESHIMA KUBWA YA MWALIMU HOTOBA HIZO NYINGI ZIMEFICHWA ILI KUMSITIRI.
Yaani nimesikiliza hotuba moja ya Mwalimu last week, I really cried. Kwa sababu yote aliyoyasema na watu walikuwa wanamshangaa vipi baba wataifa anakuwa mkali kuhusu miiko ya uongozi? Na yote aliyoyasema ndiyo yanayotokea katika nchi nyingi za africa. Amezungumzi kwa urefu kuhusu miiko ya uongozi na madhara yake ikiwa viongozi wa nchi hawatofuata miiko hiyo na nini cha kufanya kuepuka uvunjaji wa miiko hiyo ya viongozi. Jamani hizi hotuba specifically alizotoa kwa kiswahili zingetafutiwa translation na ikiwezekana serikali ianzishe "J.K. Nyerere online library" ambapo watu wataweza kuzipata hizo speech na vitabu vyake alivyotunga, hata kama ni kwa kulipa pesa kidogo, nina hakika watu wengi hawatajali kulipa ili waweze kuwa na access ya hizi information. We were blessed to have a visionary leader, kutokuwepo hapa duniani siyo sababu ya kuyasahau yale mazuri aliyoyafanya. Watoto wetu hawajui kuwa tulikuwa na nchi iliyohehimika kwa kuwa na viongozi imara na waadilifu! Speech zake zinawalenga viongozi wengi, is this the reason ya kuzibania? Tadadhali tuelezeni ukweli. Hata huku Marekani speech za Regan zipo zinauzwa online na madukani kwa nafasi yako ukitaka una nunua anytime, so how about za baba yetu wa taifa?
ReplyDeleteNabii hakubaliwa kwao. Labda ni unabii wake kama huo hapo chini tuliomuvuzishiwa na mwanazuoni fulani unaofanya waogope kurusha hotuba zake. Unabii huu Mwalimu aliutoa zamani sana kabla hata ya zama hizi za kasi mpya:
ReplyDelete"And there is in Tanzania a fantastic amount of talk about getting money from outside. Our Government, and different groups of our leaders, never stop thinking about methods of getting finance from abroad. And if we get some money or even if we just get a promise of it, our newspapers, our radio, and our leaders, all advertise the fact in order that every person shall know that salvation is coming, or is on the way. If we receive a gift we announce it, if we receive a loan we announce it, if we get a new factory we announce it – and always loudly. In the same way, when we get a promise of a gift, a loan, or a new industry, we make an announcement of the promise. Even when we have merely started discussions with a foreign government or institution for a gift, a loan, or a new industry, we make an announcement – even though we do not know the outcome of the discussions. Why do we do all this? Because we want people to know that we have started discussions which will bring prosperity"
Katika search zangu nimekuta speech za mwalimu in the following websites, so check them out!
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=N-QUwbSHwJQ&feature=related
http://www.youtube.com/watch?v=XvVtJGCw8T4&feature=related
Kummbe ni kweli hili tatizo limewakera wengi?Nilidhani niko alone:Ni majuzi tu nilitoa comment kuhusu hili suala:Serikali iziachie hizo hotuba ni nzuri sana;mimi ninayo kanda moja naitunza kama nini:Tena ziwekwe kwenye CD,TBC wanazi edit ndiyo wanazirusha
ReplyDelete"Paka akiondoka panya hutawala". Nilikuwa naandika paper kuhusu kuporomoka kwa Elimu Tanzania. Nilistaajabu kweli serikali ya Tanzania imelaaaaala ikikoroma hata huikuwa rahisi kupata takwimu au maandika ya nyerere kuhusu elimu. Isingekuwa juhudi za Haki Elimu kuweka hutuba za Mwalimu juu ya Elimu katika tovuti yao ningelamba F kwanye topic nilojichagulia. Nchi zingine wana-enzi sana waasisi wao, na hata ukitaka maandiko yao unapata kirahisi sana. Marekani hapa huwezi kumsema vibaya muasisi wa Taifa hili-utasutwa au kushughulikiwa-very unpatriotic kutothamini waasisi. Tanzania-ni ujanja ujanja tu na vidharau.
ReplyDeleteNilishangaa kuona Idi Amini ni documented zaidi kuliko nyerere. Very strange. Sijui nani ataja ibuka na kudocument au kuweka wazi vitu rahisi kama speeches za viongozi.
Nimekuwa nikihitaji mmmmno kupata video na audio za nyerere tangu miaka ya sitini hadi 90s lakini utaziona wapi Tanzania. Unajua Serikali ingepata hata fedha nyingi kwa kuandaa vitu hivi na kuuza kwa watu wanaotaka. Aibu mno that you can't get things like this from Tanzania. Sijui nani aisafishe nchi hiii????
Katika kumkumbua Mwl JKN, Nimeona nigusie hiyo taarifa ya dada ambaye anatafutwa aliyeiba kuna watu wana chuki ambazo mwl alihutubia wakati akiongea na waandishi wa habari Tarehe 27, NOV,1993,siku ya Jmosi,KUHUSIANA NA ZANZIBAR,TANGANYIKA na MUUNGANO.Aliona yajayo ingawa hakuwa Nabii. I love Mwalimu.
ReplyDeleteNatamani sana hotuba ya mwalimu aliyoitoa kuhusu muungano wetu WABUNGE WOTE waisikilize, na watanzania wote BARA na VISIWANI nao waisikilize, kisha wote waitafakari na kuitafakuri.
ReplyDeleteNi kama nabii... ila huwa naogopa sana pale anapolaani watakaovunja muungano. LAANA!
Hizi hotuba zingekuwa zinapatikana kwenye midia tofauti tofauti watu wanunue wasikulize. Jamani wajasiriamali, mnaweza kufanya mambo kwa taratibu zinazokubalika! ?
Nyerere atakumbukwa kwa mengi, ila hili la muungano, ufisadi, rushwa na 'uuzwaji' wa mali asili kusiko mjali masikini atakumbukwa daima.
Was a brilliant philosopher and one of the most greatest and respected leader. Ni kiongozi gani kama Rais (mstaafu) na mwanachama wa chama tawala anaweza kuadvocate mfumo wa vyama vingi nchini kwake ili 'aimarishe' chama chake? Who in the world?
Hata wakibania hotuba, tutakukumbuka Mwalimu.