Na Makubo Haruni wa Daily News, Tarime
WATU watano wamelazwa baada ya kukatwa mapanga katika ugomvi wa kugombea uwanja wa mpira mjini hapa kwa ajili ya kutua helikopta za kampeni za Chadema na CCM jana.
Vyama hivyo vinatumia helikopta katika hatua za mwisho za kampeni, Chadema ikiwa imeanza kuitumia kuanzia juzi, wakati ya CCM iliwasili kwa mara ya kwanza jana.
Watu waliokatwa mapanga ni Masanda Edward, Athuman Selemani, Mahende Daniel, Genya Sabai na Modesta Mwita ambao wamelazwa katika Zahanati ya Tarime mjini hapa.
Ugomvi huo ulitokea majira ya saa nne asubuhi uwanjani hapo baada ya wafuasi wa Chadema kutinga uwanjani kwa ajili ya kusubiri helikopta yao maarufu kama ya Mbowe, iliyokuwa itue kwa ajili ya kuwachukua viongozi kwenda kufanya kampeni.
Habari kutoka uwanjani hapo zilizothibitishwa na Katibu Mwenezi wa CCM wilayani Tarime, Samwel Kiboye, zilieleza kuwa uwanja huo ulikuwa umeombwa kwenye Tume kwa ajili ya shughuli maalumu kupokea helikopta ya CCM, na kwamba ugomvi ulitokea baina ya pande hizo mbili kutokana na wafuasi wa Chadema kugawa uwanja huo makundi mawili kwa ajili ya kutua helikopta hizo.
Hata hivyo muda mfupi kabla ya kufika kwa helikopta ya Chadema, kulitokea majibizano kati ya wafuasi hao na wanaodaiwa kuwa ni wa CCM, kuchomoa mapanga na kuanza kuwashambulia wenzao na kuwajeruhi.
Kitendo hicho kiliwavuta watu wengi na kufanya helikopta ya Mbowe isitue uwanjani hapo na rubani wake kulazimika kutafuta eneo jingine katika uwanja wa Kanisa la Anglikana ambako ilitua na kumchukua Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na mgombea ubunge, Charles Mwera, kwenda kwenye kampeni.
V iongozi wa Chadema akiwamo Mkurugenzi wa Vijana na Mambo ya Nje, John Mnyika na mgombea udiwani wa chama hicho waliijia juu Polisi kwa kutowakamata watuhumiwa hao, licha ya wao kuwataarifu waliohusika na gari walilokimbizwa nalo.
Wakati hayo yakitokea katika kampeni za kumsaka Mbunge wa Tarime kumrithi Chacha Wangwe, aliyekuwa kada wa CCM aliyehamia Chadema amesema kuwa alifanya hivyo badala ya kusubiri kufukuzwa.
Kada huyo, Chacha Mwikwabe, ambaye aligombea ubunge wakati wa kura za maoni CCM, ameeleza kuwa kitendo cha kumtoa uongozi wa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Mkoa na kwenda kuwa karani wa Mwenyekiti wa Taifa wa jumuiya hiyo, kingemfanya kuwa mpika chai.
Amesema ubaguzi aliofanyiwa na kuandamwa kutokana na kukemea mafisadi ndani ya CCM, kulisababisha kuchukiwa na Nchimbi na Yusuf Mkamba, hali iliyomfanya apatwe na wasiwasi na kuamua kutimka kabla ya kutimuliwa.
Ameiponda CCM kwa kile alichokieleza, kuiga Chadema kutumia helikopta katika kampeni huku akiapa kuongoza vijana wa Chadema kudai ushindi iwapo CCM itatangazwa mshindi hata ikibidi kumwaga damu.



CHADEMA iokoe nchi hii kutoka kwa mafisadi.
ReplyDeleteHakuna cha wana-ccm wala wana-chadema wote ni wachovu tu.Hapa watadanganywa kuwa hiyo ndege "edikopta" ipo kuwashughulikia wananchi lakini atakayeweza hata kuigusa atakuwa mmoja tu.UCHOVU wa kifikra umejaa sana hasa mikoani.
ReplyDeleteHakuna cha wana-ccm wala wana-chadema wote ni wachovu tu.Hapa watadanganywa kuwa hiyo ndege "edikopta" ipo kuwashughulikia wananchi lakini atakayeweza hata kuigusa atakuwa mmoja tu.UCHOVU wa kifikra umejaa sana hasa mikoani.
ReplyDeleteTungekuwa na Tarime 20 tu Tanzania wallah kingeeleweka!
ReplyDeleteHaipendezi kuona siasa za kuchomoa mapanga but at some point inafurahisha kuona level ya civic competence. Chadema inaonekana kupata support ya vijana hasa kutokana na sera zake kuwa na mlengo wa vijana na kuwafanya vijana Taifa la jana i.e Nchi imechelewa kuwashirikisha katika mipango ya maendeleo. Lakini hao vijana wa Chadema wanaperform vyema kuliko wazee wa CCM japo sikatai hata chembe mchango wa wazee lakini kwa Chadema wazee wamebaki kuwa washauri akina Bob, Prof. Baregu etc.
Nikiwaangalia akina Zito, Mdee, Mhongwa, Mnyika wanang'ara kuliko kundi kubwa la CCM. Nadhani ni wakati CCM iangalie sera zake na iache kuwaideline vijana kama akina Nape coz hao wakiamua ndio wanaweza kuwa waasi wakubwa wala si akina Malechela.
To me Chadema seems to be a only remining visionary party and worth talking about.
MIKONGONGORO sijui kama hata wilaya yako ina mwamko kama wa wanatarime wasioyumbishwa hata na propaganda mana propaganda iliyopigwa juu ya Mzee wa Bills sikujua angekanyaga lakini kakanyaga na watu wakakanyagana kumpokea!!!
Watu watatu tu ambao ni MBOWE,SLAA na Zito kabwe na helikopta yao moja wanaipelekesha puta CCM NA polisi kiasi cha kufanya CCM Uongozi karibu wote uhamie Tarime na wakuu wa polisi wa ngazi za juu karibu wote wahamie operation tarime.
ReplyDeleteHivi nchi hii ikipata wapinzani kama 30 tu kama Zitto,Slaa,Mbowe wenye helikopta 10 tu kwenye majimbo 10 wakati wa uchaguzi sijui CCM na polisi wangefanyeje.
Hapo Tarime ni watu watatu tu wanawaitoa CCM jasho hivyo!
Nilichojifunza ni kuwa watu hata wakiwa wachache kama wamedhamiria wanaweza peleka mbio na puta iwe serikali au chama tawala kikongwe.
Nadhani CCM wawe serious wanakoelekea jasho litawatoka kama hawatajali kutekeleza sera zake vizuri za maisha bora kwa kila mtanzania.Kama wataendelea kuchekeana uchaguzi ujao jasho jembamba litawatoka.
koloboi@yahoo.com
Punda ni yule hyule libadilikalo ni soji tu afrika nzima!
ReplyDeletewanasiasa hupanda majukwaani kudanganya, mlala hoi anapanda jazba anaanza kugombana na wenzake, majirani na hata familia kufika kuuwana. wakati huo huo wanasiasa wako makwao na katika maofisi wanakula raha. na wapatapo wakitakacho huwasahau waliomwaga damu zao na kupoteza nguvu zao ili mabwana wa siasa zo washinde.
mfano mzuri na wa karibu ni yalotokea kenya na zimbabwe. viongozi wamepata yao wako wanachekelea, wanyonge walopoteza nyumba, mali na ndugu hawana walopata.
watanzania amkeni! siasa za afrika hazimnufaishi mnyonge ng'o!!!!!!!!!!!
Mapanga ni ya kazi gani?
ReplyDeleteHalafu polisi ya tanzania ingeweka nembo ya ccm tu...maana imezidi kuwapendelea.
Polisi inatakiwa kuwa public body isoyofuata chama chochote. Lakini bongo...duh!
Itabidi tuzidi kupambana.