Kijana wa Kitanzania Bw. Ndalima Nzaro yuko mahututi kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan Ann Arbor, nje kidogo ya Jiji la Detroit nchini Marekani baada ya ajali iliyosababisha na kijana wa miaka 15 aliyeiba gari kugonga gari la Ndalima lililokuwa limesimama kwenye taa za kuongozea magari likisubiri rangi ya kijani.

Kijana huyo aliyegonga gari alikuwa anafukuzwa na Polisi. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mji mdogo wa Westland kijana huyo aliyeiba gari na ambaye hakuna leseni ya kuendesha gari alikuwa anaendesha gari kwa kasi zaidi ya maili 100 kwa saa na aliyagonga magari ubavuni yaliyokuwa yamesimama hapo kwenye taa za kuongezea magari kwenye barabara ya Merriman.

"Wale madereva waliokuwa wanasubiri rangi ya kijani kuwaruhusu hawakuwa na jinsi yeyote ya kukwepa ajali hiyo" alisema Chifu Jim Ridener. Bw. Ndalima aliyekuwa anaendesha gari ndogo aina ya Honda Accord alitibiwa kwa dharura kwenye hospitali ya Garden City lakini kutokana na majeraha yake aliitiwa Helikopta ya Hospitali ambayo ilimchukua na kumkimbiza kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan mjini Ann Arbor.

Hospitali hiyo ni mojawapo ya hospitali zenye uzoefu mkubwa katika kuhudumia dharura za ajali katika eneo hili la Michigan. Mtoto huyo wa miaka 15 alikuwa anaendesha gari aina ya Mercedes Benz S55MG ambalo ni la rafiki ya kiume wa mama yake.

Kutokana na kijana huyo kuwa chini ya umri jina lake halitajwi kwenye vyombo vya habari. Hata hivyo kijana huyo yuko mikononi mwa Polisi wakati uchunguzi ukiendelea na mashtaka dhidi yake yatategemea hali ya Ndalima inaendeleaje. Habari ambazo tunazipata sasa hivi, hali ya mgonjwa siyo nzuri. Tutawaletea habari zaidi kwa kadiri tunavyozipata.
klhnews.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Watu wa Michigan, update zozote?

    ReplyDelete
  2. Ninampa pole sana mdau mwenzetu.Mungu atakusaidia.Tuko pamoja.

    ReplyDelete
  3. Ndugu na marafiki popote pale mlipo, tujumuike pamoja kumuombea mwenzetu Ndali. Ndugu yetu amepambana na madhara ya ajali hii mbaya kwa zaidi ya masaa 48 sasa. Tuungane na ndugu yetu Ndali kwa njia ya maombi katika kuyakabili madhara haya.

    Tunamuomba Mwenyezu Mungu amshushie baraka zake ndugu yetu Ndali, tunamuombea amjalie tiba ya kuweza kuijenga na kuirudisha afya yake, Amen.

    Obay 87.

    ReplyDelete
  4. Unajua hili ni dili?Mlio bongo unaweza Kufoji jina na kuitwa Michuzi nzaro ukiwa na ujumbe wa watu sita katika familia mnakuja kumjulia hali mgonjwa.Tatizo wabongo mmezubaa unasubiri mpaka awe ndugu yako kweli ,MCHONGO HUO SHAURI YAKO!!!!VIZA NJE NJE HAPO.

    ReplyDelete
  5. MICHUZI MIMI NIPO UWANJA WA FISI SINA HABARI NDIYO KWANZA NAFUNGUA HII BLOG SASA NAULIZA MAREHEMU ALIKUWA ANA SPEED AMA ILIKUWAJE? HII INANIOGOPESHA SANA KWENDA ULAYA MAANA TOFAUTI NI KAMA HII UKIFARIKI INAKUWA MZIGO KWA FAMILIA NA WATU WENGINE WANAO KUSAIDIA. NAWAOMBEA WOTE WALIOFIKIWA NA HILI JANGA NA KAMA KUNA MICHANGO BASI NAOMBENI HIYO ACCOUNT YAO. ASANTE SANA WOTE MLIOTUJULISHA HUU MKASA MKUBWA KABISA....EX MUZUMBE NA ST. ANTONY MBAGALA.

    ReplyDelete
  6. Pole sana Mungu atakusaidia, je huyu ni mdogo wake Mboja Nzaro?

    ReplyDelete
  7. jamani watanzania hamenu michigani especially detroit

    ReplyDelete
  8. Kuna habari zilizo patikana punde kwamba bwana Ndali amefariki dunia.sasa jamani kama wanablog wako tunaomba wa update news hili huakika hupatikane na watu wajue jinsi gani ya kujikusanya pamoja kufuata utaratibu utakao pangwa na jumuhia ya michigan.
    Bwana ndali alikuwa mtu wa watu na mwenyezi mungu hamlaze mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  9. Yes Bwana Ndali amefariki dunia hivi punde tu.Ni habari ya kusikitisha sana dada Saada pole sana na mtoto wa marehemu pia na ndugu na wazazi wa marehemu.Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa jumatano kwenda Tanzania.Bwana ametoa na bwana ametwaa.Mdau Ohio

    ReplyDelete
  10. wewe peter nalitolela marehemu gani unayemuongelea wewe na wakati habari inasema yuko mahututi?nyie ndio mnawanga mchana mchana,embu tusimuombee mwenzetu mabaya kha!

    halafu huyo nae anaesema visa nje nje ana njaa za asubuhi,sio kila mtu anataka kuvamia marekani siku izi..been there,done that..watu wanapakimbia. bongo dili wewe

    miss keys

    ReplyDelete
  11. kama Ndalima nnayemjua mimi mdogo wao kina Mwamvita na Iddi nzaro. Mungu amjaalie nafuu nimepoteana naye siku nyingi.sasa napata habari hizi..Ugua pole Ndalima. Ondo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...