miji yote bongo ingekuwa tambarare kwa unahifu na usafi mambo yangekuwa mswano kabisa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. sijaweza bado kuiznguka Tanzania yote... inagwa nina hamu ya kufanya hivyo siku moja. Ila katika miji kadhaa niliyofika, Moshi naukubali kwa unadhifu. Moshi ni pasafi mno; wanapiga bao hata majiji makubwa ya Dar, Mwanza na Arusha

    ReplyDelete
  2. Nasikia kuna mpango madhubuti wa kuufanya mji wa Moshi uwe jiji ifikapo 2010.
    Ule mji unakua haraka sana kwa kweli, yale mambo ya mji kulala saa 11 jioni hamna tena. Nadhani pia kufunguliwa kwa vyuo vikuu kumechangia kupachangamsha kwani demand za wasomi/ wanafunzi ni tofauti.

    I think it deserves the "city" status, even more than Arusha does, it is a very well-planned town.

    ReplyDelete
  3. Eh... jamani Moshi looks good, still got the green...amazing.

    ReplyDelete
  4. Moshi will always be in my heart! No place like home...
    Wakiamua kuufanya jiji au wasiufanye mimi sijali. All that is needed is to keep up the good work
    Lakini nasikia kuamisha kiboriloni haijafanyikiwa hata kidogo. Pale Memorial wangegeuza uwanja wa michezo tu. Iwe kama theme park. haya ni maoni tu kwa town planners.

    mtoto

    ReplyDelete
  5. Sijawahi kufika Moshi bali mara kwa mara watu wana pasifia kwa usafi. Soko la Moshi mjini wana sema hakuna inzi wa harufu. Tena nasikia Moshi jijini ni kusafi kuliko hata Moshi mjini. Nashindwa kuelewa halimashauri za miji mingine zina fanya nini? Hapa kwetu Morogoro sokoni pana nuka kama yai bovu kila siku. Ningelikuwa na sauti kwenye Manispaa yetu, ninge pendelea viongozi wa Manispaa ya Moro. wapelekwe Moshi wakajifunze jinsi wenzao wanavyo tunza mji.

    ReplyDelete
  6. Mi nimeoa Uchagani na Mke wangu kwa kweli ni msafi kupita kiasi.

    Akikanyanga hata punje moja ya mchanga ndani ya nyumba lazima ashike fagio na kuiondoa.

    Kama anajisikia ahueni atapiga deki kabisa.

    Na siku moja nilijasahau nikaingia ndani na viatu, aisee nilikoma sitakuja kujisahau tena kuvua viatu.

    Kama Moshi iko hivi kwa kweli sishangai. Naona Wachaga usafi ni asili yao.

    Labda wengine mliooa Uchagani mnasemaje?

    //Mdau

    ReplyDelete
  7. Msichekeshe MOSHI gani hiyo mnayosema ni safi, au mnapita ndani ya Bus na kuona maua sehemu moja mbili hivi ndo mnasema ni msafi! ni mchafu, tembelea sehemu zote uone ulivyo mchafu, go stand ya MABUS,Sokoni na barabara, kwanza ni mchakavu na haukuwi, unadumaa tu. even the town population is too small.

    ReplyDelete
  8. Moshi pasafi pale katikati ya mji tu kama ilivyo kwa miji mingi ya TZ.Mi bado napapigia chapuo A-Town.Hiyo keep left naikumbuka,halafu ukizunguka hivi...unaelekea 'dabo rodi' unapita NewCastle Hotel kuelekea kwenye mitaa ya uchafu!!

    ReplyDelete
  9. Wewe Anony.Tarehe October 09, 2008 5:58 AM,

    Sitaki kubishana na wewe nimepata bahati ya kukaa mikoa 10 hapa Tanzania yenye majina makubwa lakini kusema kweli Moshi haina mpinzani kwa usafi hilo nakubali.

    Napenda kumjulisha mdau aliyesema kuhusu michezo ya watoto kama unakumbuka viwanja vya manispaa maarufu kwa jina la Uhuru Park - basi kunatengenezwa michezo ya watoto ya kisasa na bustani za mapumziko- TUSUBIRI.

    Kuhusu Kiboriloni kwenda Memorial ni kweli sio idea nzuri ila nadhani madiwani wetu watatafuta mahali muafaka kwa shughuli hiyo ya soko la mitumba mahali pengine.

    Soko la Moshi ni kweli hakuna uchafu - ukiingia unasikia harufu ya fresh food au viungo vya pilau nk hakuna ma-inzi kama masoko mengine kabisa.

    CHANGAMOTO KWA MABOSI YA MASHIRIKA YAFUATAYO
    TIGO, ZAIN, ZANTEL, VODA, TTCL NA MABENKI YOTE.
    Nawashauri mfikirie mradi kwa hawa akina mama wanaouza vitu nje ya soko mara soko linapofungwa. au kwa wale ambao hawana meza ndani wametengeneza tu stand za mbao tengenezeni mobile table za kuuzia vitu ambazo pia zina shade kwa juu kuzuia jua.
    Pongezi kwa VodaCom kwa mradi kwa shoe shiners.

    ReplyDelete
  10. Sina kawaida ya kuchangia but hii picha imenikuna, Yani wewe unaesema MOSHI kuchafu una CHUKI BINAFSI, Eeehee Moshi huwezi kukuta watu wanakojoa kojoa ovyo kwenye mauchochoro wala kutupa uchafu, ukishikwa ni faini elfu 20 on the spot hakuna mjadala sasa kazi kwako kama huna hiyo hela unaenda central. Moshi ni mji ambao ni msafi sana hata mvua ikinyesha huwezi kukuta maji taka yanatiririka ovyo mitaani kama kule k/koo ni kusafi haswaaaaaaaa kama unabisha ochoo kuchela.kuonyesha msisitizo.

    ReplyDelete
  11. Yaaani wadua mnapozungumza Moshi kuwa safi mnabidi msisahau walio uwezesha mjii huu kuwa msafii.. kina Waaheshimiwa Papaa Stan Meneja Masoko Mwandamizi wa masuala ya Computer kwenye kampuni flani ya Mjini moshi akishirikiana na Mh. Tito ambaye ni mkurugenzi mwakilishi wa Maswala ya Jamii na Jinsi kwa Kizazi kipya wa kampuni fulani hapa Mjini moshi.. Hao ndio tunaona wanaweza wakapewa pongezi za dhati kwa kushirikiana na hamashauri ya mjii huu wa moshi...
    Alfosi. M.Materuu.
    Mdau Moshi.

    ReplyDelete
  12. Anony. wa 5.27 usitudanganye hapa hata kidogo, huyo mkeo kazaliwa na kukulia mjini, ni sehemu ndogo sana kutoa conclusion ya kuwa wachaga ni wasafi. Pili Moshi mjini sio pa wachaga peke yao kumbuka, ule ni mji na pana mchanganyiko wa makabila mbali mbali.
    Tatu, Elewa ya kuwa usafi ni tabia ya mtu, sio suala la jamii ya watu fulani ndio wasafi.

    Nne, fika inaonesha umehudhuria shule na si kuwa umesoma. hii ni kwa mtazamo wangu kulingana na maoni yako. Mwisho, nataka nikujulishe tu ya kuwa leo nimechoka na masuala ya BOX kwa ujumla, vingenevyo ningekuchambua vilivyo. Pamoja na hayo siwezi kukuacha upite bure " Guruguja mkubwa we"!!.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...