Mpiganaji Athumani Hamisi, Mhariri wa Picha wa magazeti ya habariLeo na Habarileo Jumapili (pichani) ambaye yupo Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kupata ajali mwezi uliopita maeneo ya Kibiti akiwa njiani Kwenda Kilwa kikazi amefanyiwa operesheni jana.

Taarifa zinasema kwamba operesheni hiyo imefanikiwa. Hata hivyo haikuzungumzwa mipango yake ya tiba.

Hata hivyo inasemekana kwamba madaktari hakuwaridhishwa na jinsi mgonjwa huyo alivyocheleweshwa kufikishwa hospitalini kwa matibabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Loh.Mungu atakusaidie Athmani upone haraka.Hao madaktari wa Sauzi wasitubabaishe na sisi tuna madaktari wetu.Walitaka afike tu muhimbili na kukimbizwa tu kwao bila kufanyiwa utafiti(na madaktri wetu).Wasidharau madkatari wetu.Mimi siyo daktari lakini nadhani kabla mgonjwa hajawa 'referred' hospitali za nje lazima madaktari wetu wamchunguze mgonjwa kuona kama tatizo linaweza kutibika hapa nchini.Na kama atasafirishwa apewe huduma gani aweze kufika huko.

    ReplyDelete
  2. Sauzi, hospitali gani??. Au mji gani?. Kwa nia nzuri tuu.

    ReplyDelete
  3. Kaka michuzi nilivyoona jina la Athumani na picha yake nilishtuka kabla sijasoma nikawasitaki kuangalia chini du mungu mlinde apate nguvu kaka wa watu

    wako mdau

    ReplyDelete
  4. pole zake athuman hamisi, watajitahidi si hata hivi karibuni kuna watu walikua hospitalized uko bondeni, wanavumilia tu watu wa watu wafanyeje.

    ReplyDelete
  5. wewe usilaumu madaktari wa afrika kusini kusema amechelewa ni kweli alichelewa kwa uzembe wa mtu mmoja tu huko wizara ya afya aliyekuwa akizungusha kutia saini yake sijui alitaka rushwa au vipi. inabidi hao watiaji saini wachunguzwe kwani ndiyo wanaosababisha vifo vya ndugu zetu na fedha za serikali kupotea.

    ReplyDelete
  6. Kaka Athuman Hamis pole sana kwa ajali iliyokukuta. Mwenyezi Mungu muweza wa yote atakusaidia upone haraka!

    Rafikiyo wa Darfur, Sudan

    ReplyDelete
  7. annon wa pili juu,,,hahahahaaaa hujatulia kbs
    annon wa pili toka mwisho ni kweli yan kuna mafisadi Tz adi kero yan mtu kutia saini apo tu adi apangiwe faili akae azunguke na kiti mara ooo nna kikao,nna kazi wakati kitu ni uhai wa mtu apo??ingekuwa vingine kweli,,,nyamafu wakubwa wooote waaanguka saini wanaongojea rushwa kwa matatizo mazito ya watu,,,washindwee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...