Kaka Mithupu!
Habari za kazi? Samahani sana kwa usumbufu, naomba msaada wako. Namtafuta kaka yangu John Mashaka, ambaye ni mtoto wa baba yangu modogo .Tumepotezana mawasiliano takribani miaka 14.


Tangu tupo shule za msingi hadi leo hatujaonana Baada ya kuona video yake uliyoiweka kwenye daily news website, http://dailynews.habarileo.co.tz/streaming/?vid=USbasedTanzanianSocialactivistJohn

Mashakatalksofhisexploits.flv&id=110
nimeamua kukuomba msaada ili kuwasiliana naye, na pia kumpa pole kwa kufiwa kwake.kadhalika pongezi kwa kazi zake nzuri.

Yeyote anayeweza kunipa contcts zake, tafadhali niandikie floramarwa@gmail.com

ila sitaki uzushi kwa maana sisi ni ndugu
Asante sana wadau wote,
tuendeleze libeneke
Dada Florence,

Leeds UK.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Ndugu yako lakini huna mawasiliano naye miaka 14!!!??

    ReplyDelete
  2. watu tungekuwa tunatumia majina yetu ya kweli kwenye bulogu au forums basi tusingepata matatizo ya kama huyu mwanakijiji mwenzetu.

    ReplyDelete
  3. Dada yangu Florence, kwanza pole kwa maana waosha vinywa wanakuja kwa hasira na vishindo,jitayarishie makombora!

    Ila katika uchambuzi wangu nimeona kwamba hauna la maana kwa sababu, kwanza sidhani Mashaka anaweza kukukubali, ila nakupa ushauri mzuri

    1. Ungeenda Gym upunguzi vinyama.
    2. Uachane na mapozi ya kishamba
    3. Achana na Masupa Stars (maarufu)
    4. Ridhika na ulichonacho,
    5. Usipende sana vi- ATM
    6. Wakubali watu wa upeo wako
    7. Achana na kupiga picha vitandani
    8. Punguza kwend akwenye ma gesti
    9. Punguza Uongo, siyo ndugu yako
    10.Usitafute wanaume kwa kulazimisha

    Mashaka, anakaa nyumbani kwangu nimemuajiri katika grocery store yangu, na nitamuoza mdogo wangu.
    Kwa hiyo wasiliana na mimi kwanza ili nikupe data zake zote 0713-457-1204

    ReplyDelete
  4. Siku zoooote usimtafute...leo kwasababu jamaa mambo yake poa ..unajifanya ndugu!...Kama ulikuwa unania ya kujua ndugu yako yuko wapi kwanini usimtafute wakati huo Mashaka yuko Mkoa!!! Dada acha uzushi!.

    ReplyDelete
  5. Wewe Dada, na akili yako timamu, unakuja kumtafuta Mashaka huku? Wenzako wazuri wasomi wameshindwa, sasa wewe wazimu gani ilikuingia na kuja kuingia na gia kama hiyo ya kishamba. Haya tutaona kwa maana Manka Mushi kashindwa

    Wewe hauna lolote huku unawatafuta watu wenye vijisenti vyao? Unadhani utajiri wake aliuokota? Huyu jamaa inaonekana kapigika sana

    Heri hata Ungejaribu Kinje mtoto wa mjini ingekuwa afadhali kuliko ya Mashaka. Sikulaumu lakini kila la kheri

    Mnyamwezi

    ReplyDelete
  6. Mbona unazua maswali mengi yasiyokuwa na majibu? Ndugu yako miaka 14, alafu ushindwe kuwasiliana naye. Mtoto wa baba yako mkubwa umtafute tu kwenye mtandao? Kazi ipo bongo.

    Dada mimi nafanya biashara ya dhaabu, malipo yangu ni Dollar millioni 5 kwa mwaka. Nitakununulia Toyota Harrier, kukujengea nyumba mbezi na kukupeleka shopping Afrika kusini.

    Kwa hiyo Maswala ya Mashaka hachana nayo, mimi pia kazi yangu inashinda wall-street yake. Ikiwa hamjaonana miaka 14 basi hakuna faida tena. tuwasiliane basi 0786-221-5411

    ReplyDelete
  7. Florence, ukimaliza shuguli zako hotelini, mbona usitandike kitanda vizuri. Sasa Mashaka atakuja kulala huko kweli? Haya Jaribu bahati yako.

    ReplyDelete
  8. Hii kamwe haitasaidia kumuongezea yeyote umaarufu hapa, acheni mambo ya kuzunguka zunguka kumhusu huyu jamaa.

    Sikiliza dada, kwa nini usizuru tovuti yake ambayo ina contacts zake kama ifuatavyo hapa chini na uzitumie kuwasiliana naye?


    http://www.mashakafoundation.org/contacts.html


    The John Mashaka Foundation

    Tel: 704-469-0728

    JMfoundation@mashakafoundation.org


    Kaka Michuzi huna haja ya kunibania hii maana situsi mtu hapa nachosema ni ujumbe kwa Mashaka kuwa ;

    "TENDA WEMA UENDE ZAKO, EPUKA MATUMIZI YA MASS MEDIA YASIYO YA LAZIMA'"

    ReplyDelete
  9. Sasa picha ya kazi gani?...Miaka 14 atakukumbuka na picha ya leo?...at least ungetuma ya enzi hizo....tehehehe
    Pili: Ndugu yako unamtafuta kwenye libene ya jamii?
    Hujui kwao au ni vipi?
    Hii ishu haijatulia kabisa...
    Anyways...tutakuombea umpate

    mtoto

    ReplyDelete
  10. Huyu msichana kanishangaza sana kumtafuta kaka yake mtandaoni. Ninavyojua undugu si mtu mmoja tu, kama kaka yako basi mnao pia mama, dada, shangazi, mjomba, na wengine wengi ambao ni ndugu zenu. Ina maana hao wooote hawajui aliko Mashaka mpaka uje umtafute humu? Hapa kuna lingine!

    ReplyDelete
  11. hii imekaa vibaya dada yangu, wee ni flora marwa, utakuwa mkurya wa mara ndio, mashaka ni mjaluo wa shirati, iweje baba yako mkurya awe kaka wa baba wa mashaka ambaye ni mjaluo??
    jaribu kuunganisha huo undugu kwa staili nyingine, hiyo haingii akilini kabisa!! wapi wapi na wapi dada wa kikurya ana kaka mjaluo??
    tena waluo wasio enda jando?? mkuu wa wilaya usibane hii tasavali, ni mtizamo tu!

    ReplyDelete
  12. Dada yangu Florence wewe kweli ndo mwenyewe.
    Umesema mashaka ni ndugu yako , mtoto wa baba yako mdogo, halafu ukasema pole kwa kufiwa kwake.
    Sasa kama Mashaka ni mtoto wa baba yako mdogo, basi na wewe umefiwa na baba yako mdogo na wala sio kusema kufiwa kwake. Inaamaanisha hamna undugu wa karibu sana vile.
    Nusu ninaweza kukubaliana na wewe kwamba ni ndugu yako na hamjawasiliana miaka kwa kuwa wakurya huwa wanakuwa na wake zaidi ya kumi na watoto huwa hawajuani maana mama ni mbali mbali na wajomba pia ni mbali mbali.Labda baba ya Mashaka ni Mkurya wa Tarime na mama yake ni mjaluo wa Shirati, hivyo John mashaka alikulia kwa wajomba zake ujaluoni na wewe upande wa baba zako ukuriani. Halafu mara nyingi ukisikia mtu anaitwa Mashaka ujue kwamba baba yake alimkataa kwamba sio mtoto wake wa ndoa na labda ni wa nje alipozaliwa na kukawa na mashaka mashaka.Hivyo kukulia au kulelewa upnde wa wajomba au mama ya mama yake(bibi).
    Anyway nitakusaidia :
    Simu ya mashaka ni 704-469-0728
    pia fuatilia website hii na mtawasiliana.

    JMfoundation@mashakafoundation.org

    ReplyDelete
  13. Huyu dada, nadhani wanaigeria walimlalia vibaya, kaamka kajisahau kwamba mashaka ni ndugu yake.

    Ukitoka usingizini utakuta kwamba umefanya kosa kubwa sana. Waosha vinywa na wabeba boxi chnagmkieni hii tenda

    ReplyDelete
  14. Jamani waosha vinywa, dada wa watu anataka mawasiliano na Mashaka, kakae, ninyi mnazungumza yenu ilhali keshawaonya? Pole dada yangu. Mawasiliano ya Mashaka haya hapa

    Mashaka Marwa
    S. L. P 009
    Dar es Salaam

    Simu: +255 798 300200
    Email: haijatulia@ogopa.com

    Nakutakia kila la kheri dada, achana na waosha vinywa. Wewe kaza buti na mambo yako, na usiogope kutumia umma kwa upuuzi. Si bora wewe kuliko mafisadi, japo nyote mnatumia rasilimali vibaya?

    ReplyDelete
  15. Hala hala waosha vinywa, hamna dogo ka "wanamgambo wa city!!".



    Q

    ReplyDelete
  16. dada yangu sasa mume wangu wa ndoa wa miaka 14 umtafute kwa nguvu? wala mama yangu hapa umevuka mpaka. tena mimi ndo mke wake wa ndoa alafu itokee wewe kutaka kuninyanganya?

    yote tumechuma pamoja sasa ww unajitokeza na kutaka kutafuna usipopanda? kwa sababu umemuona kwenye Tv? thubutu

    ReplyDelete
  17. Idumu Blog ya jamii, IDUMU, Zidumu fikra za balozi wa zein, tigo, celtel, tegeta nk.. ZIDUMU, yaani kusoma comment za humu ni siku tosha, Nimepasuka mbavu mpaka nataka kukauka mapafu.. hehehe We Anon wa October 06, 2008 12:01 AM, . yaani sina la kukwambia.... UmeniachA Hoi, bin Taaban....
    LOL.
    Mida Wadau.

    ReplyDelete
  18. nyie wajingawajinga acheni kutuharibia matitle watu wa ulaya hakuna sehem leeds imechoka kama hiyo hapo ulipo achana na ubangubangu

    ReplyDelete
  19. hahahahaaaa hahahhaha uwiiiii tih tih tih,,,heeeee ama kweli duniani kuna mambo,,,wadau kweli leo nimeamini uwa mwapunguza stress sana kwa kumchambua mtu-yan mbavu sina leo kiboko

    ReplyDelete
  20. Mi nina ushauri,Nenda NYUMBANI kwa bibi MARWA,muulizie kuhusu Shangazi yenu mkubwa amehamiawapi,uende huko akuelekeze kwa binamu yako,ambae anapafahamu nyumbani kwa Mama ako mdogo, ambaye ni shemeji yake Baba ake JOHN, kwa vile John alikuwepo Bongo,basi wana habari zake.Pia nina Imani WATAJITAHIDI,kukumbuka. WINDO JEMA dada.

    ReplyDelete
  21. MAKUBWAAAAAAAAAAA!!!!! ALIYACHOKOZA HILO LIDAKE.

    ReplyDelete
  22. nilikuambia dada yangu acha kupost ppicha ukabisha ooh waosha vinywa bado wamelala unaona sasa yaliyokukuta hivi bado wengine wameenda bebeba box wakirudi utatia akili

    ReplyDelete
  23. kwanini mnakandia watu?.kwani vibaya mtu kumtafuta ndugu yake.eeh eti mnene, kitanda sijui kimefanyaje hayo yote yanausiana na nini na topic. hiyo yote kwasababu john mashaka mnamchukia. i don't care any one say anything about my comment.

    ReplyDelete
  24. Dada kama ulikuwa una watest waosha vinywa basi leo unao? Mi nakupa pole ila plz tafuta GYM yakaribu upunguze hizo nyamanyama.

    ReplyDelete
  25. MICHU ulisema utawaziba wachafue hewa, mbona hizi comments zote ni za kuchafua hali ya hewa?

    ReplyDelete
  26. Wabongo Mnakuja Kasi, Nyie wote pale.. Huyo atakuwa mashaka anatafuta PR tu-2!? Sijui mnategemea nini wabongo..

    taratibu hapo..

    = = =
    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  27. Uchovu wa kubeba boxi mchana kutwa leo umenitoka. hii ndio kiboko ya mwaka,

    Hongera dada kwa entertainment yako.Mimi nina mke na watoto wawili sijui utanikubali

    Ila kaza Buti, kuanza siyo kufika. Mwisho wa reli bado mbali

    ReplyDelete
  28. mr chibiriti alianzaga hivi hivi..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...