kaka! michuzi habari ya kazi?
kwanza napenda kukupa pongezi nyingi kwa kazi yako ya kuelimisha jamii,
mimi nikiwa kama mwana jamii nina tatizo ambalo ningependa kuliweka
wazi kwa wana jamii wenzangu iliwaweze kulisaidia kiushauri
zaidi.tafadhali naomba msaada wako kaka michuzi.........
Dear sir/madem

Dhumuni la E-mail hii nikuomba ushauri kwenu nyie wadau wa Elimu,mimi
nikijana mwenye umri wa miaka 25 naishi dar es salaam,elimu yangu ni
ya darasa la tatu,sikuweza kuendelea na masomo yangu ya shule ya
msingi kutokana na matatizo ya familia ,nipo hapa jijini dar es salaam
nafanya kazi mbali mbali ikiwepo ya ufundi wa computer, nimejifunza
computer kupitia marafiki zangu ambao ni watalaam wa mambp ya computer
na pia mimi ni mtu ambae naipenda sana computer.

Ningependa siku moja na mimi nikasoma zaidi kuhusu computer haswa somo
la IT.tatizo ambalo nimenifanya kuwaomba ushauri ni kwamba kutokana na
elimu yangu ya darasa la tatu inaniwia vigumu sana kujiendeleza
kielimu, kutokana na kutokujua kuunda herufi nikimaanisha kuwa
mwandiko wangu nisawa na mtoto ambae ndio yupo darasa la kwanza au la
pili.
Naomba mkiwa kama wadau wa maswala ya elimu naombeni ushauri wenu je
nina weza kupata mwalimu ambae ataweza kunifundisha nikaweza kuandika
vizuri? je nitampata wapi? na je naweza kujiunga na elimu ya msingi ya
watu wazima ? na inapatikana wapi kwa hapa Dar?
ndugu zangu mimi
napenda sana elimu ila kutokana mambo hayo nilio zungumzia hapo juu
ndio vikwazo vikubwa nilivyo navyo ndugu zangu.
Nimekaa nikaangalia jinsi ulimwengu unavyo kwenda kwa sasa bila mtu
kuwa na elimu utakufa masikini,ndugu zangu naombeni muongozo wenu ni
jinsi gani naweza kuondokana na tatizo ili nililo nalo ambalo ni
kikwazo kwangu.napenda kutanguliza shukrani zangu kwenu.
joseph mwendwa
Nategemea kusikia mengi toka kwenu.
E-mail
jmmwendwa@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Nasikitika kwamba sina jibu la moja kwa moja la kumsaidia mdau.
    Kwanza natoa pongezi sana kwa mdau kwa kujibidiisha kadri ilivyowezekana hata kufikia hatua ya kuweza kuwa na ufundi wa kutengeneza kompyuta. Kwa kuwa ameweza kupiga chapa ujumbe wake uliosomeka vizuri ni wazi kuwa ana uwezo wa kusoma. Ili kujiongezea zaidi ujuzi anaweza kujaribu mambo mawili:
    1. Nunua vitabu vya elimu ya msingi na fanya mazoezi ya kusoma yaliyomo na kuandika uliyoyasoma kwa muhtasari. Itakusaidia kuongeza maarifa na kuboresha uwezo wako wa uandishi kwa wakati mmoja.
    2. Tafuta mwalimu wa shule ya msingi upate tuisheni. Kwa mtindo huu wa tuisheni unaweza kusoma mpaka unapotaka wewe. Mtembelee mwalimu mkuu wa shule ya serikali iliyo karibu nawe.
    Nakutakia kila la heri!

    ReplyDelete
  2. Nakupa hongera nyingi sana kwa kutambua tatizo ulilonalo, nakwambia wako wengi wamemaliza darasa la saba na wala hawajui kusoma wala kuandika, na wengine wamemaliza form four lakini kusoma na kuandika kwao ni kazi, hata uelewa wa mambo pia ni mdogo lakini hawakubali mapungufu yao. Ushauri wangu kwanza ni haya yafuatayo:
    1. Usijali kuwa hujasoma shule ya msingi na huhitaji kusoma shule ya msingi kwa umri ulionao. Nunua vitabu kama alivyosema mdau hapo juu wa kufundisha kuandika, na madaftari yake yapo yana mistari mikubwa na midogo.
    2. Nenda kajiunge na shule za sekondari za jioni zinazofundisha elimu ya sekondari kwa watu wazima, hii ni kwa sababu walimu wetu wa shule za msingi ninawafahamu hawatakuchukulia seriously, lakini walimu wa shule za sekondari za watu wazima, wanazosoma jioni wameshakutana na watu kibao kama wewe, wengine wamemaliza hilo la saba kama nilivyosema lakini kuandika ni kazi. Huko badala ya kusoma mwaka 1 kisha ufanye mtihani wa form four walimu watakuongezea muda, mwaka mmoja utakuwa ni foundation na mwaka wa pili ndio utasoma sasa hiyo shule ya sekondari. Na midamu umeelewa mapungufu uliyonayo mafanikio kwako yako usoni, kaza buti na wala usione aibu. Kama unakaa Kinondoni jaribu shule ya watu wazima ya Mtambani, na nyingine iko Msasani kwenye shule ya sekodnary ya private siikumbuki jina lakini ni karibu na samaki. Sinza pia ziko shule za sekondari za watu wazima. Lakini shule za msingi huyo mwalimu atakunyali kama kitu gani sijui, utapoteza muda bure na kukata tamaa. Nenda shule za sekondari za jioni hao wameshazoea kukutana na watu kama wewe!

    ReplyDelete
  3. Samahani shule za sekondari za jioni za watu wazima wanasoma miaka miwili na si mmoja kama nilivyoandika. Ila huo mwaka wa kwanza wanafunzi wanafanya mtihani wa form two, kisha mwaka wa pili wanafanya mtihani wa form four. Sasa wewe unahitaji zaidi ya mwaka mmoja, pengine miwili, mmoja ni foundation na wapili utaanza hiyo sekondari.

    Kama nilivyosema mwanzo huhitaji kufanya mtihani wa primary na jinsi walivyo rigid huko hawatakukubali, kwani huwa wanawakataa watoto waliopitiliza miaka 7, au hiyo iliyowekwa wa ajili ya Memkwa, hata hiyo Memkwa ilianzishwa baada ya watoto kibao kukataliwa kujiunga darasa la kwanza simply tu wamechelewa kuanza shule kwa muda uliowekwa na serikali.

    ReplyDelete
  4. ahsanteni sana wadau wa 3 mlio tangulia hapo juu, nimefarijika sana kupata maoni yenu ambayo kwa kiasi kikubwa yamenipa faraja sana,napia nitajitahidi kuyafanyia kazi iliniweze kuondokana na tatizo ili ambalo lina nisumbua...
    pia na penda kumshukuru kaka michuzi sana kwani siku tegemea kama engeweza kupost hayo maombi yangu kwenu,kweli nime amini kuwa hii blog ipo hapa kwajili ya jamii.

    mdau joseph

    ReplyDelete
  5. Pole sana lakini inatia nguvu kama wewe umeishia darasa la tatu tu na unaingia kwenye internet. Wengi wanaelimu za sekondari lakini hata hawajui chochote.

    Kama ni mwandiko ni jinsi unavyokazana kuandika mwenyewe. Jitahidi kila siku kuandika as long unajua kusoma basi wewe huna shida sana.

    Kama ulivyoambiwa hapo juu nunua vitabu vya mazoezi sijui kuwa bongo wanakubali mtu ajiunge form one bila cheti cha daraa la saba kama zipo nenda kajiunge utamaliza. Elimu haina mwisho

    ReplyDelete
  6. shukrani ndugu yangu kwa ushauri wako,

    mdau joseph

    ReplyDelete
  7. USHAURI WANGU NI KUWA, KAMA MARAFIKI ZAKO NI WATAALAMU WA COMPUTER, WAMEJITAHIDI WAKAKUFUNDISHA KUFUNGUA EMAIL ADDRES N.K!! WAAMBIE WAGOOGLE PROGRAMS ZA KUJIFUNZA KUSOMA NA KUANDIKA HUMO KWA COMPUTER, ILI UANZE KUJISOMESHA MWENYEWE KWA WAKATI WAKO.HALAFU UTAENDELEA MBELE KIDOGO KIDOGO.Kama unataka links za mambo hayo, nijibu nitakupa email add, yangu tuwasiliane.GUD LUK.

    ReplyDelete
  8. ningefurahi sana ndugu ulietangulia hapo juu kama utaweza kunipa hizo link,ilinika weza ku-download hizo programs maana nyumbani ninayo service ya internet,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...