Dear All,
Wasalaam!
Napenda kushea nanyi hizi picha, lkn mtanisamehe kwani masharti niliyopewa ktk kuzipata picha tatu za mwanzo hayakuniwezesha kupata picha moja ambayo ni nzuri,(iliyobeba kila kitu).
Katika pitapita zangu mitaani hivi karibuni,nikiwa ktk Supermarket moja nilikuta kitu ambacho sikuwahi kujua kuwa ni chakula, aidha mfanyakazi mmoja niliyemuuliza jinsi gani kinapikwa au kuliwa naye alisema hajui chochote ila watu hugombania(ikimaanisha mahitaji ni makubwa), alichoniambia nirudi siku ya pili atakuwa na maelezo yote ya swali langu(sijapata muda).
Nimesahau jina lake naomba mnikumbushe kwa anayekumbuka tafadhali! Nimeambatanisha picha inayoonesha bei yake ni £2.99 ~ £3.00 kwa Kg. Lkn nyumbani Tanzania wengi wanatumia kama chakula cha ng'ombe.
Nawakilisha,
Bertram.
Heeh!! haya ni matoto ya ndizi, ndizi inapozaliwa hili linakuwa mwishoni kabisa ya mkungu. Du kweli njaa inafundisha watu
ReplyDeleteNataka kuangalia nani atajua jina la hii kitu kwa Kiswahili.Mie najua lakini nasubiri wengine. Nina interest kujua hasa hasa kama watu wa Bukoba watakuwa na jina la kihaya na Kiswahili kwa hii kitu.
ReplyDeleteAsante
Toto/mtoto wa ndizi/mgomba
ReplyDeleteeeh jamani ndugu yangu hata wewe umeeona? mie nilishawahi kuona Bengali people wanagombania hizi bidhaa market.Nilichoka manake kwetu ni chakula cha mbuzi. Ndio maana kumbe meno ya Bengali yana sura mbaya, kumbe yamejaa utomvu. Jina najua kwa kichaga tu ndugu 'ngunana'
ReplyDeleteHiyo bwana inaitwa NDILALILA. Kwa wale wa Kagera yetu wanatambua hilo. Sio tu kwa kulisha ng'ombe, bali pia hata kuzibia vidumu vya maji tukienda mtoni.
ReplyDeleteHahahahahaha. Nimekumbuka mbaali sana.
kwetu mkarafuuni hilo ua tunaita Tojo, tojo ni neno linalolingana na neno tone liwe la maji au alama ndogo inayojulikana kama nukta, hata mimi sikujua kama ng'ombe au watu hula hilo ua, mi ndizi yangu ikishatoka hulitupilia mbali naona kama ni takataka kuendelea kubaki kwenye mgomba.
ReplyDelete...toto la ndizi.. kwa kiswahili cha ndaaani kabisa: 'CHANANA'..sijui wangapi wanalijua neno hili!...Sijalisikia neno hili kwa miaka karibu 30!..Mdau hapo juu, hebu tuambie unalolijua wewe...UZENGERE
ReplyDeleteMaisha ya ughaibuni si kitoto....hizo "SONGA" za kukatia mbuzi nazo huko wanaziuza ghali hivyo?? kama wewe ni mfugaji wa mbuzi utajinunulia wewe au utanunulia mbuzi????Zimenikumbusha sana Moshi!!!
ReplyDeletenganana kwa kibosho chakula safi saana ya ndafu. pia huwa tuna zitumia kwa ajili ya matambiko fulani hivi.yah nimekumbuka huwa zinatumika kama sahani kwenye tambiko la "RUMAHIYO"tunapofunda morani wa kichaga after jando. duh zimenikumbusha mbali sana
ReplyDeleteinaitwa inanwa, au ua la ndizi..............
ReplyDeleteVery interesting
ReplyDeleteKitu hichi mimi najua chaitwa chanana pia mtoto wa ndizi au mtoto wa mgomba.Nafahamu pia hutumiwa kama malisho ya wanyama, sijui kama kuna anayekumbuka kuwa small girls carry them on their backs as dolls
Wakatabahu
inaonekana zinaitwa baby banana
ReplyDeleteupo nchi gani tuwaletee tupate £ maana hujasema ni nchi gani yakhe.
ReplyDeletetunakisia ni uingereza lakini £ inaweza pia kuwa inatumika nchi nyingine, malizia habari ni nchi gani tuingie mashambani.
Jamani tusishangae sana mambo ya vyakula.Mimi mwenyewe ninajua kuwa hiyo kitu inaliwa na ni safi sana. Ni sehemu ndogo tu ya ndani kabisa inayoliwa.
ReplyDeleteSio watu wanakula kwa njaa, ni chaguo tu. Hata bei yake utakuta ni ghali kuliko viazi,ugali au mchele. Ni sawa na wala vyura, panya,nyoka, mbwa, n.k si kwa sabababu ya umasikini na kukosa pesa za kununulia samaki.Tembea duniani uone mambo.
You always learn
ReplyDeleteJamaa hivi sasa kaniletea email kuhusu kidude hiki.Asema kwamba wao nyumbani kule Sri Lanka wala maua haya ya mgomba kama mboga na asema wanatumia jina la banana blossom, pia nchi nyingine kama Philipines etc pia huu ni uhondo. Kaniletea hata recipe kama mama watoto ataka kujaribu kunipikia na asema he has seen plenty of the flowers in Asian supermarkets in London
Basi ndugu huko mgombani yakaangeni maakul
Wakatabahu
jamani wa tz ni smart sana mi nilifikiri ni mahindi mekundu na wakati kwetu kuna ndizi lakini sikuwa na mawazo kabisa
ReplyDeletekm annon apo avosema 'EBU TUAMBIE NI NCHI GANI ASWAA TUANZE BIASHARA'mana bongo yanatupwa aya au ndo wala wanyama ilhali ni chakula cha nguvu na bei fresh kwa wengine!!tumeipata iyo ya Sri lanka,,,sema sema wee anon ulotuma hii newz
ReplyDeletewatu tuko kibiashara zaidi sio kustorisha apa
mbona hapo pembeni yake naona kama mirungi? wengine wanaita GOMBA? au macho yangu tuuu, tena inaonekana ni GIZA hiyo sio kangeta. duu nimelimiss sana gomba
ReplyDeleteSio kwa kagera nzima inaitwa ndilalila, sisi Kagera ya Karagwe tunaiita omkankabani na kwetu kwa sababu ya majani ya kutosha ya ng'ombe uwa tunakatia chini inakuwa kama mbole. Kwa hiyo naweza kusema kwetu faidi ya Omkankabani ni mbolea na nakumbuka wakati wa utoto wetu tulikuwa tunaitundika miguu ya vijiti na kuweka pembe ya viti na kuiita 'g'ombe na kwa wasichana walikuwa wanaibeba kama watoto, nadhani wa enzi hiyo nimewapeleka mbali. Ila kama ni mali wanende Karagwe Mikankabani ipo ya kumwaga
ReplyDeleteTembea uone, kwako takataka kwa menzako chakual
ReplyDeletemimi niliona majani ya sungura yanauzwa nikashangaa.
Halafu artichoke sikama katani vile na pia haya makaa (crabs) bongo tunakula kweli?
Nasikia italy wanakula makonokono sijawahi kufika huko sijui ni kweli
Tafadhali Bibi/Bwana uliyeleta hii picha nina ombi moja tu.
ReplyDelete"Usieleze jinsi ya kupika haya matoto ya ndizi"
Sababu kubwa ni kwamba wabongo wakiishajua nyumbani basi ndio mwisho wa kupata ndizi zilizokomaa, watakuwa wanakata vidizi vichanga si unajua bongo. We chukulia mfano wa mahindi ya kuchoma watu wanavyoibiwa mahindi machanga, wanapopoa maembe machanga, mapapai machanga yaani ni balaa ndugu USITOE TEKNOLOJIA YA KUPIKA HII KITU PLEASE.
MESSAGE TO MICHUZI AND P.S.NALITOLELA!
ReplyDeleteKAKA MICHUZI NAOMBA KUWAKILISHA. HIVI JAMANI MTU KUWA NA JINA LINAFANANA NA MTU MWINGINE NI KOSA? MIMI NI PETER NALITOLELA NA NIMEONA KUNA MTU MWINGINE ANA JINA LA PETER NALITOLELA, LAKINI KUNA TOFAUTI YEYE ANAITWA PETER S NALITOLELA MIMI SINA HIYO S KATIKATI, NINA MAJINA MAWILI TU, ISITOSHE YEYE YUPO CANADA MIMI NIPO UWANJA WA FISI HAPA TANZANIA, YEYE ANA SIGN IN MIMI NAWEKA JINA TU. SASA KAKA MICHUZI HILI NI KOSA KWELI? MIMI NIKIWEKA COMMENT NAAMBIWA NAMCHAFULIA PETER WA CANADA SIJUI YEYE HAANDIKI COMENTS KAMA ZANGU SIJUI? HII NI KWELI HATA MIMI SIANDIKI COMMENTS KAMA ZAKE JE NA YEYE ANANIHALIBIA? HIVI HAPA BONGO KUNA WATU WANGAPI WANAITWA SALIM AHMED SALIM? SASA KAMA WAKISEMA KITU DR. SALIM AWAMBIE ETI WANAMCHAFULIA JINA LAKE? NAOMBA UNISAIDIE KUMJULISHA HUYU PETER KWAMBA HII NI BONGO SIYO MALAWI WALA ZAIRE KUNA MAJINA KIBAO YA WATU YANAFANANA KUNA MCHEZAJI WA SOKA HAPA ANAITWA ABUBAKAR SALUM LAKINI SI YULE ABUBAKAR SALUM ALIYE CHEZEA YANGA ENZI ZILE TUKO WADOGO SO PETER S. OF CANADA LET ME TELL YOU THIS, WE HAVE SO MANY NALITOLELA IN THIS COUNTRY SO DO NOT PANIC IF YOU DON`T WANT THIS NAME AND THINK SOMEHOW WE INSULT YOU WHEN WE POST COMMENTS THEN FIND ANOTHER NAME LIKE BILL O`REILY OR MICHAEL JACKSON BUT I DOUBTS IF YOU WILL ALWAYS BE YOURSELF BECAUSE THERE ARE SO JACKSONS AND BILLS!SO MY FRIEND I WANT YOU TO KNOW YOU HAVE BEEN NAIVE ANYTIME I POST MY COMMENTS IN THIS BLOG, FIRST YOU DONT ACCEPT MY SACCESS THAT I FINISHED HIGHER EDUCATION HERE IN MY COUNTRY AT MUZUMBE UNIVERSITY.I KNOW YOU PROBABLY HAVE MORE EDUCANTION THAN I DO BUT MY FRIEND YOU WON`T TAKE MY PROUD AS TANZANIAN AND AS A SON OF NALITOLELA, AND I WONT CHANGE MY NAME IN THIS BLOG TO PLEASE YOUR IDEOLOGY, THANKS NO THANKS MR. PETER S NALITOLELA. THERE ARE AHUNDREDS OF BLOGS SO ARE YOU GOING TO STOP ALL NALITOLELA IN THOSE BLOGS? PLEASE..!? MICHUZI I HOPE YOU WILL UNDERSTAND WHAT I MEAN, THIS IS A FREE WORLD OF FREE PRESS IF YOU DISAGREE WITH MY COMMENTS THEN CRITISIZE MY COMMENTS BUT NEVER TELL THE WORLD THAT IM INSULTING YOU BECAUSE WE SHARE THE SAME NAME? WHAT IF YOUR DAD IS MY DAD? WHAT IF MY DAD CHEATED AND BAPTIZED ME AND YOU PETER? I WELCOME YOUR CHALLENGE BUT NEVER CHALLENGE MY NAME KILA MTU AWEKE COMMENTS ZAKE BWANA, THOSE WHO KNOW YOU WILL DIFFERANTIATE YOUR COMMENTS FROM MINE, YOURS ARE MORE ADVANCED AND MINE ARE STANDARD SEVEN BUT I TELL YOU WHAT THERE ARE SO MANY STANDARD SEVEN TOO IN THIS BLOG WHO WILL LOVE TO READ MY COMMENTS SO STAY AWAY MY BROTHER LET ME POST MY COMMENTS FREELY. LAST BUT LEAST THANK YOU MICHUZI AND THOSE STANDARD SEVEN WHO READ MY COMMENTS. AND FOR THOSE WHO ARE SURPOTERS OF P.S. NALITOLELA WE THANK YOU TOO. IT IS ME PETER NALITOLELA AGAIN EX MUZUMBE AND ST. ANTONY MBAGALA, THE SMART KID!
kula aina fulani ya vyakula sio lazima njaa, inawezekana ni mazoea na utamaduni. Mfano, huku niliko wazungu wanashangaa sana kula sehemu kama utumbo, ulimi, n.k. na wanaona kinyaa; na si utumbo tu, wengine hata moyo, figo na maini hawagusi. Ila wanakula oysters, shrimps, etc and other more "exotic" food items that would totally gross out people back home.
ReplyDeleteHAHAHA NILIKUWA VIJIJINI SIJASOMA HII NEWZZZZZZZZZ!!
ReplyDeleteHuko Uchagani kwa wale wanatahiri watoto wa kike, ukifa hujakeketwa basi wanaenda kwenye mgomba wanakata hiyo nganana kama sign ya kukeketa maiti! Mila zetu hizo jamani..
Ndio hiyo ni gomba au mrungi.. lakini Ulaya wanaita 'Asparagus'
ReplyDeletenikikumbuka nacheka, nikisahau nalia..
can you imagine watu bongo walikuwa wanatafuna vegetable alafu wanalewa!?
= = =
Buffalo,
New York
Hilo siyo sosi washikaji bali ni gomba la kufungia hiyo mirungi.Badala ya kutumia plastic bags wanatumia hilo ua la mgomba (ngunana)(ndilalila) (chanana)
ReplyDeleteHivi asparagus ndio mirungi kweli. You are kidding right? Ninapika sana hizi nyumbani kwangu na wala hatujawahi kulewa. Sijawahi kuona mirungi TZ hivyo hata sielewi lakini I doubt kama ni mirungi
ReplyDeletehivi ni kweli hawa kina nalitolela ni ndugu ama wanatuzuga? mbona sioni tofauti ya comment zao ama wanatafuta umaharufu humu kwako michuzi nini? inaonekana hawa ni ndugu lakini wanatuchezea akili ama atakuwa ni mtu mmoja anatuma na kujijibu mwenyewe
ReplyDeleteNyie ndugu zetu kina Nalitolela, napenda niwakumbushe usemi mmoja unasema kuwa ndugu wakigombana chukua jembe ukalime hata wakipatana chukua kapu ukavune ila bibilia ainasema heri wapatanishi maana hao watairithi nchi ya ahadi.
ReplyDeleteSasa nyie msitumiane maneno magumu na ya kuwekeana uadui au uhasama hapa, pengine ninyi ni ndugu wa ukoo,tafuteni wazazi wenu au ndugu wa ukoo na mfatilie kwenye koo zenu, huenda mkapata suluhisho la tatizo lenu humu ili kila mmoja wenu awe na amani na uhuru wa kumiliki na kutumia jina mnalogombea hapa, na kama si ndugu abasi undeni urafiki kwa kukuta mnatumia jina moja,almuradi hakuna anaelipia kodi jina hata moja kati ya hayo mawili au hayo matatu, na pia mchukue uangaligu na kuweka jina kamili katika mali na vitambulisho katika hali ya kuwa na utofauti kidogo na kueleweka kuwa hapa ni Peter yupi mlengwa. sasa mkiendelea tu kukalia malumbano na kunga'ng'ania mmliki halali wa jina au uchoyo wa kutaka kulimiliki jina peke yako si vema.Hayo ni mawazo yangu ndugu zetu kina NALITOLELA.
Viva bro Michuzi kutukutanisha na kutupambanisha hata tusiojuana tunapata kujuana na kusalimiana.
Hii kwa huku Kilimanjaro Tanzania inajulikana kama SONGA. kiukweli inatumika sana kwa mifugo hasa ng'ombe na mbuzi. ila kuna maonesho flani nimewahi kwenda na nikakuta wamepika. maelekezo yake ni kwamba baada ya kuikata kata vipande vidogo dogo kama mboga za majani unaiosha mara nne hivi then unaunga kama mboga za kawaida. bila kuiosha ni chungu saaana. Baada ya kuiona siku hiyo nimewahi kula kama mara nne hivi hukuhuku Kilimanjaro. Kwa maelekezo niliyopewa ina madini sana ya calcium mwilini
ReplyDelete