ule mpambano unaosubiliwa kwa hamu na mamia ya mashabiki wa Atlanta na vitongoji vyake,sasa yamebakia masaa tu nyasi kuwaka moto.
Mara ya mwisho timu hizo zilipocheza mwaka jana,Bongo United waliichakaza Tanzanite Fc 3-2.Mpambano huu ni jumamosi kwenye uwanja wa 1142 Bankhead,Nw,itawapa nafasi timu yaTanzanite Fc kulipiza kisasi.
Akiongea kwa njia ya simu muda mfupi kabla timu ya Bongo United haijaanza safari kuelekea Atlanta,kocha mkuu,Gharibu Latto aliyewahi kuchezea ushirika moshi,small simba na hatimae Taifa stars,amesema vijana wangu wapo katika hali nzuri kimchezo,na wameniahidi ushindi mnono,jana tulikua na mazoezi mepesi na kurekebisha makosa ya mabeki,tatizo lililo jitokeza mwaka jana na wenzetu wakarudisha goli mbili,hatutaki hili tatizo litokee kwenye hii mechi ya jumamosi pia tulikua tunaangalia mikanda ya video ya timu ya Tanzanite Fc,ambayo kwa sasa ipo kwenye ligi daraja la tatu,
tumeiona inavyocheza na kitu kingine bro michu,wahenga walisema,uchawi hauvuki bahari,lakini wakatuonya,tahazali kabla ya ajali,ndio maana tumeamua kusafiri na maji yetu na chakula,tunasikia kuna nyama choma,sisi hatuli nyama ya mtu mpaka hapo dakika tisini zitakapo kwisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. don't be too excited,Tanzanite FC has a league(D3) game this Sunday.Game hiyo ni muhimu kuliko hiyo friendly game na nyie.kwa maana hiyo,kucheza na nyie ni 50/50 ila guarantee mnaweza kucheza na Wakenya.we can't afford to risk our key players kwa hiyo bonanza.habari ndio hiyoooooo.

    Bofya hapo chini for reference.ama copy hiyo url then paste ili uone ratiba ya ligi.

    http://adasl.com/RESULTS_SCHEDULE.asp?searchType=date&searchDate=10/26/2008

    ReplyDelete
  2. nyie mnakuja kwa ajili ya mechi au mnakuja kumsindikiza mwali wenu Ali Kiba?wenzenu Jumapili hii wana mechi ya ligi sasa sijui kama kweli wataweza kucheza Jmosi na Jpili.watakua wamefanya vibaya kama hawajakujulisheni maana mnaonekana mmejiandaa sana alafu inakuwa noma mkifika huku na kukosa kucheza nao.

    ReplyDelete
  3. Mshaona hiyo ligi ya proffesioonal washikaji?? Hebu wakaribesheni wenzenu wamekuja kuwatembelea kazi mijungu tu. Kama Ali kiba si wao ndio wa kwanza kumuona?? ligi ligi utadhani mnalipwa?

    ReplyDelete
  4. wote mpo sahihi , wanaotaka kwenda kwa ali kiba waende. wanaotaka kucheza bonanza ya jumamosi wacheze. wenye mechi ya ligi wacheze ligi yao .
    kwani wanaoenda kwa ali kiba wanalipwa ?
    UKWELI NI KUWA ,mamia watakuwa kwa ali kiba, makumi watakuwa ktk bonanza, 15 players watakuwa ktk ligi sunday. ACHENI HASIRA .

    ReplyDelete
  5. mtoa maoni wa tatu ana hasira huyooo.wewe ndo mmoja wa waandaaji wa hiyo bonanza nini??unataka kulazimisha mambo?watakaoenda ktk hiyo bonanza PRO'S nini?teh teh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...