





SAFARI LAGER YAVAA SURA MPYA, LADHA YAKE MAARUFU YABAKI
*Sasa kuwa na muonekano wa kisasa
*Yaendeleza historia yake, ladha na desturi
*Yaendelea kuenzi wanywaji wake
*Sasa kuwa na muonekano wa kisasa
*Yaendeleza historia yake, ladha na desturi
*Yaendelea kuenzi wanywaji wake
Safari Lager, bia maarufu nchini Tanzania imebadili rasmi muonekano wake wa nje wakati huo huo ikibaki na ladha ile ile inayofahamika. Uamuzi wa kuwa na sura mpya unalenga kuendeleza muitikio wa bia hiyo kwa wanywaji wake huku ukijenga na kusisitiza uwezo wake wa kukubalika katika soko lake linaloendelea kupanuka.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Safari Lager Fimbo Buttallah alisema, “Safari Lager imekuwa sehemu ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 30 sasa na uhusiano wa muda mrefu namna hii kwa asili yake unaashiria moyo wa dhati na kukubalika baina ya pande zote mbili. Bia yetu inaendana na wakati na pamoja na mwelekeo huu hitaji la kuwakumbatia wanywaji na kukubalika linakuwa jambo la muhimu. Hivyo basi, ingawa utakachokiona kwenye chupa kitakuwa tofauti, kilichomo ndani ni ladha ile ile maarufu ambayo imekuwepo kwa miaka yote hii nab ado ianendelea kupendwa.”
Katika muonekano huo mpya, badiliko lipo kwenye chapa ambayo sasa ina umbo mfano wa yai ndani ya mraba ambao umeendelezwa toka chapa ya zamani lakini sasa na sura mpya zaidi. Ili kuitambulisha Safari Lager na historia yake, chapa mpya sasa imeongezwa maneno “Tangu 1977”, historia ambayo mnywaji wa bia hiyo anajivunia.
Chapa hiyo mpya pia inaonyesha medali ambazo Safari Lager imeshinda kama ushahidi wa ubora wa bia hiyo. Muonekano huu mpya unakusudia kuionyesha bia hiyo kuwa ya kisasa inayoendana na karne ya 21 wakati huo huo bado ikipendwa na wanywaji wake hata wa siku zote.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) David Minja alisema, “Tunaishi katika wakati ambapo ulimwengu unabadilika haraka na baadhi ya mambo tunayotambulika kwayo yanabaki kuwa sehemu yetu.
Kwa walio wengi Safari Lager ni ishara ya umoja, desturi, sifa ya kujivunia na kila kitu kinachopelekana na uchapaji kazi na kwa sababu hii tunajisikia fahari kubwa kuendeleza ladha na sifa zile zile sasa katika sura mpya. Hakuna mnywaji yeyote wa Safari Lager atakayeona tofauti ya ladha au ubora kwa sababu hizi ndizo sifa zinazoifanya bia hii kuwa na sifa ya hali ya juu.”
Kampuni ya Bia Tanzania ilianza kutengeneza Safari Lager mwaka 1977, kipindi ambacho kilitawaliwa na ari na mwamko mkubwa wa utaifa na katika utengenezaji huo Safari Lager ikajijengea heshima ya kukubalika.
Kwa kipindi chote hicho bia hiyo imeendelea kupendwa hadi kufikia kuwa bia inayouzwa kwa wingi zaidi nchini Tanzania.
Mara ya mwisho Safari Lager ilibadilisha muonekano wake mwaka 2003. Muonekano huu mpya unategemewa kuvutia wanywaji wengi vijana hasa kutokana na bia hiyo kuhusika na michezo mbalimbali inayojumuisha vijana kama vile mpira wa miguu, pool na mbio za baiskeli.
Safari Lager pia inaoanishwa na shughuli za kila siku za kazi na kwa muda mrefu sasa imekuwa ishara ya watu kujivunia uchapaji kazi ambapo kila baada ya kazi hujumuika pamoja na kujipongeza kupitia bia yao waipendayo.
Buttallah aliongeza, “Tuna hakika ya jinsi mnywaji halisi wa Safari Lager atakavyoipokea sura hii mpya tunayoizindua kwa sababu inaashiria uchangamfu, upya, umaridhawa na zaidi ya yote inaendelea kuwa sehemu ya kila mnywaji wake.”
Safari Lager yenye sura mpya itaanza mara moja kupatikana nchini kote.
Buttallah aliongeza, “Tuna hakika ya jinsi mnywaji halisi wa Safari Lager atakavyoipokea sura hii mpya tunayoizindua kwa sababu inaashiria uchangamfu, upya, umaridhawa na zaidi ya yote inaendelea kuwa sehemu ya kila mnywaji wake.”
Safari Lager yenye sura mpya itaanza mara moja kupatikana nchini kote.
hiyo ni kilaji au kinywaji? kuna tafauti kubwa baina ya maneno hayo mawili!
ReplyDeleteJamani hivi ulevi ni kitu cha kusifiwa na kusherehekewa licha ya madhara yake makubwa kwa wanywaji na jamii? Nauliza tu, kuuliza si ujinga.
ReplyDeleteTanzania ni nchi iliyofilisika kimaadili na hii hali itazidi iwapo hatutabadilisha mienendo yetu. Hela zote hizo mbona wasingetumi kufanya vitu vya maana kama kujenga mazaanati kuliko kujinadi na mambo ya kiupuuzi. Hii ndiyo maana nawapongeza watu wachache kama wakina Joni mashaka amabao wanajitolea nafsi zao kwa ajili ya nchi yao. Makampuni ya kitanzania, kuweni watu wenye busara
ReplyDeleteMungu awabariki
Wewe Anonymous wa 1:34 PM acha u@@*%+-wako.Unampongeza John Mashaka kafanya nini kwa nchi hii.Angekuwa na uchungu na nchi hii si tungemuona anapambana kama akina Kubenea?. Wewe fikiri tu kama mafisadi wameshaiharibu hii nchi watu wafanye nini? Akina JK hawataki huwawajibisha. Acha watu wakate kinywaji kodi iingie mafisadi waendelee kuneemeka na sisi makabwela tuendeleze umaskini wetu.Pengine Safari moja itatusaidia kuanzisha safari nyingine ya kwenda kupambana na maisha haya mafupi.Mimi nawapa bigup TBL kwa juhudi zao mbalimbali wanazozifanya, kama vile sponsorship ya michezo,huduma mbalimbali za kijamii na kadhalika.
ReplyDeleteNadhani wadau wanamiss a point kwamba,kampuni ya bia ni moja ya walipa kodi wakubwa,na hii inaitwa kampeni ya kisoko ili mauzo yaongezeke ambapo faida itaongezeka na ndivyo hivyo mishahara, fungu la kusaidia jamii na kadhalika na kadhalika. kwa hiyo indirect kampeni hii itasaidia jamii kama itafanikiwa.
ReplyDeleteSwala la madhara kwa watumiaji watoto wa mjini tunasema "...akili kumkichwa ukilemaa umeachwa feri...", nikimaanisha kuwa kama uwezo wa kununua na kunywa bia unaoa sioni tatizo hapo. Tatizo ni la kizidisha kipimo(kiasi) na madhara baada ya hapo. Na hii ni kwa kitu chochote kile ukizidisha kina madhara iwe kula, kufanya kazi,n.k.
Wasalaam
NAONA MDAU MTOA MAONI DD ANATAKA TUKUBALI KUKUMBATIA NA KUSHEREHEA KITU CHENYE MADHARA MAKUBWA ETI SERIKALI INAPATA KODI. HOJA KAMA HIZI ZILIKUWA ZIKITOLEWA SANA NA WATETEZI WA UTOAJI WA MATANGAZO YA SIGARA NA KUZIFANYA SERIKALI NYINGI ZIFUMBIE MACHO MADHARA YAKE KWA KUOGOPA MAPATO YA KODI KUPUNGUA.
ReplyDeleteSASA HIVI NCHI NYINGI DUNIANI ZIMEPIGA MARUFUKU MATANGAZO YA SIGARA KWENYE VYOMBO VYOTE VIKUU VYA HABARI BAADA YA KUKUBALI KUWA HASARA NA MADHARA YAKE NI MAKUBWA KULIKO HIZO KODI.MIMI SISEMI SIGARA WALA POMBE IPIGWE MARUFUKU, HILO NI SUALA LA MTU NA UAMUZI WAKE LAKINI TUKITIZAMA KODI TU ITABIDI TURUHUSU NA TUSHANGIRIE MAMBO MENGINE MENGI YENYE MADHARA KWA JAMII KAMA VILE VINYWAJI VYA WANYONGE VINAVYOITWA "HARAMU" NA VIBURUDISHO VYENGINE KAMA BANGI NA UNGA UNAOMFANYA MTUMIAJI AJISIKIE KAMA ANATEMBEA KATIKA HEWA BAADA YA KUUBUGIA.
Kwanza kwa wale waliopo ughaibuni hapa bongo bia inaitwa kilaji, ni kiswahili kipya na kinakubalika na jamii wa kataji kilaji hicho. Pili unamsema John Mashaka kafanya nini kubwa kumzidi TBL, TBL kwa taarifa ndio mchangiaji mzuri wa kodi ingawa kodi zinaliwa na Mafidi, pili ni wachangiaji wazuri wa maendeleo ya jamii, na kizuri zaidi wanasponsor michezo na Wandanganyika waliochoka kupunguzia stress zao baada ya wakubwa kusomba mipesa yote ya kodi na kutia mifukoni mwao. Wacha watangaze kilaji wandanganyika tupunguze stress zetu vinginevyo tukiwaza sana mafisadi tutakufa kabla ya wakati wetu
ReplyDeleteWe anon 2:12pm sijui kwanini umekuwa so harsh kwa mwenzako. Hii insssue inahitaji kuifikiria kwa undani kabla ya kuosha vinywa vyetu.
ReplyDeleteMimi ni mnywaji na napenda jitihada za TBL, ila tukae tujiulize kweli ni products ngapi za maana tofauti na bia ambazo nchi inazalisha? Tatizo obviously lipo. Kama tuko creative kutengeneza ulevi kwanini tusiongeza creativity ya kuzalisha vitu vingine vya maana zaidi especially techlogically. Mbona sioni matangazo makubwa ya namna hiyo kwamba kampuni ya fulani kitanzania imetengeneza simu mpya, gari jipya au computer mpya.
Yeah kuna ufisadi; je nini kifanyike kuondoa ufisadi? Hayo ndo maswali ya kujiuliza kuliko kukaa na kupongeza ulevi. Kilaji ni kizuri, ila ndugu yangu ukikalia kilaji nchi nzima itakuwa ya kilaji tu. TOO BAD
.....Wandugu, sidhani kama kuna mtu anashikiwa bunduki kununua bia. Kuna maziwa, juicy na maji kibao. Cha msingi ni kweli TBL wanatengeneza faida kubwa na ni walipa kodi wanaoongoza, je zinaenda wapi??? Sio bia. Kama mnafikiri nchi yetu watu wanthamini pombe basi umekosea, kuna nchi zinakunywa bwana mpaka ofisini na watu wanawajibika ipasavyo. TBL, rudisheni kwa jamii kinachostahili na sio kupeleka bondeni tu faida yote.
ReplyDeleteMdau
Whats wrong with you pipo??? whats new here, This is business, go and learn a thing or two about Marketing.Kila kitu kibaya, mtu akiimba dini inaingia, hivi nyinyi mnaolaumu kila kitu Mnashughulika na nini ambacho ni PERFECT,katika hii dunia, mimi si mnywaji but sioni tatizo lolote la watu kutangangaza na kubadilisha sura ya bidhaa zao katika kutafuta masoko.Stop jamani mnachosha.Mkumbuke Tz nayo nchi ni lazima iende na dunia ya leo katka ushindani wa biashara, ziwe ndani au nje ya nchi mhhhmmm jamani!!!!!
ReplyDeleteWewe kama hutumii hicho kinywaji nini kikukeracho??? Usiusome hii news? Kha! Unakera na hiyo misimamo yenu ya kutaka kulazimisha wote tuwe kama nyie. Blog yenyewe ya Michuzi inadhaminiwa na bia. Halafu mnajidai fikifiki...
ReplyDeleteNaona wamezidi kupunguza ukubwa wa vibanda...
ReplyDeleteAnyway kama kawa "Safari moja uhanzisha nyingine"