Dear Balozi
Ni mdau mkubwa wa Blog yetu ya jamii, na nafurahishwa na mabrekiing news yote yatolewayo hapa isipokuwa mambo ya Bwawa la maini tu, hizi huwa sizipendi maana mimi ni Mdau mkubwa wa Man yuuuu bingwa Ulaya na England 2008/09 unabishaaaa.
Jambo moja napenda kulicomment, kiswahili fasaha mwanangu hivi ukiandima "Mtaa wa Azikiwe Street" italeta kichefuchefu amua kuandika "Azikiwe street" au "Mtaa wa Azikiwe" lakini usichanganye mambo.
Na wajuilishe waandishi wa Zanzibar pia maana wakikusudia kurusha news au kuandika kuhusu ukumbi uliopo pale Bwawani wao huwa wanaandika "Ukumbi wa Salama Hall" aidha waandike "Ukumbi wa Salama" au "Salama Hall"
Ni katika kupamba tu Blog yetu
wasalimie
Mdau Mselem
Zenj


kumbe ulikua unafahamu sasa
ReplyDeletekutaka kujionyesha kama wewe umeshapata sheria huko uk ndio nini
ulipokua kwenu bopwe ulikua ukijua maana ya and wewe ?ushajifanya msomali na umeshapewa hiyo sheria ndio unataka kutukosoa
kawakosowe hao wazenji wenzio na sio watu wote wanaoita
RAFIKI-SHOGA
UVOOO
ma mengine mengi tu
Wageni wa hapa kijijini utawajua tu, wewe uliyeleta hii unaonyesha ni mgeni hapa, hivyo tulia uangalie mambo yanaendaje ndo umwandikie Balozi. Hapa hiyo ni lugha yetu ya kijiji...utaona mambo kama "barabara ya bagamoyo rodi", "lunch ya chakula cha mchana", Chuo kikuu cha Mlimani university" na kadhalika. Je ukisikia hii " My wife wangu" sijui ndo utasemaje? Kama wewe ni lecturer university nakushauri hiki kijiji hakikufai.
ReplyDeleteMdau UKEREWE..au hata hii UKEREWE hujui ni wapi?
We mselem, tafadhali naomba usituchafulie jamvi letu..vua viatu vyako huko kabla hujaingia humu. Kama ilivyo man u, bwawa la maini na wakali arsenal huwa wanatumia formation zao katika kulisakata kabumbu..vivyo hivyo MH.Ambasada hii ndio formation yake!! na kamwe hatubadiliki kama mnyalu!!!
ReplyDeleteSo please stepoff...
Marco
Nafikiri mdau wetu wa zenji tumekupata huku City Of Dar-es-salaam Au Jiji la Bandarisalamaa Hall sawa na ukumbi na mtaa sawa na street ila vyovyote watu wanaelewa tu kwani accent tu hizo na slang ambazo nchi mbali mbali wanatofautiana Oman Muscat na Dubai kiarabu kinatofauti UK na USA english zinatofauti japo mmoja kati ya hao kidogo inakuwa fasaha. kukosea lugha si kwenda motoni.
ReplyDeletewewe unaejiita mselem kwanza hata kiswahili hujui halafu unamrekebisha mwenzio eti inatia kichefechefu,balozi anajua anachofanya for your information balozi huwa anapamba tu blog na anajua anachofanya,kwahiyo usijifanye umjuaje kuliko yeye tena yeye anajua english kuliko hata wewe
ReplyDeletehahahaha! mseleem karibu kijijini hapa unaonekana mgeni wa blog hii.Kuna mwenzio kutoka UK aliwahi kutoa comments kama zako lakini tatizo lilikuwa palepale kwamba blog hii ina historia na utamaduni wake.Hapa ndipo kwenye uchanganyaji wa lugha kwa style hiyo na hii haikuanza leo kaka ni ya zamani mno.Kuna misemo maarufu hapa kama wako na pia kiingilishi is not richabo hii kuleta manjonjo tu na kuburudishana katika globu ya jamii lakini ukweli ni kwamba wadau hapa wameenda shule ya kufa mtu na wengi wako ughaibuni hukohuko kwenye lugha hiyo unayoirekebisha.
ReplyDeleteHaya ndugu Mselem
Msalimie my waifu wako
Mdau Finland
Du huyu inaonekana ni mgeni wetu huyu. Inabidi tumpokee kwa amani. Zamani zile tulikuwa tukisema "Mgeni siku ya kwanza, mpe mchele na paza?" nadhani nakumbuka sawasawa.
ReplyDeleteBaadae atazoea tu lugha yetu globuni.
Mdau,
Ughaibuni
we mdau vipi blog hii inaambatana na sanaa ya lugha pia ktk kupamba blog sa we unashangaa hilo kwani hujaona issah kaandika barabara ya Samora road
ReplyDeleteHuyu inaonekana ni mgeni humu. Hizi ndio lugha za humu na ndio moja ya vitu vinavyotupatia raha kuendelea kucheki blogu hii kila mara.
ReplyDeletePretlue
wanaoandika hayo si kwamba hawajui lugha,isipokuwa inaleta radha flani ukichanganya hivyo.hiyo ni Swahinglish..hahaha..pia kuna maneno kama Sukuma Push, Moja One na mengineyo mengi.
ReplyDeletekama maneno hayo yatakuwa yanachanganya basi hata swahili slang pia ina maana isitumike.nadhani labda ungeanza wewe,badala ya kuandika Man Yuuuu ungeamua Kuandika Man United au Man Utd..yote ni mapambizo ya lugha na kama wadau wanaelewa mwandishi anamaanisha nini wala sioni kama ni BIG Deal vileeee.na asiyeelewa atauliza na kueleweshwa.
naomba libeneke la mseto wa lugha liendelee.hahaha
Mdau Mselem kwa kuchangia tu nilikuwa napenda kukueleza kabla ya kumsahihisha Balozi wa Zain na mbunge wa wilaya ya nanihii kuwa akiandika wakati mwingine kunaleta kichefu chefu na wewe pia ukiandika unaleta kinyaa unapoandika KUANDIMA badala ya kuandika.
ReplyDeletemdau Dege a.k.a KOP - Leicester.
Mbona Misupu hutupi matokeo ya mpira ya Tanzania timu zetu zinapocheza, zamani tulikuwa tunaangalia hapa kupata matokeo. Sio Vizuri. Anyway Taifa Stars 3 Cape Vede 0
ReplyDeleteWewe mpemba usitake kutusahihisha lugha hapa si wote tunajua hiyo lugha vizuri...Hiyo ndio aina ya uandishi ktk globu hii...sisi wenyewe tunaelewa kama hiyo ni kitu cha kawaida HAPA...(KTK GLOBU HII).na inaweza isiwe sawa sehemu nyingine lakini HAPA ni tambarare tu...
ReplyDeleteMdau anaonyesha ugeni katika globu (hapa tena ni makusudi, tunajua neno halisi ni blog) ya jamii.
ReplyDeleteKaribu mgeni. Hiyo misamiati ndio lugha ya globu hii. Mtaa wa Samora Avenue, Jiji na New York City, Chuo Kikuu cha University, Man Yuu, Bwawa la Maini, Ukerewe, Mkuu wa Nanihii ya Nanihii nk. Pita mara kwa mara humu utazoea. Wadau wenzio hawajapata kichefuchefu bado.
JAMANI EEH!!(hapa nashauti)HEBU MWACHENI HUYO MZENJI WA WATU, HIVI HAMJUI KUWA KUKU MGENI HAKOSI KAMBA MGUUNI? NA HIYO KAMBA ISHAONEKANA MGUUNI KWAKE, CHA MSINGI NI KUMWAMBIA KARIBU KWENYE JAMVI MGENI! (sasa naongea kwa sauti ya kawaida, kwa sababu naongea na mgeni, asije akaogopa akakimbia bure nikishauti) mgeni hiki ndio kijiwe kinaitwa blogu ya jamii karibu sana wewe na my wife wako mjumuike nasi, msiugope hiyo ndio hali halisi na hiyo ndio lugha ya kijiwe chetu, utazoea tu mwanawane usikonde wala nini! Siku nyingine ukitaka kuingia kwa watu piga hodi ami yanguu! usikurupuke tuu watu hawatakulewa yakhee! hiki ni kiswahili cha bwejuu na paje ami!
ReplyDeleteHamm^mad kibindoni silaha nkononiii
ReplyDeleteHa weye ba nkwe Nselemuuu vereje kukuja humu, na kuanza kukosoa wenyewe humu? he weye weeee mhhm! ngojia wakosha majombo ya kinywa humu watovyokurukiaaa, ha weye kuntovukwa? lol.
Karibu mzee Mselem kwenye kijiji utazoea tu jinnsi ya kutumia kichwa na ulimi wako humu.
Wadau kesha elewa huyo bwa mselem,maana hata mimi alinishtua kuona kwamba lugha ya humu ndani inamsumbua sijui hajawahi kuitwa brother kaka......jamani kuuliza si ujinga eti kuna huu msemo(MTU MMOKO) una maana gani wadau kwa mwenyekujua
ReplyDeleteby usinijue1.
AISE MIE NDIO AFANDE ARONSO HIRI RIJAMA RIKO KAWPI NATAKA KURIKAMATA HIRI RISELEMU NIRIPIGE VIRUNGU VYA URIMI HIRI RIJAMAA WADAU MPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO! NEXT WEEK KUINGIA BLOG YA ITHA MITHUZI NI SH 100 NA USD 1 £ 1 Uero 5. Fande Aronso.(Alonso) asije mselem akasema oh hivi vile.
ReplyDeleteHaya wachafuzi wa lugha na waosha vinywa hebu taireni,wacheni kukiharibu kiswahili na kukitoa ladha yake,zamani kiswahili kilikuwa kikitamkwa vizuri lakini kadiri siku zikienda mbele waharibifu wachache wanakiharibu kama nyie mnao rusha makombora hapo juu kuna watu wengi wanaojifunza kiswahili kupitia blogu hii ya michuzi sasa si tunawachanganya na kiswahili kiswanglish.
ReplyDelete