Adhihaki madai anauchukia Mkoa wa Mbeya
Na Mwandishi Maalum,
Na Mwandishi Maalum,
Rungwe, Mbeya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amedhihaki na kukejeli madai ya baadhi ya watu na magazeti kuwa anauchukia mkoa wa Mbeya, na kuwa kwa sababu hiyo amekuwa anakwenda kuutembelea mkoa huo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amedhihaki na kukejeli madai ya baadhi ya watu na magazeti kuwa anauchukia mkoa wa Mbeya, na kuwa kwa sababu hiyo amekuwa anakwenda kuutembelea mkoa huo.
"Yamekuwapo maneno mengi ya kipuuzi kwamba Rais haupendi Mkoa wa Mbeya na kuwa amekuwa anakwepa kuutembelea mkoa huu," amesema Rais na kuongeza:
"Mtakumbuka, ndugu wananchi, kuwa niliutembelea Mkoa wa Mbeya Februari 19, mwaka 2006, baada ya kuwa nimeapishwa, kuja kuwashukuruni. Niliishia mjini Mbeya, lakini nikaahidi kuwa ningerudi kutembelea kila wilaya, na kila jimbo la uchaguzi katika mkoa huu, sasa nimerudi kutimiza ahadi."
Amesema kuwa amechukua muda kurejea mkoani Mbeya kwa sababu Tanzania ni nchi yenye wilaya nyingi, kwa sababu amekuwa anapitia katika mikoa mingi tu.
"Kwangu mimi hakuna mkoa bora zaidi ya mwingine. Mikoa yote ni sawa. Hakuna mkoa naupenda zaidi na kuuchukia mwingine. Haya maneno ya kwamba nauchukia mkoa wa Mbeya ni ya watu walioshiba ugali na maharage, na wakishakuwa wameshiba, basi kazi yao inakuwa ni kutunga na kubuni maneno ya kipuuzi kama haya."
Rais amesema kuwa kama angekuwa kweli anauchukia Mkoa wa Mbeya asiupatia mkoa huo mawaziri wawili waandamizi – yaani profesa Mark Mwandosya ambaye ni Waziri wa Maji, na profesa David Mwakyusa ambaye ni waziri wa afya na ustawi wa jamii. Wote wawili ni wabunge wa Wilaya ya Rungwe ambayo Rais ameitembelea leo.
"Kama nauchukia Mkoa wa Mbeya ningewateua wabunge wawili wa mkoa huo kushika nafasi za uandamizi za uwaziri? Mimi ndio mwenye mamlaka na madaraka ya kuchagua mawaziri. Silazimishwe na yoyote kumchagua yoyote," amesema Rais na kuongeza:
"Baraza nachagua mimi. Silazimishwi na yoyote kumchagua yoyote. Mara mbili nimefanya mabadiliko, lakini nikawarudisha wabunge wenu hawa kwenye baraza hilo, sasa chokochoko ni ya nini? Kama siyo maneno ya walioshiba ni nini? Ndugu wananchi, yapuuzeeni maneno haya."
Watu mbali mbali na hasa magazeti yamekuwa yanadai kuwa kutoutembelea mapema Mkoa wa Mbeya ni matokeo ya Rais Kikwete kuuchukia mkoa huo kwa sababu tu mmoja wa wabunge wa mkoa huo, profesa Mwandosya aligombea urais na kushindwa na Rais Kikwete 2005.
Mkoa wa Mbeya unakuwa mkoa wa 19 wa Tanzania Bara kutembelewa na Rais Kikwete kwa maana ya kutembelea kila wilaya tokea achukue madaraka mwaka 2005. Amebakiza mikoa miwili ambayo ni Morogoro na Tabora.
Pia hajatembelea Tanzania Visiwani.


Asanteni sana watu wa mkoa wa Mbeya kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais wetu. Shukrani za dhati ya moyo wangu kwa kujitokeza na mabango yenye ujumbe tofauti, hasa ule wa kuwashughulikia mafisadi.
ReplyDeleteMichuzi wewe ni mpambe tu wa Kikwete; nakushangaa kweli, kwani wewe huoni uchafu unaoendelea hapa Tanzania; watu kuwa wengi kumsikiliza JK sio kuwa wanampenda. Unakera sana Michuzi sometimes!..Au kwa sababu unapata kamgawo kutoka kwa mafisadi ndio maana unampamba Kikwete namna hiyo!Wewe na Silva Rweyemamu naona akili zenu zinafanana. COme back to your senses!
ReplyDeleteUkitaka kujua mtu kabarikiwa na Mungu angalia watu wanavyompenda. Huyu JK ameshika mpaka wadhifa mkubwa kabisa barani Afrika kuliko kiongozi yeyote wa Kitanzania. Hata AshaRose ni mteuliwa wake, asingemteua kuwa mbunge na waziri huenda asingeonekana. Na huenda JK asingepata uraisi basi ndiye angeshika wadhifa wa AshaRose.
ReplyDeleteHuyu jamaa alionyesha kupendwa na wananchi kila alipofanya kazi katika ngazi tofauti za majukumu.
Huyu JK huenda ndiye angekuwa raisi mwaka 1995 kama juhudi za wasioiva kidemokrasia zisingetumika.
Ukiona hivi, basi huyu mtu anaweza kuwa ni mwadilifu, si mbaguzi, mtu wa watu na mtumikia watu, ndo maana Anabarikiwa.
Kufika kileleni ghafla ni dalili ya baraka. Lakini kuna watu wanachukia baraka hizi watasema ni bahati. Ee BWANA MUNGU Muumba mbigu na nchi na vilivyomo, mbariki JK na umfanye awe FAIR (muadilifu, si mbaguzi)zaidi ya alivyo ili tuwe na amani. Maana ubaguzi ndo chanzo kikuu cha kuvunjika amani. Pasiwe na upendeleo wowote (dini, rangi, kabila, maili, wala nasaba). Tuendelee kuwa na haki sawa. Mungu, pia umshushe chini kila anayeshabikia ubaguzi kwa siri na kwa uwazi.
ReplyDeleteMungu Ibariki Tanzania na Afrika.
SIKU HIZI UMEKUWA MWANDISHI WA RAISI; TIMU YA TAIFA INACHEZA WALA HATUONI TENA MAKEKE YAKO. TARIME KUNA KAMPENI ZA UBUNGE WALA UTU HABARI KAMA ZAMANI.... NAONA UMEPATA KIKADI CHA JEMBE NA NYUNDO.
ReplyDeleteNI HAYO TU BROZA MICHUZI
(MUCH RESPECT- IMENIBIDI NISEME)
michuzi asante kwa news asha rose ni swahiba namba moja wa kikwete, huoni alimpa wizara yake mara tu alipoingia ikulu, prof mwandosya anaonekana kuwa na uwezo nae wa kutawala
ReplyDeletealiyempeleka asha rose matawi na juu si mwingine bali ni kikwete mwenyewe. sababu aliteuliwa kuwa mbunge na wala sio wa jimboni.
ReplyDelete