Bwana Michuzi,
Ahksante sana kwa kutukumbusha rafiki yetu na mjenzi wa taifa letu Mwalimu Nyerere.Ni matumaini yangu ya kwamba si mimi tu bali pia wadau wengi tutafurahia kuona picha zaidi za kiongozi wetu na matukio yatukumbushayo tulipotoka.
Pili, shukurani kwa kuendeleza libeneke la blog hii na kutufaidisha mpaka hapa nilipo karibu kabisa na ncha ya kaskazini mwa dunia! ALASKA! Niko katika mji mdogo wa Kotzebue ambao uko katika maili 33 juu ya mstari wa Aktik. Mungu Ibariki Tanzania! Naomba kuwakilisha.
Robert TuvakoKotzebue,
Alaska 99752USA
Duh Wabongo kweli noma mpaka Alaska kwa Sarah Palin mpo pia. Sasa mliwezaje kumchagua yule Illiterate Hockey Mum awe Gavana wenu?
ReplyDeleteOna sasa Mhishimiwa Misupu. Huyu jamaa kwa kuwa anakaa karibu na mwisho wa Dunia, hata jina lake ameanza kuliharibu mpaka tunashindwa kulisoma.Mimi nitamuita kwa jina la Karumazira au Karubandika tu.Maana hilo aliloandika siwezi kulisoma
ReplyDeleteNi kweli mnaiona Urusi tehee heee heee
ReplyDeleteAlaska unasomea upadre? najaribu kufikiria nini kimekupeleka huko kama sio upadri basi mwenzetu ni marine biologist hehehehhehe research za kumwaga tu huko.
ReplyDeleteNa wanasema weusi ni 2% tu.
Robert Tuvako sio wewe ulikua unaishi Michigan au majina yamefanana?
ReplyDeleteKama sio wee basi ulizia watu wa Michigan utakua una ndugu huko.
Alaska? Ok tell us the truth once and for all, Can you See Russia from your house? Yani Mchizi Putin unamcheki tu kwa mbali toka dirishani?
ReplyDeleteMdau wa 10/15/ 08:01 PM, unampata sana, ndiye yeye Pastor Robert Tuvako AKA Bob! ndo alikuwa MI, kaamia Alaska. Nafikiri mwandishi alikosea kuweka comma btn last name ya Tuvako na jina la mji. But yeye bado mmatumbi tu.
ReplyDeleteRobert hawezi kusomea upadri coz yeye ni Msabato but he's a Pastor.
Kotzebue is a city in Alaska
ReplyDeletesasa picha za nyerere we zi kusaidie nini padri?
ReplyDeleteNaam, naona mjadala umehamia kwa jina la mdau badala ya swala la kutukumbusha tulikotoka. Hakuna mahali tusipoweza kwenda kama tukinuia. Ni ukweli Alaska ni mbali sana kutoka Tanzania, lakini wanasema "waweza kumuondoa mwanakijiji toka kijijini kwake, bali huwezi kuondoa kijiji toka ndani yake." Pia, "Iwe mashariki au Magharibi, nyumbani ni bora kuliko pote". Mwalimu alijenga msingi bora wa nyumbani; tunashuhudia tunapotizama hata kutoka mbali, picha, hotuba na nasaha zake zastahili kukumbukwa.
ReplyDeleteMubarikiwe sana.