Ziara ya Mheshimiwa Rais Mkoani MbeyaRais Jakaya Mrisho Kikwete alihitimisha ziara yake ya siku 10 yenye mafanikio makubwa katika Mkoa wa Mbeya jana mchana, Jumamosi, Oktoba 18, 2008.Kwa bahati mbaya sana, baadhi ya vyombo vya habari nchini, na hasa magazeti, vimeandika baadhi ya matukio ya ziara hiyo, kwa namna ya wazi ya kuwapotosha wananchi kuhusu ziara hiyo ambako Rais alitembelea wilaya zote saba zenye halmashauri nane za Mkoa huo.
Taarifa hii inalenga kuweka bayana ukweli ulivyokuwa katika ziara hiyo ambako, kwa mara nyingine, Rais alipata nafasi nyingine nzuri kufanya kile ambacho hukifurahia sana kukifanya- yaani kukutana na wananchi, kusililiza kero zao, karaha zao, raha zao, mafanikio yao, na mahitaji yao ambayo wanaamini Rais wao anaweza kusaidia kuyatafutia majawabu.
(a) Rais akatisha ziara ya mkoa
Rais alipanga kukaa katika Mkoa wa Mbeya kwa siku 10. Amefanya hivyo. Hakukatisha ziara hiyo kama ilivyoandikwa katika baadhi ya magazeti. Aliingia Mbeya Oktoba 9, akaondoka Oktoba 13 jioni kwenda Tanga kuzima Mwenge, na akarejea jioni ya Oktoba 14 na kuondoka jana, Oktoba 18, jumla ya siku 10 kamili.
Ni vyema kujua kuwa kila Rais anapoweka mguu katika Mkoa wowote, iwe ni asubuhi, mchana ama jioni ni siku kamili ya kuwapo kwake katika Mkoa ama eneo hilo.Kilichotokea ni kwamba kwa sababu ya ratiba kuwa na shughuli nyingi, ziko shughuli mbili ambazo hakuweza kuzifanya. Ameahidi atapata nafasi ya kwenda tena Mbeya kuzifanya shughuli hizo.
(b) Mkutano wa majumuisho ya ziara kwenye Uwanja wa Sokoine
Na wala Rais hakuahirisha kuhutubia wananchi wa Mbeya kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine wakati wa majumuisho yake ya Mkoa huo kama inavyodaiwa.
Rais hakupangiwa kuhutubia mkutano kwenye uwanja huo kwa sababu alikwishakuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja huo Februari 19, 2006, alipokwenda kuwashukuru wananchi wa Mkoa huo kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuongoza nchi yetu.
Na wala Rais hafanyi majumuisho ya ziara za mikoa kwenye mikutano ya hadhara. Huifanya kazi hiyo kwa kukutana na viongozi wa kisiasa, kijamii, kiuchumi, kidini, na kiusalama wa mikoa katika mkutano wa viongozi. Ndivyo alivyofanya jana katika Ukumbi wa Mkapa mjini Mbeya.
(c) Kutotembelea Mbeya Vijijini
Kama nilivyoeleza hapo juu, Rais alitembelea wilaya zote saba za mkoa huo zenye halmashauri nane kwa sababu Mbeya yenyewe ni wilaya moja lakini ina halmashauri mbili, moja ya mjini na nyingine ya vijijini.Wakati mwingine uelewa wa waandishi wetu unapumbazisha kabisa.
Kabla ya kuingia kwenye mkutano wa majumuisho, Rais alitemebelea kiwanda cha kutotoa vifaranga vya kuku katika eneo la Songwe, ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa Songwe, pamoja na kuzindua hospitali teule ya wilaya ya Ifisi, vyote vikiwa katika eneo la Wilaya ya Mbeya lakini katika maeneo ya vijijini.
(d) JK akiri Mbeya ni pagumu
Huu pia ni upotoshaji mwingine. Kama kuna kitu Rais amekisema wakati wa majumuisho ya ziara yake ni kuumwagia sifa sana mkoa huo kwa jitihada za maendeleo ya wananchi – iwe katika elimu, iwe katika afya, iwe katika kilimo, iwe ni katika huduma za maji, iwe ni katika ufugaji, iwe katika umwagiliaji na maeneo mengine muhimu ya maendeleo.
Kile kinachoelezwa kuwa Mbeya ni pagumu, ni pale alipowasihi viongozi kujenga tabia na mwenendo wa uongozi wa pamoja akisisitiza kuwa viongozi hao wanajenga nyumba moja na hivyo hawana sababu ya kugombea fito kwa sababu ya tofauti zilizopo miongoni mwa baadhi ya viongozi wa Mkoa huo. Tofauti miongoni mwa viongozi wachache wa mkoa huo haziufanyi mkoa mzima wa Mbeya kuwa mgumu.
(e) Msafara wa Rais kupigwa mawe
Mwenendo mzima ambao uongozi wa Mkoa wa Mbeya unaweza kujivunia ni kujitokeza kwa wingi mno kwa mamia kwa mamia ya wananchi wa mkoa huo kila alipopita Rais ama kwenda kwa shughuli za maendeleo wakati wa ziara hiyo.Kila sehemu, wananchi walimtaka asimame, wamwone, awasalimie.
Na kama ilivyo ada, hakusita, hata sehemu moja, kufanya hivyo.Hamu ya wananchi wa Mbeya kumwona na kumsikiliza Rais wao ndiyo ilimfanya Mhe. Rais kusema kuwa alikuwa ameondoka Mkoa wa Mbeya akiwa na kumbukumbu nzuri za wema, ukarimu na upendo wa wananchi wa Mbeya.
Ilikuwa ni hamu hiyo hiyo ambayo wananchi wa kijiji cha Kanga walikuwa nayo wakati Rais anafanya ziara ya Wilaya ya Chunya ambako alipitia na kuhutubia mikutano mikubwa ya wananchi katika maeneo ya Chunya Mjini, Makongolosi na Mkwajuni.
Kwa bahati mbaya wakati anawasili katika kijiji cha Kanga tayari ilikuwa usiku kati ya saa moja na saa mbili kwa sababu ratiba ya maeneo mengine ilikuwa imecheleshwa mno na hamu ya wananchi wa maeneo hayo kumsimamisha na kumwona Rais wao.
Hivyo, msafara wake ukapita bila kusimama katika kijiji hicho.Kile kitendo cha kiongozi wao kutosimama katika kijiji hicho ambako wananchi walikuwa wamejitokeza kwa mamia, wakasimama barabarani kwa saa nyingi wakiwa na hamu kumwona Rais wao, kikachochea na kusisimua tahayari (frustration) kwa vijana ambao wakaanza kurusha mawe kwenye baadhi ya magari yaliyokuwa kwenye msafara.
(f) Magari ya Rais
Magari ya Rais, kwa maana ya magari yote yanayotengeneza sehemu kuu ya msafara wa Rais, hayakutupiwa hata jiwe moja. Na wala Rais mwenyewe hakupata habari za tukio hilo mpaka alipokuwa amewasili Ikulu ya Mbeya.Na alipopata habari hizo alitoa maelekezo maalum kuwa zisije zikachukuliwa hatua za kipolisi kusumbua kijiji kizima na kutaka upelelezi wa suala hilo ufanyike kwa uangalifu mkubwa bila jabza.
Magari yaliyotupiwa mawe ni yale yaliyokuwa nyuma katika sehemu ya pili ya msafara, yaani nje ya sehemu kuu ya msafara. Na mpaka Rais anaondoka Mbeya jana, ni watu watano tu walikuwa wametiwa mbaroni, tofauti na habari za kubuni za magazeti kuwa wamekamatwa watu 60.
Rais anaamini kuwa tukio hilo la kijiji cha Kanga ni tukio la uhalifu. Kamwe haiwezi kutokea Rais Kikwete asisumbuliwe na tukio lolote la uhalifu katika nchi yetu. Hili ni tuko lililomkera, lakini kama alivyoeleza kazi hiyo waachie polisi waendelee nayo.
Muhimu kusisitiza hapa ni kwamba tukio hilo siyo tukio linalowakilisha taswira ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya ambao wameonyesha mapenzi makubwa kwa kiongozi wao mkuu.
Ni makosa kwa kuuchukulia mkoa mzima wa Mbeya kama mkoa wa wahalifu kwa sababu ya tendo lililotendwa na watu wachache katika kijiji kimoja tu.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
I'm suddened by the unlawful incident in Mbeya but at the same time I see it as a wake up call to our leaders to remember that goverment is for the people and the few, Mafisadi.
ReplyDeleteRebellion, outlaw, chaos,etc are just few ways to understand that time has come for reforms.
wananchi have spoken and its time our leaders pay a close attention in it because I dont think their massage is coded straight up reality.
Time is up, wananchi need change now because of its urgency nothing come stop the change.
Michuzi bania hii hoja vilevile lakini ujumbe umefika kwako na nina imani utauwakilisha mbele.
Mlalahoi
sera ya CCM ni kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kuwafanya watu waelimike. The moment you educate your children they will start to point spots on your face. yaliyotokea Mbeya na Tarime yatatokea mengi. because people knows what is going on nchini
ReplyDeleteKilicho na mwanzo lazima kiwe na mwisho. Tunatambua kuwa kihistoria CCM kilitokana na ASP na TANU. Na wakati huo ilikuwa ni kukabiliana na changamoto za wakati huo tukawa na mabadiliko hayo.
ReplyDeleteMambo ya Tarime na Mbeya ni alama za nyakati kwamba watu wanahitaji mabadiliko ya kweli. Mambo ya ubabaishaji na kukumbatiana eti kwa itikadi za kichama,yanapitwa na wakati. Mimi najiandaa naona upepo unavyoelekea na sitaki kuwa wa mwisho nataka niwe miongoni mwa "change agent" na wengine wabishi watakubali baada ya mabadiliko na hasa mwaka 2010.
Ni hayo tu, nisiwachoshe.
Baada ya kupigwa mawe.......RAHISI akatisha ziara na kukimbia mkoa! DUH hio ni kali. Wajabe watakufuata waiti hausi na mawe sijui itakuwaje.....je utakimbia nchi?
ReplyDeleteHapo upevu wa kiongozi umepungua kwakweli. Yabidi aapolojaizi kwa wananchi, sio kuja na hivyo viprez relizi visivyo na kichwa wala mdomo bali propaganda.
Ha ha ha ha ha....
ReplyDeleteMambo ya press reliz za ikulu bwana, hawa bado wanatuona wajinga ee!!!!
Waliosoma magazeti wataamini kuwa kuna upotoshwaji wa habari (ingawa wenye matumizi mazuri ya akili wataujua ukweli halisi).Na sisi tuliohudhuria mikutano tuliona na kusikia mambo yasiyo ya ukweli? Au ukiwa mwandishi wa ikulu mchanga na mawe ni sawa na maua wanayorushiwa maharusi?
Asenti...
Michuzi usiibanie hii. Uhuru Maoni....